Author: Admin

Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2025/2026 | Ratiba ya NBC Premier league 2025/2026 Ratiba ya NBC Premier league 2025/2026 Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara TPLB imetangaza rasmi Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2025/2026, msimu mpya unaotarajiwa kuanza Jumatano, Septemba 17, 2025 na kumalizika Jumamosi, Mei 23, 2026. Ratiba hii imetolewa Agosti 29, 2025 na imezingatia kalenda ya FIFA, mashindano ya CAF na michuano ya ndani, jambo linalolenga kuruhusu klabu kushiriki bila migongano ya tarehe. Mchezo wa kwanza utawakutanisha KMC FC dhidi ya Dodoma Jiji FC kwenye uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam, huku mchezo mwingine wa ufunguzi…

Read More

Kikosi Rasmi cha Simba Sc 2025/2026 Wekundu wa Msimbazi Simba SC tayari wamekamilisha usajili wa wachezaji kutoka vilabu mbalimbali ili kuimarisha kikosi chao kuelekea msimu mpya wa 2025/2026. Msimu huu unatarajiwa kuanza kwa kishindo kupitia Kariakoo Derby, ambapo Simba SC watakutana na watani wao wa jadi Yanga SC katika fainali ya Ngao ya Jamii. Simba SC wamejipanga upya kwa kuunganisha wachezaji wenye uzoefu, vipaji vipya, pamoja na nyota waliobaki msimu uliopita, lengo likiwa ni kurejesha ubabe wao kwenye ligi kuu ya NBC na mashindano ya kimataifa ya CAF. Walinda Mlango (Goalkeepers) Moussa Camara Yakoub Suleiman Ali Mabeki (Defenders) Rushine De…

Read More

YAKIWA yamebaki masaa kabla ya tukio la Yanga Day kufanyika, kiungo mpya katika timu hiyo amejipa kazi nyingine ngumu ili awe imara zaidi. Ikumbukwe kwamba kesho Septemba 12, Yanga SC itakuwa na tukio la utambulisho wa wachezaji wapya na wale waliokuwa katika kikosi msimu wa 2024/25. Offen Chikola ambaye huyu ni ingizo jipya akitokea Tabora United ameomba ruhusa kwa kocha wake Mfaransa, Romain Folz ya kutoka kambini na kwenda gmy kufanya mazoezi binafsi. Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya Yanga, kiungo huyo ameomba ruhusa ya kufanya mazoezi muda wa mapumziko kwa ajili ya kujiweka sawa kuelekea msimu…

Read More

MENEJA wa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ali Kamwe ameahidi kuishitua Dunia Keshokutwa katika kilele cha Wiki ya Mwananchi itakayofanyika kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar. Yanga SC chini ya Kocha Mkuu, Romain Folz ambaye ni mrithi wa mikoba ya Miloud Hamdi aliyekiongoza kikosi hicho kutwaa taji la ubingwa msimu wa 2024/25. Ni Wiki ya Mwananchi ambayo inasubiriwa kwa shauku kubwa Septemba 12 2025 na Yanga SC inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na Bandari ikiwa ni mwanzo wa msimu wa 2025/26. Kamwe amesema: “Siku ya Wananchi hamjawahi kuniona kwenye kipaza wala eneo lolote nikifanya vurugu zangu ila mwaka huu nimo.…

Read More

Waziri wa Maji, Jumaa Hamidu Aweso, amewasili katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam akimuwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, kama Mgeni Rasmi katika kilele cha Wiki ya Simba (Simba Day 2025). Katika tukio hilo kubwa linaloendelea hivi sasa, Waziri Aweso ameungana na viongozi wa Simba SC pamoja na maelfu ya mashabiki waliomiminika kushuhudia burudani, utambulisho wa kikosi kipya cha msimu huu na shamrashamra zinazotambulisha heshima na hadhi ya klabu hiyo. Simba Day, ambayo imekuwa ikifanyika kila mwaka, ni sehemu ya utamaduni wa klabu hiyo kongwe barani Afrika, ikileta pamoja wapenzi wa…

Read More

Memphis Depay amekuwa rasmi mfungaji bora wa muda wote wa Uholanzi. Alifikia hatua hii muhimu wiki hii Septemba 7, 2025, wakati wa mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la FIFA dhidi ya Lithuania, ambapo alifunga mara mbili na kuiongoza timu yake kushinda 3-2. Mabao hayo yalimfanya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31 kuvuka rekodi ya awali ya Robin van Persie ya mabao 50 katika timu ya taifa. Bao la kwanza la Depay katika mechi hiyo, dakika ya 11 kutoka kwa krosi ya Cody Gakpo, lilikua bao lake la 51 la kimataifa, na kuvunja rekodi hiyo. Kisha akaongeza jingine…

Read More

Simba itakuwa uwanjani leo Jumatano kwa mara ya kwanza tangu itoke kambini Misri, lakini baada ya mshambuliaji Jonathan Sowah, kuna staa mwingine inaweza kumkosa mbele ya Yanga. Simba itamkosa Sowah kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga, lakini mashabiki wa timu hiyo watamuona mshambuliaji huyo raia wa Ghana kwenye mchezo wa leo wa Tamasha la Simba Day: Baada ya Simba Day leo, Septemba 16, 2025 Simba itakutana na Yanga kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii. Wakati leo Simba ikiadhimisha Tamasha la Simba Day pale Uwanja wa Benjamin Mkapa, taarifa mbaya ni kukosekana kwa kiungo fundi wao mpya Mohammed…

Read More

Je ni nani mchezaji wako bora kwenye wafungaji bora timu za Taifa hapa Afrika. Wachezaji kibao wanaendelea kuweka rekodi zao huku wengine wakiendelea kuzifukuzia rekodi hizo. Wakati huo huo Meridianbet inakukaribisha kutengeneza jamvi lako la ushindi hapa. Mabingwa watetezi wa Afcon 2023, Ivory Coast ambao kwenye michuano ya kufuzu Kombe la Dunia wapo nafasi ya 1 wakiwa na pointi 20, kifupi ni Taifa ambalo linafanya vizuri. Rekodi yao ya ufungaji bora bado inashikiliwa na aliyekuwa mchezaji wa timu ya Chelsea na Galatasaray Didier Drogba ambaye alifunga mabao 63 kwenye mechi 94. Rekodi hiyo kufikiwa inahitaji muda mref kwani anayemfuata ana mabao 24 hivyo inahitajika kazi…

Read More

Kikosi Kamili cha Yanga 2025/26 | Wachezaji Wote wa Yanga Licha ya kuibuka na mafanikio makubwa katika msimu wa 2024/2025, timu ya wananchi Young Africans SC (Yanga SC) imeendelea kuonesha kiu na dhamira ya kutaka kurudia mafanikio hayo kwa kishindo msimu wa 2025/2026. Uongozi wa klabu umefanya maboresho makubwa katika kikosi, wakisajili wachezaji wapya na kuimarisha nafasi muhimu ili kuhakikisha timu inabaki kwenye ubora wake wa ndani na kimataifa. Msimu mpya wa Ligi Kuu Bara pamoja na mashindano ya kimataifa unatarajiwa kuanza rasmi tarehe 17 Septemba 2025, na tayari mashabiki wa Yanga wana shauku kubwa kuona mastaa wao wapya na…

Read More

Kocha Mkuu wa klabu ya Simba Fadlu Davids amesema msimu huu ni wa kushinda makombe baada ya msimu uliopita kutengeneza kikosi chake kwa kiasi kikubwa. Akizungumza na waandishi wa habari kwa ajili ya maandalizi ya tamasha la Simba Day siku ya kesho ambapo watacheza mechi ya Kimataifa ya kirafiki dhidi ya Gormahia Fadlu ameonekana kufurahishwa na usajili mkubwa walioufanya. “Simba SC msimu uliopita tulitengeneza Foundation ila msimu huu ni wa kushinda makombe dirisha la usajili limeshafungwa, nawaamini sana wachezaji wangu wote na nimefurahishwa na kikosi changu. Kama kocha nitafocus na kikosi hiki kutengeneza timu yenye ushindani msimu huu.”- Fadlu Davids.

Read More

Beki wa kati Vedastus Masinde amejiunga rasmi na klabu ya Simba kuwa mchezaji wao mpya akitokea klabu ya TMA ya Championship kwa mkataba wa miaka 2. Masinde ambaye ni mchezaji wa mwisho kutambulishwa na Simba kuelekea msimu ujao ana umri wa miaka 19 na aliwahi kuichezea Biashara United kabla ya TMA.

Read More

Timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’ imeendelea kuweka hai matumaini ya kufuzu kombe la Dunia 2026 (WC 2026) baada ya kushinda mechi yake ya pili mfululizo ikiilaza Msumbiji 4-0 Septemba 5, 2025 kabla ya kuitandika Somalia 2-0. Allan Okello ameendelea kung’ara akiwa na The Cranes baada kutupia tena dhidi ya Somalia kwa mkwaju wa penalti huku Jude Ssemugabi akifunga bao la pili katika dimba la Mandela, Kampala. FT: Uganda 🇺🇬 2-0 🇸🇴 Somalia ⚽ 06’:Okello (P) ⚽ 39’ Ssemugabi FT: Guinea 🇬🇳 0-0 🇩🇿 Algeria FT: Guinea-Bissau 🇬🇼 2-0 🇩🇯 Djibouti FT: Madagascar 🇲🇬 3-1 🇹🇩 Chad FT: Malawi 🇲🇼 2-2 🇱🇷 Liberia MSIMAMO KUNDI G 1- 🇩🇿 Algeria 19pts 2- 🇺🇬 Uganda 15pts 3- 🇲🇿 Msumbiji 15pts 4 – 🇬🇳 Guinea 11pts 5- 🇧🇼 Botswana 9pts 6- 🇸🇴 Somalia 1pt

Read More

Kinda wa Klabu ya Ajax, Aaron Bouwman anaripotiwa kuvivutia vilabu vikubwa duniani. Kwa mujibu wa taarifa, kinda huyo mwenye umri wa miaka 18 anafuatiliwa na Chelsea, Manchester United, Barcelona, ​​Liverpool na Manchester City. Beki huyo wa kati alijiunga na Ajax mwaka 2018 na akacheza kwa mara ya kwanza Jong Ajax (timu ya pili ya Ajax) kwenye msimu wa 2023-24. Baada ya kuwachezea mechi 15, kijana huyo ambaye ana baba Mholanzi na mama Mjamaika, amefuzu kwenye kikosi cha kwanza cha Ajax.

Read More

Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Crecentius Magori, amesema yeye na wenzake wanakwenda kurudisha heshima ya klabu hiyo nchini na kuendelea kuwa ya kutisha na kuogopwa katika soka la Afrika. “Simba ni klabu kubwa sana, ni klabu ambayo haina mfano Tanzania na Afrika Mashariki na Kati. Mimi na mwenzangu hapa mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu, huyu bwana ni rafiki yangu sana, watu wanasema maneno mengi, achana na meno, achana na mambo yote, tunakwenda kufanya kazi kubwa na ya maana kwa ajili ya Simba. “Kama kweli wewe ni Simba, tunashinda wote, tukikwama ni wote, hakuna kusema fulani amekwama. Nawaomba…

Read More

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametoa rai kwa wanamichezo kufanya uchunguzi wa afya zao kwa kuhusisha vipimo vyote muhimu ikiwemo vya moyo, damu na viungo vyote vya mwili ili kuhakikisha usalama wa Afya zao. Ameliomba Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) kuendelea kushirikiana na Taasisi za Afya nchini na kuweka mfumo sahihi wa upimaji wa afya kwa wanamichezo. Dkt. Biteko ametoa rai hiyo Septemba 7, 2025 katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati akifungua rasmi mashindano ya 39 ya SHIMIWI yaliyotanguliwa na maandamano ya watumishi wa umma. Ametaja…

Read More

Kuelekea maadhimisho ya Wiki ya Mwananchi, Klabu ya Yanga imetangaza kuwa siku ya Jumanne katika Makao Makuu yake yaliyopo Jangwani kutafanyika zoezi la uchangiaji damu salama kwa lengo la kusaidia watu wenye changamoto ya upungufu wa damu. Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe, alisema shughuli hiyo itakuwa na umuhimu mkubwa kwa jamii kwani itagusa maisha ya watu wengi wanaohitaji damu hospitalini. “Tutakuwa na mambo mawili. Moja ni kuchangia damu salama kuelekea Wiki ya Mwananchi kwa ajili ya kusaidia kundi kubwa la watu wenye changamoto ya ukosefu wa damu,” alisema Kamwe. Aidha, alibainisha…

Read More

Rais wa klabu ya Yanga Eng.Hersi Said ametangaza kuwa hataondoka ndani ya klabu ya Yanga mpaka akamilishe ahadi aliyowaahidi wanachama wa klabu hiyo ya kujenga uwanja. “Najua nina deni kutoka kwa mashabiki na wanachama wa Yanga SC ambalo ni uwanja, Sisi Yanga ombi letu lilikuwa kuongeza upana na sasa tumebakiza mchakato wa kusubiri hati ya kumiliki eneo kwa mradi wa kujenga uwanja wetu.” – Eng Hersi Said (@caamil_88 ) Rais wa Yanga SC. “Mchakato wa uwanja upo safi, Mfadhili wetu GSM yupo tayari na tunasubiri hati kutoka Wizarani na siwezi kuondoka Yanga mpaka uwanja ujengwe”- Eng. Hersi Said (@caamil_88 )…

Read More

Rais wa Yanga SC Eng. Hersi Said amewataka wanachama wa klabu hiyo kulipia ada kwa kuwa gharama za uendeshaji wa klabu ni kuwa sana. Eng. Hersi amesema moja ya gharama kubwa zinazowagharimu ni juu ya kulipa mishahara huku akisema kwamba kiasi cha pesa kilichotumika kwenye kulipa Mishahara ndani ya msimu uliopita ni shilingi bilioni 7.6. Sambamba na hilo Eng. Hersi amesema msimu wa 2024-2025 wanachama wamechangia Bilioni 1.1 kitu ambacho kwa wingi wao ni kiwango kidogo.

Read More