RASMI Simba SC imemtambulisha mshambuliaji mpya ambaye atakuwa katika kikosi hicho kwa msimu ujao unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ndani ya uwanja. Nyota huyo ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa Singida Black Stars alihudumu Fountain Gate kwa mkopo kisha aliuzwa Wydad Casablanca ya Morocco, anarejea Tanzania katika kikosi cha Simba SC. Atakuwa na uzi wa Simba SC kwa mkopo kwa kuwa ni mali ya Wydad Casablanca ambayo imefikia makubaliano na Simba SC kuhusu mchezaji huyo mzawa. Ikumbukwe kwamba Simba SC kambi yake ilikuwa Misri na kikosi hicho kinatarajiwa kurejea Tanzania leo Agosti 28 2025 kwa maandalizi ya mwisho kuelekea Simba…
Author: Admin
Gwiji wa soka wa Uholanzi, Ruud Gullit amesema tatizo la Manchester United lipo kwenye klabu na si kuhusu wachezaji. Kulingana na gwiji huyo wa soka, tatizo la Manchester United ni Manchester United na si kwa wachezaji. Alisema jinsi klabu imekuwa ikiendeshwa tangu kuondoka kwa Sir Alex Ferguson, ndio tatizo lenyewe. Kwa mujibu wa Gullit wachezaji walioihama klabu hiyo na kujiunga na vilabu vingine ndani ya kipindi hiki, wameenda kufanya vyema katika timu zao mpya, akiwatolea mfano Scott McTominay, [Napoli], Marcus Rashford, [Aston Villa, Barcelona] na Antony, [Real Betis].
Ripoti kutoka nchini Kenya zimesema kuwa Kenya Police FC wamealikwa kumenyana na wababe wa Tanzania, Simba SC katika mchezo wa kirafiki siku ya Simba Day, utakaofanyika Septemba 10, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam. Kenya Police FC ni mabingwa wa ligi kuu nchini Kenya kwa msimu wa 2024/25, ndiyo timu aliyotoka nyota mpya wa Simba Mohammed Bajaber. Klabu hiyo bado haijathibitisha kushiriki, lakini tayari watakuwa nchini Tanzania kwa ajili ya michuano ya CECAFA Kagame Cup 2025, itakayoanza Septemba 2 hadi 15 jijini Dar.
Mchezaji Stella Williams wa Beauties FC ya Namibia, mwenye miaka 47 ameweka historia kwa kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kucheza mechi za kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa ya CAF Kwa ukanda wa COSAFA Stella Williams anayemudu kucheza eneo la kiungo msimu uliopita aliisaidia timu yake Kwa 90% ya mechi zake na kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu ya Namibia ya FNB na kupata nafasi ya kushiriki mashindano hayo ya kusaka tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika. Mchezaji huyo aliifunga magoli mawili Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Twiga Stars’ akiwa na mwaka 2013.
KIKOSI cha Simba leo Agosti 28 kinatarajiwa kuwasili nchini kikitokea Misri ambapo kiliweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya unaotarajiwa kuanza hivi karibuni 2025/2026, huku kukiwa na tetesi za Simba kuandika barua ya kuomba kuto kucheza mchezo wao dhidi ya Yanga. Ikumbukwe ya kwamba tarehe 16 sept kutakuwa na mtanange wa Kariakoo Dabi itakayowakutanisha miamba miwili ya soka kutoka nchini Tanzania, Simba na Yanga ukiwa ni mchezo wa Ngao ya Jamii. Ukiashiria ufunguzi wa Ligi Kuu bara ya NBC, Huku kukiwa na tetesi za Simba kuandika barua kwa TFF kuomba kuto kucheza mchezo huo hiyo ni kutokana na Simba kuwa…
WAKATI kikosi cha Simba SC kikitarajiwa kurejea Tanzania leo Agosti 28 2025 inaelezwa kuwa tayari benchi la ufundi lina jina la mrithi wa mikoba ya Mohamed Hussen Zimbwe Jr ambaye alikuwa nahodha mkuu msimu wa 2024/25. Zimbwe Jr kwa sasa hatakuwa ndani ya Simba SC msimu wa 2025/26 baada ya kupata changamoto mpya ndani ya Yanga SC. Inaelezwa kuwa benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids limechagua jina la Chamou Karabou kuwa nahodha. Chamou Karabou ni beki anatarajiwa kuwa nahodha wa timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids, rai awa Afrika Kusini. Msimu wa 2024/25 hakuwa chaguo…
Akiwa kwenye moja ya mahojiano yake na Sky Sports, aliyekuwa kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson aliwahi kunukuliwa akimtaja Ole Gunnar Solskjaer kuwa mtu hatari zaidi linapokuja suala la ufungaji wa magoli. “Ukiwaweka pamoja wafungaji wangu wakuu (Andy Cole, Eric Cantona, Van Nistelrooy, Rooney), Ruud ndiye aliyefunga magoli mengi zaidi. Lakini mfungaji bora wa asili alikuwa Solskjaer. Van Nistelrooy alifunga magoli mazuri, lakini mengi yalikuwa ‘scabby’ (magoli ya ovyo), magoli ya karibu sana na goli (six-yard box goals). “Andy Cole pia alifunga magoli mazuri, lakini mengi yalikuwa ya karibu, ya kutingishika, ya kugonga mguu, ya ‘jinyakue tu na kuingiza’…
Je unajua kuwa leo hii ni nafasi nzuri ya wewe kuondoka na mapene?. Man U, Fenerbahce, Brighton na wengine kibao wapo kwaaajili ya kuhakikisha unakuwa tajiri. Ni Meridianbet pekee unaweza ondoka na mkwanja. Mechi za kufuzu Uefa leo Club Brugge atakiwasha dhidi ya Glasgow Rangers ambapo kwenye mechi ya kwanza walipokutana mwenyeji aliondoka na ushindi mnono, hivyo leo hii mgeni anataka kufanya Comeback kwani mlima ni 3-1. Je leo hii nani ataondoka na ushindi mkali? Bashiri mechi hii yenye ODDS 1.60 kwa 5.00. Mourinho na vijana wake Fenerbahce Instanbul watakuwa ugenini kukipiga dhidi ya SL Benfica ambao ndio wanapewa nafasi ya kushinda mechi hii ya leo. Ikumbukwe kuwa…
ALIYEKUWA beki wa kushoto wa Yanga SC, Nickson Kibabage tayari amejiunga na Singida Black Stars kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya mara baada ya kuachana na timu hiyo, katika msimu ujao. Beki huyo alikuwa katika kikosi cha Yanga SC msimu wa 2024/25. Alitwaa taji la ligi chini ya Kocha Mkuu Miloud Hamdi ambaye kwa sasa hayupo ndani ya kikosi hicho. Timu hiyo inanolewa na Romain Folz ambaye ni raia wa Ufaransa kwa sasa wapo kwenye maandalizi ya msimu mpya 2025/26. Inaelezwa kuwa taratibu zote za uhamisho wa beki huyo aliyempisha Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ aliyejiunga na Yanga SC kwa mkataba…
WAARABU Wadi Degla SC 0-2 Simba SC ni matokeo kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Agost 26 2025 ikiwa ni maandalizi ya msimu wa 2025/26. Simba SC imeweka kambi Misri na inatarajiwa kurejea Tanzania Agosti 28 2025. Simba SC imecheza jumla ya mechi nne, ikipata ushindi kwenye mechi tatu na kupoteza mchezo mmoja chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids. Nyota Elie Mpanzu aliipa Simba goli la uongozi dakika ya 73 akiwa nje ya 18 mbele ya duara la katikati mwa uwanja. Mpanzu alifunga goli hilo kwa shuti kali ambalo lilizama mazima nyavuni. Wadi Degla walishuhudia dakika 79 nyavu zikitikisika kupitia kwa…
Nahodha wa timu yaTaifa ya wanawake Tanzania ‘Twiga Stars’ Opa Clement ametambulishwa rasmi kuwa mchezaji mpya wa klabu ya SD Eibar ya ligi kuu wanawake nchini Hispania. Opa nahocha wa zamani wa Simba Queens na Besitkas ya Uturuki amejiunga na timu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja hadi June 2026 akitokea timu ya FC Juarez ya nchini Mexico. Opa anakuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi Kuu Hispania.
Mshambuliaji Clement Mzize wa Yanga SC ameboreshewa mkataba wake ambapo mshahara wake inatajwa itakuwa ni milioni 40 kwa mwezi akiwa mchezaji mzawa namba mbili kukunja mshahara mrefu. Namba moja ni Feisal Salum wa Azam FC ambaye inaelezwa kuwa anakunja milioni 50 kwa mwezi. Agosti 27 2025 Yanga SC wametangaza rasmi kuongeza mkataba na mshambuliaji huyo ambaye msimu wa 2024/25 alifunga mabao 14 kwenye ligi. Mzize kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC 2024/25 alicheza mechi 30. Alitwaa ubingwa na kikosi cha Yanga SC ambacho kilikusanya pointi 82. Jina lake lipo kwa wachezaji wat imu ya taifa ya Tanzania iliyoishia robo fainali…
Mabingwa wa ligi kuu wanawake Tanzania, JKT Queens wanaowakilisha Tanzania kwenye michuano rasmi ya kimataifa wamepangwa kundi C kwenye michuano ya kuwania kufuzu michuano ya ligi ya Mabingwa Afrika ukanda wa CECAFA. JKT wamepangwa kundi C wakiwa na timu za Yei Joint Stars Fc ya Sudan Kusini na JKU Princesses FC ya Zanzibar. Makundi mengine ni haya hapa chini
MSHAMBULIAJI wa Yanga SC, Clement Mzize kuna uwezekano mkubwa akabaki ndani ya kikosi hicho kwa msimu wa 2025/26 na atakuwa anakunja mshahara mrefu kwa mwezi. Taarifa zilikuwa zinaeleza kuwa Mzize kuna timu ambazo zinahitaji huduma yake kutoka Ulaya jambo ambalo lilikuwa linasubiriwa ni kuisha kwa mashindano ya CHAN. Wakati mashindano yanaendelea Tanzania imeishia hatua ya robo fainali. Taarifa zinaeleza kuwa Mzize ambaye kwenye ligi alifunga mabao 14 akiwa mshambuliaji mzawa mwenye mabao mengi katika CHAN a2024 alifunga mabao mawili huenda hataondoka kwa ajili ya changamoto mpya atasalia Yanga SC. Mshambuliaji huyo inatajwa kuwa alikaa kikao na viongozi wa Yanga SC…
Klabu ya Bandari ya Kenya imeripotiwa kuwa wageni wa Mabingwa wa Tanzania klabu ya Yanga kwenye kilele cha WIKI YA MWANANCHI sherehe zitakazofanyika Septemba 12, 2025, Mechi itachezwa Benjamin Mkapa. Bandari anayoichezea kipa wa zamani wa Yanga Farouk Shiklao inatarajiwa kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Yanga kwaajili ya kutambulisha wachezaji wapya kwa mashabiki.
Mshambuliaji mpya wa Timu ya Taifa Stars Suleman Mwalimu amewasili jijini Dar es salaam kukamilisha taratibu za kujiunga na klabu ya Simba kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Wydad Athletic. Mwalimu ambaye alikiwasha ligi kuu Tanzania bara akiwa na Singida BS na Fountain Gate atasalia jijini Dar es akiendelea na mazoezini binafsi mpaka pale kikosi cha Simba kitakaporejea nchini kutoka Misri kilipoweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya. Simba itarejea Alhamisi ya Agosti 28 baada ya kukamilisha wiki nne za mazoezi katika kambi waliyokuwa wameiweka Ismailia na Cairo Nchini Misri.
Klabu ya Yanga imeanza mikakati ya kuhakikisha inapata ushindi katika mchezo wake wa Ngao ya Jamii dhidi ya watani zao wa jadi, Simba, unaotarajiwa kupigwa, Septemba 16, mwaka huu, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Makamu wa Rais, Arafat Haji, amesema kuwa mipango na mikakati ya mechi hiyo imeshaanza ambapo lengo ni kupata ushindi ili kuendelea kulihifadhi taji hilo. Alisema kuwa heshima ya Yanga kwa msimu wa 2025/26, itaanza kuwekwa katika mchezo huo. “Tuna kazi tarehe 16, jamaa walitamani ule mfumo ungeendelea, walitamani ungendelea kuchezwa kwa mfumo wa nusu fainali ili watukimbie tena, lakini wanasema Mungu si Athumani, kawaleta,…
Siku ya Simba ni nafasi kubwa ya kuwapa heshima watu waliofanya makubwa ndani ya Simba , tunatambua , tunakumbuka na tunathamini mchango wao , mwaka huu kwenye Simba Day tutawaalika wachezaji wetu wawili wa zamani ambao wamefanya makubwa ndani ya Simba yetu” “Nahodha wetu wa zamani ambaye amedunu Simba kwa miaka 6 , ambaye ametupa makombe 4 na ametupeleka Robo Fainali mara 4 , kwa sasa amestaafu rasmi soka hivyo ni nafasi ya sisi kumpa shukran John Rapahael Bocco” “Lakini siku hiyo hiyo tutaenda kumuaga nahodha wetu mwingine aliyeitumikia Simba kwa miaka 15 , ameondoka mwaka juzi lakini hatukupata nafasi…