Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limetangaza kuwa mashabiki wanaokaa eneo la mzunguko siku ya kesho wafike kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa na watapewa tiketi ambazo zimenunuliwa na wadau kwa ajili ya kushuhudia mchezo huo. Mashabiki hao ambao watahitaji kupata tiketi hizo watakiwa kufika katika geti A upande wa chuo cha DUCE na geti B upande wa Uhasibu. “Tupo robo fainali tunakwenda nusu fainali pamoja, njoo Benjamin Mkapa kesho suala la kuingia uwanjani tuachie sisi tayari tumelimaliza kwa wenetu wa Mzunguko, mageti yetu ni A upande wa DUCE na B upande wa Uhasibu”.
Author: Admin
Dahame Beida refa wa kimataifa mwenye Beji ya FIFA toka nchini Mauritania ameteuliwa kuwa Refa wa VAR katika mchezo wa kesho wa dhidi ya Morocco katika michuano ya CHAN. Beida alishawahi kuchezesha mechi kati ya Yanga na Mamelod akakataa goli la Azizi ki lakini pia mechi ya Simba na Berkane akampa kagoma kadi nyekundu.
Kikosi cha wachezaji pamoja na viongozi wa timu ya Taifa ya soka ya Morocco, inayofahamika kama ‘Simba wa Milima ya Atlas’, kimewasili Dar es Salaam kwa maandalizi ya mchezo wa robo fainali ya CHAN 2024 dhidi ya ‘Taifa Stars’ ya Tanzania. Mabingwa hao wa CHAN mara mbili watakutana na Tanzania katika mchezo utakaofanyika Agosti 22 mwaka huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Mashindano hayo ya CHAN 2024 yameandaliwa kwa ushirikiano wa Tanzania, Kenya, na Uganda.
PITIA MAGAZETI YA MICHEZO LEO TAREHE 21 AGOSTI 2025
Klabu ya Manchester United imeripotiwa kumtazama kiungo wa Real Madrid Eduardo Camavinga kuwa mbadala kama watamkosa Carlos Baleba wa Brighton wanayemtazama zaidi kama chaguo la kwanza. Camavinga aliyekosa nafasi ya kuanza Madrid anatazamiwa kwenda kushindania nafasi na Casemiro, Manuel Ugarte na kinda Kobee Mainoo.
Ripoti kutoka nchini Kenya zinadai kuwa baadhi ya mashabiki wa soka nchini humo wameanza zoezi la ununuzi wa tiketi za mchezo wa Tanzania dhidi ya Kenya. Lengo lao ni kuwa siku ya mchezo wa Tanzania dhidi ya Morocco uwanja usiwe na mashabiki kwasababu tiketi zitakuwa zimenunuliwa nyingi na hakuna aliyeingia.
Alexander Isak amevunja ukimya wake kuhusu mgomo wake wa Newcastle United kwa kauli mbaya ambapo anasema imani imepotea baada ya ahadi kuvunjwa. Jana alitoa taarifa ambayo anasema hakuna njia ya kurudi. ‘Nimekaa kimya kwa muda mrefu huku wengine wakizungumza,’ aliandika kwenye akaunti yake ya Instagram. “Ukimya huo umewaruhusu watu kushinikiza toleo lao la matukio, ingawa wanajua haliakisi kile kilichosemwa na kukubaliwa kwa siri. “Ukweli ni kwamba ahadi zilitolewa na klabu imejua msimamo wangu kwa muda mrefu. Kutenda kana kwamba masuala haya yanajitokeza tu ni kupotosha. ‘Ahadi zinapovunjwa na uaminifu unapotea, uhusiano hauwezi kuendelea. Hapo ndipo mambo yanaponihusu sasa hivi na…
WAKATI Tanzania Agosti 16 2025 kwenye mchezo wa CHAN 2024 ikishuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Afrika ya Kati 0-0 Tanzania, kiungo Feisal Salum amebainisha kuwa watapambana katika hatua ya robo fainali kupata matokeo mazuri. Mchezo huo uliopita hatua ya makundi ulikuwa wa kwanza kwa Tanzania kugawaa pointi mojamoja. Katika mechi tatu ambazo zilipita za makundi Tanzania ilishinda zote ikikusanya pointi 9. Baada ya mechi nne, Tanzania inaongoza kundi B ikiwa na pointi 10 itacheza na Morocco hatua ya robo fainali mchezo unaotarajiwa kuchezwa Agosti 22, 2025 Uwanja wa Mkapa. Nyota huyo ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora baada ya…
UONGOZI wa Simba SC umetaja siku rasmi itakayokuwa ni maalumu kwa uzinduzi wa uzi mpya wa timu hiyo kuelekea msimu mpya wa 2025/26 unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC ameweka wazi kuwa uzinduzi wa uzi mpya utakuwa watofauti kidogo kutokana na mpango kazi uliopo. “Jezi za Simba msimu huu tutazindua kwa namna tofauti kidogo, ipo namna ambayo tumezoea jezi huwa zinazinduliwa lakini safari hii sababu tuna mdhamini mpya wa jezi kampuni ya JayRutty akishirikiana na kampuni ya kimataifa ya Diadora tukaamua kufanya kitu kipya chenye mvuto kwa jamii na biashara…
MECHI ya Simba na Yanga inatarajiwa kuchezwa mapema ikiwa ni ufunguzi wa msimu mpya wa 2025/26 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii (Community Shield) itakayowakutanisha Yanga SC na Simba SC, Septemba 16, 2025 jijini Dar. Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limethibitisha kuwa kwa mwaka huu, Ngao ya Jamii itachezwa kwa mchezo mmoja pekee kufuatia mabadiliko ya kanuni yaliyopitishwa na Kamati ya Utendaji. Awali, mashindano haya yalikuwa yakihusisha nusu fainali mbili na kisha fainali. Mabadiliko hayo yamesababishwa na msongamano wa ratiba, ikiwemo Tanzania kuwa mwenyeji wa Fainali za CHAN zitakazomalizika Agosti 30, pamoja na mechi mbili za mchujo za…
Simba kupoteza mchezo wa kirafiki ni faida kubwa sana kwao kwa sababu itamsaidia kocha Fadlu Davids kujua changamoto zilizosalia kwenye timu yake na kuzifanyia kazi. Pia itamsaidia kujua ni eneo gani uwanjani halijakamilika kwa maana ya wachezaji na kumpa room ya yeye kwenda kusajili wachezaji wengine kabla dirisha la usajili halijafungwa. Inamsaidia pia kwenye maswala ya fitness kama wachezaji wake hawajafikia level anayoitaka basi aongeze dozi kwa wachezaji wafikie level anayoitaka. Pia kocha anaepuka kutumia nguvu kubwa ambazo zitawasababishia wachezaji wake uchovu kabla ya msimu husika kuanza hivyo hawawezi kutumia nguvu kubwa kwenye mchezo wa pre season. Hivyo kwa kocha…
Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Ally Mangungu, amesema maandalizi yote ya usajili wa wanachama yamekamilika na kwamba ndani ya miezi sita kuanzia sasa klabu hiyo itaanza rasmi mchakato wa kuwasajili wanachama wake. Mangungu ameeleza kuwa kadi za uanachama za Simba hazitakuwa za kawaida bali zitakuwa na thamani na mfumo maalumu unaotambulika rasmi. Akizungumza hivi karibuni, Mangungu alibainisha kuwa lengo kuu la hatua hiyo ni kuhakikisha klabu inakuwa na wanachama halisi na wanaotambulika kisheria, tofauti na ilivyo sasa ambapo baadhi ya mashabiki hujitambulisha kama wanachama bila kuwa na nyaraka halali. “Kila kitu kipo tayari na mchakato umekamilika,” alisema Mangungu, akisisitiza…
MASTAA wa kikosi cha Yanga SC kinachonolewa na Kocha Mkuu,Romain Folz Agosti 19 2025 walikuwa kwenye mazoezi maalumu katika fukwe za Coco Beach Dar kwa lengo la kusaka pumzi na kuwa imara zaidi. Ikumbukwe kwamba Yanga SC ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika. Msimu wa 2024/25 walikuwa chini ya Kocha Mkuu, Miloud Hamdi ambaye alipewa Thank You na mikoba yake ipo mikononi mwa Folz. Kwenye program ya ufukweni wachezaji walikuwa kwenye kazi kubwa chini ya kocha wa viungo Chyna Mok ambaye aliweka wazi kuwa ni mpango maalumu kuhakikisha kuwa wachezaji wanakuwa…
“Nimeona andiko la kaka yangu Jemedari Said kuzihusu Simba SC na Azam FC kutokutoa matokeo yao ya mechi zao za kirafiki walizocheza. Azam FC walifungwa 2-1 na JKT Tanzania pale Arusha. Simba SC wakafungwa 4-3 na Enpipp pale Misri. Kwangu ni tofauti kidogo. Nasimama na Azam FC na Simba SC waliochagua kukaa kimya na taarifa za matokeo ya mechi zao. Kuna kitu kinaitwa mechi za Indoor. Hizi ni mechi ambazo hazina mashabiki. Hazitakiwi kutoka nje ndio maana zikaitwa Indoor. Makocha wanapenda kuzitumia mechi hizi kwa ajili ya kutazama mbinu zao zinafanyaje kazi. Timu zetu huwa zinacheza sana mechi zenye sura…
Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Gianni Infantino ametuma salama za pongezi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia kwa kuchaguliwa tena kuongoza nafasi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka minne. Kupitia taarifa iliyotolewa leo na TFF imesema Rais Infantino amempongeza pia Makamu wa Rais, pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliochaguliwa katika uchaguzi huo. Aidha,Amemshukuru Rais Karia kwa juhudi, kazi na mchango wake muhimu katika maendeleo ya mpira wa miguu pamoja na kusimamia thamani yake na kumtakia heri na mafanikio.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Dk. Patrice Motsepe ametuma salamu za pongezi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia kwa kuchaguliwa tena katika nafasi hiyo. “Kuchaguliwa kwako tena ni ishara ya imani ya Wanachama wako kwa uongozi wako bora, najivunia sana bidii yako na kujitolea kwa maendeleo na ukuaji wa soka Tanzania,” alisema Dk. Motsepe. Vilevile ameipongeza Kamati ya Utendaji iliyochaguliwa, na amesema CAF itaendelea kusaidia kukuza mpira wa miguu Tanzania na Kanda ya CECAFA (Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati). Uchaguzi wa kupata Kamati mpya…
Mdau maarufu wa mchezo wa mpira wa miguu Nchini Haji Manara amewajibu waandishi wa habari wa Kenya waliosema Taifa Stars wameumaliza mwendo kwenye mashindano ya CHAN baada ya kupangwa na Morocco. “Kwani Sisi Tanzania ni Majirani wa Kenya au Watani zetu ? Au Siku hizi ni Mahasimu wa jadi? Na nani kawaambia wao tayari washafuzu kwa nusu fainali ? “Halaf hii lugha ya kusema ngoja niongee kwa kiswahili ni dharau kuonyesha Wabongo hatujui kingereza. Aliowaambia Englisha ndio Alfa na Omega nani? Pls Acheni hayo mambo ndugu zetu, Sisi ni Wamoja na ni mipaka ya kikoloni iliyotufanya tuwe Mataifa mawili tofauti!!”.…
Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba , Ahmed Ally, amesema wachezaji ambao itawatangaza si kama inamalizia zoezi la usajili, la hasha, bali imeshafanya hivyo na imeshapata vibali pamoja na Hati za Uhamisho wa Kimataifa, ITC. “Hawa tuliowatangaza ambao kila mmoja anawafahamu hawajatosha bado kuna vyuma vitatu hatujavitambulisha, safari hii hatutaki mchezo,” alisema Ahmed. Alisema wameshamaliza usajili wa wachezaji wote wa kigeni kwani mwisho wa usajili kwa nyota hao ilikuwa ni Agosti 15, mwaka huu. “Tumemaliza usajili wa wachezaji wote wa kimataifa, tumepata vibali vyao pamoja na ITC zao na tayari dirisha la usajili la wachezaji wa nje ya…
Nyota wa Brazil na klabu ya Santos Neymar Jr usiku wa kuamkia leo alitoka uwanjani akimwaga machozi baada ya kukumbana na kipigo kikubwa zaidi kwenye maisha yake ya soka klabu yake ikikumbana na kipigo cha magoli 6-0 dhidi ya Vasco da Gama kwenye mchezo wa ligi kuu Nchini humo. Akizungumza baada ya mchezo huo nyota huyo mwenye miaka 33 aliyejiunga na klabu hiyo ya nyumbani kwao mapema mwaka huu amesema amevunjika moyo na uchezaji wa timu yake. “Ninajisikia aibu,nimevunjika moyo kabisa na uchezaji wetu mashabiki wana kila haki ya kuandamana na wakitaka kulaani na kutukana wana haki hiyo” Amesema Neymar…