Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Contact Us
    • Privacy Policy
    Facebook Instagram YouTube
    Chikao Media
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • MAGAZETI YA LEO
    • TETESI ZA SOKA
    • BOXING
    • FORUM
    Chikao Media
    Home » Simba: Hatujagawa Utamu Mara Mbili kwa Mpinzani Mmoja
    KITAIFA

    Simba: Hatujagawa Utamu Mara Mbili kwa Mpinzani Mmoja

    By AdminFebruary 14, 2026No Comments2 Mins Read
    Share WhatsApp Facebook Twitter Pinterest Telegram Email Copy Link
    Follow Us
    Facebook Instagram YouTube
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email Copy Link

    SIMBA imesema haitakubali kupoteza mara mbili dhidi ya mpinzani mmoja, ikiahidi kupambana hadi mwisho kuhakikisha inapata ushindi dhidi ya Stade Malien katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa Februari 14 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
    Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Msemaji wa Simba, Ahmed Ally, amesema kikosi hicho kimejipanga kurejesha heshima na kuondoa dhana iliyojengeka kwa mashabiki kwamba hakiwezi kushinda kwenye Uwanja wa Mkapa msimu huu.

    “Msimu huu hatujapata ushindi wowote kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa katika Ligi. Matokeo haya yamefanya imani imewapotea Wanasimba ya kupata ushindi kwenye uwanja huo. Sasa tunakwenda kufuta hii dhana, tunakwenda kurudisha imani kwamba kwa Mkapa ni nyumbani kwetu na tunaweza kushinda,” amesema.

    Amesisitiza kuwa ni falsafa ya Simba kutoruhusu kupoteza mara mbili kwa mpinzani yuleyule, akitoa mfano wa michezo ya nyuma dhidi ya Al Ahly na Petro ambapo walijibu mapigo walipokutana tena nyumbani.

    Hata hivyo, Ahmed amekiri kuwa licha ya ushindi wowote utakaopatikana kutokubadili hatma yao ya kufuzu, mchezo huo ni muhimu kwa ajili ya kurejesha hali ya kujiamini kwa wachezaji kuelekea mashindano ya ndani.

    Amewataka Wanasimba kujitokeza kwa wingi uwanjani Februari 14 kuishangilia timu yao licha ya kushindwa kufuzu robo fainali msimu huu.

    “Tukubali kiroho safi kwamba mwaka huu tuliteleza. Hakuna Mwanasimba anatakiwa kubaki nyumbani siku hiyo. Twendeni tukawape ujumbe wachezaji wetu kwamba bado tupo pamoja nao,” amesema.

    Ahmed pia amewataka mashabiki kuepuka kuwatukana viongozi au kuleta mpasuko ndani ya klabu kutokana na matokeo ya msimu huu.

    “Ni kawaida kwenye maisha, kuna muda unafanya vizuri na kuna muda unateleza. Ukishindwa unakaa chini na kujipanga kwa msimu ujao,” alisema.

    Katika hatua nyingine, alitangaza viingilio vya mchezo huo kuwa ni kama ifuatavyo: Mzunguko Sh3,000; VIP C Sh5,000; VIP B Sh10,000; VIP A Sh20,000 na Platinum Sh100,000.

    Kwa mujibu wa Ahmed, wapinzani wao Stade Malien wanatarajiwa kuwasili nchini Februari 13 alfajiri na kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kabla ya mchezo wa Februari 14.

    Follow on Facebook Follow on Instagram Follow on YouTube
    Share. WhatsApp Facebook Twitter Pinterest Email Copy Link
    Previous ArticleViingilio vya Mechi ya Simba vs Stade Malien 14/02/2026
    Next Article Kenya Wafunguka “Tutaunga Mkono AFCON 2027 Endapo Ikihairishwa”

    Related Posts

    Ujenzi wa Arena, Serikali Yatenga Bil400

    April 3, 2026

    Selemani Mwalimu Yupo Anakuja, Mjiandae

    April 3, 2026

    MSIGWA AELEZA SABABU ZA KUONGEZEKA GHARAMA UWANJA WA ARUSHA

    March 31, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    Bernardo Apewa Thank You Rasmi Man City

    Ujenzi wa Arena, Serikali Yatenga Bil400

    Selemani Mwalimu Yupo Anakuja, Mjiandae

    MSIGWA AELEZA SABABU ZA KUONGEZEKA GHARAMA UWANJA WA ARUSHA

    Neymar amuachia Mungu kutoitwa timu ya Taifa

    “Nimehuzunika,Nimeumia lakini ndoto bado inaishi”Neymar Jr.

    © 2026 CHIKAO MEDIA | All Rights Are Reserved
    • Contact Us
    • Privacy Policy

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.