Kubwa La Maadui,ROMAN FOLZ Yes nikweli mbinu zake sasa hivi ni Kupiga Mbele and InshaAllah. Lakini Kocha Kumuona hafai Kabisa baada tu ya Mechi Mbili za Ligi nafikri ni Mapema sana..✍️ Kila Kocha anahitaji Muda . Mpira wa Miguu sio Kama Kupika Chai.Just give Roman Folz time ili Mwisho tuhukumu Kwa haki. Thought?? Ameandika @mzeewajambia
Author: Admin
Kocha Nasreddine Nabi amewasili Jijini Dar es Salaam leo asubuhi, hatua ambayo imezua tetesi kuwa yupo mbioni kutangazwa rasmi kuinoa moja ya timu kubwa nchini. Kwa sasa haijafahamika ni klabu ipi atajiunga nayo, lakini vyanzo vya karibu vinaeleza kuwa mazungumzo yako katika hatua za mwisho kabla ya kutangazwa rasmi. Mashabiki wanasubiri kwa hamu kujua ni timu gani itakayofanikiwa kumsajili kocha huyo mwenye rekodi nzuri kwenye soka la Afrika Mashariki.
Kocha Mkuu wa Benfica ya Ureno, Jose Mourinho, anarejea leo kwenye dimba la Stamford Bridge, uwanja wenye historia kubwa katika maisha yake ya soka. Safari hii anarejea kama mpinzani, akiiongoza Benfica kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya mabingwa wa dunia, Chelsea. Mourinho alitangazwa kuwa kocha mkuu wa Benfica wiki iliyopita na leo anakabiliwa na mtihani wake mkubwa wa kwanza akiwa na timu hiyo mpya. Akizungumza kuelekea mchezo huo, Mourinho alisema anajihisi kama yupo nyumbani lakini sasa anawakilisha Benfica na lengo lake ni moja tu — kushinda. “Najihisi kama niko nyumbani, lakini ndani ya dakika 90 sitafikiria nilikotoka.…
Simba Baada ya Kumaliza Mechi ya awali ya CAF Champions League na kumaliza wakiwa na ushindi wa magoli mawili Moja la Ugenini na lingine Nyumbani, Kwa sasa Mchezo unaofwata ni dhidi ya Nsingizini Hotspurs kutokea Eswatini, Mchezo ambao unatarajiwa kuchezwa 17 Oktoba 2025 katika mkondo wa kwanza, Simba wakianzia ugenini. Nsingizini Hotspur wameingia katika hatua hii baada ya kumuondoa Simba Bhora kutokea Zimbwabe kwa mikwaju ya penati baada ya mechi zote mbili kumalizika kwa magoli sawa 1:1 ambapo mechi ya kwanza Nsingizini walianzia ugenini na wakapokea kichapo cha goli moja na mchezo wa arudiano wakiwa nyumbani walifunga goli moja ndio…
Klabu ya Simba SC imemtolea shukrani za dhati Kocha Hemed Suleiman ‘Morocco’ kwa kuiongoza timu hiyo katika mchezo muhimu wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United. Kocha Morocco, ambaye ni Kocha Mkuu wa Taifa Stars, alijiunga na kikosi cha Simba kwa ruhusa maalum kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kufanikiwa kukiongoza timu hiyo kupata ushindi muhimu uliowavusha hatua ya awali ya michuano hiyo. “Shukrani za dhati kwa Kocha Hemed Suleiman ‘Morocco’ kwa kuongoza kikosi chetu katika mchezo muhimu wa jana wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United, na kufanikiwa kutuvusha”. “Shukrani pia kwa Shirikisho la…
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) imetoa adhabu kwa Chama cha Soka cha Afrika Kusini (SAFA) baada ya kubainika kumchezesha Teboho Mokoena, mchezaji asiye na sifa za kushiriki, katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Lesotho uliochezwa mwezi Machi mwaka huu. Kwa mujibu wa uamuzi huo, Afrika Kusini imenyang’anywa ushindi wake na sasa itaorodheshwa kupoteza mchezo huo kwa mabao 3-0. Aidha, SAFA imelazimika kulipa faini ya CHF 10,000 (takribani shilingi milioni 29 za Kitanzania) kwa FIFA. FIFA imeipa SAFA siku 10 kuanzia tarehe ya kutolewa kwa uamuzi huu ili kukata rufaa endapo itaridhika kwamba uamuzi…
Mshambuliaji wa AaB Fodbold ya Denmark, Kelvin John licha ya timu yake hiyo kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Lyngby Boldklub amezidi kuwa bora na amesema huu ni msimu wake wa kuonyesha kiwango bora. Juzi, timu ya Mtanzania huyo ilipoteza mabao 2-1 dhidi ya Lyngby Boldklub kwenye muendelezo wa Ligi Daraja la Kwanza Denmark na licha ya kufungwa, John alionyesha kiwango bora kwa kufunga bao moja ambalo linamfanya kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mechi, kura zinazopigwa na mashabiki. Bao alilofunga linamfanya kufikisha jumla ya mabao sita kwenye mechi 10 alizocheza. Timu hiyo ipo nafasi ya saba kwenye msimamo wa…
WAKATI tetesi zikieleza kuwa mabosi wa Yanga SC huenda wakaachana na Kocha Mkuu, Romain Folz ambaye amekiongoza kikosi hicho kutwaa taji la Ngao ya Jamii, Legend katika masuala ya michezo Tanzania Saleh Ally Jembe amehoji maswali mazito. Jembe amebainisha kuwa tetesi hizo haoni kama zina mashiko kutokana na sababu ambazo zinatajwa kutoeleweka kwani hakuna kitu ambacho hajakifanya kocha Folz. “Ikiwa utasema kwamba Yanga SC wanataka kumuacha Folz inabidi unaiambie kwa nini anaachwa kwa sasa? Ukiangalia ameongoza mechi tano na hajafungwa. “Mchezo wa kirafiki, mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba SC ambao ulikuwa na ushindani mkubwa. ukiachana na hilo…
Shirikisho la soka duniani, FIFA, limemchagua mwamuzi wa Tanzania, Ahmed Arajiga, kuchezesha mchezo muhimu wa kufuzu Kombe la Dunia 2026, kati ya Cape Verde na Eswatini! Mchezo huu unatarajiwa Oktoba 13, nchini Cape Verde, na ushindi wa Cape Verde utawapa fursa ya moja kwa moja kufuzu Kombe la Dunia! Tanzania iko kibao cha fahari kuona mwamuzi wake akiwakilisha taifa kwenye kiwango cha
UONGOZI wa Simba SC umebainisha hasara watakazopata kutokana na kuwakosa mashabiki kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United ya Botswana, Septemba 28 2025 Uwanja wa Mkapa. Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kuwa walipata adhabu kutokana na makosa ya mashabiki kwenye mechi zilizopita za kimataifa ikiwa ni mchezo wa Al Masry na RS Berkane. “Hasara ya kwanza tunakosa mashabiki, hasara ya pili tunakosa mapato na hasara ya tatu tunalipa faini ya USD 50,000. Vilevile tumepewa adhabu kutokana na mechi ya fainaili dhidi ya RS Berkane, huku vilevile tuliwasha fireworks. Kwenye…
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda amempongeza Sajini Alphonce Simbu kwa ushindi wa medali ya dhahabu katika Mashindano ya Mbio za Marathon ya Dunia Kilomita 42, zilizofanyika Tokyo Japan. Pamoja na pongezi hizo, Jenerali Mkunda amempandisha cheo kutoka Sajini kuwa Sajinitaji tukio lililofanyika ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi Upanga Jijini Dar es Salaam jana Septemba 25, 2025. Jenerali Mkunda amesema ushindi huu ni kwa Watanzania wote na Afrika kwa ujumla na kwamba michezo ni sehemu ya kazi jeshini, hivyo Sajinitaji Alphonce Simbu amefanya kazi nzuri. Jenerali Mkunda ametoa rai kwa maafisa na askari wote jeshini kuiga…
U in
Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limemsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wake, Auka Gecheo mara moja. Inafahamika kuwa Kamati ya Utendaji, ikiongozwa na Kaimu Rais Alexandre Muyenge, iliyokutana takriban tarehe 18 mwezi huu, iliazimia kwa kauli moja kumsimamisha Auka katika nafasi yake ya Mkurugenzi Mtendaji. CECAFA EXCO, hata hivyo, haikufichua sababu ya hatua hiyo, lakini inaeleweka Mkenya mwingine anatazamiwa kuchukua jukumu hilo. Auka amehudumu katika nafasi hiyo tangu kuteuliwa kwake Julai 2020, alipochukua nafasi ya Nicholas Musonye, aliyekuwa Katibu Mkuu.
Manchester United inamtaka mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane, 32, ambaye huenda akaondoka Bayern Munich msimu ujao wa kiangazi. Tetesi zinaonyesha kwamba nyota huyo wa zamani wa Tottenham Hotspur anaweza kutaka kumalizia kibarua chake Allianz Arena msimu ujao wa joto, licha ya kuongezewa kandarasi hadi 2027. Kulingana na gazeti la Daily Star, “Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 anaripotiwa kuwa na hamu ya kurejea Ligi Kuu ya Uingereza baada ya Kombe la Dunia la FIFA 2026, huku Manchester United ikitajwa kuwa timu inayohitaji kwa ukubwa huduma ya mchezaji huyo. Taarifa zinasema Kane ataweza kupatikana kwa ada ya pauni milioni 56.8.
Gwiji wa Manchester United Wayne Rooney hajawahi kuona haya kueleza hisia zake. Mchezaji huyo wa zamani na kocha bado anaamini kuwa Lionel Messi ndiye mchezaji bora zaidi kuliko Cristiano Ronaldo huku akisisitiza kwamba hamchukii fowadi huyo anayekipiga na klabu ya Al Nassr. Akiongea kwenye podcast ya Rio Ferdinand Rooney alisema; “Watu wanadhani namchukia! Nampenda! Ni mkali sana na anafanya maajabu. Sidhani kama watu wanatambua jinsi mimi na yeye tulivyokuwa karibu.” “Mimi napendelea jinsi Messi anavyocheza, ndio hivyo, wewe unaweza kumpenda Cristiano na mwingine akampenda Messi” akamalizia Rooney. [ez-toc][ez-toc]
SELEMAN Matola kocha msaidizi wa Simba SC amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara ya NBC dhidi ya Fountain Gate unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 25 2025. Huu unakuwa mchezo wa kwanza kwa Simba SC msimu wa 2025/26 kwenye ligi ambayo imeanza kasi Septemba 17 kwa mechi za ushindani kuendelea ndani ya uwanja. Simba SC imetoka kucheza mchezo wa kimataifa dhidi ya Gaborone United ya Botswana inakutana na Fountain Gate ambayo imetoka kupoteza mchezo uliopita wa ligi dhidi ya Mbeya City kwa kufungwa bao 1-0. Miongoni mwa wachezaji waliopo katika kikosi cha Simba SC ni Ellie…
Mshambuliaji wa zamani wa Young Africans SC, Fiston Kalala Mayele, ameendelea kuonyesha makali yake barani Afrika na duniani baada ya kufunga mabao matatu (hat-trick) yaliyoipeleka Pyramids FC ya Misri hatua inayofuata ya michuano ya Kombe la Mabara la FIFA. Pyramids FC imeiondoa Al Ahli Saudi ya Saudi Arabia kwa jumla ya mabao 3–1, licha ya wapinzani wao kuwa na wachezaji nyota kama Riyad Mahrez (winga wa zamani wa Manchester City), Franck Kessie (kiungo wa zamani wa Barcelona), na Ivan Toney (mshambuliaji wa zamani wa Brentford), ambaye alifunga bao pekee la kufutia machozi kwa mkwaju wa penati dakika ya 45. Mayele…