Meneja Habari na mawasiliano Klabu ya Yanga ametangaza kauli mbiu mpya kuelekea msimu mpya wa mashindano wa 2025/26 ikiwa ni siku chache kabla ya kuazimisha siku ya mwananchi septemba 12 mwaka huu. “Wanayanga sasa wamevuka level ya kuwa na Slogan za kupeana matumaini, tumekubaliana huu ni msimu wa vitendo na tumegundua watu bado wanataka dozi, kuanzia sasa tunaenda kupiga kichwani tu. “Hiyo ndio slogan yetu, Tukipiga kichwani tunacheza na ufahamu. Mwaka huu ni kichwa tu, tumeweka kabisa nyundo kwa ajili ya wale wanaokaza fuvu” Ally Kamwe .
Author: Admin
Mchambuzi wa soka @mzeewajambia ameandika ujumbe kuhusu kauli ya Kocha Mkuu wa Simba aliyoisema hivi karibuni ya kumuhitaji mchezaji mwingine kwenye eneo lake la ushambuliaji. “Juzi Fadlu Davids aliposema anahitaji xfactor Player mmoja ili Kikosi chake Kikamilike nafikiri hakueleweka Vizuri. Manake watu walianza Kusema Mbona ana Neo Maema,Elie Mpanzu na Bajaber? Ahoua? Lakini Fadlu anafahamu Vigezo vya sasa hivi ili uwe bingwa wa Ligi Kuu unahitaji Kuwa na Kikosi bora zaidi Kuliko Yanga Africa. Yani Kikosi chako Kikiwa sawa na au chini ya Yanga Africa ujue huna chako hapo. Kwasababu ni Ukweli Usiopingika Kwamba Kwenye Ligi Simba Sports anacheza Mechi…
Mourinho ameripotiwa kuingiza zaidi ya Tsh 300 bilioni kutokana na kutimuliwa na vilabu vinapaswa kumlipa fidia wakati wa kuvunja kandarasi mapema. Hadhi yake kama kocha mkuu inalindwa na kipengele cha mkataba kuvunja ina maana huwa anasaini mikataba mirefu na ya hela nyingi. Tangu akiwa klabu tajiri kama Chelsea, Real Madrid na Man United, malipo hayo yamekuwa makubwa. Sogeza kushoto kuona pesa alizolipwa kwa kuvunjiwa mkataba kwenye timu alizopita.
Marc Guehi ni rasmi atasalia Crystal Palace licha ya kufanyika kwa makubaliano ya kujiunga na klabu Liverpool mapema siku ya leo kabla ya Crystal Palace kubadilisha mawazo ya kumuachia baada ya kumkosa mbadala wake. Beki huyo alikamilisha vipimo vya afya baada ya ada ya ofa kukubaliwa lakini dili hilo limekufa rasmi kufuatia kukosekana kwa mchezaji mwingine wa kuziba pengo lake baada ya Palace kumkosa Julio Igor.
Pitia vichwa vya habari kwenye magazeti ya leo septemba 2 2025 na ujipatie nakala yako leo kwa undani wa taarifa za habari. HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO SEPTEMBA 2 2025
Klabu ya Manchester United imekamilisha makubaliano ya kumsajili golikipa Senne Lammens raia wa Ubeljiji akitokea Royal Antwerp FC, huku akitarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano. Lammens mwenye umri wa miaka 23 anatarajiwa kusaini mkataba mpya na mashetani hao wekundu wa old trafford kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili leo Septemba 1, 2025.
Klabu ya Liverpool imekmilisha mazungumzo na klabu ya Newcastle United ili kuinasa saini ya mshambuliaji Alexander Isak ukitarajia kuwa usajili utakaoweka historia kwenye Ligi kuu ya Uingereza. Isak mwenye umri wa miaka 25 siku ya leo atakamilisha taratibu za kuhamia Anfield ikiwa ni pamoja na kufanyiwa vipimo vya afya tayari kwa utambulisho ndani ya kikosi cha Arne Slot. Taarifa zinasema nyota huyo raia wa Sweden amesaini mkataba wa miaka 6 kuitumikia Liverpool hadi mwaka 2031.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro، Nurdin Babu (Kulia) akimkabidhi bendera ya Taifa Kanali Geoffrey Mvula (kushoto) Mwenyekiti wa timu za JKT katika hafla ya kuiga timu ya JKT Queens FC kuelekea kwenye mashindano ya CECAFA، Nairobi nchini Kenya. Hafla hiyo imefanyika mjini Moshi ambapo JKT Queens iliweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo yaliyopangwa kuanza 4 Septemba 2025. JKT Queens imeondoka leo kutoka mjini Moshi 1 Septemba 2025 kuelekea Nairobi، Kenya kushiriki mashindano hayo.
MSIMU mpya wa Kombe la Kagame (Kagame Cup) unaanza kesho Septemba 2, 2025 kwa mechi mbili kuchezwa kwenye uwanja wa Major General Isamuhyo, Dar es Salaam, mechi hizo zikitarajiwa kutangazwa mubashara na kituo cha radio cha Times FM. Times FM imeingia ubia na Baraza la Soka Afrika Mashariki na Kati ( Cecafa) kutangaza mashindano hayo yanayoanza Septemba 2-15 jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Masoko na mawasiliano wa Cecafa, Andrew Jackson Oryada amesema wameingia ubia na Times FM ambayo itatangaza mubashara mechi zote. “Tunafuraha kubwa kuwa mshirika na Times FM, kituo pekee cha radio kinachotangaza michezo hapa nchini Tanzania, tunaamini…
AC Milan wamemsajili Christopher Nkunku kutoka Chelsea kwa mkataba ambao unaweza kufikia pauni milioni 36. Nkunku mwenye umri wa miaka 27 ametia saini mkataba wa miaka 5 na kufanya mauzo ya Chelsea msimu huu kufikia pauni milioni 314. Nkunku anaondoka akiwa amefunga mabao 18 katika mechi 62 tangu asajiliwe kutoka RB Leipzig Juni 2023 kwa Pauni milioni 52.
Klabu ya Chelsea imethibitisha kukamilisha usajili wa winga chipukizi wa Kimataifa wa Argentina, Alejandro Garnacho, akitokea Manchester United kwa ada ya uhamisho ya Euro milioni 46. Garnacho mwenye umri wa miaka 21, amesaini mkataba wa miaka 7 utakaomuweka Stamford Bridge hadi mwezi Juni mwaka 2032. Nyota huyo kijana ambaye ameibukia kwenye kiwango cha juu akiwa Old Trafford, amekuwa mmoja wa wachezaji waliokuwa wakipendwa na mashabiki wa Manchester United kutokana na kasi yake, ujasiri wa kumiliki mpira na uwezo wa kufunga mabao muhimu katika mechi kubwa. Kwa kukamilika kwa dili hili, Chelsea wanaendeleza sera yao ya kusajili wachezaji vijana wenye vipaji…
Kocha wa Manchester United, Ruben Amorim, amesema hajui nini kitatokea kwenye ajira yake wakati wa mapumziko ya kimataifa. Akijibu maswali ya wanahabari jana Ijumaa, kama alikuwa na uhakika wa kutofukuzwa wakati wa mapumziko ya kimataifa, alijibu: “Sijui nini kitatokea” “Matamanio yangu ni kuendelea, lakini sitakuahidi chochote kuhusu siku zijazo itakuwaje” “Lakini mimi ni Kocha wa Manchester United na nadhani hilo halitabadilika” alisema Amorim.
MASHINE za kazi kwa ajili ya msimu mpya wa 2025/26 zimewasili ndani ya kikosi cha Yanga SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Romain Folz. Yanga SC ipo kambini Kigamboni kwa maandalizi ya msimu mpya ambapo mchezo wa ufunguzi ni Ngao ya Jamii unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa dhidi ya Simba SC, Septemba 16 2025. Ni wachezaji sita ambao walikuwa na timu ya taifa ya Tanzania iliyokuwa inashiriki CHAN 2024 na iligotea hatua ya robo fainali kwa kupoteza mchezo wake dhidi ya Morocco uliochezwa Uwanja wa Mkapa. Tayari wachezaji ambao walikuwa kwenye timu ya taifa ikiwa ni Mohamed Hussen, Clement Mzize, Shekhan,…
Klabu Fenerbahce wameamua kumfuta kazi kocha wao Jose Mourinho. Klabu hiyo ya Uturuki imeamua kuachana na Mourinho ikiwa ni siku mbili baada ya klabu hiyo kuondolewa na Benfica katika mchujo wa Ligi ya Mabingwa. Meneja huyo wa zamani wa Chelsea, Manchester United, na Tottenham alijiunga na Fenerbahce msimu wa joto wa 2024, miezi sita baada ya kutimuliwa na Roma. Aliiongoza timu hiyo kumaliza katika nafasi ya pili msimu uliopita lakini akashindwa kupata taji lolote. Fenerbahce ilifungwa 1-0 na Benfica katika mchezo wa mkondo wa pili wa mchujo wa kuwania kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa.
Bodi ya Ligi kuu Tanzana (TPLB) imetangangaza rasmi ratiba ya Ligi Kuu Tanzania bara kwa msimu wa 2025/2026 inayotarajiwa kuanza Septemba 17 2025 na kumalizika May 23 2026. Katika ratiba hiyo, mchezo mkubwa wa dabi ya kariakoo kati ya Simba dhidi ya Yanga mzunguko wa kwanza ukipangwa kuchezwa tarehe 13/12/2025. Katika ratiba hiyo pia mechi za ufunguzi wa Ligi zinazotarajiwa kuchezwa tarehe 17/9/2025 ni pamoja na mchezo wa; KMC vs Dodoma Jiji (KMC) Coastal Union vs TZ Prisons (Mkwakwani) Ratiba imezingatia nafasi za mashindano ya kimataifa kwa ngazi ya klabu na timu za taifa lakini pia mashindano ya ndani kama…
INATAJWA kuwa Simba SC imefanikiwa kumsajili beki wa kati wa Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na Klabu ya JKT Tanzania, Wilson Nangu kwa mkataba wa miaka miwili. Hivyo beki huyo aliyekuwa anatajwa kuwa kwenye rada za Yanga SC huenda msimu mpya wa 2025/26 akawa kwenye uzi wa Simba SC. Nangu amekuwa bora kwenye timu ya JKT Tanzania kwenye eneo la ulinzi jambo ambalo linatajwa kuwa sababuu ya Simba SC kuisaka saini yake kwa ajili ya kuwa naye kikosini. Kikosi cha Simba SC kilikuwa kambini Misri tayari Agosti 29 kimerejea kwenye ardhi ya Tanzania kwa maandalizi ya mechi za…
Msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2025/26 unatarajiwa kuanza rasmi Septemba 17, 2025 kwa michezo miwili ya ufunguzi. KMC FC wataikaribisha Dodoma Jiji kwenye Uwanja wa KMC Complex, Mwenge jijini Dar es Salaam, huku Coastal Union wakifungua pazia lao kwa kuvaana na Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Bodi ya Ligi (TPLB), msimu huu utamalizika Mei 23, 2026, ambapo bingwa mpya wa Ligi Kuu atajulikana. Msimu wa 2025/26 unatarajiwa kuwa na ushindani mkali zaidi, hasa ukizingatia maandalizi makubwa yaliyofanywa na vilabu vikubwa vya Kariakoo, Simba na Yanga, sambamba na Singida FG na…