Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemteua Oscar Mirambo kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa shirikisho hilo kuanzia Oktoba 1, 2025. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Mario Ndimbo, uteuzi huo unakuja kufuatia kumalizika kwa mkataba wa aliyekuwa Katibu Mkuu, Kidao Wilfred, ambao unahitimishwa tarehe 30 Septemba 2025. Mirambo, ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, ataingia rasmi kwenye majukumu yake mapya mara tu mkataba wa Kidao utakapomalizika. Atasimamia shughuli zote za kila siku za Sekretarieti ya TFF hadi pale Kamati ya Utendaji ya TFF itakapotoa uamuzi mwingine kuhusu nafasi…
Author: Admin
Baada ya taarifa kusambaa mitandaoni ikionesha wachezaji wa Pamba Jiji wakifanya mazoezi gizani katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Serikali imesema timu hiyo ilifika uwanjani hapo pasipo kutoa taarifa rasmi ya kufanya mazoezi ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga SC Septemba 24, 2025. Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeeleza kuwa wakati timu hiyo imewasili uwanjani hapo saa 12:35 jioni, wataalamu wa umeme walikuwa wamekwisha ondoka na hivyo ikawalazimu kuwarudisha kazini na kufanikiwa kuwasha taa za uwanja huo saa 1:8 usiku. “Wizara imesikitishwa na usambazaji wa picha jongefu zinazoonesha wachezaji wakifanya mazoezi gizani licha ya kuwa chanzo chake…
Beki mpya wa Yanga, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, amefunguka kuwa ni kweli kuna ushindani mkali wa namba kati yake na Chadrack Boka, lakini pia akieleza hadhani kama atakuwa anaanzia benchi mechi zote kwani kuna mashindano mengi sana mbele yao. Tshabalala, aliyejiunga na Yanga msimu huu akitokea Simba, amebainisha kuwa kwenye kikosi chote cha Yanga kuna ushindano mkali wa namba kwenye idara zote na si eneo analocheza yeye, hivyo Kocha Mkuu, Romain Folz, ndiye atakayekuwa akiamua nani anaanza na nani aingie baadaye. Beki huyo wa kushoto, alisema hayo kutokana na kuonekana akianzia benchi kwenye mechi tatu ambazo Yanga imecheza mpaka sasa. “Mwalimu…
Sidhani kama Simba wana kitu kikubwa cha kupoteza katika hili. Kuna kocha huwa anawaweka katika wakati mgumu akiamua kuondoka zake. Kuna aina ya mpira anaweza kuondoka nayo. Hadi sasa hatutajua mpira wa Fadlu ni upi hasa. Kuanzia pale alipoishika timu na mpaka pale alipokwenda likizo kisha akarudi, akahusika katika usajili na kisha kwenda na timu kambini Misri. Wakati ikiwa pale Ismailia chini ya Fadlu sidhani kama Simba imetengeneza aina yoyote ya mpira wa kushtua chini ya Fadlu. Siku hizi makocha wanatengeneza falsafa zao. Unaweza kuchagua kuwa bora katika kushambulia, au kukaa na mpira, au kujihami. Sijaona LOLOTE ambalo Fadlu amelitengeneza…
Nyota wa Barcelona raia wa Hispania na mshindi wa tuzo ya mchezaji bora kijana kwa msimu wa pili mfululizo Lamine Yamal amempongeza mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or usiku wa jana Ousmane Dembele kwa kufanikiwa kushinda tuzo hiyo ya mchezaji bora wa Dunia 2025. Lamine ametoa pongezi hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram akiandika ujumbe wa shukrani kwa tuzo aliyoitwaa mara ya pili huku akiambatanisha na pongezi hizo kwa staa huyo wa PSG. “Mpango wa Mungu ni Mkamilifu na ni lazima upande ili kufika kileleni,Nimefurahia kushinda tuzo ya Kop mara ya pili na nampongeza Ousmane Dembele kwa tuzo hiyo na…
Nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto, amesema wanataka kuanza kwa kishindo mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu tanzania dhidi ya Pamba Jiji kama walivyofanya kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuichakaza Wiliete de Benguela ya Angola mabao 3-0. Akizungumza kuelekea mchezo huo utakaopigwa kesho Jumatano, Mwamnyeto anasema kama wameanza kwa kishindo kwenye ligi ya Mabingwa kwa kumpiga mtu mabao 3-0, basi wanataka kuendeleza kishindo kwenye Ligi Kuu dhidi ya Pamba, mchezo unaotarajiwa kupigwa, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. “Tumeambizana wachezaji wenyewe hakuna kulala, mechi msimu huu zitakuwa nyingi na hakutakuwa na muda mrefu wa kupumzika, nadhani inaweza kuwa…
Klabu ya Simba SC imefanya uteuzi rasmi wa kocha Hemed Suleiman ‘Morocco’ kuwa kocha mkuu wa muda wa timu hiyo. Hemed Morocco, ambaye pia ni kocha wa timu ya taifa ya Tanzania, atachukua jukumu hili hadi klabu itakapompata kocha mpya wa kudumu. Uteuzi huu unalenga kuimarisha maandalizi ya timu katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League). Morocco anajulikana kwa uzoefu wake mkubwa katika soka la Afrika Mashariki, akiwa ameiongoza Zanzibar tangu 2014 na pia amekuwa kocha wa muda wa timu ya taifa ya Tanzania tangu Januari 2024. Katika kipindi chake cha hivi karibuni, aliongoza Taifa Stars katika…
Staa wa Timu ya Taifa ya Ufaransa na Klabu ya Paris Saint-Germain (PSG), Ousmane Dembélé, ameshinda Tuzo ya Ballon d’Or ya 2025, akiwashinda wachezaji maarufu kama Lamine Yamal wa Barcelona na Mohamed Salah wa Liverpool. Katika msimu wa 2024/25, Dembélé alifunga mabao 37 na kutoa pasi za mwisho 15, akisaidia PSG kutwaa mataji manne muhimu: Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1), Kombe la Ufaransa, UEFA Champions League, na UEFA Super Cup
Bingwa wa Dunia wa Marathon mbio za Kilometa 42, Askari wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ), Sajenti Alphonce Simbu amesema anajivunia kuiheshimisha nchi yake kwa kuibuka mshindi wa Medali ya Dhahabu Jijini Tokyo, Japan hivi karibuni. Simbu aliwasili leo saa tisa alfajiri na kupokelewa na msafara na mabasi matano huku Watumishi wenzake wa JWTZ wakiwa wamefurika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam pamoja na Bendi na Ngoma. Mbali na Watumishi wenzake, pia Mama Mzazi wa Sajenti Simbu Salome Ntandu alishiriki mapokezi hayo pamoja na ndugu na familia yake.
Klabu ya Simba imeutangaza uwanja wa Benjamini Mkapa kuwa uwanja watakaoutumia kama uwanja wao wa nyumbani katika mashindano yote kwa msimu wa mwaka 2025/26. Simba wamerejea kwenye uwanja huo ambao wamekuwa wakiutumia kama uwanja wa nyumbani kwa misimu mingi kabla ya msimu jana kuahamia KMC Complex ili kupisha marekebisho yaliyokuwa yanafanyika katika uwanja huo.
Baada ya kuagana rasmi na mabingwa wa kihistoria wa Tanzania, Simba SC, kocha raia wa Afrika Kusini Fadlu Davids sasa amejiunga na wakali wa Morocco, Raja Club Athletic, kama kocha mkuu. Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vya karibu na klabu hiyo, makubaliano yote kati ya pande mbili yamekamilika, na Fadlu anarejea katika timu aliyowahi kuitumikia kama kocha msaidizi. Wakati huo, Raja walitwaa ubingwa wa Botola Pro bila kupoteza mchezo wowote msimu mzima, rekodi iliyowaweka kileleni barani Afrika. Kwa sasa, Davids yupo nchini Afrika Kusini na anatarajiwa kuondoka kesho kuelekea Morocco ili kuanza rasmi majukumu yake. Hatua hii inafungua ukurasa…
Baada ya kuachana na vigogo wa Tanzania Simba SC, Kocha Fadlu Davids anatarajiwa kuchukua mikoba ya kuinoa klabu ya Raja Club Athletic. Makubaliano yote tayari yamekamilika na Fadlu anarudi katika klabu hiyo aliyowahi kuwa kocha msaidizi na kushinda Botola Pro bila kupoteza mchezo msimu mzima. Kwa sasa yupo nchini Afrika Kusini na kesho atasafiri kuelekea Morocco kuanza ukurasa mpya kama kocha mkuu wa Raja. Vigogo hao wa Morocco wanataka kurejea kileleni, hasa katika mashindano ya kimataifa ya CAF, na wamemhakikishia Fadlu na benchi lake la ufundi sapoti ya kutosha kufanikisha mafanikio.
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ndiyo chombo cha kikatiba kinachohusika na kusimamia na kuratibu mchakato wa uchaguzi nchini Tanzania. Kazi kubwa ya tume hii ni kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa haki, uwazi na amani, kuanzia maandalizi, uteuzi wa wasimamizi, uandikishaji wa wapiga kura, hadi kutangaza matokeo. BONYEZA HAPA KUONA MAJINA Mwaka huu 2025, Tanzania inajiandaa kwa Uchaguzi Mkuu, ambapo wananchi watachagua viongozi wao kuanzia ngazi ya Urais, Ubunge na Udiwani. Uchaguzi huu ni tukio muhimu kwa taifa kwani unatoa fursa kwa wananchi kutumia haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi wanaowataka. Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi, majina ya…
Katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL), Simba SC ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Gaborone United ya Botswana kwenye mchezo uliopigwa mjini Gaborone. Bao pekee la mchezo huo lilifungwa dakika ya 15 na Mpanzu, na kuwapa Wekundu wa Msimbazi faida kubwa kuelekea mchezo wa marudiano jijini Dar es Salaam. Kwa upande mwingine, kwenye Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC), Singida Black Stars walionyesha uimara wao baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda. Bao la ushindi lilipachikwa wavuni na Serge Tchakei dakika ya 23 na kuiweka Singida katika nafasi nzuri ya kusonga…
“Ni kweli, mijadala ipo—Simba haikucheza soka la kuvutia sana dhidi ya Gaborone United, lakini bado ikaibuka na ushindi. Wapo wanaoona kama ni dalili za udhaifu, lakini kuna mambo kadhaa ya kuzingatia kabla ya kutoa hukumu ya haraka. Kwanza, Simba walikabiliana na timu bora ambayo ilikuwa imepumzika na kujiandaa kikamilifu kwa mechi hiyo. Pili, Simba wamekusanya pointi tatu muhimu ugenini, jambo linalowapa nafasi kubwa ya kufanya marekebisho kwenye mchezo wa nyumbani. Tatu, ratiba ya safari zao ilikuwa ngumu mno—kuanzia baada ya mechi ngumu dhidi ya Yanga, kisha safari ndefu hadi Afrika Kusini, Gaborone na baadaye Francistown. Zaidi ya masaa 24 yamepotea angani na…
Klabu ya Barcelona inataka huduma ya nahodha wa Uingereza Harry Kane, 32, ambaye ameifungia Bayern Munich mara 95 katika mechi 102 za ligi. Kane anaonekana kama mbadala wa mshambuliaji Robert Lewandowski. Vyanzo vya habari nchini Uhispania vinadokeza kuwa Bayern wanaweza kuwa tayari kumuuza Kane kwa kitita cha Euro milioni 40 mpaka 50. Ikumbukwe mkataba wa Kane na Bayern utatamatika 2027, lakini thamani yake pia itaweza kushuka wakati huo kutokana na umri wake.
Kocha wa Manchester United Ruben Amorim anasema ana matumaini ya kupata muda wa kuonyesha jinsi mfumo wake utakavyobadilika, lakini anasisitiza hata Papa hataweza kumfanya abadilishe mfumo wake. Mojawapo ya shutuma za kocha huyo Mreno ni kwamba ameng’ang’ana mno na mfumo wake wa 3-4-3 na anapaswa kubadilika. Hata hivyo kocha huyo mwenye umri wa miaka 40 alikiri kuwa ana wasiwasi na kile wachezaji watafikiria ikiwa ataamua kubadili mfumo.