Author: Admin

VINARA wa kundi B Tanzania kesho watakuwa kazini kwenye msako wa pointi tatu dhidi ya Afrika ya Kati mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa. Stars ina uhakika wa kucheza hatua ya robo fainali. Kwenye mechi tatu imekusanya pointi tisa ikipata ushindi kwenye mechi zote muhimu. Ilifungua pazia Agosti 2 2025 kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Burkina Faso, mabao ya Sopu kwa mkwaju wa penati na Mohamed Hussen Zimbwe Jr kwa pigo la kichwa yalitosha kuwapa pointi tatu muhimu. Kwenye mchezo huo ni kiungo Feisal Salum Fei Toto alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo na pointi tatu zilikuwa…

Read More

Leo Alhamisi, kikosi cha Azam FC kikiwa Karatu, mkoani Arusha, kimehitimisha kambi yake ya wiki mbili ya maandalizi ya msimu mpya kwa mtindo wa kipekee – kutembelea Hifadhi ya Ngorongoro. Ziara hiyo imekuwa sehemu ya kujivinjari na kuendeleza utalii wa ndani, ikiwapa wachezaji na benchi la ufundi nafasi ya kufurahia mandhari ya asili na urithi wa kipekee wa Tanzania baada ya mazoezi ya nguvu. Wakiwa na tabasamu na shangwe, kikosi kimejionea moja ya maajabu ya dunia, kikipumzisha akili na miili huku kikijipanga kwa changamoto za msimu ujao.

Read More

Winga wa Manchester United, Jadon Sancho, yuko kwenye hatua za mwisho za kujiunga na AS Roma kwa mkopo wa mwaka mmoja.Kwa mujibu wa taarifa, thamani ya dili hilo inafikia euro milioni 20, dau ambalo AS Roma wanaamini litaivutia Manchester United kukubali. Sancho, ambaye amejiunga na Manchester United katika kipindi kilichopita, amepitia changamoto kubwa za kupata nafasi ya kudumu kikosini. Mara kadhaa ametolewa kwa mkopo ili kuimarisha kiwango chake, lakini bado ameshindwa kujipenyeza kwenye kikosi cha kwanza cha United. Ripoti pia zinaeleza kuwa uhusiano kati ya Sancho na klabu hiyo ulivunjika tangu enzi za kocha Erik Ten Hag, na kilichosalia sasa…

Read More

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi, amemteua mtangazaji wa #AzamTV, Patrick Nyembera kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBRC), baada ya kamati ya awali kumaliza muda wake. Nyembera ataiongoza Kamati hiyo ya muda ya TPBRC, yenye jumla ya wajumbe sita ikiwa na Mwenyekiti na Makamu wake. Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara iliyotolewa leo, Profesa Kabudi ameipa kamati hiyo siku 90 (kuanzia Julai 29 hadi Oktoba 29) kukamilisha marekebisho ya katiba na kuitisha uchaguzi mkuu. Wajumbe wapya walioteuliwa ni: i. Patrick Nyembera(Mwenyekiti) ii. Jackobu Mbuya (Makamu Mwenyekiti iii. Gordon Nsajigwa(Katibu) iV. Shafii Dauda (Mjumbe)…

Read More

Brighton inahitaji Pauni 100 milioni ili kumuuza kiungo wao wa kati Carlos Baleba, 21, baada ya Manchester United kuonyesha nia ya kumsajili. Baleba, aliyesajiliwa kutoka Lille mwaka 2023, amekuwa mhimili muhimu wa safu ya kiungo ya Brighton msimu uliopita akicheza mechi 33, pia alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa klabu hiyo. Hata hivyo, Man United haina mpango wa kutoa kiasi hicho ingawa ofa yao ya kwanza inaweza kufikia Pauni 60 milioni.

Read More

Manchester United wanapanga mpango wa pauni milioni 50 kumnunua kiungo wa kati wa Sporting na Denmark Morten Hjulmand, 26, iwapo watamkosa mchezaji wa kimataifa wa Cameroon mwenye umri wa miaka 21 Carlos Baleba. (Sun) Tottenham wana imani kwamba wameweka pamoja dili la Eberechi Eze, 27, ambalo litawaridhisha Crystal Palace , ambao wanamthamini kiungo wao wa kati wa England kwa pauni milioni 68. (Team Talk) Fulham wanaonyesha nia ya kumnunua mshambuliaji wa Manchester United na Denmark, Rasmus Hojlund, huku AC Milan pia wakifuatilia mpango wa kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (Mirror) Chelsea wanapiga hatua katika juhudi zao za…

Read More

Wachezaji wa klabu ya Chelsea wameamua kutoa sehemu ya bonasi zao za ushindi wa Kombe la Dunia ngazi ya Klabu kwa familia za wachezaji Diogo Jota na André Silva waliofariki kwa ajali ya gari mwezi Julai 3,2025. Chelsea walitwaa taji hilo julai 13 na kuvuna zaidi ya shilingi bilioni 302 za Kitanzania kama zawadi ya ushindi huku wachezaji wakitengewa bilioni 41 za Kitanzania kama bonasi. Wachezaji hao ambao kila mmoja anakadiriwa kupata bonasi ya Bilioni 1 walikubaliana kutoa sehemu ya bonasi hiyo kwa familia ya Jota aliyekuwa nyota wa Liverpool na mdogo wake Andre Silva waliofariki kwa pamoja Nchini Hispania.

Read More

Timu ya Mamelodi Sundowns imemuaga rasmi mchezaji wao, Neo Maema aliyetumikia klabu hiyo kwa muda wa miaka 4. Kwa sasa, Maema yupo kambini na timu ya taifa ya Afrika Kusini kwenye michuano ya CHAN, akisubiri mashindano hayo kumalizika ili ajiunge na kambi ya klabu yake mpya. Duru mbalimbali za habari zimekuwa zikiripoti kiungo huyo yupo mbioni kujiunga na Wekundu wa Msimbazi Simba, kuja kuongeza nguvu kwenye nafasi ya kiungo.

Read More

Mchezaji maarufu wa kimataifa, Paul Pogba, amefanya mazoezi yake ya kwanza rasmi na wenzake wa klabu ya AS Monaco, kufuatia kujiunga kwake na klabu hiyo kutoka ligi kuu ya Ufaransa. Pogba, ambaye amejulikana kwa kiwango chake cha juu na uchezaji wa kipekee, alijiunga na Monaco ikiwa ni sehemu ya mpango wa klabu hiyo kuongeza nguvu katika safu ya kati msimu huu. Katika picha na video zilizotolewa na klabu, Pogba anaonekana akifanya mazoezi ya kihali, akijumuika na wenzake katika mazoezi ya pamoja, akionesha kiwango cha viungo vyake, dribbling, na ufasaha wa kupiga pasi za mbali. Mazoezi haya yamevutia mashabiki wengi ambao…

Read More

MSHAHARA wa kiungo wa Tanzania ambaye anacheza ndani ya kikosi cha Azam FC kinachotumia Uwanja wa Azam Complex kwa mechi za nyumbani unatajwa kuwa tishio kutokana na ukubwa wake na thamani ya kiungo huyo mzawa. Ilikuwa inatajwa kuwa Yanga SC na Simba SC zilikuwa kwenye hesabu za kuwania saini ya kiungo huyo. Simba SC walikuwa wanapewa nafasi kubwa kuipata saini yake jambo ambalo limekwama mazima kutimia. Taarifa zinaeleza kuwa Azam wamempa Feisal hela binafsi ya kusaini mkataba mpya (Sign on fee ya Tsh 800m cash). Mshahara wa Tsh 50m (take home), kwa mwezi hii ni baada ya makato na kodi.…

Read More

Uongozi wa Yanga SC umetoa ufafanuzi kuwa mchango wa Shilingi milioni 100 uliotolewa CCM tarehe 12 Agosti 2025, ulitolewa na GSM Foundation inayosimamiwa na mdhamini wa klabu, Ghalib Said Mohammed, na haukutoka kwenye hela za wanachama au mfuko wa klabu. Yanga pia imesema radhi kwa wanachama na mashabiki kwa sintofahamu iliyotokea kutokana na taarifa hiyo.

Read More

Klabu ya Simba imemtambulisha rasmi mchezaji Naby Camara raia Guinea kuwa mchezaji wao kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Al Waab ya Qatar aliyojiunga nayo akitokea CS Sfaxien ya Tunisia. Camara mwenye umri wa miaka 23 ana uwezo mkubwa wa kucheza kama mlinzi wa kushoto na kiungo mkabaji tayari amejiunga na kambi ya Simba inayoendelea nchini Misri na alikuwepo kwenye kikosi kilichoibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Karhaba SC wikiendi iliyopita.

Read More

Ukiwa muwekezaji mzuri wa kubashiri michezo, basi unatambua kwamba kila nafasi ya kuongeza ushindi unayoipata ni kama dhahabu. Meridianbet, kwa kulitambua hilo inawapa wateja wake fursa ya kipekee kupitia huduma ya Bet Boost, ambayo inaleta mapinduzi ya kuongeza odds na kukuweka hatua moja karibu na ushindi wa kiwango cha juu. Huduma ya Bet Boost imetengenezwa mahususi kwa wabashiri wanaotamani kupata faida kubwa zaidi kuliko odds za kawaida zinazotolewa sokoni. Kwa kutumia kipengele hiki, unaweza kuongeza ukubwa wa odds kwenye mechi uliyochagua, na hivyo kukuwezesha kuongeza zaidi nafasi ya wewe kupata malipo makubwa. Iwe wewe ni shabiki wa soka, mpira wa kikapu, au…

Read More

Manchester City wanafikiria namna ya kuuteka nyara uhamisho wa Chelsea wa kumnunua winga wa RB Leipzig wa Uholanzi Xavi Simons, 22. (Sport) Brighton watahitaji zaidi ya pauni milioni 100 kwa Carlos Baleba baada ya Manchester United kuonyesha nia ya kumnunua kiungo huyo wa kati wa Cameroon mwenye umri wa miaka 21. (Telegraph – subscription required) Mshambulizi wa Denmark Rasmus Hojlund yuko tayari kuondoka Manchester United msimu huu wa joto huku AC Milan ikijaribu kufanya mazungumzo ya mkataba wa mkopo na chaguo la kununua. (Gazzetta dello Sport – In Italian) Manchester City wamemuongeza Maghnes Akliouche wa Monaco kwenye orodha ya wanaolengwa…

Read More

Ofisa Habari wa klabu ya Azam FC, Hasheem Ibwe, amesema moja ya uwekezaji mkubwa wa maana ilioufanya msimu huu ni kumpata, Florent Ibenge, ambaye wana matumaini naye kuwa safari hii atawapeleka kwenye hatua za makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza. Ibwe amesema hayo siku chache baada ya droo ya Kombe la Shirikisho, ambapo timu hiyo imepangwa kuanzia ugenini dhidi ya Al-Merreikh Bentiu ya Sudan Kusini, Septemba 19, kabla ya kurudiana, Septemba 26, mwaka huu jijini Dar es Salaam. Ofisa habari huyo alisema pamoja na ugumu wa mashindano hayo, lakini uwapo wa Ibenge, kocha ambaye amekuwa na…

Read More

Mchezo wa Madagascar na Afrika ya Kati umemalizika kwa Madagascar kushinda 2-0. Masikitiko makubwa ni namna mashabiki wa soka Tanzania hususani Dar es Salaam walivyojikausha kujitokeza viwanjani hususani kwenye mechi za wageni na kuibua sura mpya ya mapenzi ya soka kwa Watanzania kama ambavyo wageni walivyokuwa wanatutazama kwenye mechi za vilabu za kimataifa. Kutojitokeza kwa wingi kwa mashabiki kunatupunguzia credit kuelekea michuano mikubwa zaidi ya Afcon. Jumamosi Taifa Stars inacheza naomba tujitokeze kwa wingi tuje tuweke rekodi ya kumaliza makundu bila kufungwa na kuongoza kundi huku Kenya akijichanganya tuje tumnyoe robo fainali. Binafsi nimenunua tiketi 100 nitazozigawa kwa mashabiki kuunga…

Read More

Klabu ya Royal Charelorioi ya nchini Ubelgiji imetuma ofa ya USD 750,000 (Tsh Bilioni 1.9) kwenda kwenye klabu ya Gor Mahia ya Kenya ili kuinasa saini ya kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo na timu ya Taifa ya Kenya Austin Othiambo. Gor Mahia bado hawaijibu ofa hiyo.Lakini kwa mujibu wa tetesi zinaeleza kuwa huenda miamba hiyo ya Kenya ikamruhusu nyota huyo kuondoka baada ya michuano ya CHAN.

Read More

“Yanga walishataka kumpeleka Clement Mzize huko Singida kwa mkopo na tayari walishamuingiza kwenye Mfumo ‘system’ ya TFF ila ni mimi nikamwambia Nabi usikubali huyo Mtoto aende Singida.” “Walitaka kumtoa wakati hajafanya hata mazoezi na timu kubwa.Hata Marseille walipotuma barua kumtaka, wao wakasema tumpeleke Singida tu maana Wachezaji watapatikana wengine” Mwinyi Zahera, Kocha wa zamani wa Young Africans kuhusu sakata la Mzize alipoihojiwa na Kituo cha ITV

Read More

Everton wametangaza kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Jack Grealish kwa mkopo kutoka Manchester City. Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 29 ataitumikia The Toffees msimu mzima wa 2025/26 na atavaa jezi namba 18. Grealish, ambaye ameshinda mataji makubwa akiwa na City ikiwemo Ligi Kuu mara tatu, Kombe la FA mara mbili, Ligi ya Mabingwa, UEFA Super Cup na Kombe la Dunia la Klabu, anakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa na David Moyes majira haya ya joto baada ya kuwasili kwa Charly Alcaraz, Thierno Barry, Mark Travers, Adam Aznou na Kiernan Dewsbury-Hall. Akihojiwa na Everton Tv, Grealish alisema: “Nimefurahi sana kusaini Everton.…

Read More

Bodi ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) imeipiga Kenya faini ya dola 50,000 za Marekani (sawa na takribani TZS milioni 127.8) kutokana na makosa ya kiusalama yaliyojitokeza katika mchezo dhidi ya Morocco uliofanyika kwenye Uwanja wa Moi, Kasarani. CAF imeonya kuwa iwapo kasoro hizo zitaendelea, mechi zijazo za timu ya taifa ya Kenya zinaweza kuhamishiwa nchini Uganda au Tanzania.

Read More