Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Contact Us
    • Privacy Policy
    Facebook Instagram YouTube
    Chikao Media
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • MAGAZETI YA LEO
    • TETESI ZA SOKA
    • BOXING
    • FORUM
    Chikao Media
    Home » ILE STORI YA CHAMA KWENDA AZAM FC UKWELI HUU HAPA….FEI TOTO BYE BYE?
    KITAIFA

    ILE STORI YA CHAMA KWENDA AZAM FC UKWELI HUU HAPA….FEI TOTO BYE BYE?

    By AdminJuly 22, 2025No Comments2 Mins Read
    Share WhatsApp Facebook Twitter Pinterest Telegram Email Copy Link
    Follow Us
    Facebook Instagram YouTube
    chama
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email Copy Link

    WAKATI Azam FC ikimpigia hesabu aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Clatous Chama ikiwa ni pendekezo pia la kocha wa timu hiyo, Florent Ibenge, kikosi hicho kinakabiliwa na ushindani kutoka kwa Zesco United ya Zambia inayomuhitaji.

    Nyota huyo aliyezichezea timu mbalimbali zikiwemo Ittihad Alexandria SC ya Misri, Lusaka Dynamos FC ya Zambia, Simba ya Tanzania na RS Berkane ya Morocco, kwa sasa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake na Yanga kufikia tamati.

    Chama aliyejiunga na Yanga Julai 1, 2024, kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya kuachana na Simba, inadaiwa ameshindwa pia kuongeza mwingine na mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara, hivyo yupo huru kutafuta changamoto mpya.

    Wakati hayo yakiendelea, chanzo cha ndani kutoka Azam kimesema kuwa Chama ni miongoni mwa nyota wanaohitajika kwa ajili ya kuongeza nguvu, ingawa dili hilo bado halijakamilika na sasa Zesco United imeingilia kati ikimhitaji pia.

    “Baada ya Azam kuona kuna nafasi ya kumpata ilianza mazungumzo haraka na menejimenti yake, wanaamini ni mchezaji mzoefu na mkubwa atakayewasaidia sana hasa katika michuano ya ndani na ile ya kimataifa kwa msimu ujao,” kilisema chanzo hicho.

    Chanzo hicho kilidokeza , Chama anaonekana ni mtu sahihi anayeweza kuvaa viatu vya kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Feisal Salum ‘Fei Toto’, ambaye bado hatima yake ya kubakia au kuondoka kikosini humo haijafahamika hadi sasa.

    “Viongozi wamechoka na suala la Feisal na kinachofanyika kwa sasa wao wapo tayari mkataba wake wa mwaka mmoja uishe ili aondoke bure kuliko kuendelea kumzungumzia yeye kila siku, ndio maana wanamuangalia Chama zaidi,” kilisema chanzo hicho.

    Hata hivyo, wakati Azam ikipiga hesabu hizo, Zesco United ambayo mchezaji huyo aliwahi kuitumikia mwaka 2013 hadi 2017, akitokea Nchanga Rangers FC ya Zambia, inadaiwa pia inamhitaji kumrejesha na mazungumzo yanaendelea vizuri.

    Msimu uliomalizika 2024-2025, Chama amehusika katika mabao tisa ya Ligi Kuu Bara, baada ya kufunga sita na kuasisti matatu, huku akiwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilichotwaa mataji matano msimu huo ambayo ni Kombe la Toyota, Ngao ya Jamii, Kombe la Muungano, Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho (FA).

    Azam FC
    Follow on Facebook Follow on Instagram Follow on YouTube
    Share. WhatsApp Facebook Twitter Pinterest Email Copy Link
    Previous ArticleKOCHA WA MAMELOD SUNDOWN KUULA YANGA….JAMAA ANA MIAKA 34 TU
    Next Article YANGA SC YAMALIZANA NA MASHINE YA MABAO

    Related Posts

    Ujenzi wa Arena, Serikali Yatenga Bil400

    April 3, 2026

    Selemani Mwalimu Yupo Anakuja, Mjiandae

    April 3, 2026

    MSIGWA AELEZA SABABU ZA KUONGEZEKA GHARAMA UWANJA WA ARUSHA

    March 31, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    Bernardo Apewa Thank You Rasmi Man City

    Ujenzi wa Arena, Serikali Yatenga Bil400

    Selemani Mwalimu Yupo Anakuja, Mjiandae

    MSIGWA AELEZA SABABU ZA KUONGEZEKA GHARAMA UWANJA WA ARUSHA

    Neymar amuachia Mungu kutoitwa timu ya Taifa

    “Nimehuzunika,Nimeumia lakini ndoto bado inaishi”Neymar Jr.

    © 2026 CHIKAO MEDIA | All Rights Are Reserved
    • Contact Us
    • Privacy Policy

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.