Klabu ya Azam FC imeendelea na harakati zake za kusaka ubingwa kwa msimu ujao kwa kumsajili rasmi winga hatari Pape Doudou Diallo, raia wa Senegal mwenye umri wa miaka 21. Mchezaji huyo ametambulishwa leo katika viunga vya Azam Complex, Chamazi. Diallo amesaini mkataba wa miaka miwili utakaoendelea hadi Juni 2027, huku Azam ikieleza matumaini makubwa juu ya uwezo wake uwanjani. Historia Fupi: Klabu ya zamani: Generation Foot (Senegal) Kwa mkopo: Msimu uliopita alicheza katika Linguère de Saint-Louis Taji binafsi: Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya Senegal msimu uliopita
Author: Admin
NI majeraha ambayo yalifanya asionyeshe ubora wake akiwa katika uwanja msimu wa 2024/25 na alipata maumivu makubwa kwenye mchezo dhidi ya TaboraUnited alipokomba dakika 10 pekee, Uwanja wa Azam Complex. Ilikuwa ni Novemba 6 2024 zama za Kocha Mkuu, Miguel Gamondi. Anaitwa Aziz Andambilwe alicheza jumla ya mechi tano za ligi akikomba dakika 125, hakufunga wala kutoa pasi ya bao kiungo ambaye alikuwa anacheza nafasi ya beki wakati mwingine. Katika mchezo dhidi ya JKT Tanzania uliochezwa Uwanja wa Azam Complex alikomba dakika 90 na ubao ukasoma Yanga SC 2-0 JKT Tanzania. Ilikuwa ni Oktoba 22 2024, mwamuzi alikuwa Ahmed Arajiga,…
Klabu ya Simba SC imesitisha mchakato wa kumpa mkataba beki wa kushoto Khadim Diaw kutoka Al Hilal na wameweka nguvu kwa Pascal Msindo wa Azam FC na Anthony wa Namungo FC Uamuzi huo umekuja baada ya kocha Fadlu Davids kutoridhishwa na kiwango chake, na Khadim Diaw alikuwa alishakamilisha makubaliano binafsi na Simba SC Diaw ni mchezaji wa Mamelod Sundowns ambaye alikuw anakipiga kwenye klabu ya Al Hilal kwa mkopo.
FIFA imewaondolea Singida Black Stars,adhabu ya kutosajili baada ya kulipa madeni yote ya wachazaji wao watatu. Awali Singida walikumbana na Rungu la FIFA baada ya kushindwa kulipa Stahiki za wachezaji wao watatu ambao ni Mbaraka Hamza,Amade Momade na Manu Bola. Ila kwa sasa Singida wako huru kusajili kwani kila kitu kimewekwa sawa
Kwa mujibu wa taarifa ni kuwa kocha Fadlu amepiga pause baadhi ya sajili kuelekea msimu ujao akiwataka viongozi kutafuta Quality zaidi na kama watakosa basi ndio wachukue hao wa chezaji na miongoni mwa sajili hizo ni pamoja na ya Khadim Diaw na Rodriguez Kossi Kiungo Rodriguez Kossi anakaribia kujiunga na klabu ya Hassania Union Sport Agadir ya nchini Morocco akiwa mchezaji huru Beki Khadim Diaw bado anamkataba wa miaka miwili na Al Hilal na hana ofa nyingine kwa sasa tofauti na hiyo ya Simba Sc’
CHE Malone ndo basi tena ndani ya kikosi cha Simba SC baada ya kupata changamoto mpya nje ya Tanzania hivyo msimu wa 2025/26 hatakuwa ndani ya kikosi cha Simba SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids. Che Malone anatajwa kupata timu nchini Algeria kwa ajili ya changamoto mpya na tayari Simba SC wamempa Thank You beki huyo aliyekuwa chaguo la kwanza kikosi cha Simba SC. Mrithi wa Che Malone ni mchezaji wa kwanza kutambulishwa Simba SC raia wa Afrika Kusini ambaye aliwahi kucheza Mamelod Sundowns anaitwa Rushine De Reuck. Julai 30 2025, Che Malone amekutana na Thank You hivyo hatakuwa…
INAELEZWA kuwa nyota wa zamani wa Yanga SC, Clatous Chama anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Singida, Singida Black Stars inayotumia Uwanja wa Liti. Chama aliwahi kucheza Simba SC kabla ya kuibukia ndani ya Yanga SC msimu wa 2024/25 akiwa mchezaji huru na hakuwa na nafasi kikosi cha kwanza kutokana na uwepo wa Aziz KI. Taarifa zinaeleza kuwa Yanga SC hawana mpango na Chama mara baada ya mkataba wake kuisha hivyo atasajiliwa na Singida Black Stars akiwa mchezaji huru. Chama alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za Azam FC na Zesco United ambapo huko alikuwa anafanya mazoezi licha ya kwamba…
Lamine Yamal pichani na Wazazi wake wote wawili ambao wametengana huku Mama yake akiwa ameolewa tayari, lakini kwasasa wanakutanishwa zaidi na Mtoto wao katika shughuli mbalimbali ikiwemo za maisha yake ya mpira, wawili hao pia walisafiri pamoja na Mtoto wao kwenye Ndege ya kukodi kuelekea nchini China kwa ajili ya tukio la kibiashara la Mtoto wao. Ikumbukwe Mama yake Lamine tayari ana Mtoto mwingine kwenye ndoa yake mpya, huku Mzazi mwenzake akiwa bado anadunda tu Mwarabu wa Morocco. Japo sina maana hiyo na naelewa unachowaza ila sidhani kama inawezekana maana inaonekana ana misimamo sana
Habari mwanafamilia wa SokaLeo Pitia Kurasa za Magazeti ya michezo leo Jumatano ya July 30, 2025
WAKATI jina la kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Feisal Salum likitajwa kuwa miongoni mwa wale ambao wamefuatwa kwenye sanduku la usajili la Simba SC katika kina cha Bahari ya Hindi inaelezwa kuwa jina hilo halipo. Taarifa zinaeleza kuwa jina la Fei limekutana na ugumu mzito kuwa ndani ya Simba SC hivyo jitihada zinaendelea kufanyika mpango ukiwa sawa utaratibu utafuatwa ili jina lake liongezwe katika orodha. Ikumbukwe kwamba Fei ana mkataba wa mwaka mmoja na Azam FC amekuwa akitajwa kuwa katika rada za Simba SC inayonolewa na Kocha Mkuu,Fadlu Davids. Simba SC leo Julai 29 2025 ina jambo lake katika Hotel…
MTAMBO wa mabao ndani ya kikosi cha Simba SC msimu wa 2024/25 kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC Jean Ahoua huenda akaondoka ndani ya Bongo kwenda kupata changamoto mpya. Inaelezwa kuwa kiungo mshambuliaji wa Simba SC raia wa Ivory Coast, Ahoua yupo kwenye rada za Klabu ya JS Kabylie ya nchini Algeria kwa ajili ya msimu ujao wa 2025/26. Habari zinaeleza kuwa kuna mazungumzo ambayo yanaendelea kati ya Simba SC na timu ambayo inamuhitaji mchezaji huyo mwenye uwezo mkubwa kutumia mguu wake wa kulia katika kufunga. Ahoua ni namba moja kwa utupiaji ndani ya ligi alifunga jumla ya…
KIKOSI cha Simba SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids kwa maandalizi ya msimu wa 2025/26 kitaweka kambi nchini Misri. Ikumbukwe kwamba leo Julai 29 2025 Simba SC inatarajiwa kutangaza mdhamini mpya na ratiba nzima ya maandalizi kuelekea msimu wa 2025/26 unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Kuna wachezaji wapya ambao watatambulishwa hivi karibuni ndani ya kikosi cha Simba SC na wengine watauzwa kutokana na kupata ofa kubwa. Miongoni mwa majina ya wachezaji ambao wanatajwa kuwa watauzwa ni Che Malone ambaye ni beki huku kiungo Jean Ahoua naye inaelezwa kuwa kuna timu ambazo zinahitaji saini yake. Julai 30 2025 kikosi cha…
MTENDAJI Mkuu wa Simba SC, Zubeda Sakuru amesema kuwa mkataba ambao wameingia na wadhamini wapya ambao ni BetWay unakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye mchezo wa mpira wa miguu Tanzania kutokana na thamani iliyopo kwenye mkataba huo wa miaka mitatu. “Mkataba ambao tumeingia unakwenda kuleta mapinduzi kwenye mchezo wa soka hapa Tanzania na unakwenda kuongezea nguvu dhamira ya Simba kuwa klabu namba moja barani Afrika. “Udhamini huu ambao thamani yake ni Bilioni 20 kwa miaka mitatu, unaonyesha namna Simba imedhamiria kuleta mabadiliko ya kuwa klabu kubwa,”. Ni Julai 29 2025 Simba SC imetangaza jambo hili kubwa kwa Watanzania na mashabiki wa…
NI kama vile mabosi wa Simba sasa wameamua kujibu kwa vitendo baada ya kuwepo kwa kelele nyingi mtandaoni juu ya kushindwa kufanya usajili na badala yake kutoa ‘thank you’ tu kwa waliokuwa nyota wa timu hiyo, kwa kumshusha beki wa kushoto wa kurithi nafasi ya Mohammed Hussein ‘Tshabalala’. Tshabalala aliyedumu Msimbazi kwa muda wa miaka 11 ameaga rasmi baada ya kumaliza mkataba na inadaiwa ameshamalizana na Yanga kwa ajili ya msimu mpya wa mashindano wa 2025-2026, huku pia beki mwingine wa kushoto, Valentin Nouma naye akipewa ‘thank you’ mapema na klabu hiyo. Hata hivyo, kitu cha kuvutia ni kwamba mabosi…
AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kuwa Fadlu yupo likizo ila anafanya kazi kwa moyo mkubwa akiwa Tanzania. “Katika vitu ambavyo tunapaswa kujivunia kwa hali na mali Wanasimba ni uwepo wa Kocha Mkuu, Fadlu Davids. Yupo likizo lakini alitoka Afrika Kusini na kuelekea Dubai kuongea na Mo. “Kwa sasa Fadlu yupo Tanzania akifuatilia hatua kwa hatua wachezaji atakaowasajili na kufanya mipango ya msimu ujao. Anafanya kazi kwa moyo mkubwa mno katika kutimiza majukumu yake. Wanasimba tunapaswa kujivunia kuwa na kocha huyu,”. Simba SC msimu wa 2024/25 ilikuwa chini ya Fadlu ambaye dakika 180 mbele…
Habari mwanafamilia wa SokaLeo Pitia Kurasa za Magazeti ya michezo leo JUmanne ya July 29, 2025
Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania Marcio Maximo ametambulishwa kama kocha mkuu mpya wa klabu ya KMC FC akichukua mikoba ya Kally Ongala aliyetupiwa virago mwezi Mei kutokana na mwenendo usioridhisha wa klabu hiyo. Maximo (63) raia wa Brazil ambaye pia amewahi kuinoa Young Africans Sc anakumbukwa zaidi kwa kuiwezesha Taifa Stars kufuzu Michuano ya CHAN kwa mara ya kwanza mwaka 2009.
Klabu ya Yanga imetangaza kumuongezea mkataba wa miaka miwili mshambuliaji wao raia wa DR Congo Maxi Mpia Nzengeli wa kuendelea kusalia kwa Mabingwa hao wa Nchi hadi mwaka 2027. Nyota huyo alijiunga na wananchi mwaka 2023 akitokea Union Maniema inayoshiriki ligi kuu ya nyumbani kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mwanza, Julai 28, 2025 – Klabu ya Pamba Jiji FC imetangaza kufikia makubaliano ya kusitisha mkataba na kocha wao mkuu Fred Felix Minziro, baada ya pande zote mbili kuridhiana kuhitimisha ushirikiano wao. Taarifa rasmi ya klabu imethibitisha kuwa hatua hiyo imefikiwa kwa mazungumzo ya amani, bila mvutano wowote, na kwamba uongozi unatoa shukrani kwa Kocha Minziro kwa mchango wake katika maendeleo ya timu hiyo katika kipindi alichokinoa kikosi hicho. Fred Minziro, ambaye pia ni mmoja wa makocha wenye uzoefu mkubwa katika soka la Tanzania, amekuwa na klabu hiyo katika kipindi cha mabadiliko na kujenga kikosi chenye ushindani katika ligi za…