Kaimu Kocha Mkuu wa Manchester United, Michael Carrick, ameteuliwa kuwa Kocha Bora wa Mwezi Januari 2026 katika Ligi Kuu ya Soka England. Uchaguzi huu unatambua mafanikio yake ya kistratejia na uwezo wa kuongoza timu kwa matokeo mazuri mwezi uliopita, na kuonesha jinsi Carrick anavyosimamia kikosi cha Manchester United kwa ufanisi. Hii ni ishara ya kuthaminiwa kwa juhudi zake na ushawishi wake ndani ya ligi, huku wapenzi wa soka wakimsifu kwa uongozi thabiti na matokeo chanya.
Author: Admin
Rais wa Klabu ya Yanga SC, Eng. Hersi Said, amefunguka kwa kina kuhusu dira ya klabu hiyo katika kipindi hiki cha mageuzi makubwa, akieleza kwa msisitizo dhamira ya kujenga uwanja wa kisasa utakaokuwa nyumbani rasmi ya mabingwa hao wa kihistoria. Katika maelezo yake, alibainisha kuwa Yanga haijajikita tu katika mafanikio ya uwanjani, bali pia katika kuweka misingi imara ya muda mrefu itakayoifanya klabu hiyo kuwa taasisi thabiti na ya mfano barani Afrika. Akizungumzia azma ya ujenzi wa uwanja mpya, Eng. Hersi alisema, “Tunapotazama mbele Yanga SC matarajio yetu yapo wazi, tumejitolea kujenga uwanja wa kisasa wa nyumbani Jangwani unaoakisi historia…
Kamati ya Ndani ya Maandalizi ya AFCON nchini Kenya imesema itaunga mkono kuahirishwa kwa michuano ya AFCON 2027 hadi mwaka 2028, kutokana na uwezekano wa vurugu zinazoweza kuhusiana na uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti 2027. Timu ya ukaguzi kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa sasa ipo Tanzania na inatarajia kufanya kikao kuhusu maandalizi ya michuano hiyo.
SIMBA imesema haitakubali kupoteza mara mbili dhidi ya mpinzani mmoja, ikiahidi kupambana hadi mwisho kuhakikisha inapata ushindi dhidi ya Stade Malien katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa Februari 14 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Msemaji wa Simba, Ahmed Ally, amesema kikosi hicho kimejipanga kurejesha heshima na kuondoa dhana iliyojengeka kwa mashabiki kwamba hakiwezi kushinda kwenye Uwanja wa Mkapa msimu huu. “Msimu huu hatujapata ushindi wowote kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa katika Ligi. Matokeo haya yamefanya imani imewapotea Wanasimba ya kupata…
Viingilio vya Mechi ya Simba vs Stade Malien 14/02/2026 Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wametangaza rasmi viingilio vya mchezo wao wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wageni wao Stade Malien utakaochezwa Jumamosi, Februari 14, 2026 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 19:00. Tangazo hilo linaweka wazi madaraja ya tiketi pamoja na gharama zake kwa mashabiki watakaohudhuria pambano hilo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, viingilio vimepangwa katika makundi tofauti kulingana na maeneo ya kukaa uwanjani. Mzunguko umewekwa kwa shilingi 3,000, huku VIP C ikiwa shilingi 5,000. Tiketi za VIP B zinauzwa kwa shilingi 10,000 na…
KUELEKEA mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Kabylie, Kocha Mkuu wa Yanga, Pedro Goncalves amesema kikosi chake kipo tayari kwa mapambano makali dhidi ya wapinzani hao wanaoheshimika barani Afrika. Akizungumza kuelekea mchezo huo muhimu wa hatua ya makundi utakaochezwa katika Uwanja wa New Amaan Complex,Pedro amesema JS Kabylie ni timu imara yenye uzoefu mkubwa, hasa katika michuano ya kimataifa. Amebainisha kuwa wapinzani wao wamewekeza kwa kiasi kikubwa msimu huu wakilenga kurejea katika historia yao ya mafanikio. Kocha huyo ameweka wazi kuwa maandalizi ya Yanga yamekamilika kwa kiwango cha kuridhisha, huku benchi la ufundi likifanya uchambuzi…
Mechi ya Yanga vs Kabylie CAF ni Lini? Tarehe, Saa na Mahali Timu ya Wananchi Yanga SC itashuka dimbani kuikabili JS Kabylie katika mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, huku wakisaka matokeo chanya kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mchezo huo ndio mchezo utakao hitimisha michezo ya hatua ya makundi na unatarajiwa kufuatiliwa na mashabiki wengi, huku ratiba, saa ya kuanza na njia ya kuutazama zikithibitishwa rasmi. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, Yanga itakuwa dimba la New Amaan Complex siku ya Jumapili, Februari 15, ikimenyana na wapinzani wao kutoka Algeria katika pambano lenye umuhimu wa kiushindani ndani…
Timu Zilizofuzu Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika 2025/2026 CAF Msimu wa 2025/2026 wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika umeendelea kushuhudia ushindani mkali katika hatua ya makundi, huku raundi ya tano ikitoa matokeo yaliyoanza kuamua hatma ya vilabu katika mbio za kufuzu hatua ya mtoano. Ushindi muhimu na alama zilizopatikana katika michezo hiyo ziliihakikishia Pyramids FC, Al Ahly na Stade Malien tiketi ya robo fainali kabla ya kukamilika kwa ratiba ya makundi. Pyramids FC Wafuzu Kupitia Kundi A Mabingwa watetezi Pyramids FC walithibitisha kufuzu baada ya ushindi wa mabao 4–1 dhidi ya Rivers United ugenini. Timu hiyo ilitoka nyuma kufuatia bao la Stephen…
Kikosi cha wachezaji 25 cha Azam FC kimesafiri leo asubuhi kuelekea Morocco kwa ajili ya mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Wydad Athletic Club, utakaochezwa Jumapili. Mchezo huo una umuhimu mkubwa kwa timu zote, huku ukiwa ndio utakaoamua hatma ya Azam FC katika safari yao ya mashindano hayo msimu huu. Kwa sasa Azam FC ipo nafasi ya tatu kwenye kundi ikiwa na pointi tisa, idadi inayolingana na Maniema Union ya DR Congo, wakati Wydad Athletic Club wanaongoza kundi kwa pointi 12. Pamoja na changamoto ya ushindani mkali, Kocha Mkuu Florent Ibenge…
Vyuo vya Diploma nchini Tanzania (au vyuo vinavyotoa Ordinary Diploma au NTA Level 4-6) ni taasisi za elimu ya ufundi na kitaalamu zinazodhibitiwa na NACTVET (National Council for Technical and Vocational Education and Training). Hizi ni vyuo vya kati (technical/vocational colleges) vinavyotoa kozi za diploma (miaka 2-3) katika nyanja mbalimbali kama afya, uhandisi, biashara, kilimo, IT, na zaidi. Vyuo hivi ni tofauti na vyuo vikuu (universities zinazodhibitiwa na TCU). Kwa mwaka wa masomo 2025/2026, orodha kamili na updated inapatikana katika NACTVET Admission Guidebook for Certificate and Diploma Programmes 2025/2026, ambayo inaorodhesha vyuo vyote vilivyosajiliwa, kozi, mahitaji ya kujiunga, nafasi (admission capacity), na ada (tuition fees). Aina za…
MSHAMBULIAJI wa Simba SC, Kibu Denis, ameaga rasmi klabu hiyo baada ya kuitumikia kwa miaka minne na nusu, akieleza kuwa amepata changamoto mpya ya kwenda “kutengeneza familia” katika klabu ya Al Nasr ya Libya. Kibu amejiunga na Al Nasr kwa ada ya uhamisho ya dola za Marekani 300,000 (takribani Sh milioni 776) na kusaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu. Akizungumza kwa hisia baada ya kukamilisha uhamisho huo, Kibu aliwashukuru wachezaji wenzake, benchi la ufundi na uongozi wa Simba kwa sapoti waliyompa katika kipindi chote alichokuwa klabuni hapo. “Nimefanya kazi Simba kwa miaka minne na nusu, nimepata sehemu nyingine ya…
KOCHA wa Yanga, Pedro Goncalves, ameweka wazi kuwa kikosi chake hakina jambo jingine kichwani kwa sasa zaidi ya kushinda na kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Kwa mujibu wa kocha huyo, malengo ni moja tu Jumapili hii kuibuka na ushindi dhidi ya JS Kabylie na kusonga mbele katika hatua inayofuata ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika. Yanga watakuwa wenyeji katika mchezo huo wa mwisho wa hatua ya makundi utakaopigwa Jumapili, Uwanja wa New Amaan Complex, visiwani Zanzibar. Faida ya kucheza nyumbani inatajwa kuwa moja ya silaha muhimu kwa Wananchi, huku wakitarajia sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wao watakaofurika…
WAKATI uongozi wa klabu ya Simba ukiendelea kusukuma mbele ajenda ya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji, mwekezaji na Rais wa Heshima wa klabu hiyo, Mohammed Dewji (Mo Dewji), ameibua sintofahamu kubwa baada ya kuhoji hadharani hatua iliyofikiwa katika mchakato huo, akionekana kutoridhishwa na mwelekeo unaochukuliwa. Sintofahamu hiyo imejitokeza kufuatia Simba kusaini mikataba ya makubaliano na Mainstream Group pamoja na Nexus Pesa kwa ajili ya urejeshaji wa zoezi la usajili wa wanachama na utoaji wa kadi za uanachama kwa kuzingatia katiba ya klabu, kuanzia ngazi ya matawi hadi makao makuu. Hata hivyo, wakati uongozi ukieleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya…
Serikali ya Tanzania imeiomba Jamhuri ya Watu wa China kuunga mkono juhudi za Tanzania katika kuimarisha miundombinu ya kisasa ili kujiandaa vyema na uenyeji wa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027). Wito huo umetolewa hivi karibuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, James Millya, wakati wa hafla ya kusherehekea Mwaka Mpya wa China iliyofanyika katika Ubalozi wa nchi hiyo jijini Dar es Salaam. Millya amesisitiza kuwa maandalizi ya AFCON 2027 ni zaidi ya michezo, akiyataja mashindano hayo kama fursa ya kimkakati kwa ajili ya mabadiliko ya kiuchumi kwa kuchochea ukuaji wa…
Al Nasr imefikia makubaliano rasmi na Simba ya kumnunua mshambuliaji Kibu Denis baada ya klabu hiyo ya Libya jana kukubaliana maslahi binafsi na nyota huyo wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’. Baada ya awali Simba kuonyesha utayari wa kumuuza Kibu Denis, kilichobakia kilikuwa ni makubaliano binafsi baina ya Al Nasr na Kibu Denis ambayo yalichelewa kufanyika kwa vile mchezaji huyo alikuwa Angola akiitumikia Simba katika mchezo wa raundi ya tano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu. Lakini baada ya nyota huyo kurejea, jana, Jumatatu, Februari 9, 2026, miamba hiyo ya Libya ilikutana na upande wa mchezaji huyo…
Kocha Mkuu wa Simba, Steve Barker, amezungumzia maandalizi ya timu yake kuelekea mchezo wa Ligi Kuu utakaopigwa kesho Jumatano, Februari 11 kwenye uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam saa 1:00 usiku kwa muda wa Tanzania. Barker amesema maandalizi ya kikosi chake yamekwenda vizuri hadi sasa, na amesisitiza umuhimu wa kucheza mchezo huo kwa kiwango cha juu ili kupata ushindi unaotakiwa. “Tunahitaji kucheza mechi hii vizuri ikiwa ni pamoja na kutawala mchezo na kupata ushindi kama ambavyo malengo yetu yalivyo,” amesema kocha huyo raia wa Afrika Kusini. Simba inaingia katika mchezo huu ikiwa na hamu kubwa ya kuendeleza mfululizo…
GWIJI wa Ligi Kuu England, Wayne Rooney, ameonya kuwa Mikel Arteta anaweza kufukuzwa kazi endapo atashindwa kuipa Arsenal taji la Ligi Kuu msimu huu 😳🏆 Arsenal kwa sasa inaongoza ligi kwa pointi sita mbele ya Manchester City, na imekuwa vinara wa kubashiriwa kushinda taji lao la kwanza tangu mwaka 2004. Kwa mujibu wa Rooney, nafasi hiyo nzuri inaondoa kabisa visingizio kwa Arteta. Akizungumza kwenye kipindi cha The Wayne Rooney Show, amesema: “Arsenal wamemuunga mkono Arteta kwa kiwango kikubwa na wamempa kikosi bora sana. Kama hawatashinda mwaka huu, kutakuwa na presha kubwa kwake, bila shaka.” Rooney pia anaamini ushindi wa kusisimua…
LUIS DIAZ yupo kiwango bora cha maisha yake akiwa na Bayern Munich hii ni ‘material’ ya Ballond’or kabisa, tangu atue kwa wabishi hao wa soka la Ujerumani amekuwa nyota muhimu mno kwenye kikosi hicho. Hadi sasa amehusika kwenye mabao 30 ndani ya michezo 30 aliyoiwakilisha nembo ya mabosi zake. Kama Bayern Munich watashinda mataji makubwa na timu yake ya taifa ya Colombia ikafanya vizuri kwenye Kombe la Dunia basi huenda tukazungumza mengine kwenye Ballon d’or mwaka huu.
MENEJA Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba, Ahmed Ally, ameonya wapinzani wa Ligi Kuu Tanzania Bara kuhusu ubora wa safu ya kiungo wa timu hiyo, akisema kuwa itakuwa changamoto kubwa msimu huu. Kauli hiyo inakuja baada ya kiungo mshambuliaji, Iñno Jospin Loemba, kuonyesha kiwango cha juu katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Petro de Luanda ya Angola. Ahmed amesema Loemba, ambaye alijiunga na Simba katika dirisha dogo la usajili, ameanza kuonyesha umuhimu wake katika timu kwa kuungana vyema na Clatous Chama. “Loemba anacheza kama namba 8 au 10, lakini ana uwezo mkubwa, mawinga wanapaswa kujua jinsi…
UONGOZI wa klabu ya Yanga umeweka wazi msimamo wao wa kutokubali kushindwa, wakisema hawataki kutokea kile kilichotokea kwa wapinzani wao Simba, walishindwa kufuzu kwa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Yanga ilikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa AS FAR Rabat kwenye mchezo wa ugenini uliochezwa dimbani Olymique, mji wa Rabat nchini Morocco. Kipigo hiki kimeachia Yanga changamoto kubwa ya kupambana kwenye mechi yao ya mwisho ya makundi dhidi ya JS Kabylie ili kuepuka hatma ya kushindwa kufuzu kama ilivyotokea kwa Simba. Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe, amesema kwamba kwa sasa klabu inawaona mbele tu, huku wakijua kwamba…