Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Contact Us
    • Privacy Policy
    Facebook Instagram YouTube
    Chikao Media
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • MAGAZETI YA LEO
    • TETESI ZA SOKA
    • BOXING
    • FORUM
    Chikao Media
    Home » MCHAKATO UJENZI UWANJA WA YANGA WAFIKIA PATAMU
    KITAIFA

    MCHAKATO UJENZI UWANJA WA YANGA WAFIKIA PATAMU

    By AdminFebruary 15, 2026No Comments2 Mins Read
    Share WhatsApp Facebook Twitter Pinterest Telegram Email Copy Link
    Follow Us
    Facebook Instagram YouTube
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email Copy Link

    RAIS wa Yanga, Hersi Said amesema mchakato wa ujenzi wa uwanja wa klabu hiyo utakaojengwa  Jangwani umefikia hatua nzuri baada ya kupokea mchoro wa kwanza wa mradi huo.

    Akizungumza mjini Zanzibar katika mwendelezo wa vikao vya Kamati ya Utendaji ya Yanga, Hersi amesema tayari klabu imepata mshirikw katika utekelezaji wa mradi huo, akibainisha mahitaji mahsusi ya uwanja wanaoutaka.

    “Mradi wa uwanja ambao utajengwa kwenye ardhi ya Jangwani, mita 250, tayari tumetangaza wa kushirikiana naye na tumemwandikia nini hasa tunataka kwenye uwanja huo,” amesema Hersi.Amongeza kuwa kampuni ya GSM  imewahakikishia upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kuanza hatua ya kwanza ya majengo, huku akisisitiza kuwa ndani ya wiki moja  watakutana tena  kamati ya utendaji kujua imefika wapi.

    “Dhamira ni kukusanya fedha kwa ajili ya kuanza utekelezaji. Ndani ya wiki moja tunatarajia hatua ya kwanza ya majengo iwe imekamilika kwenye maandalizi yake,” amesema.

    Hersi amesema kupokewa kwa mchoro wa kwanza ni ishara kuwa ndoto ya muda mrefu ya Wanayanga sasa inakwenda kutimia, kwani mradi huo haujawahi kukamilika tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo 1935.

    “Leo tumepokea mchoro wa kwanza. Hii inakwenda kuwa historia. Mradi huu haujawahi kukamilika tangu kuanzishwa kwa Yanga. Sasa tunaenda kuujenga uwanja wa kihistoria na kutimiza ndoto ya Wanayanga,” amesema kwa msisitizo.

    Amebainisha kuwa baada ya kupatikana kwa mchoro kamili, mkataba utaainisha majukumu ya kila upande, huku wiki ijayo wakitarajia  kujadili gharama za mradi kwenye hatua ya pili.

    Kuhusu ushiriki wa mdhamini, Kampuni ya GSM, Hersi amesema hadi sasa hawajasaini mkataba rasmi wa ujenzi, lakini kampuni hiyo imeshinda zabuni ya kutekeleza mradi huo na imewahakikishia kuwa fedha zipo tayari kwa kuanza kazi pindi taratibu zitakapokamilika.

    “Hatujasaini mkataba na GSM, lakini yeye ameshinda tenda ya ujenzi. Ametuhakikishia kuwa pesa ipo na kila kitu kikikamilika, mradi utaanza mara moja,” amesema.

    “Mkataba utaainisha majukumu. Baada ya kikao cha leo, ndani ya wiki moja mambo yawe yamekalilika, na wiki inayofuata tutakaa kuzungumzia gharama za mradi kwenye hatua ya pili,” amesema.Wiki mbili zilizopita, Yanga ilitangaza kuwa GSM ndiyo mshindi wa zabuni ya ujenzi wa uwanja huo.

    Follow on Facebook Follow on Instagram Follow on YouTube
    Share. WhatsApp Facebook Twitter Pinterest Email Copy Link
    Previous ArticleMichael Carrick Achaguliwa Kocha Bora wa Mwezi Januari 2026
    Next Article Imethibitishwa AFCON 2027 Kufanyika Kama ilivyopangwa, Achana na Tetesi Kuwa Itahairishwa

    Related Posts

    Ujenzi wa Arena, Serikali Yatenga Bil400

    April 3, 2026

    Selemani Mwalimu Yupo Anakuja, Mjiandae

    April 3, 2026

    MSIGWA AELEZA SABABU ZA KUONGEZEKA GHARAMA UWANJA WA ARUSHA

    March 31, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    Bernardo Apewa Thank You Rasmi Man City

    Ujenzi wa Arena, Serikali Yatenga Bil400

    Selemani Mwalimu Yupo Anakuja, Mjiandae

    MSIGWA AELEZA SABABU ZA KUONGEZEKA GHARAMA UWANJA WA ARUSHA

    Neymar amuachia Mungu kutoitwa timu ya Taifa

    “Nimehuzunika,Nimeumia lakini ndoto bado inaishi”Neymar Jr.

    © 2026 CHIKAO MEDIA | All Rights Are Reserved
    • Contact Us
    • Privacy Policy

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.