Author: Admin

Tangu achukue mikoba ya kuinoa Liverpool, kocha Arne Slot sasa amefikiwa na rekodi ya kusononesha sana ya kupoteza mechi 4 mfululizo kwenye ligi kuu Uingereza. Mechi hizo ni dhidi ya; ❌ 2-1 vs Crystal Palace ❌ 2-1 vs Chelsea ❌ 1-2 vs Manchester United ❌ 3-2 vs Brentford Kutoka kuwa timu inayotetea Ubingwa hadi sasa nafasi ya 6 kwenye msimamo wa Ligi.

Read More

Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champions Oktoba 26,2025 unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa ikiwa ni mchezo wa maamuzi. Ipo wazi kwamba katika mchezo wa kwanza uliochezwa Oktoba 19 2025 Eswatini, Simba SC iliibuka na ushindi wa mabao 3-0. Kwenye mchezo huo wa ugenini, Kibu Dennis alifunga mabao mawili na bao la ufunguzi lilifungwa na beki wa kati Wilson Nangu kwa pigo la kichwa akimalizia kona ya Maema. Ahmed Ally, Meneje wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC ameweka wazi kuwa huo ni mchezo muhimu na Wanasimba wanapaswa kujitokeza kwa wingi. “Kuelekea mchezo huu tumeweka viingilio vya kitajiri. Viingilio…

Read More

Cristiano Ronaldo ameishauri klabu yake ya Al-Nassr kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Robert Lewandowski ambaye atapatikana bila malipo mwishoni mwa msimu wa 2025-26. Mpaka sasa hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanywa na Barcelona kuhusu mustakabali wa Lewandowski, lakini inafahamika kuwa huu utakuwa msimu wake wa mwisho akiwa Camp Nou. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 amefunga mabao 105 na kusajili mabao 20 katika mechi 156 alizochezea Barcelona katika michuano yote, ikiwa ni pamoja na mabao manne katika mechi tisa msimu huu. Atletico Madrid na vilabu vingine vya Uingereza pia vihusishwa na kumtaka mchezaji huyo.

Read More

Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Morocco imeandika historia baada ya kutwaa taji la Kombe la Dunia la Vijana (FIFA U-20 World Cup) kwa mara ya kwanza, ikipata ushindi wa mabao 2–0 dhidi ya Argentina katika mchezo wa fainali uliopigwa Jumapili. Shujaa wa pambano hilo alikuwa mshambuliaji Yassir Zabiri, aliyetikisa nyavu mara mbili katika dakika ya 12 na 29, akiiongoza Morocco kutwaa ubingwa huo wa kihistoria. Ushindi huo umeifanya Morocco kuwa taifa la kwanza kutoka Afrika kushinda taji hilo tangu Ghana ilipofanikiwa mwaka 2009. Argentina, ambayo ilikuwa haijapoteza mchezo wowote hadi kufika fainali, ilikosa huduma ya nyota…

Read More

Klabu ya Azam FC siku ya leo itakuwa uwanjani majira ya saa 10:15 jioni kusaka tiketi ya kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza. Azam FC watakuwa ugenini dhidi ya KMKM ya Zanzibar katika mchezo wa mkondo wa kwanza ambao pengine ukawapa matumaini ya kuandika historia mpya kama watapata matokeo mazuri kabla ya mchezo wa pili utakaopigwa nyumbani. Unawapa asilimia ngapi za ushindi Matajiri wa Chamazi katika mchezo huo ?.

Read More

Nsingizini Hotspurs vs Simba SC, mchezo unaofuata kwa Simba SC katika anga la kimataifa ikiwa ni CAF Champions League unatarajiwa kuchezwa ugenini. Hii ni kete ya kwanza kimataifa kwa Meneja Mkuu wa Simba SC, Dimitar Pantev huku wachezaji wapya wa timu hiyo ikiwa ni Neo Maema, De Reuck wakipewa angalizo kuhakikisha kwamba wanapambana kupata matokeo mazuri. Ikumbukwe kwamba mshindi wa jumla katika mchezo huu atakwenda hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.  Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amebainisha kuwa wachezaji wote wana kazi kuelekea mchezo ujao kimataifa kuhakikisha wanaendeleza utamaduni wa timu hiyo kupata…

Read More

MABORESHO ya benchi la ufundi la Simba yanaendelea, baada ya ujio wa Dimitir Pantev na msaidizi wake, Simeonov Boyko Kamenov waliotokea Gaborone United ya Botswana, sasa ameshushwa mtu mwingine. Simba SC imemshusha kwa siri sana kocha wa makipa kutoka Bulgaria kwa ajili ya kuimarisha benchi la ufundi la timu hiyo linaloongozwa na Dimitir Pantev. Mtaalamu huyo aliyetua majira ya saa 9:05 alfajiri na ndege ya Shirika la Uturuki, ni Vitomir Vutov mwenye umri wa miaka 53 ambapo amekuja kuungana na wenzake siku chache baada ya kuondoka kwa Fadlu Davids. Ujio wa Vutov, unalifanya benchi la ufundi la Simba kuwa na…

Read More

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeufungia Uwanja wa Sokoine uliopo jijini Mbeya kutumika kwa michezo ya Ligi, kutokana na kushindwa kukidhi vigezo vya kikanuni na masharti ya sheria za mpira wa miguu. TFF imesema miundombinu ya uwanja huo haikidhi matakwa ya Kanuni za Leseni za Klabu, kama ilivyoainishwa kwenye masharti ya kanuni hizo. Kutokana na uamuzi huo, timu zinazotumia uwanja huo kwa michezo yao ya nyumbani zitalazimika kuutumia uwanja mwingine kwa mujibu wa Kanuni, hadi pale marekebisho yatakapokamilika na ukaguzi kufanywa upya na TFF. TFF imezikumbusha klabu zote nchini kuendelea kutunza na kuboresha miundombinu ya viwanja vyao ili…

Read More

Rais wa Klabu ya Yanga, Injinia Hersi Said, amefunguka kuwa wakati anapewa jukumu la kuiongoza klabu hiyo, baadhi ya wanachama na mashabiki hawakuwa na imani naye kutokana na umri wake kuwa mdogo ukilinganisha na viongozi waliowahi kuiongoza timu hiyo hapo awali. Akizungumza kuhusu safari yake ndani ya uongozi wa Yanga, Hersi alisema mashaka ya wanachama yalikuwa ya kawaida kwani wengi walikuwa wakijiuliza kama kijana kama yeye angeweza kuhimili presha na majukumu makubwa ya kuiongoza klabu yenye historia na mashabiki wengi kama Yanga SC. “Ni kweli kulikuwa na mashaka, na niliyaelewa. Nilikuwa kiongozi kijana zaidi kuliko waliowahi kuongoza Yanga, hivyo ilikuwa…

Read More

Saudi Arabia itakuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia la 2034 litakalochezwa mnamo Januari 2035, badala ya ratiba ya kawaida ya Novemba hadi Disemba, mabadiliko ya kihistoria yaliyofanywa ili kuzuia mwingiliano na Ramadhani. Ripoti zinaonyesha uamuzi huo unalenga kuhakikisha wachezaji Waislamu wanaweza kushindana bila vikwazo vya kufunga wakati wa mchana. Hatua iliyopendekezwa itafanya hili kuwa Kombe la Dunia la kwanza kuwahi kufanyika katika mwaka uliofuata wa kalenda. Rais wa FIFA Gianni Infantino hivi majuzi amesisitiza hitaji la kubadilika katika ratiba ya mashindano, akitaja hali ya hewa, msongamano wa kalenda, na uzingatiaji wa kidini kama sababu kuu. Michuano hiyo itafunguliwa na kufungwa…

Read More

UONGOZI wa Simba SC umeweka wazi kuwa haukubaliani na vitendo vya kihuni kwenye mpira wa miguu kwa kuwa unarudisha nyuma maendeleo ya wachezaji na timu kiujumla. Simba SC inapeperusha bendera katika Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa hatua ya pili inatarajiwa kucheza mchezo wake wa kimataifa dhidi ya Nsiginzini Hotspurs Oktoba 19 2025 pia inaongoza ligi ikiwa na pointi sita baada ya mechi mbili. Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kuwa vitendo vya kihuni ambavyo vinatokea uwanjani kwa wachezaji kuchezeana rafu mbaya vinaumiza wachezaji na kudumaza maendeleo ya mpira kutokana na wachezaji kukaa nje muda…

Read More

KAMPENI ya Simba SC ambayo ina lengo la kutokomeza jezi feki inaendelea ambapo Wananchi wamezidi kupewa elimu kuhusu faida za kununua jezi Original. Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC ameweka wazi kuwa kununua jezi Original ni jambo ambalo kila Mtanzania anapaswa kujivunia. Oktoba 9 uongozi wa Simba SC uliweka kambi Mwanza na kutembelea baadhi ya vituo na kuzungumza na Wananchi wa Buhongwa, Nyegezi, Nyamagana, Kisesa na Machinjioni. Ahmed Ally amesema kuwa kununua jezi feki kunadumaza ustawi wa maendeleo kwa muwekezaji, timu na taifa kiujumla hivyo ni muhimu kununua jezi orijino ambazo zipo kwenye maduka maalumu.…

Read More

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesimamisha kwa muda mchezaji wa klabu ya Yanga Queens, Princess Jeanine Mukandiyisenga, raia wa Rwanda, kupisha uchunguzi wa kina kuhusu jinsia yake. Hatua hii imekuja baada ya sintofahamu kuibuka mitandaoni na katika baadhi ya duru za michezo, ambapo mashabiki na wadau wameanza kuhoji hali halisi ya jinsia ya mchezaji huyo, ambaye amekuwa akionesha kiwango cha juu mno katika michezo ya Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania. Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya TFF, uchunguzi huo unalenga kuthibitisha ukweli bila upendeleo, kwa mujibu wa kanuni za shirikisho hilo na taratibu za Shirikisho la Soka Duniani (FIFA)…

Read More

Djigui Diarra Ashinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Septemba 2025/2026 Mlinda mlango wa klabu ya Yanga SC, Djigui Diarra, amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Septemba wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara msimu wa mwaka 2025/2026, baada ya kuonesha kiwango cha juu katika michezo miwili ambayo timu yake ilicheza ndani ya mwezi huo. Diarra aliiongoza Yanga SC kupata matokeo mazuri ikiwemo ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Pamba Jiji FC na sare tasa ya 0-0 dhidi ya Mbeya City FC, michezo yote miwili ikimalizika bila kuruhusu bao (clean sheets). Mchezaji huyo raia wa Mali alionesha ubora mkubwa langoni…

Read More

Maswali mbalimbali ya usaili yanayoweza kuulizwa kwa waombaji wa nafasi ya kusimamia uchaguzi mkuu, Maswali haya ni kwa Makarani, wasimamizi wasaidizi na wasimamizi wakuu wa vituo. Maswali ya usaili kusimamia uchaguzi Elezea kwa kifupi lengo la uchaguzi mkuu utakaofanyika 29 october 2025 Uchaguzi utakaofanyika 29 october 2025 ni uchaguzi wa ngapi tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa? Ni hatua gani utachukua kuhakikisha wapiga kura wanapata haki sawa na kupiga kura bila upendeleo? Elezea wajibu wa wafuatao katika kituo cha kupiga kura. Msimamizi wa kituo Msimamizi Msaidizi wa kituo Karani Askari

Read More

Msemaji Mkuu wa Serikali, Mhe. Gerson Msigwa, amekanusha taarifa zinazosambaa kuwa Uwanja wa Benjamin Mkapa umefungwa kwa miezi sita. “ACHENI KUPOTOSHA. Hatujatangaza kuufunga Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa miezi 6 kama baadhi ya watu wanavyopotosha. Tumekaa na TFF na pia timu za Yanga na Simba zilioomba kutumia uwanja wa Benjamin Mkapa kwa ajili ya mechi za ligi na kufanya tathmini ya uharibifu wa sehemu ya kuchezea (pitch) ya uwanja wa Benjamin Mkapa baada ya mechi mfululizo zilizopita za Kimataifa na za ligi. Tumekubaliana kuwa Yanga na Simba watafute viwanja vingine kwa ajili ya michezo ya ligi na uwanja wa Benjamin…

Read More

WAKATI tetesi zikieleza kuwa huenda Romain Folz akafutwa kazi ndani ya kikosi cha Yanga SC rekodi zinaonyesha kuwa amekiongoza kikosi kwenye mechi 6. Katika mechi hizo ushini ni mechi tano na aliambua sare mchezo mmoja wa ligi ugenini dhidi ya Mbeya City uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya. Sababu kubwa inayotajwa kumuondoa Folz kwenye benchi la ufundi ni timu kucheza katika kiwango cha chini katika mechi za ushindani. Hizi hapa rekodi za mechi ambazo alikaa benchi ndani ya msimu wa 2025/26 mrithi wa mikoba ya Miloud Hamdi:- Yanga 1-0 Bandari ya Kenya. (Mechi ya kirafiki) Yanga SC 1-0 Simba SC, (Ngao…

Read More