LICHA ya nyota wawili Mbwana Samatta na Simon Msuva kuwa na umuhimu mkubwa kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars takwimu zinaonyesha msimu huu bado hawajaonyesha viwango vikubwa wakiwa kwenye klabu wanazozitumikia. Katika mechi 13 alizocheza msimu huu wa Ligi Kuu Ufaransa, mshambuliaji huyo bado hajafunga bao wala kutoa asisti tofauti na msimu uliopita alipokuwa PAOK ya Ugiriki. Akiwa PAOK, Samatta alifunga mabao manne na kutoa asisti moja katika mechi 12, takwimu zilizothibitisha bado ana uwezo wa kumalizia nafasi. Hata hivyo, ni kama uhamisho wake wa kwenda Le Havre umeambatana na ugumu wa ligi, kasi ya mechi na majukumu…
Author: Admin
MAHODHA wa Simba, Shomari Kapombe aibua gumzo baada ya kushindwa kuweka wazi maana halisi ya staili yake mpya ya kushangilia mabao, inayohusisha kutembea kama mzee anayesaidiwa na mkongojo, akisema ni staili atakayoendelea nayo kila anapofunga. Kapombe alionekana kwa mara ya kwanza akitumia staili hiyo katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Esperance de Tunis, uliochezwa hivi karibuni, ambapo alishangilia kwa namna iliyowaacha wengi njia panda. Katika kushangilia huko, beki huyo wa kulia alionekana akishika mfano mkongojo, ishara iliyozua tafsiri tofauti miongoni mwa mashabiki, huku baadhi wakiamini ni ujumbe maalum aliokusudia kuuwasilisha. Akizungumza kuhusu staili hiyo, Kapombe amesema ameamua…
UONGOZI wa Klabu ya Yanga umeweka mezani dau nono kama sehemu ya kuhamasisha kikosi kuelekea mchezo wao muhimu wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS FAR Rabat. Mchezo huo wa marudiano unachezwa leo majira ya saa 4:00 usiku katika dimba la Olympique De Rabat lililopo jijini Rabat, Morocco, ukiwa na uzito mkubwa kwa hatma ya timu hiyo kwenye michuano hiyo mikubwa barani Afrika. Inaelezwa kuwa mfadhili mkuu wa klabu hiyo, GSM, ameahidi kutoa kiasi cha Shilingi milioni 500 endapo Yanga itaibuka na ushindi katika pambano hilo la hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Ahadi hiyo imekuja katika…
LICHA ya kucheza pungufu kwa zaidi ya kipindi kimoja, Simba SC imeonyesha roho ya kishujaa baada ya kuvuna alama moja muhimu ugenini dhidi ya Petro de Luanda, katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa Uwanja wa November 11, jijini Luanda, Angola. Mchezo huo uligubikwa na presha mapema baada ya nahodha wa Simba, Shomari Kapombe, kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza, hali iliyoifanya Simba kulazimika kucheza wakiwa pungufu dhidi ya wenyeji waliokuwa wakisaka ushindi nyumbani. Licha ya changamoto hiyo, wachezaji wa Simba walionyesha mshikamano mkubwa, wakipambana kwa nguvu kutafuta matokeo chanya huku Petro de Luanda wakijaribu…
Mwanamitandao maarufu, Clemence Mwandambo, amewapa somo vijana kuhusu masuala ya mahusiano, akisisitiza kuwa si busara kurudiana na mpenzi wa zamani (Ex). Akizungumza kupitia mitandao ya kijamii, Mwandambo amedai kuwa mwanamke hapendi kuachwa mara mbili, hivyo endapo mwanaume atarudiana na mpenzi wake wa zamani, anaweza kukumbana na changamoto au madhara makubwa baadaye. “Ex harudiwi. Mwanamke hapendi kuachwa mara mbili, hivyo akirudi kwako anaweza kukufanyia jambo lolote ili kuhakikisha haumwachi tena. Unaweza kujikuta ukijuta,” amesema Mwandambo. Katika kauli yake, aligusia pia sakata la wasanii Harmonize na Kajala, akieleza kuwa kurudiana kwao ni jambo lisilo na busara kwa upande wa Harmonize, japokuwa amesisitiza…
Man City Yapindua Meza Kibabe Ikiicharaza Liverpool Nyumbani Manchester City imeandika ushindi muhimu wa mabao 2-1 dhidi ya Liverpool katika dimba la Anfield, matokeo yaliyokuja baada ya dakika za mwisho zenye presha kubwa na yaliyoweka hai matumaini yao ya ubingwa wa Ligi Kuu England. Mabingwa watetezi walijikuta wakipoteza mwelekeo wa mchezo licha ya kuongoza kipindi cha pili, huku mabao ya kuchelewa kutoka kwa Bernardo Silva na penalti ya Erling Haaland yakigeuza kabisa matokeo ya mechi hiyo yenye ushindani mkali. Kwa ushindi huo, City imepunguza pengo dhidi ya vinara hadi alama sita, ikiimarisha msimamo wao katika mbio za ubingwa, wakati Liverpool…
Azam Yaandika Historia Mpya CAF Baada ya Kuvunja Rekodi ya Simba Klabu ya Azam FC imeandika historia mpya katika michuano ya CAF baada ya kufanikiwa kuvuna jumla ya pointi 9 katika ushiriki wake wa kwanza kabisa wa hatua ya makundi, mafanikio yaliyoweka alama ya kipekee katika soka la Tanzania. Rekodi hiyo imeivunja ile iliyokuwa ikishikiliwa na Simba SC, ambao waliwahi kukusanya pointi 7 mwaka 2003, huku Yanga SC wakipata pointi 2 pekee katika ushiriki wao wa kwanza mwaka 1998. Hakuna timu nyingine ya Tanzania iliyowahi kufikia idadi hiyo ya pointi katika hatua ya makundi kwa mara ya kwanza. Rekodi ya…
Droo ya Hatua ya 64 Bora Kombe la Shirikisho la CRDB Kufanyika Februari 09 Michuano ya Kombe la Shirikisho la CRDB inatarajiwa kuendelea Jumatatu hii, Februari 09, kwa kufanyika droo ya Hatua ya 64 Bora, hatua ambayo itashuhudia kuanza kwa ushiriki wa timu za NBC Premier League katika mashindano hayo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, droo hiyo itafanyika kuanzia saa 6:00 mchana na itarushwa moja kwa moja kupitia AzamSports1HD. Droo ya Hatua ya 64 Bora Kombe la Shirikisho la CRDB kufanyika Februari 09 inaweka wazi upangaji wa michezo kwa hatua inayofuata ya mashindano hayo.
VINARA wa Ligi Kuu ya England, Arsenal hawatanii kabisa msimu huu, wanaendelea kukusanya pointi kwenye kila mchezo wanaocheza na kuwakimbia wale wanaowafukuza ambao ni Manchester City. Jana waliichabanga Sunderland 3-0 na kuongeza wigo wa pointi dhidi yake na City na sasa ubao unasoma tofauti ya pointi tisa huku Man City akiwa na mchezo mgumu leo dhidi ya Liverpool. Kwa kasi waliyonayo msimu huu kuna kila dalili vijana hawa wa Mikel Arteta wakatwaa ubingwa wa EPL msimu.
IKICHEZA ugenini kwenye Uwanja wa Prince Moulay Abdellah, Yanga imekubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa AS FAR Rabat katika mechi ya tano ya kundi B kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. Kipigo hicho kimeifanya Yanga kubaki na pointi tano ikishuka hadi nafasi ya tatu, huku AS FAR Rabat ikipanda nafasi ya pili ikifikisha pointi nane, huku mechi za mwisho zikishikilia hatma ya wawili hao mmoja kufuzu robo fainali. Katika mechi hiyo iliyochezwa Februari 7, 2026, bao lililoizamisha Yanga limefungwa na Anas Bach dakika ya 85 kufuati walinzi wa Yanga kujichaganya katika kuokoa hatari na mpira kumkuta mfungaji aliyeachia shuti ndani…
Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC imeeleza kusikitishwa na vitendo vya baadhi ya watu kuitisha mkutano usio rasmi na kutoa maneno ya kashfa pamoja na kauli zisizo na staha dhidi ya mwekezaji wa klabu hiyo, Ndugu Mohammed G. Dewji. Klabu imesisitiza kuwa vitendo hivyo havikubaliki na haitatabari wala kuvumilia mtu yeyote atakayeharibu taswira ya klabu kwa namna yoyote ile, huku wakitoa pole rasmi kwa Ndugu Dewji kutokana na usumbufu huo. Kutokana na hali hiyo, uongozi wa Simba umeliandikia Jeshi la Polisi ili kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wote waliohusika katika mkutano huo ama “kula njama,” kwa lengo la…
MMILIKI wa Mbeya Kwanza, Yusuph Kitumbo, amesema hana mpango wowote wa kuiuza timu hiyo kwa sasa kama inavyodaiwa, baada ya hivi karibuni kuibuka taarifa za Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuanza kufanya mazungumzo ya kina ya kutaka kuinunua. Akizungumza na Soka la Bongo, Kitumbo, amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote na zimeandaliwa makusudi na watu wenye nia ovu juu yao, kwa lengo la kutaka kurudisha chini morali ya kikosi hicho kutokana na mwenendo mzuri iliyonayo kwa msimu huu. “Tunajua kuna watu wanatumika kwa ajili ya kutuvuruga, ila niwaambie ukweli sisi hatutatetereka hata kidogo kwa sababu tumejipanga vya kutosha, malengo yetu…
MWENYEKITI wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu, amesema mabadiliko ya ghafla katika benchi la ufundi yamechangia kwa kiasi kikubwa kutokuwa na mwanzo mzuri wa msimu huu kwa timu hiyo. Mangungu amesema msimu uliopita Simba ilikuwa chini ya kocha mpya, Fadlu Davids, ambaye alihitaji aina maalumu ya wachezaji watakaokwenda sambamba na falsafa yake ya soka, jambo lililowasaidia kumaliza msimu katika nafasi ya pili na kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Ameeleza kuwa walipoanza msimu huu, uongozi uliingia sokoni kusajili wachezaji kulingana na mapendekezo ya kocha huyo, lakini ujio wa ofa kubwa kwa Davids uliwalazimu kumuacha aondoke, hali iliyovuruga mipango yao…
BAADA ya kukosa ushindi kwenye mechi tano mfululizo za Ligi Kuu Bara, uongozi wa Mashujaa upo katika mazungumzo ya kumalizana na kocha wa kikosi hicho, Salum Mayanga ili kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba. Hatua hiyo inakuja ikiwa ni baada ya timu hiyo kuchapwa bao 1-0 na KMC, kwenye Uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi, Februari 3, 2026, kikiwa ni kichapo cha tatu mfululizo, ingawa ni mechi ya tano ya Ligi Kuu bila ya kuibuka na ushindi. Katika mechi tano zilizopita za timu hiyo katika Ligi Kuu Bara, Mashujaa imetoa sare mbili na kuchapwa tatu, huku mara ya mwisho kushinda ilikuwa ni…
Kocha wa zamani wa Simba SC, Abdelhak Benchika, anaendelea kuonyesha umahiri wake nchini Algeria baada ya kuiongoza klabu yake ya USM Alger kukaa kileleni mwa Kundi A katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup). Chini ya uongozi wake, USM Alger imefanikiwa kukusanya alama tisa (9) katika mechi tatu za kwanza, ikiwa na rekodi ya ushindi wa asilimia 100 baada ya hivi karibuni kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Djoliba AC. Benchika, akiwa na beki wake imara raia wa Cameroon, Chemalone, wanatuma salamu nzito kwa wapinzani wao kuwa msimu huu wamedhamiria kulitwaa kombe hilo kwa mara…
Katika kumbukumbu za hivi karibuni za kuelekea dirisha la usajili, nukuu ya Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Jayrutty Investment Company Limited, CPA Joseph Rwegasira, inaendelea kuishi vichwani mwa Wanasimba. Kauli yake ya kishujaa isemayo, “Kila mwaka tutasajili mchezaji mmoja ambaye Wanasimba wanamtaka, tutakuwa tunaambiwa na sisi tutakuwa tunamsajili,” ilikuwa ni zaidi ya ahadi; ilikuwa ni tangazo la vita ya kiuchumi na ushindani dhidi ya wapinzani wao wa jadi. Rwegasira, kupitia kampuni yake, amejipambanua kama mdau mkubwa anayeamini katika kuwapa mashabiki kile wanachokihitaji ili kurejesha furaha ya Msimbazi kupitia usajili wa “Galacticos” wa kiwango cha juu. Ahadi hii imeweka shinikizo chanya kwa…
Beki wa kimataifa wa Mauritania, Khadim Diaw (27), amekuwa lulu sokoni mwezi huu wa Januari 2026 baada ya kuvunja mkataba wake na klabu ya Al Hilal Omdurman kutokana na madai ya kutolipwa mishahara kwa miezi kadhaa. Hivi sasa, beki huyo mzoefu yuko kwenye mazungumzo ya kina na miamba kadhaa ya soka barani Afrika, ikiwemo Simba SC ya Tanzania, pamoja na klabu za Algeria za MC Alger na JS Kabylie ambayo inatajwa kumpa ofa ya mkataba wa miaka mitatu ili kuimarisha safu yao ya ulinzi. Licha ya Simba SC {@simbasctanzania} kuonyesha nia ya dhati ya kumnasa Diaw kwa ajili ya mashindano…
Kinda wa kimataifa wa Tanzania, Miano Danilo van den Bos (22), amepiga hatua kubwa katika soka la kulipwa baada ya kujiunga na klabu ya FK Panevėžys inayoshiriki Ligi Kuu ya Lithuania (A Lyga). Huu unakuwa mkataba wake wa kwanza wa soka la kulipwa kwa beki huyo wa kati ambaye pia anaweza kucheza kama beki wa kulia na kiungo mkabaji, akitokea klabu ya FC Eindhoven ya Uholanzi. FK Panevėžys ni miongoni mwa klabu imara nchini Lithuania, ikiwa imetwaa ubingwa wa ligi hiyo mwaka 2023 na kushiriki michuano ya kukufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) hivi karibuni. Miano , ambaye…
Klabu ya Yanga SC imezua taharuki katika soko la usajili barani Afrika baada ya kuripotiwa kugomea ofa mbili nono kutoka kwa vigogo wa soka la Kaskazini, Zamalek ya Misri na CR Belouizdad ya Algeria, zilizokuwa zikimhitaji mlinda mlango wao namba moja, Djigui Diarra. Matajiri hao wa Kiarabu wamevutiwa na kiwango cha hali ya juu alichokionyesha kipa huyo mwenye umri wa miaka 30 kwenye michuano ya AFCON 2025 nchini Morocco, ambapo alikuwa mhimili mkuu wa timu ya taifa ya Mali kabla ya kutolewa katika hatua ya robo fainali. Licha ya ofa hizo kutajwa kuwa na thamani kubwa, uongozi wa Yanga umetoa…
Majina ya waliochaguliwa JWTZ 2026/2027 Jeshi la Ulinzi la Wananchi, www.jwtz.go.tz 2026 News, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ni taasisi ya kijeshi inayowajibika na ulinzi wa mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na usalama wa taifa kwa ujumla. Kila mwaka, JWTZ hufanya mchakato wa kuandikisha vijana waliomaliza elimu ya sekondari, vyuo na wale waliopitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili kujiunga rasmi na utumishi wa kijeshi. Mwaka 2025, JWTZ kwa kushirikiana na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wametoa tangazo la majina ya vijana waliopitishwa kujiunga na Jeshi hilo baada ya kufuzu taratibu na…