INAELEZWA kuwa Jean Ahoua kiungo mshambuliaji wa Simba SC chaguo la kwanza la Kocha Mkuu Fadlu Davids kwenye mechi za ushindani ndani ya msimu wa 2024/25 yupo kwenye rada za mabosi wa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini. Ahoua ni anayevaa jezi namba 10 mgongoni ana uwezo kwenye kufunga na kutoa pasi za mabao akiingia kwenye orodha ya wakali wa mapigo huru ndani ya ligi msimu wa 2024/25. Katika mabao 15 aliyofunga mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia akiwa kafunga mabao 14 na kwa pigo la kichwa alifunga bao moja kwenye mchezo dhidi ya Pamba Jiji alipotumia pasi ya…
Author: Admin
Meridianbet wamekuja na fursa ya kipekee kwa wateja wake ambapo kwa shilingi 5000 pekee inampa nafasi ya kuondoka na simu janja aina ya Samsung A25, hivyo shiriki sasa uwe moja ya washindi watakaotangazwa siku maalumu. Kushiriki promosheni hii lazima uwe umejisajili na Meridianbet na ubashiri mechi za ligi ya mpira ambapo kwenye promosheni hii dau ambalo linatakiwa kuweka ni shilingi 5000 na kuendelea ndipo uwe moj ya watu ambao wanashindania Samsung A25. Ofa hii imeanza tarehe 01 Juni na mwisho wake utakuwa ni tarehe 30 mwezi Juni. Hivyo changamkia fursa hii ya kipekee ambayo imekujia na wakali wa ubashiri. Mteja atabashiri mechi…
SIMBA imekataa ofa ya Sh 500Mil kutoka Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini ya kumuuza kiungo wake mshambuliaji , Kibu Denis katika msimu ujao. Inaelezwa sababu ya kugomea kumuachia kiungo huyo, udogo wa dau hilo ambalo alijawashawishi Bodi ya Wakurugenzi ya timu hiyo. Hivyo lazima dili hilo la Kibu kuuzwa Chiefs limekufa rasmi, kiungo huyo ataendelea kubakia hapo katika msimu ujao kukipambania kikosi hicho.
Percy Muzi Tau amefikia makubaliano kuvunja mkataba wake na Qatar SC baada ya miezi Sita tu klabuni hapo… Tau sasa ni mchezaji huru sokoni anaweza kujiunga na klabu yoyote itayofikia makubaliano nae.
Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, inatarajiwa kushuka dimbani usiku wa leo kuwakabili wenyeji wao, Bafana Bafana ya Afrika Kusini, katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaopigwa kwenye Uwanja wa Peter Mokaba kuanzia saa 2:30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Mchezo huu unatoa nafasi ya kutengeneza pesa kubwa kwa wabashiri kupitia Meridianbet. Licha ya kuwa ni mchezo wa kirafiki, pande zote mbili zimeupokea kwa uzito mkubwa, zikilenga kuutumia kama sehemu ya maandalizi ya mashindano ya COSAFA yanayoendelea nchini Afrika Kusini. Kwa upande wa Tanzania, mchezo huu pia ni sehemu ya maandalizi kuelekea michuano ya CHAN inayotarajiwa kufanyika mwezi Agosti, sambamba na kujiandaa kwa…
NYOTA wawili kutoka Azam FC ambao wanatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Yanga SC wametajwa na bosi wa kutoka mitaa ya Jangwani. Ni Feisal Salum kiungo mshambuliaji ambaye ni kinara kwa utengenezaji pasi za mwisho akiwa nazo 13 na Giblil Sillah mwenye pasi mbili za mabao. Mbali na pasi mbili za mabao alizonazo Sillah kiungo huyo mshambuliaji katupia jumla ya mabao 9 kwenye ligi huku Feisal akiwa katupia mabao manne. Mastaa hawa wanatajwa kuwa kwenye rada za timu mbalimbali na miongoni mwa timu ambazo zinatajwa ni Yanga SC. Kuhusu Fei mabosi wa Azam FC waliweka wazi kuwa bado mchezaji…
Aliyekuwa kocha mkuu wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag amesaini rasmi leo kuwa kocha mpya wa Bayer Leverkusen. Klabu ya Bayer Leverkusen imethibitisha kuwa Ten Hag amerithi rasmi mikoba ya aliyekuwa kocha wao Xabi Alonso, Huku Ten Hag amesaini mkataba wa miaka miwili hadi Juni 2027. Xabi ametimkia Real Madrid ambayo imemtambulisha rasmi jana.
KIUNGO mshambuliaji mpya ndani ya kikosi cha Wydad Casablanca, Aziz Ki tayari ameanza mazoezi na timu hiyo mara baada ya kumtambulisha. Ikumbukwe kwamba Ki aliibuka ndani ya timu hiyo akitokea kikosi cha Yanga SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi. Mchezo wa mwisho akiwa na uzi wa Yanga SC ilikuwa dhidi ya JKT Tanzania ambao ulikuwa ni CRDB Federation Cup hatua ya nusu fainali. Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga baada ya dakika 90 ubao ukasoma Yanga SC 2-0 JKT Tanzania. Mei 25 alitambulishwa rasmi ndani ya kikosi cha Wydad Casablanca kiungo huyo mshambuliaji ambaye alikuwa anavaa jezi…
Alonso aliyekuwa mchezaji na mshindi wa taji la Ligi ya Mabingwa akiwa na Real Madrid anaenda kurithi mikoba ya aliyekuwa kocha wake akiwa Madrid Carlo Ancelotti aliyeaga jana. Alonso atahudumu Bernabeu hadi Mwaka 2028.
FT: Uwanja wa New Amaan Complex Simba SC 1-1 RS Berkane, (1-3) RS Berkane wanapata bao la kuweka usawa dakika ya 90. Dakika ya 70 Steven Mukwala alipachika bao ambalo VAR limefuta kwa kueleza kuwa alikuwa kwenye mtego wa kuotea. Yusuph Kagoma kiungo wa Simba SC ameonyeshwa kadi mbili za njano na kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 50. Mapumziko. Simba SC 1-1 RS Berkane, (Agregate 1-3) Dakika ya 41 Joshua Mutale anachezewa faulo na Ayoub wa RS Berkane ambaye anaonyeshwa kadi ya njano. Fadlu Davids Kocha Mkuu wa Simba SC na Seleman Matola, kocha msaidizi wa Simba SC, Shomari Kapombe…
Katika ardhi ya Tanzania Mnyama Simba hajawahi kushindwa kitu. Mifano iko mingi. Mingi mno. Naamini kila shabiki wa Simba SC atatimiza jukumu pake mama kimsingi. Kushangilia na kuzomea, lakini wachezaji ndio wafanisi wenyewe kwenye vita hii ya kihistoria katika nchi na klabu kiujumla. Wachezaji ndio waliobeba dhamana na matumaini ya kubakisha kombe nyumbani au kombe liondoke. Wafahamu fika historia itawakunbuka kwa mengi, lakini kumfanya Simba SC ainue kwapa la Kombe la Shirikisho historia itawakumbuka na kuwapa heshima zaidi.
Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu katika bunge jana Tarehe 24, May alikumbusha bunge hilo kuwa Jumapili ya leo kuna jambo muhimu la kitaifa. Akizungumza wakati akihitimisha shuguli za bunge, Zungu amesema historia inakwenda kuandikwa siku ya Jumapili. Ifahamike kwamba Jumapili kikosi cha Simba kitacheza fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane ya Morocco. Mchezo wa kwanza Simba ilipoteza 2-0, lakini wanaamini watapindua meza na kutwaa ubingwa siku ya leo Jumapili visiwani Zanzibar.
BAADA ya kiungo mshambuliaji wa Yanga SC Aziz Ki taarifa kueleza kuwa anaondoka ndani ya kikosi hicho kuelekea Wydad inaelezwa kuwa kuna nyota mwingine tena anaondoka katika kikosi hicho. Aziz Ki amekuwa kwenye mwendo mzuri ndani ya Yanga SC akiwa kacheza jumla ya mechi 114 na kutoa pasi 57 za mabao huku akifunga jumla ya mabao 32. Ni Clement Mzize chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Miloud Hamdi anatajwa kuwa kwenye hesabu za mabosi wa Zamalek ambao wanahitaji kupata huduma yake. Mshambuliaji huyo kafunga jumla ya mabao 13 kwa msimu wa 2024 kwenye ligi akiwa ni mzawa namba moja mwenye…
WABABE wawili ndani ya ardhi ya Tanzania kwenye eneo la mpira wa miguu ndani ya ligi ya vijana huko kwao mambo ni magumu kutokana na aina ya matokeo ambayo wanayaoata ndani ya uwanja. Ni Yanga SC na Simba SC katika NBC Youth League 2024/25 mambo ni magumu kwao kutokana na mwendo ambao wapo nao katika makundi tofauti waliyopo kila mmoja kwa wakati wake. Katika nane bora, Yanga SC Youth ipo kundi B ambalo kinara ni Kagera Sugar mwenye jumla ya pointi 4 baada ya mechi mbili ndani ya dakika 180. Ushindi ni kwenye mchezo mmoja na sare mchezo mmoja huku…
WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye anga la kimataifa Simba SC chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids hesabu kubwa ni kuingia kwa mkakati kuwakabili wapinzani wao RS Berkane kwenye mchezo wa fainali ya pili Kombe la Shirikisho Afrika. Fadlu Davids, Kocha Mkuu wa Simba SC ameweka wazi kuwa wanatambua mchezo uliopita walipoteza ila mchezo wa pili kwa kuwa watakuwa nyumbani kazi kubwa itafanyika kupata matokeo. Ugenini Mei 17 2025 baada ya dakika 90 ubao ulisoma RS Berkane 2-0 Simba SC, mchezo wa pili utaamua nani atatwaa taji hilo utapigwa Mei 25, Jumapili kwenye ardhi ya Tanzania, Uwanja wa New Amaan, Zanzibar. RS…
SIMBA SC wawakilishi wa Tanzania kwenye anga la kimataifa katika Kombe la Shirikisho Afrika, Mei 25 2025 watakuwa na kazi nzito mbele ya RS Berkane kwenye mchezo wa fainali ya pili la Kombe la Shirikisho Afrika huku beki wao akiwa kwenye asilimia kubwa kurejea uwanjani. Jina lake ni Abdulrazack Hamza, yupo kwenye orodha ya wachezaji ambao wanapewa nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza mara baada ya kukwama kukamilisha dakika 90 dhidi ya RS Berkane kwenye mchezo uliopita ugenini alipopata maumivu. Ipo wazi kwamba Mei 17 2025, Hamza alipata maumivu dakika ya 21 kwenye mchezo huo na nafasi yake ilichukuliwa na…
MTENDAJI Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin, maarufu kwa jina la Popat baba yake mzazi ametangulia mbele za haki Mei 23 2025. Taarifa iliyotolewa na Azam FC imeeleza namna hii: Asalaam Aleykum wa Rahmatullahi wa Barakatuhu! “Kwa masikitiko makubwa, Azam FC inatangaza kifo baba mzazi wa Mtendaji wetu Mkuu (CEO), Abdulkarim Amin ‘Popat’, Mzee MohamedAmin Nurdin Haldey, kilichotokea alfajiri ya leo Ijumaa, Hospitali ya Aga Khan. “Mwili wa marehemu utaswaliwa msikiti wa Maaamur, Upanga – Dar es Salaam, baada ya swala ya Ijumaa, na mazishi yatafanyika kwenye makaburi ya Kijitonyama barabara ya Rose Garden. Inna lillahi waina ilaiyhi raajiun. Pumzika…