Author: Admin

Kiungo mahiri kutoka Ivory Coast, Pacome Zouzoua,inasemekana ameshasaini mkataba mpya na klabu ya Yanga SC siku nyingi zilizopita, muda mfupi tu baada ya fainali ya Kombe la CRDB. Kwa mujibu wa taarifa za ndani, mkataba huo wa miaka miwili ulitayarishwa na kusainiwa kipindi hicho, huku mpunga ukishalipwa rasmi fedha ambazo Zouzoua hakupoteza muda kuzitumia kujenga jumba la kifahari kwao Ivory Coast. Kwa sasa, kinachosubiriwa ni kurejea kwake Bongo, muda wowote kuanzia sasa, ili aungane na timu katika maandalizi ya msimu mpya (Pre-season). Kumbuka, msimu wa 2024/25 ulikuwa wa kifalme kwa Zouzoua, baada ya kutwaa tuzo ya MVP kutokana na kutikisa…

Read More

Rashford Kuvaa Jezi Namba 14 Barcelona Marcus Rashford rasmi atangazwa kuwa mchezaji wa Barcelona baada ya kukamilisha uhamisho wa mkopo kutoka Manchester United. Nyota huyo wa timu ya taifa ya England amepewa jezi namba 14, namba yenye uzito mkubwa katika historia ya klabu hiyo, ikiwa ni kumbukumbu ya wachezaji wakubwa waliowahi kuivaa, akiwemo Thierry Henry, Javier Mascherano, na Jordi Cruyff. Katika hafla ya utambulisho iliyohudhuriwa na Rais wa Klabu Joan Laporta, Mkurugenzi wa Michezo, pamoja na wajumbe wa bodi ya FC Barcelona, Rashford alisaini mkataba wake kama mchezaji mpya wa klabu hiyo, mkataba ambao unatarajiwa kudumu hadi Juni 30, 2026,…

Read More

Katika kipindi hiki cha dirisha kubwa la usajili, habari kuhusu wachezaji wakuu na usajili wao huwa kivutio cha umma. Miongoni mwao ni Ellie Mpanzu, kiungo mahiri wa Simba SC, ambaye hivi karibuni amezungumzia uwezekano wa kuondoka katika klabu hiyo na kujiunga na wapinzani wao wa jadi, Yanga SC. Katika mahojiano yake, Mpanzu alieleza kuwa amekuwa akipokea shinikizo kutoka kwa mashabiki na wanachama wa timu kuhusu mustakabali wake. Alikiri kuwa, ingawa anaipenda Simba, anahitaji kufanya maamuzi bora kwa ajili ya maendeleo yake binafsi na ya taaluma yake. “Soka ni kazi, na kila mchezaji anahitaji fursa ya kuonyesha uwezo wake,” alisema…

Read More

Klabu ya Yanga imeendelea kujiimarisha kuelekea msimu mpya baada ya kumtambulisha rasmi kiungo mkabaji wa Mlandege, Abdulnassir Mohammed Abdallah, maarufu kama “Casemiro”, kwa mkataba wa miaka mitatu. Usajili wa kiungo huyo mahiri ulimalizika tangu Julai 2, 2025, lakini klabu hiyo imemtambulisha rasmi leo, ikiwa ni sehemu ya mipango yao ya kusuka kikosi imara na chenye ushindani wa hali ya juu. Katika kumsajili, Yanga walishinda vita kali ya saini yake dhidi ya klabu kama Azam FC, JKT Tanzania na Singida Black Stars, ambazo zote zilikuwa kwenye harakati za kumchukua kiungo huyo tegemeo kutoka Zanzibar. Abdulnassir, anayefahamika kwa jina la utani la…

Read More

YANGA SC hawana jambo dogo mara baada ya kumalizana na mashine ya mabao ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhamiwaniwa na NBC. Msimu wa 2024/25 nyota huyo alikuwa kwenye ubora akiwa ni chaguo la kwanza ndani ya kikosi cha Tabora United. Ni Kiungo mshambuliaji aliyekuwa Tabora United, Offen Chikola alitambulishwa Yanga SC Julai 22 2025 kwa kandarasi ya miaka miwili.2024/25 akiwa na Tabora United alifunga mabao 8 kati ya 28 yaliyofungwa na timu hiyo. Ni nafasi ya tano kwenye msimamo pointi 38 baada ya mechi 30 ilikusanya Tabora United. Ipo wazi katika mchezo wa mzunguko wa kwanza, Uwanja wa Azam…

Read More

WAKATI Azam FC ikimpigia hesabu aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Clatous Chama ikiwa ni pendekezo pia la kocha wa timu hiyo, Florent Ibenge, kikosi hicho kinakabiliwa na ushindani kutoka kwa Zesco United ya Zambia inayomuhitaji. Nyota huyo aliyezichezea timu mbalimbali zikiwemo Ittihad Alexandria SC ya Misri, Lusaka Dynamos FC ya Zambia, Simba ya Tanzania na RS Berkane ya Morocco, kwa sasa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake na Yanga kufikia tamati. Chama aliyejiunga na Yanga Julai 1, 2024, kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya kuachana na Simba, inadaiwa ameshindwa pia kuongeza mwingine na mabingwa hao wa Ligi Kuu…

Read More

YANGA inaendelea na marekebisho kadhaa ya kiufundi kwenye kikosi chake kuelekea kwenye maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa. Mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara mara nne mfululizo, inaripotiwa kwamba wataweka kambi ya maandalizi nchini Rwanda wiki chache zijazo. Lakini habari mpya ni kwamba jina la Kocha kijana Mfaransa mwenye uzoefu na soka la Afrika limetua mezani kwao. Kocha huyo ni Romain Folz (34) lakini sifa yake kubwa ikitajwa ni soka la kushambulia lenye pasi nyingi na mtu makini kazini. Kazi yake ya mwisho ilikuwa Msaidizi kwenye benchi la Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini mwaka…

Read More

NDOTO ya mshambuliaji wa Simba SC na Taifa Stars, Kibu Dennis kucheza soka la kulipwa Marekani inakaribia kutimia baada ya klabu ya Nashville kumwongezea wiki ya majaribio kutokana na kile kinachoelezwa ni kivutio kwa makocha wa kikosi hicho. Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vya karibu na mchezaji huyo, Kibu ambaye yuko Marekani tangu mwisho wa mwezi Juni, alikuwa amepewa wiki mbili za awali za kuonyesha uwezo wake. Hata hivyo, baada ya kipindi hicho kukamilika, uongozi wa Nashville SC inayoshiriki Ligi Kuu Marekani umevutiwa na mwenendo wake na kuamua kumwongeza wiki nyingine ya tathmini ya kiufundi. “Kibu anapambana kweli kweli,”…

Read More

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba SC msimu wa 2025/26 wameweka wazi kuwa mpango kazi wa kufanya usajili upo chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids. Ikumbukwe kwamba msimu wa 2023/24 Simba SC iligotea nafasi ya tatu kwenye msimamo ikapeperusha bendera kwenye Kombe la Shirikisho Afrika. Kwa msimu wa 2024/25 iligotea kuwa mshindi wa pili Kombe la Shirikisho Afrika na bingwa alikuwa ni RS Berkane. Kwa mujibu wa Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC Ahmed Ally ameweka wazi kuwa mpango mkubwa kwa msimu ujao ni kufanya vizuri zaidi na watafanya usajili makini. “Kwenye kufeli msimu…

Read More

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2024/25, Yanga SC chini ya Kocha Mkuu, Miloud Hamdi wamekamilisha dili lao na kiungo kiraka Mudathir Yahya. Mudathir Yahya mkataba wake ulikuwa umeisha mara baada ya msimu kufika ukingoni alikuwa kwenye mazungumzo na mabosi wa timu hiyo kuhusu kuongeza mkataba wake. Ilikuwa inatajwa kuwa kiungo huyo alikuwa kwenye rada za Simba SC ambayo ilikuwa inafanya naye mazungumzo alipokuwa huru ili awe ndani ya kikosi chao. Julai 22 2025, Yanga SC wamemtambulisha rasmi Mudathir kuwa ameongeza mkataba wa miaka miwili kuwa ndani ya kikosi hicho. Ni 2025 mpaka 2027 Mudathir atakuwa kwenye majukumu…

Read More

Aliyekuwa mtathimini viwango ‘Performance Analysist’ wa klabu ya Simba raia wa Zambia Culvin Mavunga ametangaza kuondoka ndani ya klabu hiyo baada ya misimu mitano aliyodumu ndani ya timu hiyo. Kupitia ukurasa wake wa instagram amewashukuru mashabiki na viongozi wa klabu hiyo kwa kipindi chote walichofanya kazi pamoja. “Ukurasa wangu na Simba SC imefika mwisho. Imekuwa misimu 5 ya kuvutia na timu. Tulishinda, tukashindwa na kutoka sare pamoja. “Pongezi zangu za dhati ziwaendee Mashabiki wa Simba, nyie watu wa muhimu, kwa Bodi na Uongozi wa Simba, asante kwa kila jambo. Kwa Benchi la Ufundi la Simba, upendo sana na nyinyi ni…

Read More

Timu ya Taifa ya Kenya Harambee Stars imejiondoa kwenye mashindano ya CECAFA yanayojumuisha timu nne, yaani Tanzania, Kenya, Uganda na Senegal ikiwa ni masaa machache kabla ya kutakiwa kucheza mchezo wa ufunguzi dhidi ya Uganda majira ya saa 9 jioni. Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la mpira la Nchi hiyo limeweka wazi kuwa sababu ya timu hiyo kujiondoa ni baada ya kocha mkuu wa Taifa hilo Benni McCrthy kutoridhishwa na mazingira ya mashindano hayo. Awali timu ya taifa ya CONGO BRAZA VILLE ilijiondoa kwenye mashindano hayo wiki moja kabla ya michuano hiyo kuanza kutokana na kupata changamoto ya kusafiri, na baadaye…

Read More

CV ya Moussa Balla Conte Mchezaji Mpya wa Yanga Sc 2025/2026 Klabu ya Yanga imekamilisha dili la kiungo wa ulinzi mwenye uwezo mkubwa, Moussa Balla Conte, ambaye anatokea CS Sfaxien ya Tunisia, kwa mkataba wa miaka miwili unaotarajiwa kudumu hadi Juni 30, 2028. Conte ni mchezaji wa kwanza kutambulishwa rasmi na Yanga SC katika dirisha la usajili la msimu wa 2025/2026, hatua inayodhihirisha dhamira ya klabu hiyo kuimarisha safu ya kiungo kufuatia kuondoka kwa Khalid Aucho. Taarifa Binafsi za Moussa Balla Conte Jina kamili: Moussa Balla Conte Tarehe ya kuzaliwa: 15 Aprili, 2004 Umri: Miaka 21 (2025) Uraia: Guinea Mji…

Read More

AZAM FC matajiri wa Dar wamepanga kutumia michuano ya Kimataifa Afrika (Chan) kwa ajili ya kufanya usajili wa msimu ujao wa 2025/26. Ipo wazi kwamba CHAN mchezo wake wa ufunguzi unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Agosti 2 kati ya Tanzania ambao ni wenyeji itakuwa dhidi ya Burkina Faso. Tayari Azam FC imekamilisha usajili wa kipa mzawa Aishi Manula ambaye alikuwa ndani ya kikosi cha Simba SC amerejea kwa mara nyingin ndani ya kikosi hicho kwa changamoto mpya 2025/26. Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Azam, Thabit Zakaria amesema kuwa wamepanga kusajili wachezaji wa kigeni wenye uzoefu wa kimataifa wakati wakijiandaa…

Read More

Mchezaji wa Real Madrid, Jude Bellingham kupitia ukurasa wake wa Instagram amepost picha akiwa kweye kitanda cha Hospitali ikiwa ni baada ya kufanyiwa upasuaji wa jeraha la bega ambalo litamuweka nje mpaka mwezi October. Kwenye chapisho lake amewashukuru manesi na madaktari walioshiriki kufanikisha upasuaji huo.

Read More

Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwatuliza mashabiki wa Simba huku akithibitisha kuwa ni kweli kiungo Moussa Balla Conte aliyetambulishwa na wapinzani wao usiku wa leo alikuwa kwenye orodha ya kocha Fadlu. “Wana Simba hakuna sababu ya kujisikia unyonge na wala tusijitie presha.Hii sio hadithi ya sizitaki mbichi hizi bali uhalisia wa jambo lenyewe. “Iko hivi kwenye ripoti za Makocha hua kuna orodha ya majina mengi ya Wachezaji wanaopendekezwa Ni kweli jina la mchezaji huyo lilikuwa kwenye orodha ya Kocha wetu kama yalivyokua majina mengine mengi Afrika nzima “Wakati…

Read More

Beki wa kati wa klabu ya Simba raia wa Cameroon Che Malone Fondoh huwenda akaondoka klabuni hapo na kujiunga na klabu ya USM Alger inayoshiriki ligi kuu Nchini Algeria. Mchezaji huyo aliyejiunga na Simba Julai 2023 akitokea Cotton Sport ya ligi kuu Nchini kwao anaondoka Simba kwa makubaliano ya pande zote mbili. Taarifa zinasema wekundu hao wa msimbazi tayari wamepata mbadala wa beki huyo na wapo katika hatua nzuri ya kumalizana naye ili kurithi mikoba ya Che Malone aliyekuwa chaguo la kwanza la Kocha Fadlu.

Read More

NAHODHA wa Simba SC, Mohamed Hussen msimu wa 2024/25 kuna uwezekano mkubwa akaibukia ndani ya kikosi cha Yanga SC akiwa ni mchezaji huru. Ikumbukwe kwamba Zimbwe aliongeza mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba SC mwaka 2023 tayari 2025 umefikika tamati Julai 10 2025 hivyo kwa sasa mchezaji huyo ni huru. Julai 19 2025, Zimbwe Jr aliandika ujumbe wa kuwashukuru Simba SC akiwaaga mashabiki na wachezaji aliokuwa nao ndani ya kikosi cha Simba SC. Kuna asilimia kubwa Zimbwe Jr akatambulishwa ndani ya Yanga SC akiwa ni mchezaji huru kwa kuwa taarifa zinaeleza kuwa wamefikia hatua nzuri kwenye mazungumzo. Rekodi zinaonyesha kuwa…

Read More