Author: Admin

Serikali imezindua mpango mkubwa wa kuimarisha sekta ya burudani na michezo nchini kwa kutenga zaidi ya Shilingi bilioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa michezo na burudani (Arena) pamoja na studio kubwa za kisasa za utengenezaji wa filamu. Hatua hii imetangazwa na Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA, akisisitiza kuwa mradi huo utafungua ukurasa mpya kwa wadau wa sanaa na michezo hapa nchini. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Arena hiyo itajengwa mkoani Dodoma na itaambatana na miundombinu ya kisasa ya studio zitakazowezesha utengenezaji wa kazi za filamu…

Read More

Hadi sasa msimu ukiendelea kushika kasi, mbio za kuwania Kiatu cha Dhahabu katika Ligi Kuu ya NBC zimezidi kuwa kali na zenye ushindani mkubwa. Mshambuliaji Selemani Mwalimu ameendelea kuwa moto, akifikisha jumla ya mabao sita (6) na kujipanga sambamba na washambuliaji wengine hatari kama Prince Dube, Depu na Saleh Karabaka kwenye orodha ya wafungaji bora. Kinara wa ufungaji kwa sasa ni Fabrice Ngoy mwenye mabao nane (8), akifuatiwa kwa karibu na Feisal Salum ‘Fei Toto’ aliyefunga mabao saba (7). Hali hii inaonyesha wazi namna ushindani ulivyo mkali, huku Mwalimu akithibitisha ubora wake mbele ya lango na kuendelea kuwa miongoni mwa…

Read More

Serikali imeeleza sababu za kuongezeka kwa gharama za ujenzi wa uwanja wa mpira unaojengwa mkoani Arusha, ambapo sasa zimefikia shilingi bilioni 338.54 kutoka makadirio ya awali ya shilingi bilioni 187. Akizungumza kuhusu maendeleo ya mradi huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema kuwa ongezeko hilo linatokana na maboresho yaliyolazimika kufanyika ili kukidhi viwango vya kimataifa vilivyowekwa na Confederation of African Football (CAF). Amefafanua kuwa mabadiliko hayo yalihusisha kuboresha miundombinu ya uwanja huo, ikiwemo huduma za kisasa, usalama, pamoja na uwezo wa kuhimili mashindano makubwa ya kimataifa.…

Read More

Baada ya Neymar Jr kuachwa nje ya kikosi cha Brazil kwa ajili ya mechi zijazo za kimataifa, na kocha wa timu hiyo Carlo Ancelotti kueleza sababu za uamuzi huo, Nyota huyo ametoa ujumbe mpya kupitia ukurasa wake wa mitabdao ya kijamii. “Neymar hatakiwi kuitwa kwa sababu hayuko sawa kwa asilimia 100. Bado anaweza kuitwa kwa ajili ya Kombe la Dunia. Anahitaji kuendelea kucheza michezo ili kudumisha hali nzuri ya kimwili.” alisema Kocha wake. Kupitia Instagram yake nyota huyo alichapisha picha na kuandika maneno “Yohana 13:7” usemao “Yesu akajibu, akamwambia, nifanyalo hujui sasa, lakini uralufahamu baadae” Wakati huo huo, Endrick ameitwa…

Read More

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Brazil na Klabu ya Santos Neymar Jr amefunguka baada ya kutojumuishwa kwenye kikosi cha Timu yake ya Taifa kitakachocheza mechi 2 za kirafiki kujiandaa na Kombe la Dunia 2026. Neymar ameweka wazi kuwa ameumizwa kukosekana kwenye kikosi hicho kilichoitwa na Carlo Ancelotti huku akisema kuwa bado kuna nafasi moja ya mwisho. “Nimehuzunika, nimeumia lakini ninalenga kabisa kila siku mazoezi baada ya mazoezi, mchezo baada ya mchezo kwa sababu bado kuna nafasi moja ya mwisho, NDOTO BADO INAISHI na tutaifikia lengo letu!”, amesema Neymar Jr .

Read More

MSHAMBULIAJI wa Yanga Laurindo Dilson ‘Depu’ amechaguliwa kuwa mchezaji Bora wa mwezi Februari wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa mwaka 2025/26, huku kocha wa Simba, Steve Barker akichaguliwa kuwa Kocha Bora wa ligi hiyo kwa mwezi huo. Katika taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi, imesema: Laurindo alionesha kiwango kizuri chenye mwendelezo kwa mwezi huo ikiwa ni pamoja na kufunga mabao mawili katika michezo miwili ambayo Young Africans ilicheza na kuisaidia timu yake kusalia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC. Mshambuliaji huyo aliwashinda beki Rushine De Reuck wa Simba na kiungo Idd Selemani ‘Nado’ wa Azam alioingia nao…

Read More

Mamlaka za Dubai zimesema kwamba moto umeteketeza eneo la karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai baada ya shambulio la kutumia drone kugonga tangi la mafuta karibu na Uwanja huo wa Ndege.  Moto ulizuka baada ya drone kushambulia na kugonga tangi la kuhifadhia mafuta, jambo lililosababisha moto mkubwa katika eneo hilo.  Shambulio hili lilihusiana na mzozo unaoendelea wa kijeshi katika eneo la Mashariki ya Kati.  Timu za Zimamoto na Uokoaji za Dubai zinashughulikia tukio hilo na juhudi zinaendelea ili kudhibiti moto huo. Mamlaka zimekuwa zikichukua hatua zote muhimu kuhakikisha usalama kwa watu katika eneo hilo.…

Read More

Timu ya Taifa ya Tanzania national football team imepata pigo kubwa katika safu yake ya ulinzi baada ya mabeki wake watatu kupata majeraha makubwa yaliyowalazimu kufanyiwa upasuaji, hali itakayowafanya kukaa nje ya uwanja hadi mwishoni mwa msimu wa 2025/26. Mabeki waliopata majeraha hayo ni Wilson Nango wa Simba SC, Dikson Job wa Young Africans S.C. pamoja na Abdulrazack Hamza ambaye pia anakipiga katika klabu ya Simba SC. Kukosekana kwa mabeki hao kunatajwa kuwa pengo kubwa kwa kikosi cha Taifa Stars kuelekea mechi zake zijazo. Kutokana na hali hiyo, kocha wa Taifa Stars Miguel Gamondi atalazimika kutafuta mbadala katika safu ya…

Read More

Mchezo wa dabi ya jiji la Dar es Salaam kati ya Azam FC na Young Africans S.C. unatarajiwa kupigwa usiku wa leo, Machi 15, 2026, saa 2:30 usiku kwenye dimba la Benjamin Mkapa Stadium. Mchezo huu unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini kutokana na ushindani mkubwa uliopo kati ya timu hizi mbili ambazo zimekuwa zikikutana mara kwa mara katika michezo yenye mvuto mkubwa. Dabi hiyo pia ina uzito wa kipekee kwa upande wa benchi la ufundi la Yanga, kwani itakuwa mtihani wa kwanza kwa kocha mpya wa timu hiyo, Pedro Gonçalves, tangu akabidhiwe rasmi jukumu la kuinoa…

Read More

Kocha mkuu wa Chelsea FC, Liam Rosenior, amesema klabu hiyo “imepata mchezaji bora zaidi duniani katika nafasi yake” baada ya beki wa kulia Reece James kusaini mkataba mpya wa miaka sita. James, mwenye miaka 26, alijiunga na timu kubwa ya Chelsea na kucheza mechi yake ya kwanza katika kikosi cha wakubwa mwezi Septemba 2019 akitokea timu ya vijana ya ‘the blues’. Rosenior alisema hawezi kuacha kutabasamu kutokana na habari kwamba James ataendelea kubaki klabuni kwa muda mrefu, “Siwezi kuacha kutabasam Reece James amesaini mkataba mpya na tumehakikisha mchezaji bora zaidi duniani katika nafasi yake anaendelea kubaki hapa!” “Alikuwa na fursa…

Read More

Dar Young Africans wanazidi kuchanja mbuga baada ya kuendeleza mwenendo mzuri kwenye michuano ya ndani ikiwemo ligi na FA lakini kwa isivyo bahati walitolewa kwenye michuano ya CAF. Inawezekana huu ukawa ni msimu wa Yanga ambao umebeba hisia mchanganyiko fahari ya kutawala ligi ya nyumbani na maumivu ya kuishia njiani kwenye anga la kimataifa. Hata hivyo, picha kubwa inaonyesha timu yenye uthabiti, malengo na mwelekeo wazi wa mafanikio. Kwenye ligi kuu yaani (NBC)Tanzania Bara, Yanga wamekuwa mfano wa kuigwa baada ya kuwa na matokeo mazuri, wameonyesha uwezo wa kushinda mechi kwa mitindo tofauti iwe ni kwa mabao mengi au ushindi mwembamba wa…

Read More

Waziri wa Michezo na Vijana wa Iran, Ahmad Donyamali, amesema timu ya taifa ya wanaume ya nchi hiyo huenda isishiriki katika michuano ya FIFA World Cup 2026 kutokana na hali ya usalama na mvutano wa kisiasa unaoendelea. Akizungumza katika mahojiano na kituo cha televisheni cha michezo cha Islamic Republic of Iran Broadcasting (IRIB) siku ya Jumanne, Donyamali alisema mazingira ya sasa hayaruhusu Iran kushiriki katika mashindano hayo makubwa ya soka duniani. “Kwa kuzingatia kwamba serikali hii imehusika katika kumuua kiongozi wetu, hatuna kabisa mazingira sahihi ya kushiriki Kombe la Dunia. Wachezaji wetu hawako salama, na hali iliyopo hairuhusu ushiriki,” alisema.…

Read More

Mshambuliaji wa timu ya Al Nassr Benghazi, Steven Mukwala, ameendelea kuonyesha kiwango kizuri baada ya kufunga bao lake la pili tangu ajiunge na klabu hiyo. Mukwala alifunga bao hilo usiku wa kuamkia leo katika mchezo wa ligi, ikiwa ni mechi ya pili mfululizo kwake kufunga tangu aanze kuitumikia timu hiyo. Mafanikio hayo yanaonyesha dalili nzuri kwa mshambuliaji huyo ambaye taratibu anazidi kuzoea mfumo wa timu na kuanza kuwa msaada mkubwa kwenye safu ya ushambuliaji. Kwa sasa Al Nassr Benghazi wanaendelea kushikilia nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 32, wakifuatiwa kwa karibu na wapinzani wao Al Ahly…

Read More

Mchambuzi nguli wa soka nchini, Edo Kumwembe, ametoa tathmini yake kuhusu kiwango cha kiungo wa Simba SC, Clatous Chota Chama, katika mchezo wa dabi dhidi ya Yanga uliopigwa hivi karibuni. Katika uchambuzi wake, Kumwembe amebainisha kuwa ingawa Simba walionyesha uhai kupitia kwa Inno Loemba, hali imekuwa tofauti kwa upande wa Chama ambaye amekuwa mhimili wa timu hiyo kwa miaka mingi. ​Katika andiko lake, Edo Kumwembe ameeleza upungufu huo wa kiwango cha Chama kama ifuatavyo: SOMA: Hii Hapa Orodha ya Waamuzi wa Dabi ya Kariakoo 2026 ​”Katikati ya uwanja Inno Loemba alionekana kuwapa Simba uhai huku akicheza sambamba na kaka yake,…

Read More

Afisa Habari wa Young Africans, Ally Kamwe, ametoa malalamiko mazito dhidi ya wapinzani wao Simba SC, akidai kuwa mambo mengi yasiyo ya michezo yalitawala kuelekea kupatikana kwa sare ya 0-0 katika dabi iliyopita. Kamwe amedai kuwa kulikuwa na matukio ya utata ya uamuzi pamoja na vitendo vya ushirikina ambavyo viliisaidia Simba kupata alama hiyo moja. ​Katika andiko lake, Ally Kamwe amefunguka yafuatayo: ​”Kwanza ilikuwa OFFSIDE.. Pili, AKASHIKA. Move ikaruhusiwa kuendelea kama hakijatokea kitu. Sitaki kabisa kukumbusha kuwa Mchezaji huyu alitakiwa kufungiwa MECHI 5 kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Dodoma Jiji … Sitaki kuwakumbusha, kuwa Waamuzi walishatishiwa kufungiwa Maisha…

Read More

KIPUTE cha watani wa jadi kati ya Yanga na Simba kinatarajiwa kupigwa Jumapili, Machi 01, 2026, kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar kuanzia saa 2:15 usiku. Mchezo huo unakuja katika kipindi ambacho Yanga wanaingia wakiwa na rekodi bora dhidi ya watani wao, baada ya kushinda mechi sita mfululizo za mwisho za Dabi ya Kariakoo. Katika michezo hiyo sita, Yanga waliibuka na ushindi wa mabao 5-1, 2-1, 1-0, 1-0, 2-0 na 1-0 dhidi ya Simba, wakionesha ubabe wa wazi katika miaka ya karibuni. Takwimu hizo zinaweka presha kubwa kwa Simba ambao wataingia dimbani wakihitaji kuvunja mwendelezo huo na kurejesha heshima…

Read More

Bodi ya Ligi imetangaza orodha ya waamuzi watakaoongoza mchezo wa Dabi ya Kariakoo utakaopigwa Jumapili, Machi 01, 2026, katika dimba la New Amaan Complex, Zanzibar. Kwa mujibu wa tangazo la Bodi ya Ligi: Mwamuzi wa Kati: Nassoro Mwinchui kutoka Tanga Mwamuzi Msaidizi 1: Kassim Mpanga kutoka Dar es Salaam Mwamuzi Msaidizi 2: Hamdani Said kutoka Mtwara Mwamuzi wa Akiba: Ramadhan Kayoko kutoka Dar es Salaam Mtathimini wa Waamuzi: Israel Mjuni kutoka Dar es Salaam Dabi ya Kariakoo ni mojawapo ya mechi zinazovutia zaidi nchini, ikichanganya ushindani mkali kati ya Simba na Yanga, na kushirikisha mamia ya mashabiki wa mpira wa miguu. Kuteuliwa kwa waamuzi hawa kunalenga kuhakikisha mchezo…

Read More

Angel Benard – NIMEONA Mp3 Download Tanzanian gospel powerhouse Angel Benard returns with a soul-stirring new single titled “NIMEONA,” a heartfelt worship anthem that reflects gratitude, testimony, and unwavering faith. RELATED: Angel Benard – Siteketei Known for her emotive delivery and ability to connect deeply with listeners, Angel Benard uses this release to inspire hope and celebrate God’s faithfulness in every circumstance. On “NIMEONA,” Angel’s expressive vocals glide over a polished instrumental layered with gentle keys, rhythmic percussion, and harmonious backing vocals. The production balances contemporary gospel sensibilities with traditional Swahili worship influences, creating a worship experience that is both…

Read More

Wafungaji Bora Ligi Kuu ya NBC Tanzania 2025/2026 | Vinara wa Magoli NBC Premier league 2025-26 | Wafungaji Bora Ligi Kuu ya NBC 2025/2026 | Wafungaji bora wa Ligi kuu Tanzania bara | Wafungaji NBC 2025/26 Wafungaji Bora Ligi Kuu ya NBC Tanzania 2025/2026 Ligi Kuu ya Tanzania Bara, almaarufu kama NBC Premier League, imeanza kwa kishindo msimu wa 2025/2026. Michuano hii inashirikisha timu 16 bora kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania, zikishindana kwa ari na nguvu ili kufukuzia heshima ya kuwa mabingwa. Yanga SC, mabingwa watetezi, wanaingia msimu huu wakiwa na jukumu la kulinda taji lao, huku nyota wao Clement…

Read More

Yanga Yatuma Salamu Msimbazi Baada ya Ushindi wa 5-0 Dhidi ya JKT Tanzania Ubingwa haujitangazi kwa maneno bali kwa matokeo. Ndivyo ilivyokuwa kwa vinara wa Ligi Kuu Bara, Young Africans Sports Club, walipoonyesha makali yao baada ya ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC, Dar es Salaam. Matokeo hayo yamezidi kuimarisha nafasi ya Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi kwa kufikisha pointi 28, huku yakitafsiriwa kama salamu ya wazi kuelekea Msimbazi kabla ya pambano lijalo dhidi ya watani wao wa jadi. Katika mchezo huo, Yanga ilionesha ubora wa hali ya juu katika…

Read More