Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Contact Us
    • Privacy Policy
    Facebook Instagram YouTube
    Chikao Media
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • MAGAZETI YA LEO
    • TETESI ZA SOKA
    • BOXING
    • FORUM
    Chikao Media
    Home » SIMBA SC KUINGIA KWA MKAKATI KUWAKABILI RS BERKANE MEI 25 2025
    KITAIFA

    SIMBA SC KUINGIA KWA MKAKATI KUWAKABILI RS BERKANE MEI 25 2025

    By AdminMay 24, 2025No Comments1 Min Read
    Share WhatsApp Facebook Twitter Pinterest Telegram Email Copy Link
    Follow Us
    Facebook Instagram YouTube
    fadlu simba
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email Copy Link

    WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye anga la kimataifa Simba SC chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids hesabu kubwa ni kuingia kwa mkakati kuwakabili wapinzani wao RS Berkane kwenye mchezo wa fainali ya pili Kombe la Shirikisho Afrika.


    Fadlu Davids, Kocha Mkuu wa Simba SC ameweka wazi kuwa wanatambua mchezo uliopita walipoteza ila mchezo wa pili kwa kuwa watakuwa nyumbani kazi kubwa itafanyika kupata matokeo.


    Ugenini Mei 17 2025 baada ya dakika 90 ubao ulisoma RS Berkane 2-0 Simba SC, mchezo wa pili utaamua nani atatwaa taji hilo utapigwa Mei 25, Jumapili kwenye ardhi ya Tanzania, Uwanja wa New Amaan, Zanzibar.


    RS Berkane walianza kupata mabao ndani ya dakika 15 za mwanzo yalidumu mpaka mwisho wa mchezo huo wa kwanza ilikuwa kupitia kwa Mamadou Camara dakika ya 8 na Ousama Lamlioui dakika ya 15 waliomtungua Mousa Camara kipa namba moja wa Simba SC.


    Fadlu amesema: “Kazi ni kubwa baada ya kupoteza mchezo wetu wa kwanza tuliangalia makosa, wachezaji walifanya kazi kubwa hivyo kwenye mchezo wetu wa pili tunapaswa kujitoa zaidi ili kupata matokeo mazuri.”
    Simba SC ili kutwaa taji la Kombe la Shirikisho Afrika ni lazima ipate ushindi wa mabao 3-0 kwenye mchezo wa pili wakiwa nyumbani.

    Follow on Facebook Follow on Instagram Follow on YouTube
    Share. WhatsApp Facebook Twitter Pinterest Email Copy Link
    Previous ArticleBEKI WA KAZI SIMBA SC KAMILI KUWAKABILI RS BERKANE MEI 25 2025
    Next Article YANGA SC NA SIMBA SC MAMBO MAGUMU KWENYE LIGI 2024/25

    Related Posts

    Ujenzi wa Arena, Serikali Yatenga Bil400

    April 3, 2026

    Selemani Mwalimu Yupo Anakuja, Mjiandae

    April 3, 2026

    MSIGWA AELEZA SABABU ZA KUONGEZEKA GHARAMA UWANJA WA ARUSHA

    March 31, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    Bernardo Apewa Thank You Rasmi Man City

    Ujenzi wa Arena, Serikali Yatenga Bil400

    Selemani Mwalimu Yupo Anakuja, Mjiandae

    MSIGWA AELEZA SABABU ZA KUONGEZEKA GHARAMA UWANJA WA ARUSHA

    Neymar amuachia Mungu kutoitwa timu ya Taifa

    “Nimehuzunika,Nimeumia lakini ndoto bado inaishi”Neymar Jr.

    © 2026 CHIKAO MEDIA | All Rights Are Reserved
    • Contact Us
    • Privacy Policy

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.