Shomari Kapombe anaripotiwa kuwa tayari amekubaliana na klabu ya Simba kuhusu kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuwatumikia Wekundu wa Msimbazi, licha ya mkataba wake wa awali kumalizika rasmi Juni 30, 2025. Vyanzo vya kuaminika kutoka ndani ya klabu vinadai kuwa hakuna presha yoyote baina ya pande hizo mbili, na kwamba mkataba mpya upo tayari na utatiwa saini muda wowote kuanzia sasa. Kapombe, ambaye kwa sasa yupo kwenye mipango ya moja kwa moja ya kocha mkuu Fadlu Davids, anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji ambao kocha huyo anawategemea mno katika kikosi chake. Inadaiwa kuwa Davids alisisitiza asiondoke, jambo lililochangia kwa kiasi kikubwa…
Author: Admin
UONGOZI wa Yanga SC umeweka wazi kwamba kazi inaanza kwenye usajili kwa kuwa kuna wachezaji wengine wa maana watatambulishwa hivi karibuni. Mpango mkubwa wa Yanga SC ulikuwa ni kufungua ukurasa Julai 22 kutambulisha wachezaji wapya ila ngoma ilibadilishwa hewani baada ya kufungua ukurasa rasmi Julai 18. Ni Moussa Conte alitambulishwa na Yanga SC ikiwa ni mchezaji wa kwanza kutambulishwa Yanga SC ambao ni mabingwa wa ligi kuelekea msimu wa 2025/26. Ali Kamwe ameweka wazi kuwa huo ni mwanzo watatambulisha wachezaji wengine wakubwa na wenye uwezo ili kuendelea pale ambapo waliishia msimu wa 2024/25. “Huu ni mwanzo, niliona kwamba wanasema wamekamilisha…
UONGOZI wa Simba SC umebainisha kwamba utafanya kweli kwenye usajili hivyo mashabiki wasiwe na presha mipango inaendelea. Ikumbukwe kwamba timu hiyo msimu wa 2024/25 ilikosa mataji yote iliyokuwa inayapambania jambo ambalo linawafanya waje na hasira zaidi. Miongoni mwa wachezaji ambao wanatajwa kuwa katika rada za Simba SC ni Feisal Salum wa Azam FC. Kwenye ligi ilimaliza ikiwa nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 30. Katika dakika 2,700 uwanjani ushindi ulikuwa katika mechi 25, sare tatu na ilipoteza mechi mbili. Mechi zote mbili ambazo ni dakika 180 ilikuwa dhidi ya Yanga SC ambao ni mabingwa wa ligi inayodhaminiwa na NBC.…
Kiungo fundi wa kimataifa, Debora Fernandes Mavambo (24), mwenye uraia pacha wa Congo-Brazzaville na Gabon, ameaga rasmi klabu ya Simba SC, takribani mwaka mmoja tu tangu asajiliwe kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Mutondo Stars ya Zambia. Mavambo ambaye anachezea timu ya taifa ya Gabon, ametangaza kuondoka kwake kupitia ujumbe wa kuushukuru uongozi na mashabiki wa klabu hiyo maarufu ya Msimbazi, akisisitiza kuwa ataikumbuka Simba daima kwa sapoti na mapokezi aliyoyapata wakati wote wa uwepo wake. “Asante sana familia ya Simba SC kwa sapoti yao katika kipindi chote nilichokuwa ndani ya klabu hii. Hakika nitaikumbuka klabu hii, mashabiki na viongozi…
Mabingwa wa Ligi Kuu Uganda, Vipers Sc wamethibitisha kumsajili winga, Mnigeria Odili Chukwuma kwa mkataba wa miaka miwili utakaombakisha klabuni hapo mwisho wa msimu wa 2026/27. Chukwuma (23) raia wa Nigeria anajiunga na Mabingwa hao mara 7 wa Ligi Kuu Uganda kutoka klabu ya Police Fc ya Rwanda. Msimu uliopita Chukwuma alifunga magoli matano na kusaidia ‘assists’ mengine 8 akiisaidia Polisi Fc kumaliza nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu Rwanda wakiwa na pointi 48. Chukwuma ambaye pia amewahi kuichezea Bugesera Fc ya Rwanda anakuwa usajili wa nne wa Vipers Sc baada ya mshambuliaji Mark Yallah raia wa Liberia,…
KUELEKEA msimu mpya wa 2025/26, Simba SC wamebainisha kuwa watafanya usajili mkubwa kupata timu imara ya ushindani kitaifa na kimataifa. Ipo wazi kuwa Aishi Manula ambaye ni kipa huyu atakuwa ndani ya Azam FC, Omary Omary amepelekwa kwa mkopo Mashujaa FC, Fabrince Ngoma mkataba wake umeisha, Kelvin Kijili atakuwa ndani ya Singida Black Stars ni baadhi ya wachezaji ambao hawatakuwa ndani ya kikosi cha Simba SC msimu ujao. Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC ameweka wazi kuwa wanakuja na kishindo. Ikumbukwe kwamba msimu wa 2024/25 Simba SC ilipishana na mataji yote iliyokuwa ikisaka. Taji la…
Yanga SC imekamilisha usajili wa kiungo wa CS Sfaxien ya Tunisia Balla Conte akiwa ni mchezaji wa kwanza kutambulishwa na mabingwa hao watetezi. Conte rasmi ni njano na kijani baada ya kutambulishwa na Yanga SC, Julai 18 2025 tayari kwa maandalizi ya msimu wa 2025/26. Ikumbukwe kwamba nyota huyo alikuwa anatajwa kuwa katika rada za watani wa jadi wa Yanga SC ambao ni Simba SC nao walikuwa kwenye hesabu za kuwania saini yake. Hivyo vita ya watani hawa wa jadi imegota mwisho na Yanga SC akiwa mshindi kwenye vita ya kwanza ya usajili kuelekea msimu mpya unaotarajiwa kuwa na ushindani…
Mashabiki wa Sporting CP wametoa jumbe za majibu yao kwa mshambuliaji wa kimataifa Viktor Gyokeres huku nyota huyo wa Sweden akikaribia kuhamia Arsenal kwa pauni milioni 62.4. Gyokeres amedhamiria kuhama Ligi Kuu msimu huu, huku kikosi cha Mikel Arteta kikiwa ndicho anachopendelea zaidi. Mazungumzo ya muda mrefu kati ya pande hizo yamepelekea Gyokeres kushindwa kurejea kwenye mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya akiwa na Sporting Ijumaa iliyopita. Rais wa michezo Frederico Varandas alimtishia Gyokeres kwa hatua za kinidhamu, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Sweden akionekana kuwa na uwezekano wa kuharibu sifa yake katika klabu hiyo, licha ya misimu miwili…
Klabu ya Simba imeripotiwa kupokea mwaliko kutoka nchini Rwanda wa klabu ya APR kucheza mechi ya kirafiki. APR ambayo itaiwakilisha Rwanda kwenye michuano ya ligi ya mabingwa (CAF CL) msimu ujao, imeomba kujipima na Simba katika mchezo ambao umepangwa kupigwa kati ya August 1 na August 03 Bado Simba haijathibitisha kushiriki mchezo huo kwani itategemea na mipango yake ya Pre-Season Endapo Simba itaweka kambi yake ya Pre-Season nje ya Tanzania huenda ikashindwa kushiriki mchezo huo katika tarehe iliyopangwa Kulingana na taarifa za awali, kikosi cha Simba kinatarajiwa kuanza maandalizi ya pre-season Julai 25, siku ya Ijumaa.
Habari mwanafamilia wa SokaLeo Pitia Kurasa za Magazeti ya taarifa za michezo za leo July 18, 2025
Mpango wa Manchester United kumsajili mshambuliaji wa Brentford Bryan Mbeumo, 25, umekwama baada ya klabu hiyo ya London kuongeza bei yao hadi paini milioni 70. United haitaki kulipa zaidi ya £65m. (Guardian) Liverpool wameanza mazungumzo na Eintracht Frankfurt kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Hugo Ekitike, 23. (Sky Sports), Hata hivyo, Newcastle United wanasonga mbele na jaribio lao la kumsajili Ekitike kwa matumaini ya kumpanga pamoja na mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 25, msimu ujao. (Telegraph – subscription required) Aston Villa ni miongoni mwa klabu za Ligi ya Primia zinazopania kumnunua winga wa Manchester United na Argentina Alejandro Garnacho, 21. (Mail) Manchester…
Tetesi za Usajili Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara 2025/2026 Baada ya msimu wa 2024/2025 kumalizika kwa shamrashamra za mafanikio kwa baadhi ya vilabu, sasa ni muda wa timu mbalimbali kujipanga upya kwa ajili ya msimu ujao wa 2025/2026. Msimu huu mpya unatarajiwa kuwa na ushindani mkali zaidi, hasa ikizingatiwa kuwa Yanga SC ilimaliza msimu uliopita kwa kuzoa mataji yote ya ndani – jambo linaloweka presha kwa wapinzani wao kuimarisha vikosi Dirisha la Usajili Lafunguliwa Rasmi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilitangaza rasmi kuwa dirisha kubwa la usajili kwa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, Championship, First League, Ligi Kuu…
Kinda mahiri wa FC Barcelona, Lamine Yamal, ametia saini mkataba mpya wa muda mrefu na klabu hiyo, ambao utamuweka Camp Nou hadi tarehe 30 Juni 2031. Tangazo hilo lilifanywa rasmi na Barcelona Jumanne, na limeambatana na hatua ya kihistoria ambapo Yamal amekabidhiwa rasmi jezi namba 10, namba yenye heshima kubwa katika historia ya klabu hiyo. Jezi hiyo imewahi kuvaliwa na vigogo wa soka kama Ronaldinho Gaucho, Lionel Messi, na hivi karibuni Ansu Fati, na sasa ni zamu ya Yamal kuibeba, ishara ya imani kubwa ya klabu kwake. Yamal, ambaye hivi karibuni alitimiza miaka 18, amekuwa gumzo barani Ulaya kutokana na…
FADLU Davids, Kocha Mkuu wa Simba SC amekabidhiwa rungu la kufanya maamuzi kwa wachezaji ambao wanapaswa kuondoka katika kikosi hicho na wale ambao watabaki kwa msimu wa 2025/26. Miongoni mwa wachezaji ambao Fadlu amebainisha kwamba anahitaji wabaki inaelezwa ni beki Mohamed Hussen ambaye mkataba wake umeisha akiwa anatajwa kuwa katika rada za Yanga SC. Kocha huyo alifanya kikao na Rais wa Simba SC, Mo Dewji hivyo kuna uwezekano mkubwa akaendelea kuwa katika kikosi hcho kwa msimu mpya wa 2025/26. Muda mfupi walipokutana Mo aliandika namna hii: “Tulia. Tathmini. Panga upya. Nimefurahi kuwa na mazungumzo ya maana na Kocha Fadlu katika…
KHALID Aucho kiungo mkabaji wa Yanga SC huenda akaongeza mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia timu hiyo yenye maskani yake Jangwani. Yanga SC ni mabingwa wa ligi msimu wa 2024/25 na miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa kwenye kikosi cha kwanza ni Aucho. Baada ya mechi 30 ambazo ni dakika 2,700, Aucho alicheza mechi 22 akikomba dakika 1,735. Katika mabao 83 yaliyofungwa na Yanga SC kwenye ligi alihusika kwenye mabao mawili, alifunga moja na kutoa pasi moja ya bao. Mkataba wa Aucho umegota mwisho baada ya msimu kukamilika. Taarifa zinaeleza kuwa huenda akaongeza mkataba wa mwaka mmoja kusalia ndani ya Yanga SC…
FEISAL Salum kiungo mshambuliaji wa Azam FC kuna asilimia ndogo kuondoka kwenye viunga hivyo kutokana na dau ambalo mabosi wamemuongezea kuelekea msimu wa 2025/25. Taarifa zilikuwa zinaeleza kuwa kiungo huyo asilimia kubwa ataondoka hapo na timu ambayo ilikuwa inatajwa kwa ukaribu ilikuwa ni Simba SC. Mkataba wake na Azam FC ni mwaka mmoja umebaki hivyo atautumia wote kuwa hapo msimu ujao. Simba SC inatajwa kuwa jitihada za kumpata mchezaji huyo zimegonga mwamba. Rekodi zinaonyesha kuwa Feisal ni kiungo namba moja kwenye kutengeneza pasi nyingi ambazo ni 13 za mabao. Pasi yake ya kwanza alitoa kwenye mchezo dhidi ya KMC FC…
INAELEZWA kuwa Celestin Ecua ambaye ni kiungo wa Zoman FC huenda akasaini mkataba wa miaka miwili kuwa katika kikosi cha mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC. Yanga SC baada ya mechi 30 ambazo ni dakika 2,700 walikusanya jumla ya pointi 82 ikiwaacha watani zao wa jadi Simba SC kwa tofauti ya pointi nne. Simba SC iligotea nafasi ya pili ikiwa na pointi 78. Mchezo wa Kariakoo Dabi, Juni 25 2025 uliamua bingwa wa msimu baada ya Yanga SC kushinda kwa mabao 2-0 yakifungwa na Pacome kwa pigo la penalti na Clemet Mzize ambaye alitumia pasi ya Pacome.…
MABINGWA mara 31 ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC inatajwa kuwa imefikia makubaliano na kiungo mshambuliaji wa Tabora United, Offen Chikola kwa ajili ya msimu ujao baada ya kufikia makubalian mazuri. Tetesiz za hivi karibuni zilieleza kiungo huyo kuwepo katika mazungumzo na Simba kwa ajili ya kuiimarisha safu ya kiungo ya timu hiyo, katika msimu ujao wa 2025/26. Kiungo tayari amemalizana na Yanga SC kwa kumpa mkataba wa miaka miwili, ambao utaanza kufanyakazi katika msimu ujao hivyo kuna uwezekano akapishana na Simba SC ambao walikuwa wanampigia hesabu.
SIMBA SC iliyogotea nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC 2024/25 bado ipo kwenye mchakato wa kuendelea kujenga kikosi. Ikumbukwe kwamba msimu wa 2024/25 ndani ya ligi namba nne kwa ubora bingwa ni Yanga SC akitwaa taji la 31 chini ya kocha Miloud Hamdi ambaye hatakuwa katika kikosi hicho kwa msimu wa 2025/25. Kwa mujibu wa Rais wa Heshima wa Simba SC, Mohamed Dewji maarufu kwa jina la Mo amebainisha kuwa msimu uliopita haukuwa mwepesi ulikuwa na changamoto nyingi lakini wanaendelea kuimarika taratibu. “Msimu uliopita haukuwa mzuri kwetu na haukuwa rahisi. Tumepitia mengi na…
Rulani Mokwena ametambulishwa rasmi na MC Alger kuwa kocha mkuu wa Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Nchini Algeria akichukua nafasi ya Khaled Ben Yahiam aliyepewa mkono wa kwaheri hivi karibuni. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 38 raia wa Afrika Kusini ambaye ambaye alikuwa anakinoa kikosi cha Wydad Casablanca msimu uliopita amepewa mkataba wa miaka miwili ndani ya klabu hiyo MC Alger atakaoanza kuutumikia kuanzia msimu ujao.