Author: Admin

SHOMARI Kapombe beki wa Simba SC amebainisha kuwa watajitoa kwa nguvu zote kuzuia makosa kwenye mchezo dhidi ya Yanga SC ili wasifungwe. Mchezo wa funga kazi msimu wa 2024/25 kwa wababe hawa wawili ulichezwa Juni 25 2025 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga SC 2-0 Simba SC, mabao ya Pacome na Mzize yaliwapa pointi tatu Yanga SC. Leo Septemba 16 2025 unakwenda kuchezwa mchezo wa kwanza ikiwa ni kufungua pazi la Ligi Kuu Tanzania Bara 2025/26 inayotarajiwa kuanza rasmi Septemba 17 2025 na mabingwa watetezi wakiwa ni Yanga SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Romain Folz.…

Read More

JOTO la Kariakoo Dabi linazidi kupanda kwa kasi ambapo watani hawa wa jadi wanatarajiwa kukutana Uwanja wa Mkapa, Septemba 16 2025 katika mchezo wa fainali. Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, Cliford Ndimbo ametaja orodha ya waamuzi ambao watakuwa kwenye mchezo huo muhimu wa ufunguzi wa msimu mpya wa 2025/26. Ikumbukwe kwamba waamuzi hao watakabidhiwa vifaa vya kazi kutoka JustFit ambao wamebainisha kuwa watatoa na mipira maalumu kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara. Hawa hapa waamuzi wa  Kariakoo Dabi, Septemba 16 2025, Ngao ya Jamii namna hii:-Mwamuzi wa kati ni Ahmed Arajiga, mwamuzi msaidizi ni Mohamed…

Read More

Mwanariadha Alphonce Felix Simbu ashinda mbio za riadha za dunia ambazo zinafanyika jijini Tokyo, nchini Japani na kumshinda mpinzani wake kwa tofauti ya sekunde 0.03 ambaye ni mwanariadha kutoka Ujerumani Amanol Petros. Alphone Simbu ameshinda mbio za dunia kwa kukimbia kwa saa 2:09:48 na kufanikiwa kupata medali ya kwanza ya dhahabu kwa Tanzania katika mashindano ya dunia ya Tokyo 2025 .

Read More

Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davids amethibitisha kuwa siku ya kesho watawakosa wachezaji wawili katika mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Yanga wachezaji hao ni Mohamed Bajaber na Alassane Kante. “Bajaber ana majeraha, Allasane Kante naye pia aliumia kwenye pre season hivyo hao wawili wataukosa mchezo wa Yanga lakini Semfuko naye alikuwa ana majeraha japo amerejea mazoezini sasa hivyo yeye anaweza kuwepo kwenye mchezo huo ” – Fadlu Davids, Kocha Simba SC.

Read More

Staa wa muziki wa bongefleva Mbosso Khan amewashukuru mashabiki,wanachama na viongozi wa Simba kwa kupata nafasi ya kutumbuiza kwenye tamasha la Simba Day huku akiweka wazi almanusura apoteze uhai wake. “Barua Kwa Uongozi na Mashabiki Wa Simba Sports Club @simbasctanzania Asanteni Sana Kwa kuniamini na kwa kunipa nafasi hii adhimu ambayo mngeweza kumpa mtu yoyote mumtakae na badala yake mkanichagua mimi kuwa headliner wa tamasha hili kubwa la kihistoria SIMBA DAY. Kwangu mimi hili ni tamasha langu kubwa la kwanza kuwahi kulifanya la uwanjani linalohusiana na mpira wa miguu katika maisha yangu ya mziki , ndo maana nilichagua kufanya kila…

Read More

Kocha Mkuu wa Simba amezungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa kesho wa dabi ya kariakoo huku akiweka wazi hawana presha ya mchezo huo ila Yanga ndiyo wenye presha. “Sisi tuna faida ya kuwa na benchi lilelile la ufundi lakini tuna wachezaji wapya ambao tunao kwa wiki kama tatu hadi nne na tumekuwa na mazoezi ya pamoja kwa siku chache na waliopo CHAN hivyo naamini tuko vizuri. Lakini presha kubwa ipo kwa Yanga kwasababu wana makocha wapya ambao hawajawahi kucheza hii dabi lakini pia presha ya muendelezo wa matokeo yao lakini kwetu hatuna presha kwasababu benchi ni lile lile…

Read More

Yamebaki masaa kabla ya mchezo wa Kariakoo Dabi kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 16 2025 ikiwa ni mchezo wa Ngao ya Jamii. Ikumbukwe kwamba msimu wa 2024/25 Yanga SC walitwaa taji hilo kwa ushindi kwenye mchezo wa fainali mbele ya Azam FC katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa. Simba SC iligotea kuwa mshindi wa tatu kwa kuwa mashindano hayo yaliendeshwa kwa kuanzia hatua ya nusu fainali.Kwenye hatua ya nusu fainali Simba SC ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga SC bao la ushindi likifungwa na Maxi Nzengeli. Tayari viingilio vimetangazwa na Shirikisho la Soka Tanzania kuelekea kwenye mchezo huo…

Read More

JEAN Ahoua kiungo mshambuliaji namba moja wa Simba SC kwenye mtihani mwingine ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids itakuwa Septemba 16 2025. Ahoua ni namba moja kwenye utengenezaji mipango ndani ya kikosi hicho, msimu wa 2024/25 alitengeneza jumla ya pasi 9 za mabao. Mbali na kutengeneza pasi hizo 9 za mabao alifunga jumla ya mabao 16 akiwa ni mshambuliaji namba moja kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC. Katika pasi na mabao aliyofunga alikwama kufunga mbele ya watani zao wa jadi Yanga SC na alikwama kutengeneza pasi mbele ya watani zake hao jambo ambalo linamfanya…

Read More

Mohmaed Hussen Zimbwe Jr beki wa kushoto ndani ya kikosi cha Yanga SC kinachonolewa na Kocha Mkuu Romain Folz amesema kuwa anafurahia mapokezi makubwa aliyoyapata kutoka kwa mashabiki anamini watajituma kufanya vizuri ndani ya uwanja. Ipo wazi kwamba Zimbwe Jr ni miongoni mwa wachezaji waliopokewa kwa shangwe kubwa ndani ya Yanga SC katika utambulisho wake, beki huyo 2024/25 alikuwa katika kikosi cha Simba SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids. “Tamasha limeenda vizuri kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Mashabiki wamejitokeza wengi na hii ni ishara kuwa huu ni mwanzo mzuri kuelekea katika msimu mpya. “Kuna vipaji vingi ambavyo vipo ndani ya…

Read More

YANGA SC vs Simba SC wababe hawa wawili wanatarajiwa kuwa kwenye kazi ya kusaka ushindi ndani ya Uwanja Septemba 16 2025. Zimebaki siku tatu kwa watani hawa wa jadi kupambania taji la Ngao ya Jamii ikiwa ni mchezo rasmi wa ufunguzi wa msimu mpya wa 2025/26. Ikumbukwe kwamba msimu wa 2024/25 taji la Ngao ya Jamii lilichukuliwa na Yanga SC iliyopata ushindi kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Mkapa. Simba SC iliondolewa na Yanga SC katika hatua ya nusu fainali kwa kufungwa bao 1-0 na mtupiaji alikuwa ni Maxi Nzengeli alimtungua kipa namba moja Moussa Camara…

Read More

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta anasema mazungumzo ya kandarasi za Bukayo Saka na William Saliba yanakwenda vizuri. Wachezaji hao wawili muhimu wa Arsenal mikataba yao inategemewa kutamatika 2027, na sasa Washika Bunduki hao wa jiji la London wapo kwenye majadiliano mazito na wachezaji hao ili waweze kuwaongezea mikataba. “Nadhani jambo zuri ni kwamba wachezaji wanataka kubaki hapa na wanataka kuwa sehemu kubwa ya historia ya klabu hii katika miaka michache ijayo na hilo ni jambo jema.” alisema Arteta

Read More

Pep Guardiola amepinga madai ya kocha wa Liverpool Arne Slot kwamba mchezaji wake mpya Alexander Isak ya kwamba ndiye mshambuliaji bora zaidi duniani, huku akisema anamuweka mshambuliaji wa Manchester City Erling Haaland juu kidogo ya Isak. Guardiola aliongea hayo jana Ijumaa alipokuwa akijibu maswali ya waandishi waliotaka kujua mtazamo wake kwenye kuwalinganisha Haaland dhidi ya Isak. “Isak ni mchezaji wa kipekee lakini ukiniuliza kuhusu Haaland naona yuko juu kidogo ya Isak” alisema kocha huyo wa kihispania.

Read More

Kila msimu wa mpira wa miguu unapokaribia kuanza nchini Tanzania, macho na masikio ya mashabiki huzamia kwenye matamasha mawili makubwa Simba Day na Yanga Day (Siku ya Wananchi). Matamasha haya yamekuwa zaidi ya hafla za michezo, yamegeuka kuwa majukwaa ya burudani, biashara na ubunifu huku kila klabu ikijitahidi kuonyesha ubora na kuwavutia mashabiki wake. Simba Day 2025 iliyofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam na kwa mara nyingine tena ilithibitisha heshima yake kama waanzilishi wa matamasha haya ya vilabu nchini. Mashabiki walijitokeza kwa wingi mapema asubuhi, na kufurika uwanjani hadi tiketi zikaisha. Burudani kali kutoka kwa wasanii…

Read More

Kocha wa Simba SC ameweka wazi msimamo na mikakati ya kikosi chake kuelekea mchezo muhimu wa ngao ya jamii dhidi ya Young Africans (Yanga). Akizungumza baada ya mapumziko mafupi, kocha huyo amesema kikosi chake kimeanza maandalizi mapya kwa mchezo huo wa heshima kabla ya kuelekeza nguvu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. “Tumepumzika jana na kisha leo tunaanza maandalizi ya mechi ya Yanga. Huo ni mtihani mkubwa, ni fainali, ni mechi ya heshima. Baada ya hapo tutaelekeza nguvu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. Tutafanya uchambuzi, mikutano binafsi na ya pamoja, ili kuweka mambo sawa,” alisema kocha. Aidha, amesisitiza umuhimu wa mashabiki…

Read More

Mchezaji wa zamani Nigeria Mikêl Obi ameunga mkono suala la nyota wa zamani wa taifa hilo Jay Jay Okocha kuhitaji kuwa Rais wa shirikisho la soka nchini humo. Mikêl Obi “Ninajiunga na watu wa nigeria walio ughaibuni kumtawaza bwana, Austin Jãy Okōcha kama mwenyekiti mpya wa Ñff, nataka turudi nyumbani na kufanyia kazi masuala yetu ya soka kwa ujumla” “Tutaleta wawekezaji kuwekeza katika soka letu, kuifanya iwe ya ushindani, kuweka kiwango cha ligi ya taifa, nitakuwa mtu mwenye furaha zaidi kuona bwana Jãy akifanikiwa katika safari hii” alisema Mikel kupitia kipindi chake cha mtandaoni Obi one Jumatano tarehe 10 Septemba…

Read More

Kiungo mshambuliaji wa Azam FC na timu ya Taifa ya Tanzania, Feisal Salum maarufu kama FeiToto, ameongeza kandarasi yake ya kuitumikia klabu hiyo kwa msimu mmoja zaidi. Hatua hiyo inamaanisha kuwa FeiToto atasalia ndani ya viunga vya Chamazi hadi mwaka 2027. FeiToto, ambaye ni mmoja wa viungo bora nchini, ameendelea kuwa nguzo muhimu katika kikosi cha Azam FC kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutawala eneo la kiungo na kutoa msaada katika safu ya mashambulizi. Uamuzi wa Azam kumwekea mezani kandarasi mpya unatajwa kuwa ni mkakati wa kuhakikisha nyota huyo anaendelea kuisaidia timu katika harakati zake za kutafuta mataji ya…

Read More

Klabu ya Yanga imetangaza kuingia mkataba na kampuni ya BlackBird kutokea Rotterdam Uholanzi kwa ajili ya teknolojia ya Akili Mnemba ‘Artificial Intelligence’ (AI), mfumo ambao utaisaidia klabu hiyo kukusanya taarifa za wachezaji wake. Rais wa klabu hiyo Eng. Hersi amesema klabu hiyo imeingia mkataba huo siku ya leo Septemba 11, 2025 huku akiweka wazi kuwa Young Africans ndio klabu ya kwanza Afrika kuingia mkataba huo. “Leo tumeingia mkataba na kampuni ya BlackBird kutokea pale Rotterdam Uholanzi. Mkataba huu ni kwa ajili ya teknolojia ya Artificial Intelligence (AI). Mfumo huu utatusaidia kukusanya taarifa za wachezaji wetu. Klabu ya Yanga ndio klabu…

Read More

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania @taifastars_ Nassor Saadun ameongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia Azam FC hadi mwaka 2027. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 ameongeza mkataba wa mwaka mmoja zaidi kuwatumikia matajiri wa Chamazi kwani mkataba aliokuwa nao awali ulikuwa unatamatika Juni 2026 kabla ya kuongeza mwingine.

Read More