Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Contact Us
    • Privacy Policy
    Facebook Instagram YouTube
    Chikao Media
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • MAGAZETI YA LEO
    • TETESI ZA SOKA
    • BOXING
    • FORUM
    Chikao Media
    Home » KOCHA WA MAMELOD SUNDOWN KUULA YANGA….JAMAA ANA MIAKA 34 TU
    KITAIFA

    KOCHA WA MAMELOD SUNDOWN KUULA YANGA….JAMAA ANA MIAKA 34 TU

    By AdminJuly 22, 2025No Comments3 Mins Read
    Share WhatsApp Facebook Twitter Pinterest Telegram Email Copy Link
    Follow Us
    Facebook Instagram YouTube
    yanga
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email Copy Link

    YANGA inaendelea na marekebisho kadhaa ya kiufundi kwenye kikosi chake kuelekea kwenye maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa.

    Mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara mara nne mfululizo, inaripotiwa kwamba wataweka kambi ya maandalizi nchini Rwanda wiki chache zijazo. Lakini habari mpya ni kwamba jina la Kocha kijana Mfaransa mwenye uzoefu na soka la Afrika limetua mezani kwao.

    Kocha huyo ni Romain Folz (34) lakini sifa yake kubwa ikitajwa ni soka la kushambulia lenye pasi nyingi na mtu makini kazini. Kazi yake ya mwisho ilikuwa Msaidizi kwenye benchi la Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini mwaka jana. Habari ambazo zinasema kwamba Yanga wako kwenye mazungumzo na Kocha huyo miongoni mwa tageti zao kuchukua nafasi ya Miloud Hamdi aliyetimkia Ismailia ya Misri.

    Msemaji wa Yanga, Ali Kamwe amenukuliwa akitamba kwamba tayari wameshamalizana na kocha mmoja kijana na watamshusha muda wowote ingawa akaficha jina lake.

    Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika ni kuwa; “Makubaliano na kocha Romain Folz kujiunga na Yanga yako karibu kukamilika. Kuna mazungumzo yanayoendelea kuhusu mkataba wa miaka miwili pamoja na chaguo la mwaka mmoja wa ziada. Kulikuwa na makocha wengine waliokuwa wanatazamwa, lakini klabu imeonyesha nia kubwa kwa Kocha Folz.”

    Awali Yanga ilitajwa kuonyesha nia ya kumuajiri Kocha kijana na maarufu wa Afrika Kusini, Rulani Mokwena lakini badae dili hilo likashindikana.

    Lakini katika wiki za hivikaribuni amekuwa akitajwa zaidi, kocha wa ASEC Mimosas, Julien Chevalier, ingawa yeye inaelezwa kuwa uongozi wake umempa ofa nzuri na mikakati mipya asalie kwenye timu hiyo kutengeneza mifumo imara zaidi ya vijana na kuimarisha malengo ya klabu hiyo kimataifa. Hivyo Yanga huenda wakamkosa, ingawa lolote linaweza kutokea.

    “Yanga inaamini kuwa Folz anaweza kuipandisha zaidi na kuendana na mipango yao ambayo ni kucheza pia soka la kuvutia, kufanya vizuri zaidi katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao. Wana imani kuwa wana kikosi bora na kuwa na Romain Folz kama kocha kutawawezesha kwenda mbali zaidi kwenye mashindano hayo,” kilieleza chanzo chetu.

    Folz amejijengea jina Barani Afrika baada ya kuifundisha Township Rollers ya Botswana, alihamia Afrika Kusini mwaka 2022 kujiunga na Marumo Gallants, ambapo alikua kocha mdogo zaidi katika Ligi Kuu wakati huo. Baadaye alihamia AmaZulu FC, kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu hiyo mwaka 2023.

    Katika msimu wa 2024/25, alijiunga na Mamelodi Sundowns kama kocha msaidizi lakini aliacha kazi pamoja na kocha mkuu Manqoba Mngqithi, miezi michache baada ya msimu kuanza.

    DONDOO ZAKE

    Kuzaliwa: Juni 28, 1990 (34)

    Sehemu: Bordeaux, Ufaransa

    UKOCHA

    2018-West Virginia United

    2019-Uganda (Msaidizi)

    2019–2020-Pyramids (Msaidizi)

    2020-Bechem United

    2020–2021-Niort (Msaidizi)

    2021-Ashanti Gold

    2021–2022-Township Rollers

    2022-Marumo Gallants

    2022–2023-AmaZulu

    2023–2024-Horoya

    2024-Mamelodi Sundowns (Msaidizi)

    Yanga SC
    Follow on Facebook Follow on Instagram Follow on YouTube
    Share. WhatsApp Facebook Twitter Pinterest Email Copy Link
    Previous ArticleKIBU NAYE KUIPA ‘THANK YOU’ SIMBA?….WAMAREKANI WAZIDI KUDATA NAYE KILA SIKU
    Next Article ILE STORI YA CHAMA KWENDA AZAM FC UKWELI HUU HAPA….FEI TOTO BYE BYE?

    Related Posts

    Ujenzi wa Arena, Serikali Yatenga Bil400

    April 3, 2026

    Selemani Mwalimu Yupo Anakuja, Mjiandae

    April 3, 2026

    MSIGWA AELEZA SABABU ZA KUONGEZEKA GHARAMA UWANJA WA ARUSHA

    March 31, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    Bernardo Apewa Thank You Rasmi Man City

    Ujenzi wa Arena, Serikali Yatenga Bil400

    Selemani Mwalimu Yupo Anakuja, Mjiandae

    MSIGWA AELEZA SABABU ZA KUONGEZEKA GHARAMA UWANJA WA ARUSHA

    Neymar amuachia Mungu kutoitwa timu ya Taifa

    “Nimehuzunika,Nimeumia lakini ndoto bado inaishi”Neymar Jr.

    © 2026 CHIKAO MEDIA | All Rights Are Reserved
    • Contact Us
    • Privacy Policy

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.