Yanga Yatuma Salamu Msimbazi Baada ya Ushindi wa 5-0 Dhidi ya JKT Tanzania Ubingwa haujitangazi kwa maneno bali kwa matokeo. Ndivyo ilivyokuwa kwa vinara wa Ligi Kuu Bara, Young Africans Sports Club, walipoonyesha makali yao baada ya ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC, Dar es Salaam. Matokeo hayo yamezidi kuimarisha nafasi ya Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi kwa kufikisha pointi 28, huku yakitafsiriwa kama salamu ya wazi kuelekea Msimbazi kabla ya pambano lijalo dhidi ya watani wao wa jadi. Katika mchezo huo, Yanga ilionesha ubora wa hali ya juu katika…
Author: Admin
KLABU ya Yanga imerejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo uliopigwa kwa ushindani mkubwa.l katika dimba la KMC Complex uliopo Mwenge Dar es Salaam. Katika pambano hilo, Yanga ilionyesha ubora mkubwa kuanzia dakika za mwanzo hadi mwisho wa mchezo, ikitawala umiliki wa mpira na kutengeneza nafasi nyingi za mabao. Ushindi huo umeipa timu hiyo morali kubwa kuelekea michezo ijayo, hususan Kariakoo Derby inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki. Mabao ya Yanga yalifungwa na Mohamed Hussein, Laurindo Dilson ‘Depu’, Mudathir Yahya, Prince Dube na…
Kikosi cha Simba vs Dodoma Jiji Leo 25/02/2026 Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, leo Februari 25, 2026 wanatarajiwa kushuka dimbani kuwakabili wenyeji Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC utakaopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, kuanzia saa 1:00 usiku. Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na nafasi za timu hizi kwenye msimamo pamoja na rekodi zao za hivi karibuni. Simba inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na morali ya juu baada ya kuichapa Tanzania Prisons mabao 2-0 katika uwanja huohuo wa Jamhuri wikiendi iliyopita. Matokeo hayo yaliipa Simba alama tatu muhimu na kuiweka kwenye nafasi ya…
SIMBA SC imeweka wazi kuwa kwa sasa fikra zake ziko kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Dodoma Jiji FC, huku Kariakoo Derby dhidi ya Yanga SC ikiwa bado ni suala la baadaye. Beki wa Simba, David Kamenta “Duchu”, amesema kuwa kikosi chake kitapambana kwa nguvu zote katika mchezo wa Dodoma ili kukamilisha kampeni yao ya kupata alama sita katika michezo miwili mfululizo. “Tutakamilisha kampeni yetu ya kupata alama sita, tatu tayari tumepata, bado tatu za Dodoma ziko mbele yetu. Baada ya mechi hiyo, tutakaa chini na kuanza kupanga mikakati ya Kariakoo Derby,” amesema Duchu. Simba itashuka dimbani kesho kwenye Uwanja…
KOCHA Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, ameweka wazi kuwa ubora wa viwanja vinavyotumika katika mechi za Ligi Kuu Bara ndiyo jambo linalompa wasiwasi mkubwa kwa sasa, hasa katika kipindi hiki ambacho timu yake inaelekea kwenye michezo muhimu. Barker amesema hali ya baadhi ya viwanja inampa hofu kuhusu usalama wa wachezaji wake, kuwa jambo la msingi kwake ni kuhakikisha kikosi chake kinamaliza mechi kikiwa salama bila majeraha, hususan kuelekea michezo mikubwa ikiwemo Kariakoo Derby. Ameeleza kuwa viwanja vyenye mashimo au nyasi zisizo katika hali nzuri vinaweza kusababisha madhara makubwa kwa wachezaji, hasa wanapokutana na timu zinazocheza soka la nguvu. “Nazingira…
Mgombea Urais Barcelona Victor Font Aahidi Kumrejesha Messi Camp Nou Barcelona, Hispania. Mgombea Urais Barcelona Victor Font Aahidi Kumrejesha Lionel Messi Camp Nou endapo atashinda uchaguzi wa klabu hiyo, akisisitiza kuwa nyota huyo wa Argentina anapaswa kustaafu soka akiwa katika dimba la Camp Nou na kupewa heshima anayostahili. Victor Font, anayewania nafasi ya urais wa FC Barcelona, ameweka wazi azma yake ya kuhakikisha Lionel Messi anamaliza safari yake ya soka mahali alipojijengea jina. Kauli hiyo inakuja wakati mjadala kuhusu mustakabali wa Messi ukiendelea kushika kasi kuelekea uchaguzi ujao wa klabu hiyo ya Hispania. Messi aliondoka FC Barcelona mwaka 2021 kufuatia…
Mayele Aendelea Kupambana na Ukame wa Mabao Pyramids FC Hali bado ni tete huko Misri ambako mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Fiston Mayele, anaendelea kukabiliwa na ukame wa mabao akiwa na Pyramids FC. Licha ya timu yake kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ceramica Cleopatra katika Ligi Kuu ya Misri, nyota huyo alishindwa tena kufumania nyavu. Ushindi huo umeifanya Pyramids FC kufikisha pointi 34 na kujikita nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi. Hata hivyo, kwa upande wa Mayele, mchezo huo umeongeza idadi ya mechi alizocheza bila kufunga kufikia 21 mfululizo katika mashindano tofauti. Tangu alipofunga mara…
KOCHA Mkuu wa Fountain Gate, Mohamed Ismail ‘Laizer’, amesema kuwakosa wachezaji watatu waliofikia makubaliano ya kutua ndani ya kikosi hicho katika dirisha dogo la Januari 2026, ni pigo kubwa kwake, kutokana na matarajio aliyokuwa nayo. Nyota walioshindwa kujiunga na timu hiyo katika dirisha dogo ni, mshambuliaji wa Mbeya Kwanza, Boniface Mwanjonde, winga, Tariq Mohamed Mkonga aliyetoka JKU SC ya visiwani Zanzibar na kiungo, Saleh Masoud Abdallah ‘Tumbo’ aliyetokea Pamba Jiji. Wachezaji wote watatu, walifikia makubaliano ya kujiunga na timu hiyo na tayari walisaini mikataba ya miaka miwili kwa kila mmoja wao, ingawa dili hizo zilikufa mwishoni, baada ya Fountain Gate…
MTIBWA Sugar 1-3 Singida Black Stars, (SBS) ni matokeo rasmi mchezo wa NBC Premier League uliochezwa mapema leo Februari 22,2026 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma. Wageni Singida Black Stars wamewatuliza wenyeji kwenye mchezo wa leo ambao ulichezwa saa 8:00 mchana katika msako wa pointi tatu muhimu. Magoli ya SBS yamefungwa na Ndumumwe Mossi dakika ya 5, Horso Malanga dakika ya 16 na Kennedy Juma dakika ya 58. Goli pekee la wenyeji Mtibwa Sugar limefungwa na Raizin Hafidhi dakika ya 89. Pointi tatu zimechukuliwa na mgeni. Mara baada ya mchezo huo Horso alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo akikabidhiwa zawadi na…
Barcelona Yatakiwa Kulipa Pauni 26M Kumng’oa Rashford Manchester United Manchester United imeweka wazi kuwa haitashusha ada ya Pauni 26 milioni iliyokubaliwa kwa ajili ya uhamisho wa kudumu wa mshambuliaji wake wa kimataifa wa England, Marcus Rashford, ambaye kwa sasa anaitumikia Barcelona kwa mkopo. Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali kutoka vyombo vya habari vya Uingereza, United “hawako tayari” kujadiliana kuhusu kupunguza bei hiyo na “wanatarajia kupokea ada kamili” ili kukamilisha dili hilo majira ya joto. United Wasisitiza Thamani ya Mchezaji Rashford, mwenye umri wa miaka 28, ameonyesha kiwango kizuri tangu kujiunga na Barcelona, akicheza mechi 34 katika michuano yote, akifunga mabao…
MWENYEKITI wa Simba, Muhtaza Mangungu, amesema uongozi wa klabu hiyo umepokea rasmi maboresho ya Katiba kutoka Serikalini na tayari umeanza kuyafanyia kazi kwa kuzingatia taratibu na sheria za nchi. Kauli hiyo imekuja kufuatia hatua ya Msajili wa Vyama vya Michezo kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuikabidhi Simba Katiba yao iliyofanyiwa marekebisho, huku wakisisitiza klabu kuendelea na mchakato huo kama ilivyoelekezwa. Mangungu ameeleza kuwa uongozi umepokea maelekezo hayo na unahitaji muda wa kuyapitia na kuyatekeleza kwa umakini, ili kuhakikisha kila kipengele kinafanyiwa kazi kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa ndani ya Katiba hiyo pamoja na miongozo ya kisheria. Amesisitiza kuwa…
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuwa linatafuta kampuni moja kwa ajili ya haki za kipekee za ubashiri (exclusive betting rights) katika mechi ya Yanga na Simba utakaochezwa Machi 01, 2026 katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar kuanzia saa 2.15 usiku. Kupitia taarifa yake ya leo Februari 18, 2026, TFF imewakumbusha wadau wote wa michezo ya kubashiri kuwa haki zote za Ligi Kuu ya NBC ni mali ya TFF na washirika wake (partners) na kusisitiza kuwa kampuni yoyote itakayobashiri mechi hiyo na nyingine ambazo ni mali ya TFF itachukuliwa hatua kali za kisheria.
Kocha mkuu wa Azam FC, Florent Ibenge, amekiri kuwa timu yake ilionesha kiwango kizuri katika hatua ya makundi ya CAF Confederation Cup, licha ya kushindwa kufuzu kwenda hatua inayofuata ya mashindano msimu huu. Azam FC walikuwa na nafasi nzuri ya kusonga mbele hadi mchezo wa mwisho wa Kundi D. Waliingia katika mechi za mwisho wakiwa nafasi ya tatu na pointi tisa, sawa na waliokuwa nafasi ya pili, AS Maniema Union. Azam walihitaji ushindi dhidi ya Wydad AC pamoja na matumaini kwamba Maniema wangeshindwa nyumbani dhidi ya Nairobi United ili wafuzu. Hata hivyo, Azam walipoteza kwa mabao 2-0 nchini Morocco wakati…
Mshambuliaji wa kimataifa kutoka Angola, Depu, anaendelea kuthibitisha ubora wake ndani ya kikosi cha Young Africans SC kwa kuwa tegemeo muhimu la mabao tangu alipojiunga na klabu hiyo ya Jangwani. Katika michezo sita aliyocheza hivi karibuni, Depu amehusika moja kwa moja kwenye mabao sita akifunga mabao matano na kutoa pasi moja ya bao takwimu zinazoonyesha ufanisi wake mkubwa katika safu ya ushambuliaji. Ameonyesha makali zaidi katika michezo dhidi ya Kabylie na Dodoma Jiji, akifunga mabao mawili kila timu, huku akiongeza bao moja dhidi ya Mashujaa. Hata hivyo, hakufanikiwa kufunga katika michezo miwili dhidi ya Al Ahly pamoja na mchezo mmoja…
BAADA ya wimbi la wachezaji wa Namungo kuzidi kukosa penalti katika mechi za Ligi Kuu Bara msimu huu, kocha wa kikosi hicho cha ‘Wauaji wa Kusini’, Juma Mgunda amesema hakuna mtu wa moja kwa moja wa kupiga isipokuwa aliyekuwa na utayari. Kauli ya Mgunda inajiri baada ya Cyprian Kipenye kukosa penalti moja kati ya mbili ilizopiga juzi katika kichapo cha mabao 3-2, dhidi ya maafande wa Tanzania Prisons, kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Akizungumza na Soka la Bongo, Mgunda amesema upigaji wa penalti hauna ufundi na ni utayari wa mchezaji mwenyewe, isipokuwa suala hilo kwa sasa anaendelea kulifanyia kazi…
BAADA kuondolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, ameweka wazi malengo yake mapya akiwataka wachezaji wake kuhamishia nguvu zote kwenye mashindano ya Ligi Kuu Tanzania Bara. Barker aliyasema hayo mara baada ya kumalizika kwa dakika 90 za mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Stade Malien, ambapo Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Licha ya ushindi huo, matokeo ya jumla hayakutosha kuiwezesha Simba kusonga mbele, jambo lililowafanya kuaga rasmi mashindano hayo. Barker amesema amefurahishwa na…
Msanii wa Bongo Fleva kutoka Weusi, George Sixtus Mdemu, anayejulikana kwa jina la sanaa G Nako, ameachia video ya wimbo wake mpya unaoitwa “Kula Bia”. Wimbo huu unaelezea maisha ya kijamii na burudani, ukichanganya midundo ya kisasa ya Bongo Fleva na mtindo wa kipekee wa G Nako. Video hiyo inaonyesha mandhari ya sherehe, uhusiano wa marafiki, na burudani ya kila siku, ikilenga kuwafurahisha mashabiki na kushirikisha hisia za kila siku. G Nako amesema katika mahojiano yake: “Wimbo huu ni kuhusu furaha, marafiki, na kusherehekea maisha. Nimeweka nguvu zangu zote kwenye muziki na video hii, na natumai mashabiki watafurahia kila kipande…
Msimamo Kundi la Yanga Klabu Bingwa 2025/2026 Pos Timu P W D L GF GA GD Pts 1 Al Ahly 6 2 4 0 8 3 5 10 2 AS FAR 6 2 3 1 3 2 1 9 3 Young Africans 6 2 2 2 3 4 -1 8 4 Kabylie 6 0 3 3 1 6 -5 3 Pos: Nafasi katika msimamo. Timu: Jina la timu. P: Mechi zilizochezwa. W: Mechi zilizoshinda. D: Mechi zilizotoka sare. L: Mechi zilizopoteza. GF: Mabao yaliyofungwa (Goals For). GA: Mabao waliyofungwa (Goals Against). GD: Tofauti ya mabao (GF – GA). Pts:…
Kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam , Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), imethibitisha kuwa michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika 2027 haitaahirishwa, licha ya kuwepo kwa wasiwasi kuhusiana na maandalizi ya Miundombinu na hali ya hewa ya kisiasa katika nchi waandaaji. Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika Juni-Julai 2027, licha ya wito kutoka kwa Mwenyeji mwenza Kenya kufikiria kuahirishwa kutokana na hatari ya vurugu zinazohusishwa na Uchaguzi uliopangwa kufanyika kwa muda huo huo. CAF imesalia kuwa na msimamo imara, huku timu ya ukaguzi ikiendelea na kazi yake katika nchi tatu za Tanzania,Kenya na Uganda. CAF…
RAIS wa Yanga, Hersi Said amesema mchakato wa ujenzi wa uwanja wa klabu hiyo utakaojengwa Jangwani umefikia hatua nzuri baada ya kupokea mchoro wa kwanza wa mradi huo. Akizungumza mjini Zanzibar katika mwendelezo wa vikao vya Kamati ya Utendaji ya Yanga, Hersi amesema tayari klabu imepata mshirikw katika utekelezaji wa mradi huo, akibainisha mahitaji mahsusi ya uwanja wanaoutaka. “Mradi wa uwanja ambao utajengwa kwenye ardhi ya Jangwani, mita 250, tayari tumetangaza wa kushirikiana naye na tumemwandikia nini hasa tunataka kwenye uwanja huo,” amesema Hersi.Amongeza kuwa kampuni ya GSM imewahakikishia upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kuanza hatua ya kwanza ya…