Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Contact Us
    • Privacy Policy
    Facebook Instagram YouTube
    Chikao Media
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • MAGAZETI YA LEO
    • TETESI ZA SOKA
    • BOXING
    • FORUM
    Chikao Media
    Home ยป Ubabe wa Yanga Ndani Wazidi Kuonekana Msimu wa 2025/26
    KITAIFA

    Ubabe wa Yanga Ndani Wazidi Kuonekana Msimu wa 2025/26

    By AdminMarch 12, 2026No Comments2 Mins Read
    Share WhatsApp Facebook Twitter Pinterest Telegram Email Copy Link
    Follow Us
    Facebook Instagram YouTube
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email Copy Link

    Dar Young Africans wanazidi kuchanja mbuga baada ya kuendeleza mwenendo mzuri kwenye michuano ya ndani ikiwemo ligi na FA lakini kwa isivyo bahati walitolewa kwenye michuano ya CAF.

    Inawezekana huu ukawa ni msimu wa Yanga ambao umebeba hisia mchanganyiko fahari ya kutawala ligi ya nyumbani na maumivu ya kuishia njiani kwenye anga la kimataifa. Hata hivyo, picha kubwa inaonyesha timu yenye uthabiti, malengo na mwelekeo wazi wa mafanikio.

    Kwenye ligi kuu yaani (NBC)Tanzania Bara, Yanga wamekuwa mfano wa kuigwa baada ya kuwa na matokeo mazuri, wameonyesha uwezo wa kushinda mechi kwa mitindo tofauti iwe ni kwa mabao mengi au ushindi mwembamba wa kulinda matokeo.

    Nguvu ya Yanga haijaishia tu kwenye ubora wa wachezaji, bali pia katika umoja wa timu. Mshikamano kati ya wachezaji, benchi la ufundi na uongozi umeonekana wazi katika namna wanavyokabiliana na presha ya mechi kubwa. Hili limewafanya waonekane kama timu yenye malengo makubwa na inayojua nini inakitafuta.

    NB: Mbali na kubashiri mechi za kandanda, Meridianbet pia inakupa nafasi ya kucheza michezo ya kasino mtandaoni kama Aviator, Keno, Super Heli, ambapo unaweza kujishindia zawadi kama simu mpya aina ya Samsung A26. PIGA *149*10# AU tembelea tovuti yao meridianbet.co.tz

    Katika michuano ya kimataifa ya CAF Champions League, mambo hayakwenda kama ilivyotarajiwa. Ushindani mkali na changamoto za mechi za ugenini uliwaweka kwenye mazingira magumu, na hatimaye walishindwa kufikia hatua waliyoikusudia. Kutolewa huko kumeumiza, lakini pia kumefungua ukurasa wa kujifunza na kujipanga upya.

    Kwa sasa, nguvu zote zimeelekezwa katika kuhakikisha wanadumisha ubora wao kwenye ligi na kutetea taji lao. Malengo ni wazi  kumaliza msimu wakiwa kileleni na kurejea tena kwenye michuano ya kimataifa wakiwa imara zaidi, wakiwa na uzoefu wa kutosha wa kukabiliana na presha ya mashindano ya juu.

    Timu hiyo ambayo ipo chini ya kocha mkuu Pedro Goncalves wanatarajiwa kuwa na mafanikio msimu huu ya kuchukua makombe makubwa ikiwemo la ligi kuu ya Tanzania kwani ana wachezaji wazuri sana.

    Wachezaji wao muhimu wameendelea kubeba majukumu ipasavyo, huku wakifanya ongezeko la wachezaji msimu huu wakiwemo Allan Okelo, Depu, Damaro, Mwanengo, Buba na wengine wengi.

    Je vijana hawa wa Jangwani wanaweza kutetea taji lao msimu huu?. Au wanaweza wakabeba mataji mangapi msimu huu wa 2025/26. Bashiri hapa na Meridianbet.

    Follow on Facebook Follow on Instagram Follow on YouTube
    Share. WhatsApp Facebook Twitter Pinterest Email Copy Link
    Previous ArticleIran Yatangaza Huenda Isishiriki Kombe la Dunia 2026
    Next Article “Reece James ni beki bora zaidi wa kulia Duniani”-Rosenior.

    Related Posts

    Ujenzi wa Arena, Serikali Yatenga Bil400

    April 3, 2026

    Selemani Mwalimu Yupo Anakuja, Mjiandae

    April 3, 2026

    MSIGWA AELEZA SABABU ZA KUONGEZEKA GHARAMA UWANJA WA ARUSHA

    March 31, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    Ujenzi wa Arena, Serikali Yatenga Bil400

    Selemani Mwalimu Yupo Anakuja, Mjiandae

    MSIGWA AELEZA SABABU ZA KUONGEZEKA GHARAMA UWANJA WA ARUSHA

    Neymar amuachia Mungu kutoitwa timu ya Taifa

    “Nimehuzunika,Nimeumia lakini ndoto bado inaishi”Neymar Jr.

    Makocha wa Simba na Yanga Wagawana Tuzo za Mwezi Februari

    © 2026 CHIKAO MEDIA | All Rights Are Reserved
    • Contact Us
    • Privacy Policy

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.