Author: Admin

Bao la dakika ya 89 lililofungwa na beki mahiri Shomari Kapombe limeipa Taifa Stars ushindi wa pili mfululizo katika Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN 2024), baada ya kuichapa Mauritania kwa bao 1-0 katika dimba la Benjamin Mkapa. Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa ulionekana kuelekea sare tasa kabla ya Kapombe kutokea kama shujaa wa Stars kwa kupachika bao safi dakika za lala salama na kuihakikishia Tanzania pointi tatu muhimu. Kwa ushindi huo, Stars inaendelea kuongoza Kundi B kwa alama 6 baada ya michezo miwili, ikiwa katika nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya robo…

Read More

MRITHI wa kitambaa cha unadhoa ndani ya kikosi cha Simba SC kwa sasa anatafutwa mara baada ya beki huyo wa kushoto kutambulishwa Jangwani. Zimbwe Jr alikuwa nahodha wa Simba SC msimu wa 2024/25 mkataba wake ulipogota mwisho hakuongeza kandarasi nyingine hivyo katambulishwa Jangwani akiwa mchezaji huru. Inatajwa kuwa mabosi wa Simba SC na benchi la ufundi linafanyia kazi orodha ya wachezaji waliopo ndani ya Simba SC huku jina la Shomari Kapombe likitajwa kuwa miongoni mwa majina yanayopewa kipaumbele. Mbali na Kapombe, Mzamiru Yassin na Ellie Mpanzu ni miongoni mwa majina ambayo yanatajwa kuwa kwenye hesabu za mastaa hao kupewa hadhi…

Read More

Klabu ya Dodoma Jiji imemsajili kiungo wa Tabora United Mkongomani Nelson Munganga. Munganga amejiunga na kikosi hicho kwa miaka miwili na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa kikosi hicho Moses Mpunga amethibitisha. Munganga ni mchezaji mwingine aliyesajiliwa na kikosi hicho baada ya jana mchana Dodoma Jiji kutangaza kumsajili mlinzi wa kushoto Miraji Abdallah.

Read More

KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Hemedi Selemani, amesema kuwa ana imani kubwa na kikosi kuelekea mchezo unaofuata wa Agosti 6, 2025 dhidi ya Mauritania unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa. Kocha huyo amesisitiza kuwa lengo kuu ni kupata ushindi bila kujali idadi ya mabao kwenye mchezo wa leo unaotarjiwa kuwa na ushindani mkubwa. Suleiman amesema kuwa ushindi ndio jambo la msingi zaidi katika mashindano ndani ya uwanja jambo ambalo wanalitarajiwa baada ya dakika 90 za mchezo. “Naamini sana katika kupata ushindi haijalishi tutafunga magoli mangapi cha msingi ni kupata ushindi. Wachezaji wapo tayari na morali ni…

Read More

Mshambuliaji wa Real Madrid, Kylian Mbappe amesisitiza kwamba ana njaa ya kupata mafanikio makubwa msimu huu. Mbappe ameyasema hayo kupitia chapisho lake kwenye mtandao wake wa Instagram. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alisema: “Msimu mpya. Nina njaa ya kufanya jambo kubwa, Twende sote pamoja, Madridistas. HALA MADRID.” Nahodha huyo wa Ufaransa alijiunga na Real Madrid kutoka Paris Saint-Germain mwaka jana.

Read More

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Ally Samatta ametambulishwa rasmi kuwa mchezaji mpya wa klabu ya Le Havre inayoshiriki Ligi kuu nchini Ufaransa. Samatta anakuwa mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kucheza kwenye mataifa manne 5 Barani Ulaya akianzia Ubeljiji,Uingereza,Uturuki,Ugiriki na Ufaransa.

Read More

Klabu ya Yanga imemtambulisha rasmi aliyekuwa nahodha wa klabu ya Simba Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ kwa mkataba wa miaka 2 hadi mwaka 2027. Tshabalala amejiunga na Yanga baada ya kumaliza mkataba wake na wekundu wa msimbazi alipohudumu kwa takribani miaka 10.

Read More

UONGOZI wa JKT Tanzania umebainisha kuwa wachezaji wao wote muhimu wana mipango nao hivyo itakuwa ngumu kwao kuondoka kwenda kupata changamoto mpya kwa msimu ujao. Ilikuwa inaelezwa kuwa timu zenye maskani yake Kariakoo ikiwa ni Simba SC na Yanga SC zilikuwa zinawania saini ya beki wa JKT Tanzania huku Simba SC ikipiga hesabu kupata saini ya kipa wa JKT Tanzania. Kwa maana hiyo kipa Yacoub Selemani na Wilson Nangu ambaye ni beki bado wapo ndani ya JKT Tanzania kuelekea msimu mpya wa 2025/26 baada ya madili yao kuzuiwa. Nangu na Yacouba ambao wapo katika kambi ya timu ya taifa ya…

Read More

ELLIE Mpanzu, winga chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Fadlu Davids amewasili kambini rasmi Agosti 5 2025 kwa maandalizi ya msimu mpya wa 2025/26. Nyota huyo alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za watani wa jadi wa Simba SC ambao ni Yanga SC kuelekea msimu mpya wa 2025/26. Inaelezwa kuwa alichelewa kambini kutokana na matatizo ya kifamilia jambo ambalo lilimfanya akachelewa kujiunga na Simba SC kambini nchini Misri. Tayari kikosi cha Simba SC kimeanza maandalizi mapema kabla ya ligi kuanza. Ligi inatarajiwa kuanza kushika kasi Septemba 16 2025 ikiwa ni mwanzo wa msimu mpya. Baada ya kuripoti kambini, Mpanzu amekabidhiwa vifaa…

Read More

Mchezaji wa zamani wa Simba sc Mohamed Hussein (Zimbwe Jr), amekerwa na kauli ya msemaji wa Yanga, Ally Kamwe, aliyedai kuwa wachezaji wanaosajiliwa na Simba kuziba pengo lake ni wa kiwango cha ndondo. “Sio vyema kuwashusha hadhi wachezaji wazawa wanaopewa nafasi na klabu kubwa kama Simba SC, Hata mimi nilipojiunga na Simba sikutokea timu kubwa nilitokea Kagera Sugar, Sikuwa na jina kubwa lakini kwa kuaminiwa na kupewa nafasi, nilikuwa na kiwango bora sana, “Kusema wachezaji wanaokuja Simba kuziba nafasi yangu ni wa ndondo ni dharau kubwa, Hata mimi nilipojiunga na Simba sikutoka klabu kubwa. Heshima ya mchezaji hujengwa na kazi…

Read More

BAADA ya kutambulishwa katika Klabu ya USM Algers ya nchini Algeria beki Fondoh Che Malone ameanza mazoezi katika kikosi hicho. Beki huyo anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga ndani ya kikosi cha Simba SC kwenye mechi za ligi ilikuwa Uwanja wa KMC, Mwenge Dar. Katika mchezo huo Che Malone alifungua ukurasa wa mabao kwa kutumia pasi ya kiugo mshambuliaji Jean Ahoua ambaye ni namba moja kwa kufunga mabao mengi akiwa nayo 16 kibindoni. Che Malone ambaye alifungua ukurasa wa mabao kwenye mchezo dhidi ya Tabora United dakika ya 13 kwa pigo la kichwa  wiki hii alitambulishwa USM Algers…

Read More

INAELEZWA kuwa Yanga SC wamefikia makubaliano ya kumuuza mshambuliaji wa mabao ndani ya kikosi hicho ambaye ni mzawa namba moja kufunga mabao mengi msimu wa 2024/25. Ni Clement Mzize ambaye alikuwa chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Miloud Hamdi. Mzize anashikilia rekodi ya kucheza mechi zote 30 za ligi msimu uliopita. Mshambuliaji huyo alifunga jumla ya mabao 14 akiwa anaongoza chati ya wafungaji wazawa. Mshambuliaji namba moja ni Jean Ahoua wa Simba SC ambaye alifunga mabao 16 kibindoni. Taarifa zinaeleza kuwa mezani Yanga SC itavuna Dola 900,000 (Sawa na Sh 2.2Bil) kumuuza Klabu ya klabu ya Al-Sadd SC ya nchini…

Read More

Mshambuliaji wa Slovenia kutoka RB Leipzig, Benjamin Sesko (22), anatumia mbinu za kisiasa katika usajili kwa kuzitumia Newcastle na Manchester United kuzipambanisha ili apate dili bora zaidi. Newcastle wameonyesha nia mpya ya kumsajili beki wa kati wa England, Marc Guehi, kwa ofa ya takriban pauni milioni 40, lakini Crystal Palace wanataka pauni milioni 50 ili kumuachia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. Kocha David Moyes anataka kufanya usajili wa hadi wachezaji sita zaidi kwa ajili ya Everton, ikiwa ni pamoja na viungo wa kati wawili na wachezaji wa pembeni wawili. Tottenham wameambiwa watalazimika kulipa euro milioni 30 (pauni milioni…

Read More

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta ameripotiwa kuwa kwenye hatua za mwisho kujiunga na klabu ya Le Havre AC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Ufaransa (Ligue 1). Samatta ambaye ni nahodha wa timu ya taifa Tanzania ‘Taifa Stars’ amemaliza mkataba na waliokuwa waajiri wake timu ya PAOK Thessaloniki kutoka Ugiriki aliyokuwa aliokuwa akiwatumikia kwa misimu miwili iliyopita. L’Équipe imeripoti kuwa Samatta tayari amewasili nchini Ufaransa kukamilisha dili hilo la kujiunga na klabu hiyo ya Normandy. Baada ya kuweka historia nyingi sasa Captain Diego anaenda kuweka Rekodi nyingine mpya ya kuwa mchezaji wa Kwanza raia wa Tanzania kucheza Ligue 1, ambayo…

Read More

Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally amezungumza kuhusu taarifa zilizoibuka asubuhi ya leo kuhusu mshambuliaji wao raia wa DR Congo Ellie Mpanzu kuwa amegoma kuwasili kambini mpaka sasa na amewazimia simu viongozi wake. Ahmed Ally ameandika ujumbe huku akiwajibu wazushi wa taarifa hizo na kuwataka wamtambulishe kwa sasabu nyota huyo hayupo kambini na wanahisi yupo kwao. “Waliosema Mpanzu harudi Simba ndio wanaohangaika kusema yupo Misri😀😀Waliojibadilisha majina na kujiita Eliiiza ndio wanapambana kutuma watu waandike Mpanzu amewasili kambini Misri leo”. “Yaani ghafla wamekua wasemaji wa kambi yetu.Na sisi tunawaambia mtambulisheni sasa huku kwetu hayupo tunahisi yupo kwenu😀😀”Ameandika…

Read More

SIMBA SC chini ya Kocha Mkuu Fadlu Davids wanaendelea na matizi ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya wa 2025/26. Katika kambi iliyopo Misri wachezaji wapya na wale waliokuwa katika kikosi cha Simba SC iliyogotea nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi wapo kambini. Miongoni mwa wachezaji waliopo ndani ya kikosi cha Simba SC ni Kibu Dennis ambaye huyu alikuwa nchini Marekani wakati wa likizo huku Moussa Camara ambaye ni kipa namba moja naye akiwa yupo kwenye orodha ya wachezaji waliopo katika kikosi. Camara ni kipa namba moja kwa kukusanya hati safi msimu wa 2024/25 alipokusanya jumla ya hati safi 19…

Read More

Je safari hii nani anaweza kuongoza ligi, ambapo wakali wa ubashiri wameweka ODDS kubwa sana. Nani atapokea kijiti cha Liverpool ambao msimu uliopita ndio waliongoza ligi wakiwa na pointi zao 39? Liverpool kuongoza ligi amepewa ODDS 3.00. Ikumbukwe kuwa Jogoo wa Anfield hadi sasa amefanya usajili wa wachezaji wakubwa kabisa akiwemo Frimpong, Wirtz, Ekitike na wengine kibao. Lakini pia haijawaacha wachezaji wao wengi kwenye dirisha hili kubwa la usajili ndio maana Meridianbet imempa nafasi kubwa ya kushinda. Je wewe beti yako utampa Liverpool? Wakati nafasi ya pili ya kuongoza ligi siku ya Christmas inaenda kwa vijana wa Arteta Arsenal ambao msimu uliopita walimaliza…

Read More

YANGA SC mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2025/26 hawapoi kutokana na kasi yao kwenye utambulisho wa wachezaji wapya. Ikumbukwe kwamba msimu wa 2024/25 Yanga SC ilitwaa taji la Ligi Kuu Bara inayodhaminiwa na NBC likiwa ni taji lao la 31. Baada ya mechi 30 walikusanya jumla ya pointi 82 na safu ya ushambuliaji ilifunga jumla ya mabao 83. Ni Agosti 3 2025 Yanga SC ilimtambulisha kiungo, Mohamed Doumbia. Nyota mwenye miaka 26 amejiunga na Yanga SC kutokea FC Slovan Liberec ya Jamuhuri ya Czech. Staa huyo ana uwezo mkubwa wa kupiga mashuti ya mbali na kutengeneza…

Read More