Author: Admin

Vin Diesel amethibitisha hadharani kwamba staa wa soka Cristiano Ronaldo anaweza kushiriki katika filamu ijayo ya Fast & Furious, ambayo huenda ikawa ni sehemu ya mwisho, Fast X: Part 2. Kupitia chapisho la Instagram lenye picha ya wawili hao wakiwa pamoja, Diesel aliandika: “Kila mtu aliuliza, angekuwa katika simulizi za Fast … I gotta tell you he is a real one. Tuliandika jukumu kwa ajili yake … “. Ronaldo anatazamiwa kucheza filamu ya mwisho ya Fast & Furious, ambayo mara nyingi hujulikana kama Fast & Furious 11 au Fast X: Sehemu ya 2, ambayo ina tarehe ya kuachiwa mnamo Aprili…

Read More

Baada ya jana kutoa asisti ya goli la pili la Hugo Ekitike kwenye ushindi wa 2-0 wa Liverpool dhidi ya Brighton, Mohamed Salah sasa amekuwa mchezaji wa tatu kwa wachezaji waliochangia mabao mengi wa muda wote wa Ligi Kuu Uingreza, akiwa amewapita Frank Lampard na Ryan Giggs huku akiwa amechangia mabao 280 (Magoli 190, Assists 90). Wachezaji wawili walio mbele yake ni Alan Shearer na Wayne Rooney. 1 Alan Shearer 324 2 Wayne Rooney 308 3 Mohamed Salah 280 4 Frank Lampard 279 5 Ryan Giggs 272 Salah alifanikisha hatua hii katika michezo michache zaidi kuliko wachezaji wengine katika tano…

Read More

Mshambuliaji wa zamani wa klabu za TP Mazembe, AS Vita Club na Yanga SC, Chico Ushindi Wakubanza, amefariki dunia leo mchana akiwa nyumbani kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Chico Wakubanza alikuwa mmoja wa washambuliaji waliopata heshima kubwa katika soka la Afrika na Kati na Mashariki, akitambulika kwa uwezo wake wa kufumania nyavu, nguvu ya kimwili na uzoefu mkubwa katika ligi mbalimbali. Enzi zake akiwa uwanjani zilimpa jina la “Striker la Mabao”, akiacha alama isiyofutika kwa mashabiki na vilabu alivyovitumikia. Kifo chake ni pigo kubwa kwa familia, marafiki, jumuiya ya soka barani Afrika na mashabiki wa Yanga, TP Mazembe…

Read More

Mchezaji wa zamani wa Yanga anayekipiga klabu ya Wydad kwa sasa Stephane Aziz Ki ameandika ujumbe mzito kwenye ukurasa wake wa Instagram akimtakia kila la kheri mke wake mwanamitindo wa Tanzania Hamisa Mobetto katika kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa. Aziz Ki ambaye alifunga ndoa na mwanamitindo huyo wa Tanzania mapema mwaka huu kwa sasa anakipiga Nchini Morocco huku mpaka sasa wakiwa bado hawajajaliwa kupata mtoto pamoj licha ya kila mmoja kuwa na watoto nje ya ndoa yao. “Mpenzi wangu Hamisamobetto, Katika siku hii maalum, nataka nikukumbushe umuhimu wako maishani mwangu. Kila mwaka nikiwa pembeni yako ni zawadi ya thamani—sura…

Read More

Alphonso Davies alipata shangwe kutoka kwa mashabiki wa Bayern Munich na kukumbatiwa na wachezaji wenzake baada ya kurejea kutoka kwa jeraha la ACL (anterior cruciate ligament) baada ya siku 262. Beki huyo wa kushoto wa Kanada aliingia kama mbadala wa Serge Gnabry dakika ya 88 wakati Bayern iliposhinda 3-1 Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Sporting CP Jumanne, Desemba 9, 2025. Hii ilikuwa mechi yake ya kwanza tangu kupata jeraha baya la goti la kulia alipokuwa akiichezea Canada katika mechi ya Ligi ya Mataifa ya CONCACAF Machi 2025. Ninaweza kutoa ulinganisho wa uchezaji wa Alphonso Davies kabla na baada ya…

Read More

Kiungo wa Yanga Pacome Zouzoua hajajumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Ivory Coast kitakachoshiriki fainali za mataifa ya Afrika AFCON zinazotarajia kuanza kurindima mwisho wa mwezi huu nchini Morocco. Pacome aliitwa hivi karibuni kwenye kampeni za kutafuta tiketi ya kufuzu fainali za kombe la Dunia huku akikabidhiwa jezi namba 7 mgongoni. Wachezaji wote walioitwa Timu ya Taifa ya Ivory Coast wanacheza nje ya Bara la Afrika akiwemo Mshambuliaji wa Manchester United Amad Diallo.

Read More

Mchezaji wa Mbeya City, Vitalis Mayanga amefungiwa kucheza mechi tano sambamba na kutozwa faini ya Tsh Milioni 1 kwa kosa la kumpiga kiwiko beki wa kushoto wa Simba, Anthony Mligo kwenye mchezo wa ligi kuu uliopigwa katika dimba la Meja Isymuhyo disemba 4 mwaka huu. Uamuzi huo umetolewa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) katika taarifa ya TPLB siku ya leo kwa mujibu wa kanuni ya 41;21 ya ligi kuu kuhusu udhibiti wa wachezaji.

Read More

Real Madrid walizomewa walipolala kwa mabao 2-0 wakiwa nyumbani dhidi ya Celta Vigo katika mechi waliyomaliza wakiwa na wachezaji tisa. Celta walikuwa mkiani mwa La Liga kabla ya safari yao ya Bernabeu Jumapili usiku na bila ushindi wa ligi dhidi ya Real Madrid katika mechi 22. Lakini mabao ya Williot Swedberg kipindi cha pili yalihitimisha ushindi wa kwanza wa Celta dhidi ya Madrid tangu Mei 2014 na kuongeza shinikizo kwa kocha Xabi Alonso. Real Madrid sasa wameshinda mchezo mmoja tu kati ya michezo mitano iliyopita ya ligi na watashuka hadi nafasi ya tatu kwenye La Liga iwapo Villarreal watashinda mchezo…

Read More

Nyota wa Timu ya Taifa ya Brazil na klabu ya Santos Neymar Jr siku ya jana alifanya maamuzi ya kucheza mchezo muhimu wa klabu yake wa vita ya kujinusuru kushuka daraja licha ya jeraha la goti alilonalo ambalo alitakiwa kufanyiwa upasuaji. Neymar Jr siku kadhaa zilizopita aliripotiwa kupata jeraha jipya la goti ambalo madaktari walishauri afanyiwe upasuaji licha ya ripoti hiyo nyota huyo alifanya maamuzi ya kucheza mchezo wa Santos dhidi ya Sport akiisaidia kuibuka na ushindi wa magoli 3-0 baada ya kufunga bao na kutoa pasi ya bao huku akiimbwa na mashabiki wa timu yake. Baada ya mchezo huo…

Read More

Rais wa klabu ya Estudiantes Juan Sebastian Veron amepigwa marufuku ya miezi sita na Chama cha Soka cha Argentina kwa sababu alikataa kusimama kutoa heshima kwa mabingwa wapya Rosario Central. Kiungo huyo wa zamani wa Manchester United na Chelsea pamoja na wachezaji wake wa Estudiantes walikuwa wakipinga Rosario kutangazwa ‘Bingwa wa Ligi’ kutokana na mabadiliko ya sheria yaliyofanywa na FA ya Argentina wiki iliyopita. Wachezaji wa Estudiantes waliwapa kisogo wachezaji wa Rosario walipoingia uwanjani kabla ya mechi yao ya mtoano ya hatua ya 16 bora ya ligi ya Clausura Jumapili iliyopita, ambayo vijana wa Veron walishinda 1-0. Veron amefungiwa miezi…

Read More

Florent Ibenge Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa wachezaji walijitoa kwa asilimia kubwa licha ya kukosa matokeo kwenye mchezo wa CAF Confideration Cup. Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa New Amaan Complex ulisoma Azam FC 0-1 Wydad Casablanca ikiwa ni mchezo wa hatua ya makundi. Bao la ushindi lilifungwa na Nordin Amrabat dakika ya 57 kipindi cha pili lilidumu mpaka mwisho wa mchezo ikiwa ni mechi ya pili Azam FC kupoteza baada ya kuanza ugenini kufungwa 2-0 dhidi ya AS Maniema. Ibenge amesema wachezaji walifanya kazi kubwa ndani ya uwanja wanastahili pole licha ya kukwama kupata ushindi.…

Read More

JOSHUA Mutale ni chaguo la kwanza kwa Meneja Mkuu, Dmitar Pantev je ataanza tena mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika? Orodha ya wachezaji wa Simba SC waliopo kwenye msafara ulioelekea Mali kwa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Stade Malien Novemba 30,2025:- Makipa Yakoub Suleiman na Hussen Abel Mabeki Shomari Kapombe David Kameta Anthony Mligo Karabou Chamou Rushine De Reuck Wilson Nangu Viungo Yusuph Kagoma Allasane Kante Naby Camara Neo Maema Morice Abraham Jean Ahoua Hussen Semfuko Ladack Chasambi Elie Mpanzu Joshua Mutale Washambuliaji Steven Mukwala Seleman Mwalimu Jonathan Sowah

Read More

Kikosi cha Simba kimeondoka leo alfajiri kuelekea nchini Mali kwa ajili ya mchezo wao ujao dhidi ya Stade Malien. Maandalizi ya mwisho yamekamilika na wachezaji wamepewa maelekezo ya kimsingi kuhusu mikakati ya mchezo, huku lengo likiwa ni kuendelea na ushindi na kufanikisha maendeleo ya klabu katika mashindano ya kimataifa.

Read More

Timu Tatu za Tanzania Zashindwa Kung’ara Katika Michezo ya Kwanza ya Makundi CAF Simba inayoiwakilisha Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, pamoja na Azam FC na Singida Black Stars wanaopeperusha bendera ya nchi katika Kombe la Shirikisho, zimeanza kampeni zao za hatua ya makundi kwa vichapo vinavyozua maswali mapya kuhusu maandalizi na mwelekeo wa safari ya kimataifa ya klabu za Tanzania. Matokeo hayo yametokea wakati Yanga pekee ikipata ushindi mwembamba nyumbani, huku tatu nyingine zikiambulia hasara ambazo zimeanza kutengeneza presha ya mapema katika mbio za kutafuta nafasi ya robo fainali. Yanga Yapata Nafuu, Lakini Kazi Bado Ni Nzito…

Read More

Timu za Ligi Kuu ya Uingereza zimetawala timu za LaLiga hadi sasa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu. Haya ni matokeo ya mechi zilizokutanisha timu za ligi hizo 2 msimu huu wa UEFA; ✅ Athletic Club 0-2 Arsenal ✅ Arsenal 4-0 Atletico Madrid ✅ Liverpool 3-2 Atletico Madrid ✅ Liverpool 1-0 Real Madrid ✅ Chelsea 3-0 Barcelona ✅ Villarreal 0-2 Man City ✅ Tottenham 1-0 Villarreal ✅ Newcastle 2-0 Athletic Club ❌ Newcastle 1-2 Barcelona Je, hii ni tafsiri rahisi ya kuwa La Liga ni ligi dhaifu kuliko EPL?

Read More

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeufungia Uwanja wa Mkwakwani, uliopo Tanga, kutokana na kutokidhi vigezo vya matumizi ya ligi kwa sasa. Uamuzi huo umefikiwa baada ya ukaguzi uliofanyika hivi karibuni kubainisha kasoro kadhaa zinazohitaji marekebisho kabla ya uwanja kuruhusiwa kutumika tena kwenye michezo ya Ligi Kuu na mashindano mengine yanayosimamiwa na Bodi. Kwa mujibu wa TPLB, uwanja huo utabaki kufungwa hadi pale matakwa yote ya kiufundi na kiusalama yatakapokamilishwa na kuthibitishwa na kamati husika.

Read More

MSAFARA wa kikosi cha Yanga SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Pedro unatarajiwa kuanza safari mapema leo Novemba 24,2025 kuelekea nchini Algeria. Yanga SC baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AS FAR Rabat ina kibarua kingine kwenye kundi B Novemba 28,2025 mchezo wa kwanza ugenini katika hatua ya makundi. Ipo wazi kuwa ni Prince Dube alifunga bao la ushindi kwenye mchezo uliopita Uwanja wa New Amaan Complex akitumia pasi ya kiungo Mudathir Yahya. Inatajwa kuwa Yanga SC wanahitaji kuondoka mapema ili kufanya maandalizi mazuri kwa wakati na kupata matokeo kwenye mchezo ujao. Leo Yanga SC wataanza safari kuelekea…

Read More

Mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba SC na Petro de Luanda ya Angola umemalizika kwa Wekundu wa Msimbazi kupokea kichapo cha bao 1-0 katika dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Simba, ambayo ilihitaji ushindi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuendelea na mbio za kutinga robo fainali, ilijikuta ikicheza chini ya kiwango huku wageni kutoka Angola wakionyesha ubora mkubwa katika dakika nyingi za mchezo. Bao pekee la Petro liliamsha presha kwa mashabiki wa Simba, lakini juhudi za kusawazisha hazikuzaa matunda. Matokeo hayo yanaifanya Simba kuburuza mkia katika kundi lake, ikiwa nafasi ya…

Read More

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Ufaransa na Mshambuliaji wa Real Madrid Kylian Mbappé ameondoka kwenye kambi ya Timu ya Taifa na kurejea kwenye klabu yake kwa ajili ya kufanyiwa vipimo zaidi ya jeraha lake. Mbappe licha ya kucheza mchezo wa jana dhidi ya Ukraine na kuandika historia ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kwa karne ya 21 kufunga magoli 400 katika michezo 537 bado anasumbuliwa na jeraha la kifundo cha mguu wake wa kulia. Mshambuliaji huyo ni rasmi ataukosa mchezo unaofuata wa Nchi yake dhidi ya timu ya Taifa ya Azerbaijan siku ya Jumapili.

Read More