Author: Admin

Bodi ya Azam Football Club, imemtangaza, Octavi Anoro, (42), kama Mtendaji Mkuu (CEO) mpya wa klabu, kwa mkataba wa miaka miwili, hadi 2027. Nafasi hiyo ilikuwa wazi kufuatia aliyekuwa akiishikilia, Abdulkarim Nurdin maarufu kama Popat, kupandishwa cheo na kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais. Anoro, raia wa Hispania, anakuja na maarifa na uzoefu mkubwa wa kimataifa katika nyanja ya maendeleo ya utawala na biashara ya mpira wa miguu. Aidha, Bodi pia imemteua, Rashid Seif Mohamed, kuwa msaidizi wa Mtendaji Mkuu (Assistant CEO). Rashid ni mhitimu wa Shahada ya Umahiri ya utawala wa michezo (Master’s in Sports Management) pamoja na ngazi…

Read More

Kocha wa zamani wa Mamelodi Sundowns Ian Gorowa ameachana na kazi hiyo ya kufundisha mpira wa miguu alikojipatia umaarufu na kuwa muhubiri wa Injili. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Cape Town Spurs mwenyewe miaka 53, amefichua kuwa sasa ni mchungaji wa wakati wote katika kanisa la Apostolic Faith Mission, na hana mpango wa kurejea kwenye soka. Kazi ya mwisho ya Gorowa katika soka ilikuwa mwaka wa 2014 kama kocha wa timu ya taifa ya Zimbabwe, karibu muongo mmoja baada ya kuachana na Sundowns. “Ndiyo, nimeachana na ukocha kama taaluma sitarudi ,Ninashinda roho sasa,Safari kama mchungaji imekuwa nzuri sana. Ninaifurahia inatimiza…

Read More

AHMED Ally, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba SC, ameweka wazi kuwa tofauti ya pointi kwenye msimamo wa ligi inasababishwa na idadi ya mechi ambazo timu zimecheza. Kwa mujibu wa mwenendo wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2025/26, vinara kwa sasa ni Yanga SC inayoongozwa na Kocha Pedro Gonçalves, ikiwa imecheza michezo minne na kujikusanyia pointi 10. Simba SC inashika nafasi ya pili, ikiwa imeshuka dimbani mara tatu pekee sawa na dakika 270, na imekusanya jumla ya pointi 9. Mchezo wao wa mwisho kabla ya ligi kusimama ulikuwa dhidi ya JKT Tanzania ugenini, ambapo Simba ilipata…

Read More

Msimu wa 2025/26 umeendelea kuwa mgumu kwa mshambuliaji wa Simba SC, Steven Mukwala, ambaye bado hajafanikiwa kufungua akaunti ya mabao kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara. Mukwala hajaonyesha ubora unaotarajiwa kutoka kwake, licha ya kupata nafasi kadhaa za kufunga katika mechi za ushindani. Kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania uliochezwa Novemba 8, 2025, straika huyo alikosa nafasi tatu za wazi, moja kati ya hizo ikiwa ni clear chance ambayo alishindwa kutumia vyema na badala yake kumpasia mlinda mlango wa JKT Tanzania aliyeokoa hatari hiyo. Mchezaji huyo alitumia dakika 60 uwanjani kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Jonathan Sowah, ambaye alifunga bao…

Read More

Rais wa TFF, Wallace Karia ametembelea mazoezi ya Timu ya Taifa @Taifastars_ inayojiandaa na mchezo wa kirafiki kwenye kalenda ya FIFA dhidi ya Kuwait utakaochezwa Novemba 15,2025 Nchini Misri. Taifa Stars ambao wameingia kambini siku ya jana wanafanya mazoezi katika dimba la Gymkhana kabla ya kusafiri kuelekea Nchini Misri kwa ajili ya mchezo huo.

Read More

Taarifa zinaeleza kuwa Senzo Mazingiza, aliyewahi kuwa Mtendaji Mkuu (CEO) wa vilabu vikubwa vya Tanzania — Simba SC na Yanga SC, anatarajiwa kujiunga na TRA Sports Club kama CEO mpya wa klabu hiyo. Senzo anatajwa kupewa jukumu la kuboresha mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo, kuijenga katika misingi imara ya kisasa ya soka, na kuhakikisha TRA Sports Club inakuwa miongoni mwa timu bora nchini katika miaka ijayo. Kama akiteuliwa rasmi, itakuwa ni hatua nyingine kubwa kwa Senzo, ambaye amejizolea sifa kubwa katika usimamizi wa soka la Afrika Mashariki.

Read More

UONGOZI wa Simba SC umeweka wazi kuwa unajivunia uwepo wa kiungo mshambuliaji Abraham Morice kutokana na kazi kubwa anayofanya kwenye mechi za ushindani. Nyota huyo amekuwa kwenye ubora katika mechi ambazo anapata nafasi ya kucheza akianzia benchi ama kikosi cha kwanza amekuwa akionyesha kitu. Katika mchezo wa Ligi Kuu Bara ya NBC dhidi ya JKT Tanzania uliochezwa Novemba 8,2025 alitoa pasi ya bao kwa Jonathan Sowah alipoanzia benchi. Wachezaji hao wote wawili kwenye mchezo huo walianzia benchi na mwisho ubao ulisoma JKT Tanzania 1-2 Simba SC walipovuna pointi tatu muhimu. Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba…

Read More

Jonathan Sowah, mshambuliaji wa Simba SC, amezua mjadala baada ya bao lake dhidi ya JKT Tanzania kutajwa kuwa lina utata, ikidaiwa huenda alikuwa ameotea wakati akifunga. Bao hilo lilifungwa Novemba 8, 2025 kwenye Uwanja wa Meja Isamuhyo, mchezo ambao uliisha kwa JKT Tanzania 1-2 Simba SC. Katika mchezo huo uliojaa ushindani, JKT Tanzania walitangulia kupata bao kupitia Edward Songo, kabla ya Simba SC kusawazisha na kuongeza kupitia mabao ya Wilson Nangu aliyefunga kwa kichwa, na Jonathan Sowah aliyepachika bao baada ya kupokea pasi kutoka kwa Morice Abraham. Akizungumzia ushindi huo, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC…

Read More

Tottenham Hotspur wamemfanya winga wa Everton, Iliman Ndiaye, 25, kuwa mchezaji anayelengwa zaidi, lakini Newcastle United, Juventus, AC Milan na Atletico Madrid pia wanamfuatilia mchezaji huyo. (TeamTalk) Chelsea na Tottenham wanafikiria uhamisho wa Januari kwa mshambuliaji wa Juventus na Canada Jonathan David, 25 (TuttoMercatoWeb) Everton inaweza kuhamia kwa mshambuliaji wa Midtjylland, Franculino Dju, 21, mwezi Januari lakini inakabiliwa na ushindani kutoka Bologna kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Guinea-Bissau. (Sun) Liverpool wako tayari kutoa euro milioni 100 (£88m) kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Italia Alessandro Bastoni, 26, kutoka Inter. (Il Giorno) Real Madrid watakuwa tayari kutumia euro milioni 250 (£220m)…

Read More

Klabu ya JKT Tanzania iliyowakaribisha Simba SC kwa maneno makali kabla ya mchezo, ikiwemo kuahidi kuwa Wekundu wa Msimbazi “hawatatoka salama” katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, imejikuta ikiondoka uwanjani hapo ikiwa na hasara ya pointi tatu. Katika mchezo uliochezwa jana, Simba SC walifanikiwa kushinda kwa mabao 2-1, ushindi uliokuja kama majibu ya moja kwa moja kwa kauli za JKT zilizowahi kuenea mitandaoni muda mfupi kabla ya mchezo. JKT Tanzania walikuwa wanajivunia matokeo yao ya hapo nyuma dhidi ya Azam FC, ambapo walitoka sare ya 1-1, na kuamini kuwa na wao pia wangeweza kuidhibiti Simba katika uwanja huo. Hata hivyo,…

Read More

Leo hii ukiwa na Meridianbet unaweza ukabadilisha maisha yako kirahisi sana kwani Meridianbet wamekupa nafasi kubwa kwa kukuletea mechi zote za ligi mbalimbali ambazo pia zina machaguo zaidi ya 1000. Tukianza na LALIGA kule Hispania itaendelea ambapo bingwa wa mtetezi wa ligi Real Madrid atakuwa ugenini kumenyana dhidi ya Rayo Vallecano ambao wapo nafasi ya 10, huku takwimu ikionesha kuwa msimu uliopita Real waliondoka na pointi 4. Je Alonso kuchukua ushindi huu na kuendelea kukaa kileleni?. Beti hapa. Vilevile Real Betis atakiwasha dhidi ya Valencia kule ugenini huku wakali wa ubashiri Meridianbet wakiipa mechi hii ODDS KUBWA na machaguo zaidi ya 1000. Kila mtu anataka ushindi siku ya leo. Je…

Read More

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limetangaza rasmi kuwa Tuzo za CAF 2025 zitafanyika mjini Rabat, Morocco siku ya Jumatano, Novemba 19, 2025. Kwa mujibu wa taarifa ya CAF, hafla hiyo ya kifahari itaanza saa 1 jioni kwa saa za Morocco (saa 3 usiku kwa saa za Cairo), katika ukumbi ambao bado haujatajwa. Tuzo hizo ni mojawapo ya matukio makubwa zaidi katika kalenda ya soka la Afrika, zikilenga kutambua na kuheshimu wanamichezo bora wa bara katika vipengele mbalimbali. Miongoni mwa tuzo zitakazotolewa ni: 🏆 Mchezaji Bora wa Afrika (Wanaume na Wanawake) 🎯 Kocha Bora wa CAF (Wanaume na Wanawake) 🌍…

Read More

Mchezo mkali wa Ligi Kuu NBC msimu wa 2025/26 unaendelea kupamba moto, ambapo timu ya JKT Tanzania inatarajiwa kuikaribisha Simba SC katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo mnamo Novemba 8, 2025. Katika mchezo wa mwisho kukutana msimu uliopita, Simba SC ilivuna pointi tatu ugenini baada ya kushinda kwa bao 1-0, bao lililofungwa na Fabrince Ngoma ambaye kwa sasa hayupo kwenye kikosi cha Simba msimu huu. Hivyo, mchezo wa safari hii unatarajiwa kuwa na upeo tofauti kutokana na mabadiliko ya vikosi na mbinu za makocha. Akizungumza kuelekea mchezo huo, Kocha Msaidizi wa Simba SC, Seleman Matola, amesema maandalizi wameyafanya kikamilifu na…

Read More

Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) ni taasisi ya serikali iliyoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Na. 21 ya mwaka 1973 kwa lengo la kusimamia na kuratibu Mitihani ya Kitaifa nchini Tanzania. Kabla ya kuanzishwa kwake, mitihani yote ya kitaifa ilikuwa ikishughulikiwa na Kitengo cha Mitaala na Mitihani kilichokuwa chini ya Wizara ya Elimu. Hatua ya kuanzisha NECTA ilikuja baada ya Tanzania Bara kujitoa katika Baraza la Mitihani la Afrika Mashariki (EAEC) mwaka 1971, ambapo Zanzibar yenyewe ilijitoa mwaka 1970. Hivyo, NECTA ilipewa jukumu kamili la kusimamia mitihani, huku masuala ya mitaala yakiendelea kusimamiwa na Wizara ya Elimu kwa kushirikiana na…

Read More

Mshambuliaji wa Yanga SC, Clement Mzize, ataukosa mchezo ujao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC FC utakaopigwa Novemba 9, 2025 saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa KMC Complex, kutokana na majeraha ya goti. Mzize, ambaye amefanyiwa upasuaji wa goti lililokuwa likimsumbua kwa muda mrefu, anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki nane hadi kumi, hali inayomfanya kukosa michezo kadhaa muhimu ya ligi. Nyota huyo pia alikosekana katika mchezo uliopita ambapo Yanga SC iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar Oktoba 28, 2025 kwenye uwanja huohuo, mabao yakifungwa na Zimbwe Jr pamoja na Ecua.…

Read More

Klabu ya Simba itaanzia nyumbani mchezo wake wa kwanza wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Petro Atlético de Luanda ya Angola. Ratiba ya Simba katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika (CAFCL). KUNDI D Mechi ya Kwanza Kati ya Nov 21-23 Simba vs Atletico Petroleos Mechi ya Pili Kati ya Nov 28-30 Stade Malien vs Simba Mechi ya Tatu Kati ya Jan 23-25 ES Tunis vs Simba Mechi ya Nne Kati ya Jan 30-1 Feb Simba vs ES Tunis Mechi ya 5 Kati ya Feb 6-8 Atletico Petroleos vs Simba Mechi ya 6…

Read More

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara TPLB imetangaza rasmi kurejea kwa michezo ya Ligi Kuu tarehe 08 mwezi Novemba, 2025 baada ya kusitishwa siku kadhaa zilizopita kutokana na sababu za kiusalama. Novemba 8 itachezwa michezo miwili ambapo Pamba Jiji atamkaribisha Singida BS CCM Kirumba saa 10 jioni na saa 01 Jioni utachezwa mchezo wa pili kwenye dimb la Meja Isamuhyo kati ya JKT Tanzania dhidi ya Simba. Wananchi watashuka dimbani KMC Complex Novemba 9 kucheza dhidi ya KMC saa kumi jioni wakati Azam FC akiwa mgeni wa Namungo Majaliwa Stadium saa 1 Jioni.

Read More

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemtangaza Kocha wa Singida Black Stars, Miguel Angel Gamondi kutoka Argentina, kuwa Kaimu Kocha Mkuu wa Taifa Stars. Uteuzi huu unakuja baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Hemed Suleiman “Morocco”, kuachana na TFF kwa makubaliano ya pande zote mbili. Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na TFF leo, Novemba 4, 2025, mazungumzo kati ya TFF na uongozi wa Singida Black Stars tayari yamekamilika, na Gamondi amekubali kuchukua majukumu hayo mapya. Kocha huyo ambaye aliwahi pia kuinoa Young Africans SC (Yanga), anatarajiwa kuiongoza Taifa Stars kwenye michuano ya Fainali za Kombe la Mataifa…

Read More

Kwa mara ya kwanza kwenye historia, Ligi kuu soka Tanzania imeingiza timu 4 kwenye hatua ya makundi ya michuano ya CAF kwa ngazi ya klabu. Timu za Tanzania zilizofuzu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu ni Simba SC na Yanga SC. Timu za Tanzania zilizofuzu kwenye Kombe la shirikisho Afrika msimu huu ni Azam FC na Singida Black Stars FC.

Read More