Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Contact Us
    • Privacy Policy
    Facebook Instagram YouTube
    Chikao Media
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • MAGAZETI YA LEO
    • TETESI ZA SOKA
    • BOXING
    • FORUM
    Chikao Media
    Home ยป RASMI AL NASR YAMCHOMOA KIBU DENIS MSIMBAZI KWA MILIONI 776
    KITAIFA

    RASMI AL NASR YAMCHOMOA KIBU DENIS MSIMBAZI KWA MILIONI 776

    By AdminFebruary 10, 2026No Comments1 Min Read
    Share WhatsApp Facebook Twitter Pinterest Telegram Email Copy Link
    Follow Us
    Facebook Instagram YouTube
    kibu denis
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email Copy Link

    Al Nasr imefikia makubaliano rasmi na Simba ya kumnunua mshambuliaji Kibu Denis baada ya klabu hiyo ya Libya jana kukubaliana maslahi binafsi na nyota huyo wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

    Baada ya awali Simba kuonyesha utayari wa kumuuza Kibu Denis, kilichobakia kilikuwa ni makubaliano binafsi baina ya Al Nasr na Kibu Denis ambayo yalichelewa kufanyika kwa vile mchezaji huyo alikuwa Angola akiitumikia Simba katika mchezo wa raundi ya tano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

    Lakini baada ya nyota huyo kurejea, jana, Jumatatu, Februari 9, 2026, miamba hiyo ya Libya ilikutana na upande wa mchezaji huyo na wakakubaliana rasmi na hivyo mchezaji huyo ataungana na Al Nasr.

    Uhamisho huo utaifanya Simba ivune kiasi cha Dola 300,000 (Sh776 milioni) kwa kukubali kumuachia Kibu ambaye mkataba wake ulibakia miezi mitano ufikie tamati.

    Msimamizi wa Kibu Denis, Carlos Sylivester amesema kuwa taarifa zozote kuhusu mshambuliaji huyo zitatolewa na Simba.

    Ndani ya Al Nasr, Kibu atakutana na nyota wawili aliocheza nao Simba hivi karibuni ambao ni kiungo Fabrice Ngoma na mshambuliaji Steven Mukwala pamoja na Aziz Ki anayecheza Al Ittihad.

    Follow on Facebook Follow on Instagram Follow on YouTube
    Share. WhatsApp Facebook Twitter Pinterest Email Copy Link
    Previous ArticleKOCHA WA SIMBA AICHIMBA MKWARA KMC FC
    Next Article Tanzania Yaiomba China Msaada Kukamilika Miundo Mbinu ya AFCON 2027

    Related Posts

    Ujenzi wa Arena, Serikali Yatenga Bil400

    April 3, 2026

    Selemani Mwalimu Yupo Anakuja, Mjiandae

    April 3, 2026

    MSIGWA AELEZA SABABU ZA KUONGEZEKA GHARAMA UWANJA WA ARUSHA

    March 31, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    Bernardo Apewa Thank You Rasmi Man City

    Ujenzi wa Arena, Serikali Yatenga Bil400

    Selemani Mwalimu Yupo Anakuja, Mjiandae

    MSIGWA AELEZA SABABU ZA KUONGEZEKA GHARAMA UWANJA WA ARUSHA

    Neymar amuachia Mungu kutoitwa timu ya Taifa

    “Nimehuzunika,Nimeumia lakini ndoto bado inaishi”Neymar Jr.

    © 2026 CHIKAO MEDIA | All Rights Are Reserved
    • Contact Us
    • Privacy Policy

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.