Author: Admin

Baba mzazi wa mchezaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta, Mzee Ally Samatta, amefariki dunia asubuhi ya leo, Julai 6, 2025. Msiba upo Mbagala, jijini Dar es Salaam, ambapo familia, ndugu, jamaa na marafiki wamekusanyika kuomboleza msiba huo mzito. Timu ya Global TV ipo eneo la tukio na itaendelea kukuletea taarifa kamili kuhusu msiba huu, ikiwemo ratiba ya mazishi, ujumbe wa familia, na yale yote yanayoendelea nyumbani kwao Samatta. Taarifa zaidi zitafuata. Pole kwa familia ya Samatta, wapendwa na mashabiki wote wa soka nchini.

Read More

Mchezaji wa soka wa kimataifa kutoka Ghana, Bernard Morrison, ametoa andiko la kugusa moyo kupitia ukurasa wake rasmi, akieleza safari yake ya mateso kutokana na jeraha la goti ambalo lilimweka nje ya uwanja kwa karibu mwaka mmoja. Katika andiko hilo, Morrison amewashukuru watu mbalimbali waliomsaidia katika kipindi hicho kigumu cha maisha yake ya soka na kuweza kumrudisha uwanjani. Morrison alianza kwa kueleza kuwa tangu mwezi Januari 2024, aliporejea Tanzania kwa ajili ya matibabu ya goti lake, alikumbana na changamoto nyingi, ikiwemo ukosefu wa huduma sahihi na ucheleweshwaji wa matibabu sahihi, hali iliyosababisha kuendelea kwa maumivu kwa muda mrefu. Baada ya…

Read More

Mwaka uliopita, Chama cha Umoja wa Vilabu Afrika (ACA) chini ya uongozi wa Eng. Hersi Said, kilifanikiwa kushawishi CAF kutoa dola 50,000 kwa kila klabu iliyoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL) na Kombe la Shirikisho (CAF CC) katika hatua ya awali. Kwa msimu huu mpya, ACA imeendelea kupigania maslahi ya vilabu barani Afrika kwa mafanikio zaidi. Kupitia mazungumzo na ushawishi wao kwa CAF, imeidhinishwa kuwa klabu zitakazoshiriki hatua ya awali ya CAF CL na CAF CC zitalipwa dola 100,000 kila moja kwa ajili ya maandalizi. Ikumbukwe, kabla ya uwepo wa ACA, klabu shiriki katika hatua za awali za mashindano…

Read More

Afisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ali Kamwe, ameonyesha kushangazwa na mauno ya Queen Fraison maarufu kama Bonge la Dada, kupitia video iliyosambaa mtandaoni. Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Kamwe aliandika kwa utani: “Bora mimi nilikuwa naangalia nywele…” 😂😂😂😂 Kauli hiyo imeibua vicheko na mijadala miongoni mwa mashabiki, huku wengine wakiongeza maneno yao ya utani na maoni mbalimbali juu ya video hiyo inayomwonyesha Queen Fraison akionesha ujasiri na mvuto wa kipekee. Queen Fraison ameendelea kuwa gumzo mitandaoni kutokana na muonekano wake na ujasiri wake wa kujiamini, huku akiwavutia maelfu ya wafuasi.

Read More

KATIKA kurejesha kwa jamii wachezaji, Nassor Kapama ambaye ni kiungo wa Kagera Sugar pamoja na mshambuliaji wa JKT Tanzania, Mohammed Bakari ‘Muddy Beka’ Julai 12, mwaka huu wanatarajia kucheza mechi ya hisani ikiwa na lengo maalum la kusaidia watu wasiojiweza. Mechi hiyo imeeandaliwa maalum na nyota hao ambao wanashiriki Ligi Kuu Bara ambapo itafanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kigamboni, Dar huku kiasi chote ambacho kitapatikana katika mechi hiyo kitatolewa kwa wahitaji. Muandaaji wa mchezo huo, Kapama amesema, kuwa maandalizi ya mchezo huo hadi sasa yanaendelea ambapo lengo kubwa la kufanya hivyo ni kutaka kusaidia wanajamii wa eneo hilo.…

Read More

BEKI wa kazi ndani ya kikosi cha Yanga SC Dickson Job huenda akaongeza kandarasi nyingine ndani ya kikosi hicho. Nyota huyo mkataba wake msimu wa 2024/25 unagota mwisho. Kwa sasa bado hajaongeza mkataba mwingine na inaelezwa kuwa mazungumzo yameanza kwa pande zote mbili. Juni 29 2025 ulikuwa ni mchezo wa mwisho kwa msimu wa 2024/25 hivyo jambo lake litafanyiwa kazi haraka. Uongozi wa Yanga SC uliweka kando mazungumzo na wachezaji wengi kutokana na mechi ngumu ambazo zilikuwa juu yao. Kariakoo Dabi Juni 25, Yanga SC 2-0 Simba SC na fainali ya CRDB Federation Cup Juni 29, Yanga SC 2-0 Singida…

Read More

Rais wa Yanga SC, Mkandarasi Hersi Said amechukua Fomu ya kuwania Ubunge katika Jimbo la Kigamboni lililopo Jijini Dar es Salaam. Hersi mwenye ushawishi mkubwa katika masuala ya soka amechukua fomu hiyo leo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM). Ikumbukwe Jimbo hilo liliondokewa na aliyekuwa Mbunge wake Faustine Ndugulile aliyefariki dunia mwanzoni mwa mwaka huu alipokuwa nchini India kwa ajili ya matibabu.

Read More

UONGOZI wa Klabu ya Yanga SC umeweka wazi dhamira yao ya kuhakikisha wanarejesha nyumbani Kombe la CRDB Federation Cup, wakisisitiza kuwa wao ni mabingwa watetezi licha ya kupangwa kucheza dhidi ya timu ngumu, Singida Black Stars, kwenye fainali. Mchezo huo wa fainali unatarajiwa kuchezwa leo, Jumapili, Juni 29, 2025, ambapo macho ya Watanzania wengi yataelekezwa kwenye uwanja huo mkubwa wa kihistoria. Yanga SC inashuka dimbani ikiwa na morali ya juu, baada ya kutwaa taji la 31 la Ligi Kuu Bara, kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya watani wa jadi Simba SC. Klabu hiyo imemaliza ligi ikiwa na pointi 82,…

Read More

SIMBA SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids raia wa Afrika Kusini ipo katika harakati za kumsajili kipa wa JKT Tanzania, Yakoub Seleman katika msimu ujao. Kipa namba moja kwa sasa ndani ya Simba SC ni Moussa Camara. Ni hati safi 19 amekusanya msimu wa 2024/25 akiwa kipa namba moja mwenye hati nyingi ndani ya ligi namba nne kwa ubora. Inaelezwa Simba SC wanamtaka kipa huyo haraka na hivi sasa wapo katika harakati za mwishoni za kimyakimya za kumpata Yacoub. Simba SC kama watampata kipa huyo, basi wataachana na Hussein Abel katika msimu ujao ambaye ni kipa namba tatu wa…

Read More

KIUNGO wa Simba SC, Deborah Mavambo ambaye ni ingizo jipya katika kikosi hicho kwa msimu uliogota mwisho wa 2024/25 yupo kwenye mtego ndani ya kikosi hicho kutokana na kiwango chake kuporomoka mwanzo mwisho. Nyota huyo kwenye mechi za awali alianza kuonyesha ubora wake lakini kadri siku zilivyokuwa zinazidi uwezo wake ulikuwa unaporomoka. Atakumbukwa kwenye mchezo wa Simba Day, jina lake liliimbwa kutokana na kiwango bora katika matumizi ya nguvu kwenye mguu wake wa kulia. Ni jezi namba 17 alikabidhiwa ambayo ilikuwa inavaliwa na kiungo Clatous Chama ambaye yupo ndani ya Yanga SC kwa msimu wa 2024/25. Mavambo alikuwa anapewa nafasi…

Read More

HASHEEM Ibwe, Ofisa Habari wa Klabu ya Azam FC inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, ametangaza nia ya kuwania ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, (CCM) Ibwe amesema: “Salamu kwa Vijana wenzangu. Huu ni wakati wa kusimama imara, kuchukua nafasi na kuwa sehemu ya mabadiliko tunayoyataka kuyaona katika jamii zetu. Maendeleo hayaji kwa kusubiri, yanajengwa na watu wenye maono, bidii, na moyo wa kujitolea. Na hakuna kikundi chenye nguvu, maarifa, na ari kubwa kama sisi vijana. “Tuna nguvu. Tuna uwezo. Tuna wajibu. Tushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ikiwemo suala la uongozi kuchora dira yetu wenyewe. Kama si sisi, ni…

Read More

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewataka waombaji wote wa nafasi ya uongozi kwenye Uchaguzi Mkuu wa TFF utakaofanyika Agosti 16 mwaka huu Jijini Tanga kuhakikisha wanakuwa na Kanuni za Uchaguzi. Taarifa ya Juni 17, 2025 iliyotolewa na TFF imeeleza kuwa wagombea hao wanapochukua fomu za kuwania uongozi katika uchaguzi huo wanatakiwa kuhakikisha wanapata na Kanuni hizo na kubainisha kuwa kwa wale ambao tayari wameshachukua fomu, wanatakiwa kuwasiliana na Sekretarieti ya TFF ili kupata Kanuni hizo. TFF imesema nafasi zinazowaniwa katika uchaguzi huo utakaoendeshwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF ni saba. Nafasi hizo ni Rais, na wajumbe sita…

Read More

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara wametua Mbeya kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons. Mchezo huo ni wa mzunguko wa pili unatarajiwa kuchezwa saa 10:00 jioni Uwanja wa Sokoine kwa wababe hao kutafuta pointi tatu muhimu. Yanga SC imebakiza mechi tatu, baada ya kumalizana na Prisons itakuwa na mchezo dhidi ya Dodoma Jiji kisha kete ya mwisho kwenye ligi ni dhidi ya Simba SC, Juni 25.

Read More

KUELEKEA kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili kati ya KenGold vs Simba SC Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, hesabu kali zinapingwa kwa timu zote mbili kuhitaji kusepa na pointi tatu muhimu. Simba SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids walipokutana na KenGold Desemba 18 2024, ubao wa Uwanja wa KMC Complex ulisoma Simba SC 2-0 KenGold. Pointi tatu zilikuwa mali ya Simba SC. Leo wanatarajiwa kukutana kwa mara nyingine kukamilisha dakika 180 za msako wa pointi sita ambapo zile za mwanzo ni Simba SC alisepa nazo baada ya dakika 90 kugota mwisho. Seleman Matola, kocha msaidizi wa…

Read More

KOCHA Mkuu wa Yanga SC, Miloud Hamdi amesema kuelekea kwenye mchezo wao wa mzunguko wa pili dhidi ya Tanzania Prisons msimu wa 2024/25 ambacho wanahitaji ni pointi tatu muhimu ndani ya dakika 90. Yanga SC itakaribishwa na Tanzania Prisons kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sokoine, Juni 18 2025 saa 10:00 ikiwa ni mzunguko wa pili. Miloud amesema:”Tunawaheshimu sana Tanzania Prisons, lakini sisi ni Yanga. Nina wachezaji wenye uzoefu na uwezo mkubwa. Tunajua utakuwa mchezo mgumu lakini hatuna sababu ya kuwaza sana kuhusu hilo. Tumekuja kushindana kwa tahadhari kubwa na ambacho tunahitaji ni pointi tatu muhimu.” “Tumekuja Mbeya…

Read More

Uongozi wa timu ya Fountain Gate FC yenye makazi yake Babati mkoani Manyara imemsimamisha nyota wao Salum Kihimbwa kwa muda usiojulikana kutokana na utovu wa nidhamu. Kihimbwa msimu huu amekuwa na kiwango bora katika Ligi Kuu Bara, ambapo amehusika katika mabao tisa ndani ya timu hiyo, akifunga nne na kutoa pasi za mabao matano. Amesimamishwa kwa muda usiojulikana baada ya kumpiga mwamuzi katika mchezo wa kirafiki ambao Fountain Gate ilicheza dhidi ya Wapolo FC katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo jijini Arusha. Katika mchezo huo wa kirafiki Kihimbwa alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea madhambi mchezaji wa Wapolo FC…

Read More

Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inapenda kuwataarifu wadau wote wa mpira wa miguu kuwa Uchaguzi Mkuu wa TFF utafanyika tarehe 16 Agosti, 2025 katika jiji la Tanga. Nafasi Zitakazogombewa: Rais wa TFF – Nafasi 1 Wajumbe wa Kamati ya Utendaji – Nafasi 6 Gharama za Fomu za Kugombea: Rais: TSh 500,000 Mjumbe wa Kamati ya Utendaji: TSh 200,000 Utoaji wa Fomu: Fomu zitatolewa kuanzia Jumatatu, tarehe 16 Juni hadi 20 Juni 2025, saa 10:00 jioni. Fomu zinapatikana katika Makao Makuu ya TFF na pia kupitia tovuti rasmi ya TFF: www.tff.or.tz Wadau wote wenye sifa…

Read More

Klabu ya Yanga imejibu mapigo baada ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kudai klabu hiyo fedha zao za zawadi katika mashindano mbalimbali zikatwe kulipia malipo wanayotakiwa kuilipa kwa TFF huku ikidai kuwa haijawahi kulipwa fedha yoyote ya Ubingwa wa Kombe la Shirikisho kwa Misimu mitatu mfululizo, (2021/2022, 2022/2023 na 2023/24). Taarifa ya Juni 10, 2025 iliyotolewa na klabu hiyo imeeleza taarifa ya TFF Madai hayo imeshindwa kufafanua deni lenyewe na kubainisha kuwa TFF wamekuwa wakishikila fedha hizi za Ubingwa kwenye akaunti zao kila Msimu unapomalizika huku wakifahamu ni makosa na ni kinyume cha utaratibu. Yanga Sc imesema hakuna uthibitisho wowote…

Read More

HAWAJAWEKA wazi lakini tafsiri ya kiufundi ni kwamba Azam FC wako kwenye harakati za kujiandaa na lolote kwenye nafasi ya Feisal Salum ‘Fei Toto’ Staa huyo ambaye bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Azam amekuwa akihusishwa na kujiunga na Simba, Yanga na Kaizer Chiefs msimu ujao ambapo kila mmoja kwa wakati wake anapambana kupata ahueni ya dau. Azam wamekuwa wakisisitiza kwamba mchezaji wao anauzwa kwa zaidi ya Sh1 bilioni. Ili kuziba pengo lake, Azam FC iko kwenye mazungumzo na Vipers ya Uganda kuhusu kiungo wake Allan Okelo  ambaye Simba pia iliwahi kumtaka, lakini ilijibiwa kwamba mchezaji huyo hauzwi. Hapo…

Read More

BEKI wa zamani wa Yanga SC Gift Fred ambaye alishindwa kupata namba kikosi cha kwanza na kupewa Thank You anatajwa kupata dili nono kwa ajili ya changamoto mpya. Gift Fred anakaribia kujiunga na Klabu ya KCCA ya nchini Uganda katika msimu ujao wa 2025/26 kwa ajili ya kutimiza majukumu yake. Gift anakwenda kujiunga na KCCA akiwa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake wa mkopo St George ya nchini Ethiopia kumalizika. Ni Yanga SC ya Tanzania ilimpeleka beki huyo kwa mkopo St George  baada ya kutovutiwa na kiwango chake akishindwa kuwapa ushindani Ibrahim Bacca, Dickson Job na Bakari Mwamnyeto. Gift…

Read More