Author: Admin

Klabu ya Simba Queens imetangaza kuachana na wachezaji 11 waliohudumu katika kikosi chao katika misimu iliyopita. Wachezaji hao ambao wamepewa mkono wa kwaheri na wekundu wa msimbazi ni Precious Christopher, Asha Djafar, Riticia Nabossa, Saiki Atinuke, Josephine Julius, Gelwa Yona, Asha Mwalala, Jackline Wilbert, Daniela Ngowi, Wincate Kaari na golikipa Caroline Rufaa.

Read More

Tetesi Za Usajili Yanga Leo 2025/2026 | Habari Mpya za Usajili Yanga SC Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League), Yanga SC, wameanza harakati kabambe za kuimarisha kikosi chao kwa msimu wa 2025/2026. Hii ni baada ya baadhi ya wachezaji wao muhimu kuondoka rasmi, hali iliyowalazimu viongozi wa klabu kusuka upya kikosi kwa lengo la kuendelea kuwa na ushindani kwenye mashindano ya ndani na ya kimataifa, yakiwemo Ligi Kuu NBC, Kombe la Shirikisho la CRDB, na michuano ya CAF Champions League. Katika dirisha hili la usajili, tetesi za usajili Yanga leo 2025/2026 zimekuwa gumzo kubwa kwenye vyombo…

Read More

Huyu Hapa Kocha Mpya wa Yanga 2025/2026: CV Yake ni Moto Klabu ya Yanga SC imethibitisha rasmi kuwa tayari ina kocha mpya kwa ajili ya msimu wa 2025/2026. Ingawa jina lake bado halijawekwa wazi hadharani, taarifa zinaeleza kuwa kocha huyo tayari yupo nchini Tanzania na anaendelea kuishi kwenye hoteli ya kifahari jijini Dar es Salaam, akifuatilia kwa karibu mwenendo wa kikosi chake kipya kabla ya kuanza kazi rasmi. Kwa mujibu wa Afisa Habari wa klabu hiyo, Ali Kamwe, kilichobaki kwa sasa ni kukamilisha mchakato wa kuwaaga baadhi ya wachezaji waliomaliza mikataba yao kabla ya kocha huyo mpya kuanza kazi kwa…

Read More

KIUNGO wa Yanga SC Pacome Zouzoua ambaye mkononi ana tuzo ya mchezaji bora ndani ya Ligi Kuu Bara inayodhaminiwa na NBC msimu wa 2024/25 ndani ya Juni 2025 anatajwa kuwa atasalia ndani ya kikosi hicho kwa msimu ujao wa 2025/25. Pacome alikuwa kwenye mwendo bora ndani ya uwanja msimu uliopita akiwa ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Miloud Hamdi ambaye naye alitwaa tuzo ya kocha bora ndani ya Juni. Ipo wazi kwamba msimu wa 2025/26 Yanga SC itakuwa na kocha mpya baada ya Miloud kuondoka. Tayari kocha mpya wa Yanga SC ameshatua ndani ya Dar muda wowote kuanzia sasa…

Read More

FIFA Club World Cup 2025 mashindano haya yalianza kurindima Juni 14 na kugota mwisho Julai 13 2025 ambapo ni Chelsea kutoka England ilitwaa taji hilo mbele ya PSG kwa ushindi wa mabao 3-0 ni usiku wa kuamkia Juni 14 fainali ilichezwa. Ni mabao ya Cole Palmer ambaye alifunga mabao mawili dakika 22 na 30 mbele ya PSG na bao moja likifungwa na Joao Pedro dakika 43. Kazi iliisha kabla ya mapumziko mbele ya Rais wa Marekani Donald Trump ambaye alikuwa sambamba na Rais wa FIFA Gianni Infantino. Enzo Maresca aliwapa mbinu wachezaji wa Chelsea kupata ushindi mbele ya PSG. Mashabiki…

Read More

KLABU kongwe nchini, Simba na Yanga, zimetembeza panga kwa upande wa wachezaji wa kimataifa kuelekea msimu mpya, huku zikilenga kuboresha vikosi vyao zaidi kwa ajili ya malengo makubwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, imefahamika. Simba na Yanga zipo kwenye harakati za kuviboresha vikosi vyao kwa ajili ya mashindano msimu ujao, zikilenga zaidi Ligi ya Mabingwa Afrika, ambapo inatajwa kuwa vitaacha kadhaa wa kigeni. SIMBA Imeelezwa kuwa Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids, katika wachezaji wa kigeni waliopo kwa sasa, amependekeza kubakiwa na saba tu, majina ni Steven Mukwala na Joshua Mutale, yakitajwa kutakiwa kusalia Msimbazi kwa msimu ujao…

Read More

Klabu ya Simba imeanza rasmi mpango wa kusuka upya kikosi chake kwa msimu ujao kwa kufanya mabadiliko makubwa, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Kocha Mkuu Fadlu Davids na uongozi wa klabu hiyo kuhakikisha wanarejea kwenye ubora wa juu kitaifa na kimataifa. Kwa mujibu wa taarifa zilizovuja kutoka ndani ya klabu hiyo, tayari wachezaji sita wa kigeni wametajwa kuwa sehemu ya wale wanaoachwa katika kikosi cha wekundu wa Msimbazi: Orodha ya Wachezaji Wanaotarajiwa Kuachwa: Valentino Nouma Augustine Okejepha Che Marlone Fondoh Christian Leonel Ateba Fabrice Ngoma Deborah Fernandes Mavambo

Read More

KIKOSI cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinaendelea na mazoezi kwenye kambi yake nchini Misri kujiandaa na Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) zinazotarajiwa kuanza Agosti 2 hadi 30, mwaka huu. Taifa Stars imekuwa ikifanya mazoezi viwanja vya Mercure Jijini Ismailia, Misri tangu iwasili Julai 8 kujiandaa na fainali hizo zinazoandaliwa kwa pamoja na Tanzania na nchi jirani za Kenya na Uganda. Kikosi kipo chini ya Kocha Mkuu, Hemed Suleiman Ali ‘Morocco’ anayesaidiwa na wazawa wenzake, Juma Ramadhani Mgunda ‘Pep Guardiola Mnene’ na Jamhuri Mussa Kihwelo ‘Julio’ na kinaundwa na wachezaji 27 kutoka klabu…

Read More

Dar es Salaam, Tanzania – Klabu ya Yanga SC kupitia kwa Msemaji wake, Alikamwe, leo imezindua rasmi kampeni mpya iitwayo “Tofali la Ubingwa” inayolenga kuchangisha fedha kutoka kwa mashabiki na wanachama ili kusaidia timu katika usajili wa wachezaji wenye ubora wa hali ya juu. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Kamwe amesema kampeni hii ni sehemu ya mkakati wa klabu kujitegemea na kuwa na nguvu ya kiuchumi inayotokana na mashabiki wake, ambao wamekuwa mstari wa mbele kuiunga mkono timu katika mafanikio yake. “Kampeni hii itaiwezesha Yanga kusajili wachezaji bora kwa kutumia fedha zitakazotokana na michango ya mashabiki. Tunataka kila mshabiki ajihusishe…

Read More

SIMBA SC katika anga la kimataifa msimu wa 2024/25 imegotea nafasi ya pili kwa kupoteza mchezo wa fainali dhidi ya RS Berkane ya Morocco. Katika dakika 180, Simba SC ilifungwa jumla ya mabao 3-1, bao la kufutia machozi kwa Simba SC lilifungwa na Joshua Mutale mchezo uliochezwa Uwanja wa New Amaan Complex. Kibu Dennis ni miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa katika ubora kwenye mashindano ya kimataifa kwa kufunga mabao muhimu katika mechi za ushindani Kombe la Shirikisho Afrika. Katika Ligi Kuu Bara 2024/25 haukuwa msimu bora kwa Kibu D kutokana na namba kuwa chini hasa katika eneo la kutengeneza pasi…

Read More

Mpanzu wa Simba kwenye Rada za Waarabu INAELEZWA kuwa winga chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Fadlu Davids ndani ya kikosi cha Simba SC, Ellie Mpanzu yupo kwenye rada za RS Berkane,Waarabu wa Morocco. Mpanzu ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa tegemeo katika kikosi cha Simba SC msimu wa 2024/25 kwenye anga la kimataifa na kitaifa. Ndani ya ligi rekodi zinaonyesha kuwa alicheza jumla ya mechi 17 kati ya 30. Ikumbukwe kwamba Mpanzu aliibuka ndani ya Simba SC kwenye dirisha dogo la usajili. Simba SC ikiwa imefunga mabao 69 kahusika kwenye mabao 7, akifunga manne na kutoa pasi tatu. Ni dakika…

Read More

Kocha Mpya wa Yanga 2025/2026: Siri Yafichuka Jangwani! KLABU ya Yanga SC imethibitisha kuwa tayari imepata Kocha Mpya wa Yanga kwa msimu wa 2025/2026, ambaye sasa ndiye anasimamia kikamilifu harakati za usajili kuelekea msimu mpya wa mashindano. Ingawa jina lake halijatangazwa rasmi, kocha huyo tayari yupo nchini na anaishi kwenye hoteli ya kifahari jijini Dar es Salaam akijifunza kikosi chake kwa undani kabla ya kuanza kazi rasmi. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ali Kamwe, kilichosalia kwa sasa ni kumalizia mchakato wa kuwaaga baadhi ya wachezaji waliomaliza mikataba yao, na mara baada ya hapo kocha…

Read More

Singida BS Yamnyatia Kipa wa Simba Hussein Abel Baada ya Kumaliza Mkataba Singida Black Stars (Singida BS) inayoongozwa na Kocha Miguel Gamondi, imeingia sokoni kwa kasi msimu huu wa usajili, ikiwa katika mazungumzo ya kumvuta kipa wa Simba SC, Hussein Abel, baada ya nyota huyo kumaliza rasmi mkataba wake na Wekundu wa Msimbazi. Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, hadi sasa hakuna dalili ya mazungumzo mapya baina ya kipa huyo na uongozi wa Simba kwa ajili ya kumbakisha msimu ujao – hali iliyofungua milango kwa klabu nyingine kumshawishi. Singida BS imechukua hatua ya haraka kufuatia taarifa kuwa Hussein Abel hayupo tena…

Read More

KIKOSI cha Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Julai 08 2025 kiliingia kambini Dar es Salaam kisha alfajiri ya kuamkia Julai 9 kimekwea pipa kuelekea nchini Misri kwa ajili ya kambi ya wiki tatu. Hivyo kuelekea CHAN mambo ni moto na maandalizi yanaendelea kwa kasi ikiwa ni mwendelezo wa ukarabati wa Uwanja wa Mkapa ambao upo tayari kwa asilimia kubwa kuelekea CHAN. Stars Agosti 02, 2025 itacheza mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Chan 2024 dhidi ya Burkina Faso kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam. Miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye msafara ni Aishi Manula, Mohamed Hussen Zimbwe, Dickson…

Read More

Staa wa muziki wa kizazi kipya nchini, Harmonize a.k.a Konde Boy, amefunguka kwamba ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho iliyotwaa Yanga msimu huu vimempa furaha kubwa kwani, kulikuwa na kelele na hila nyingi kabla ya msimu wa 2024-2025 kufikia tamati. Harmonize ambaye ni shabiki wa Yanga, amesema anajiona mwenye bahati kwa kuishabikia timu yenye kubeba makombe kila uchao. “Najiona ni mtu mwenye bahati sana kuishabikia hii klabu yenye kubeba makombe kila kukicha. Najiona ni mwenye bahati sana kuishi kwenye hii karne  nakuweza kuiona Yanga SC noma kuliko Yanga ya msimu wowote,” alisema Harmonize na kuongeza; “Kuna muda…

Read More

Tetesi Za Usajili Simba Leo 2025/2026: Nani Anaingia? Nani Anatoka Msimbazi? Wakati pazia la msimu wa 2024/2025 likikaribia kufungwa, macho ya vilabu vikubwa barani Afrika tayari yameelekezwa kwenye dirisha la usajili, likiwa ni wakati wa kusaka vipaji vipya kwa ajili ya msimu ujao. Klabu ya Simba SC, maarufu kama Wekundu wa Msimbazi, inabaki kuwa miongoni mwa timu zilizoonesha dhamira kubwa ya mabadiliko msimu huu, baada ya kufanya usajili mkubwa ulioiwezesha kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho CAF 2024/25, pamoja na kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC, tofauti ya pointi moja tu nyuma ya…

Read More

SIMBA SC katika anga la kimataifa msimu wa 2024/25 imegotea nafasi ya pili kwa kupoteza mchezo wa fainali dhidi ya RS Berkane ya Morocco. Katika dakika 180, Simba SC ilifungwa jumla ya mabao 3-1, bao la kufutia machozi kwa Simba SC lilifungwa na Joshua Mutale mchezo uliochezwa Uwanja wa New Amaan Complex. Kibu Dennis ni miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa katika ubora kwenye mashindano ya kimataifa kwa kufunga mabao muhimu katika mechi za ushindani Kombe la Shirikisho Afrika. Katika Ligi Kuu Bara 2024/25 haukuwa msimu bora kwa Kibu D kutokana na namba kuwa chini hasa katika eneo la kutengeneza pasi…

Read More

Mchezo wa Ufunguzi wa kombe la mataifa ya Afrika kwa wanawake (WAFCON) kati ya timu ya Taifa ya Zambia dhidi ya wenyeji Morocco umemalizika kwa sare ya 2-2. Kwenye mchezo huo. Magoli ya timu ya Taifa ya Zambia yalifungwa na nahodha Barbra Banda na Rachel Kundananji huku ya Morocco yakifungwa na nyota wao Ibtssam Jraidi na Chebbak. Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Twiga Stars’ watacheza mchezo wao wa kwanza wa makundi siku ya kesho Jumatatu ya Julai 7 dhidi ya timu ya Taifa ya Mali.

Read More

Klabu ya Azam FC Julai 5, 2025 imemtambulisha rasmi Florent Ibenge kuwa kocha mkuu mpya wa kikosi hicho, kupitia ukurasa wao wa Instagram kwa ujumbe mfupi lakini mzito uliosema: “Karibu Azam FC, kocha bora Afrika – Florent Ibenge.” Utambulisho huo umethibitisha kile ambacho mashabiki wa soka walikuwa wanakisubiri kwa hamu: ujio wa kocha mwenye rekodi kubwa na uzoefu mpana katika soka la Afrika. Florent Ibenge anasifika kwa mafanikio katika klabu na timu za taifa. Ametamba na klabu kubwa kama AS Vita (DR Congo) ambako alifikisha timu hiyo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, RS Berkane (Morocco) ambapo alinyakua taji la…

Read More