Author: Admin

Mabingwa wa soka la Tanzania, Yanga SC wamepangiwa timu ya Wiliete Benguela ya nchini Angola. Ratiba hiyo ya CAF imetoka leo na Yanga SC wameangukia kwa vigogo hao wa soka la nchini Angola.

Read More

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Azam FC Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ amethibitisha ujio wa kiungo wa zamani wa Simba SC, Sadio Kanoute ambaye anakuja kujiunga na Azam FC. Kiungo huyo raia wa Mali atawasili kesho nchini kwa ajili tataratibu za mwisho za kujiunga na kikosi hicho cha Azam FC ambacho kwa sasa kipo chini ya kocha Florent Ibenge.

Read More

KLABU ya Azam FC ya Tanzania imepangwa kucheza na El Merriekh Bentiu ya Sudan Kusini kwenye hatua za awali michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika. KMKM ikipangwa kucheza dhidi ya AS Port ya Djibouti. Azam FC msimu wa 2024/25 ilikuwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu itakuwa katika Kombe la Shirikisho Afrika. Kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) ambapo Tanzania inawakilishwa na klabu tatu jumla. Klabu mbili kutoka Tanzania bara na moja kutoka Zanzibar. Singida Black Stars ya Tanzania kwenye anga la kimatafa itaanzia ugenini ambapo kwenye mchezo wa awali wa Kombe la Shirikisho Afrika. Ni Rayon…

Read More

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC Yanga SC wanatarajiwa kuelekea Rwanda. Timu hiyo inaenda Rwanda kwa mualiko maalum kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki. Mchezo huo unatarajiwa kuwa dhidi ya kikosi cha Rayon Sports. Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC amesema: “Hivi karibuni tulizindua kampeni ya Tofali la ubingwa. Hii ililenga kuwapa wanachama nafasi ya kuchangia timu yao kwa ajili ya kuipa misuli ya kifedha. “Mahitaji haya ni kwa ajili ya kufanikisha usajili na maandalizi ya kambi ya kabla ya msimu ‘Pre-season’. Ikumbukwe maandalizi ni bora ili kuweza kutimiza malengo yetu ya ubingwa kwa msimu…

Read More

MSHAMBULIAJI mpya wa Simba SC 2025/26 Jonathan Sowah raia wa Ghana ametuma ujumbe kwa mashabiki kwa kubainisha kuwa watafurahi msimu mpya. Nyota huyo yupo kambini nchini Misri chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids. Sowah alitambulishwa ndani ya kikosi cha Simba SC akitokea Singida Black Stars. Msimu wa 2024/25 alifunga jumla ya magoli 13. Katika mabao hayo aliwafunga watani wa jadi Yanga SC kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa KMC Complex. “Mimi Jonathan Sowah ni Simba mweusi. Ninapenda kuwaambia mashabiki wa Simba SC kuwa watafurahi. Kwa kila shabiki ambaye atakuja uwanjani na yule ambaye atakuwa nyumbani hakika atafurahi. “Kuna mengi…

Read More

KAMA unadhani Yanga SC mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara wamemaliza usajili, bado kazi haijaisha kwa kuwa kuna wachezaji wengine wapya bado hawajatambulisha. Ikumbukwe kwamba Yanga SC ni mabingwa mara 31 wa Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC hii ni ligi namba nne kwa ubora Afrika.Ni pointi 82 Yanga SC ilikusanya baada ya mechi 30 mafasi ya pili ipo mikononi mwa Simba SC yenye pointi 78 kibindoni. Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC amesema kuwa bado hawajamaliza usajili kwa msimu wa 2025/26. Tayari Yanga SC imetambulisha wachezaji 9 wapya akiwemo beki wa kushoto Mohamed Hussen Zimbwe Jr, Offen…

Read More

Manchester United na Chelsea wapo kwenye mazungumzo ya kuuziana mchezaji Mu-Argentina Alejandro Garnacho. United inamthaminisha Alejandro mwenye umri wa miaka 21 kwa Pauni milioni 50, ingawa Chelsea wanaamini wanaweza kujadiliana na kumpata kwa bei ya chini zaidi. Garnacho ameambiwa atafute klabu mpya na mabosi wa United na aliondolewa katika ziara ya Marekani na kocha Ruben Amorim. Amekuwa akifanya mazoezi nje ya kikosi cha kwanza tangu kikosi hicho kiliporejea Carrington siku ya Jumanne. Winga huyo wa Argentina ameweka wazi kuwa anachopendelea ni kuhamia Stamford Bridge.

Read More

Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo Agosti 9 2025 inatarajiwa kucheza mchezo wa  Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN 2024). Huo utakuwa ni mchezo wa tatu kwa Tanzania. Ni Tanzania vs Madagascar CHAN 2024 Uwanja wa Mkapa. Mechi mbili zilizopita Tanzania ilipata ushindi kwa kuvuna pointi sita muhimu. Inatarajiwa kukutana na upinzani mkubwa kutoka kwa Madagascar. Timu hizi zote mbili zipo Kundi B ambalo vinara ni Tanzania. Hemed Suleman Kocha Mkuu wa Tanzania amesema kuwa kila mchezo ni muhimu. Kocha huyo alibainisha kuwa hakuna timu ambayo haifikirii kupata ushindi. Licha ya yote…

Read More

Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba amethibitisha kuwa mchezaji wao mpya ameanza kwenye kikosi cha timu yake ya Taifa katika mashindano ya CHAN na ndiye atakayekuwa Nahodha wa Taifa lake. “Mchezaji wetu mpya anaanza kwenye mechi ya Taifa lake na tena ndio nahodha…. Automatic hii timu yetu ya pii kushangilia kwenye CHAN”Ameandika Ahmed Ally. Ikumbukwe klabu ya Simba inatajwa kumalizana na mchezaji wa Mamelodi Sundowns Neo Maema ambaye ndiye Nahodha wa Afrika Kusini kwenye mchezo wa leo dhidi ya Algeria.

Read More

KLABU ya Yanga ipo katika mazungumzo ya mwishoni katika kuipata saini ya winga wa Singida Black Stars, Edmund John ili awe sehemu ya kikosi hicho katika msimu ujao. Inadaiwa makubaliano binafsi kati ya mchezaji na Yanga tayari yamekamilika na mchezaji yupo tayari. Nyota huyo alikuwa tishio katika mchezo wa Nusu Fainali wa Kombe la CRDB dhidi ya Simba. Yanga wamempatia mkataba wa miaka mitatu winga huyo, kilichobakia makubaliano kati ya Yanga na Singida Black Stars yapo hatua za mwishoni kukamilika ili nyota huyo asaini. Tayari Yanga SC ipo kambini kwa maandalizi ya msimu mpya wa 2025/26 wakiwa kwenye mazoezi ya…

Read More

Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kesho Agosti 9 2025 inatarajiwa kucheza mchezo wa Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN 2024). Huo utakuwa ni mchezo wa tatu kwa Tanzania. Ni Tanzania vs Madagascar CHAN 2024 Uwanja wa Mkapa. Mechi mbili zilizopita Tanzania ilipata ushindi kwa kuvuna pointi sita muhimu. Inatarajiwa kukutana na upinzani mkubwa kutoka kwa Madagascar. Timu hizi zote mbili zipo Kundi B ambalo vinara ni Tanzania. Hemed Suleman Kocha Mkuu wa Tanzania amesema kuwa kila mchezo ni muhimu. Kocha huyo alibainisha kuwa hakuna timu ambayo haifikirii kupata ushindi. Licha ya yote…

Read More

Jicho la kiungo mkabaji wa kikosi cha timu ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’ Ahmed Bakari ‘Pipino’ @_ahmed_pipino limevimba baada ya kupigwa kiwiko katika mchezo wa jana wa Stars dhidi ya Mauritania. Pipino alipata jeraha hilo lililomfanya ashindwe kuendelea na mchezo huo na akatolewa na nafasi yake akaingia kiungo mwingine Shekhan Khamis. Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Stars iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Shomary Kapombe.

Read More

MARCIO Maximo, Kocha Mkuu wa KMC ameweka wazi kuwa wanatambua namna ushindani ulivyo ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC hivyo muda wa maandalizi watatengeneza kikosi chenye ushindani. Timu hiyo yenye maskani yake Kinondoni inatumia Uwanja wa KMC Complex kwa mechi za nyumbani tayari ipo kambini Zanzibar kwa maandalizi ya msimu mpya wa 2025/26. Rasmi leo Agosti 7 2025 KMC imemtambulisha mchezaji mpya ambaye atakuwa chini ya benchi la ufundi la Maxime ambaye alikuwa ndani ya Mashujaa msimu wa 2024/25 anaitwa  Ibrahim Nindi . Ibrahim alikuwa sehemu ya kikosi cha Mashujaa msimu uliopita, alikuwa sehemu kikosi cha Timu…

Read More

KOCHA Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids amesema kuwa wamefanya maboresho makubwa kwenye kikosi kwa kupata saini za wachezaji ambao watakuwa na kazi kupambana kwenye mashindano ambayo watashiriki. Simba SC msimu wa 2024/25 ilishiriki Kombe la Shirikisho Afrika na kugotea hatua ya fainali ikiwa nafasi ya pili na bingwa alikuwa RS Berkane. Msimu wa 2025/26 Simba SC itapeperusha bendera kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. Fadlu ameweka wazi kuwa watakuwa kwenye aina tofauti ya mashindano ambayo yanahitaji ushindani mkubwa na aina ya wachezaji waliopo watakuwa na kazi kupambania ushindi. “Unaona kuna wachezaji ambao wamesaini kwenye kikosi. Ni aina ya wachezaji wazuri…

Read More

YANGA SC itavuna kiasi cha shilingi bilioni 3.3 kutokana na kuongeza mahusiano na kampuni ya Haier wakisaini mkataba wa miaka mitatu rasmi Agosti 7 2025 katika Hotel ya Hyatt Regency, Dar. Rais wa Yanga SC, Injinia Hersi Said amesema kuwa wana matumaini makubwa na mkataba huo kuwa ni faida kwa pande zote mbili kutokana na ukubwa wa Yanga SC na ubora wa bidhaa kutoka Haier. “Uhusiano wa Haier na Yanga SC ulikuwa na baraka kubwa. Ni matumaini yetu kuwa mkataba huu mpya utakuja na mafanikio zaidi. Msimu wa kwanza na Haier tulifika fainali ya Shirikisho Afrika. Mkataba huu utakuwa wa…

Read More

Baada ya Manchester United kutoa ofa ya kumhitaji kiungo Carlos Baleba, klabu yake yake Brighton imeweka dau la pauni milioni 100 (zaidi ya Tsh Bilioni 320) kwa kiungo huyo lakini United wanahisi kwamba dili hilo linapaswa kukaribia pauni milioni 70 (zaidi ya Tsh Bilioni 230). Baleba anaripotiwa kuwa tayari kujitolea kusaidia kufanikisha uhamisho huo kwa kuwaomba Brighton kupunguza ada ya uhamisho, Baleba ameripotiwa kutaka kujiunga na Manchester United. Mchezaji anafurahia kuona jinsi hatua hii inayofuata kwa United inavyoendelea kwani Brighton wanajua jinsi ya kuweka thamani kutoka kwa kila mchezaji wanayemuuza.

Read More

Mchezaji wa kimataifa wa Tanzania Rahim Shomary ametambulishwa rasmi kuwa mchezaji mpya wa Ghazl El-Mahalla F.C ya Ligi kuu Misri aktokea KMC FC ya ligi kuu Tanzania. Beki huyo wa kushoto aliyecheza Simba, KMC ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya vijana (Ngorongoro Heroes) atacheza Ligi kuu nchini Misri kuanzia msimu ujao.

Read More