Author: Admin

Tume ya Uchaguzi mkuu Tanzania INEC kupitia Halmshauri mbalimbali imetoa Orodha ya majina ya walioitwa kwenye usaili kusimamia wapiga kura na kuongoza zoezi la kupiga kura Hapo chini kuna PDF ya majina walioitw kwenye usaili halmashauri mbalimbali: Halmshauri ya Rombo Manispaa ya Bukoba Mjini Manispaa ya Newala Mjini Halmashauri ya Lindi Mjini Jimboa la Dodoma mjini Wilaya ya Kisarawe Halmshauri ya wilaya ya Bagamoyo Jimbo la Lulindi na Ndanda Jimbo la Mbeya Vijijini Jimbo la Mtumba Halmashauri ya Mbulu Musoma Vijijini Wilaya ya Nkasi Wilaya ya Korogwe Pangani Kilosa Jimbo la Hai Jimbo la Kasulu vijijini Mtwara Mjini Tabora Mjini…

Read More

Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga Ally Kamwe amefunguka muda mfupi baada ya aliyekuwa Skauti Mkuu wa Simba kutangaza kujiuzulu nafasi yake. Ally Kamwe ameandika ujumbe unaohusishwa kuwa unawalenga watani zao Simba akisisitiza kuwa taarifa alizozipata kupata kwa jasusi wao ni kuwa muda wowote taarifa ya CEO kujiuzulu itatoka. “Jasusi wetu Hana Bayaaa.. Jana alisema Kuna Kikao na Leo watu wameanza kujiuzulu mmoja mmoja” “Muda wowote Taarifa ya CEO kujiuzulu itatoka .. Wanajaribu kumshauri asiondoke Lakini mpaka asubuhi ya Leo, Bi Dada kashikilia msimamo wake” “Hoja ya Dada ni kupelekwa pelekwa kama Ng’ombe bila kushirikishwa.. Viongozi wa Juu…

Read More

Klabu ya Simba Sc imemtambulisha kocha Dimitri Pantev kama meneja wa timu hiyo huku vyanzo vikieleza kocha mkuu wa Wekundu hao wa Msimbazi atakuwa Selemani Matola kwenye makaratasi ingawa Pandev atakuwa kiongozi na mtendaji mbele ya benchi la ufundi wakati wa michezo. Kocha huyo raia wa Bulgaria ana leseni ya UEFA A hivyo hana vigezo ya kusimama kama Kocha Mkuu kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika kwa kuwa anatakiwa kuwa na leseni za CAF A au CAF Pro Licence au UEFA Pro Licence kwa Kocha anayetumia leseni kutoka Mashirikisho mengine nje na CAF. Hali hii ilishawahi kutokea huko Azam Fc…

Read More

Aliyekuwa Kocha wa Gaborone Utd,raia wa Bulgaria Dimitar Pantev (49) ameagwa rasmi ndani ya klabu hiyo. Kocha huyo ambaye ameisadia klabu ya Gaborone kuibuka mabingwa wa ligi kuu ya Botswana taarifa zinasema tayari amemalizana na Wekundu wa Msimbazi kuwa kuchukua mikoba ya Fadlu Davids.

Read More

INAELEZWA kuwa Bulgaria Dimitar Pantev mwenye miaka 49 huenda akapewa mikoba ya kukinoa kikosi cha Simba SC ambacho kwa sasa hakina kocha mkuu. Taarifa zinaeleza kuwa muafaka mzuri umefikiwa kwa pande zote mbili ambapo mpango kazi ukikamilika atakuja Tanzania kuchukua nafasi ya Fadlu Davids aliyepata dili Raja Casablanca na tayari ameanza kazi. Inaelezwa kuwa Simba wamekubali kulipa fidia za kuvunja mkataba wa kocha huyo aliyekuwa anaifundisha Klabu ya Gaborone United ya Botswana. Ikumbukwe kwamba Gaborone United ilicheza na Simba SC katika Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali, katika mchezo uliochezwa Dar kocha huyo alikuwa kwenye benchi la ufundi la…

Read More

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Uingereza Thomas Tuchel ametangaza kikosi cha wachezaji kitakachoingia kambini kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Wales na mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Latvia Octoba 14. Katika kikosi hicho cha wachezaji 24 Tuchel hajawajumuisha nyota Jack Grealish, Jude Bellingham na Phil Foden huku akiweka wazi kuwa ni kwa kuzingatia mbinu za mechi na ratiba za wachezaji na kusema bado wana nafasi ya kurejea katika  mechi zijazo.

Read More

Wakati tetesi za aliyekuwa kocha wa Gaborone United raia wa Bulgaria Dimitar Nikolaev Pantev kujiunga na wekundu wa Msimbazi kuwa kocha mkuu mpya wa klabu hiyo upande wa pili kwa Mabingwa wa Tanzania tetesi za kuachana na kocha wao Romain Folz zimeshika kasi. Taarifa hizo zinazohusisha wababe wa soka la Tanzania kama zikiwa za kweli basi makocha hao watapishana mmoja akiondoka kwenye klabu yenye makao makuu mitaa ya Jangwani huku mwingine akijiunga na klabu yake ya mitaa ya Msimbazi.

Read More

Cv ya Dimitar Pantev Kocha Mpya wa Simba Sc 2025 Klabu ya Simba SC imethibitisha rasmi kumteua Dimitar Pantev kuwa kocha mkuu mpya wa timu hiyo kwa msimu wa 2025, akichukua mikoba iliyoachwa wazi na Fadlu Davids aliyetimkia Raja Casablanca ya Morocco. Pantev, raia wa Bulgaria mwenye umri wa miaka 49, anakuja nchini akiwa na rekodi ya mafanikio barani Afrika baada ya kuinoa klabu kadhaa na kushinda mataji ya ligi katika mataifa mawili tofauti. Kocha huyu aliyetambulika kwa falsafa yake ya soka la kushambulia, amesaini mkataba wa miaka miwili na Simba SC, klabu inayolenga kurejea kwenye utawala wa soka la…

Read More

Uongozi wa Klabu ya Coastal Union umetangaza rasmi kufikia makubaliano ya pande zote mbili kusitisha kandarasi ya Kocha Mkuu, Ali Mohammed Ameir. Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imemshukuru Ameir kwa mchango na huduma yake kwa kipindi chote ambacho aliiongoza timu, ikisisitiza mchango wake kuwa wa thamani kubwa katika maendeleo ya kikosi hicho. Coastal Union wameweka wazi kuwa watatoa taarifa kwa umma hivi karibuni kuhusu mabadiliko na muundo mpya wa benchi la ufundi muda mchache ujao.

Read More

Mwanahabari wa michezo, @abdulmkeyenge1, amemtolea povu mchezaji Elie Mpanzu Kibisawala, akimtaka kurejea katika ubora wake wa awali na kucheza kama staa halisi wa timu. “Mpanzu Kibisawala ajifunze kucheza kama staa wa timu. Staa wa timu hachezi anavyocheza yeye. Anacheza kwa kumiminika jasho na kuwanyima raha wapinzani muda mwingi sio kutolewa kama ilivyo kwake. Now days ameanza kuwa mchezaji wa kawaida. Ni kawaida mno, lakini watu wanajua quality kubwa iliyoko miguuni mwake. Huyu sio yeye. Arudi nyuma na kuzitazama video zake atajua nini Simba inataka kutoka kwake.” Alisema @abdulmkeyenge1

Read More

Beki Rushine De Reuck amefunga bao lake la pili la msimu na kuwa kinara wa magoli akiwa na magoli mawili sawa na Paul Peter wa JKT Tanzania na Faisal Salum ‘Feitoto’ wa Azam FC Akizungumza amesema “Kwangu mimi ushindi wa timu ndio jambo muhimu, kuhakikisha tunafikia malengo na mafanikio ya juu, Sijui ni bahati tu kuzipata nafasi za kufunga ila lengo ni kuleta ushindi kwenye timu na nafasi ikipatikana unajarib kuitumia” Alisema Rushine De Reuck. Lakini pia Selemani Mwalimu ‘Gomez’ amefungua akaunti yake ya magoli kwenye Ligi Kuu bara msimu wa 2025/26 wakati Simba Sc ikiibuka na ushindi wa 3-0…

Read More

WAKATI tetesi zikieleza kuwa kuna uwezekano wa Roman Folz, Kocha Mkuu wa Yanga SC akakutana na Thank You taarifa zinaeleza kuwa bado yupoyupo ndani ya kikosi hicho. Yanga SC ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara ya NBC msimu wa 2025/26 wamecheza mechi mbili pekee ambazo ni dakika 180. Mechi ya ufunguzi walipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Pamba Jiji FC mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar. Mchezo wa pili walitoshana nguvu kwa kushuhudia ubao wa Uwanja wa Sokoine, Mbeya ukisoma Mbeya City 0-0 Yanga SC. Ilikuwa ni Desemba 30 2025 walipogawana pointi mojamoja ikiwa ni sare ya kwanza…

Read More

INAELEZWA kuwa mabosi wa Simba SC wapo na hesabu za kumpa kazi Miguel Gamondi ambaye kwa sasa ni Kocha Mkuu wa Singida Black Stars. Inaelezwa kuwa Simba SC mara baada ya Fadlu Davids kubwaga manyanga walianza kufikiria kupata huduma ya Gamondi ambaye aliwahi kuinoa Yanga SC na kuipa ubingwa. Uzoefu wake kwenye soka la Afrika unatajwa kuwa sababu kubwa kwa Simba SC kutuma ofa ndani ya Singida Black Stars kupata saini yake. Taarifa zinaeleza kuwa uwezekano wa Simba SC kumpata Gamondi ni mdogo kwa sasa kutokana na mpango kazi uliopo kwa mabosi wa Singida Black Stars. Ushiriki wa Singida Black…

Read More

WAKIWA kwenye hesabu za kumtafuta kocha mpya, Msimbazi wataendelea kukosa huduma ya wachezaji wawili kwenye mchezo wa leo Oktoba Mosi 2025 Uwanja wa Mkapa dhidi ya Namungo. Simba SC kwa sasa ipo chini ya kocha msaidizi Suleman Matola ambaye atakiongoza kikosi hicho kwenye mchezo dhidi ya Namungo FC. Katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United, Simba SC ilikuwa chini ya Kocha Mkuu Hemed Morocco ambaye alikuwa hapo kwa muda maalumu kwa mchezo huo. Hayo yote yalitokana na Fadlu Davids ambaye alikuwa na timu nchini Misri kwenye kambi kupata dili katika timu nyingine ambayo ni Raja Casablanca…

Read More

Msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania 2025/2026 Msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania 2025/2026Msimu wa 2025/2026 wa Ligi Kuu NBC Tanzania umeanza rasmi leo, Septemba 17, ambapo mashabiki wa soka nchini wamefurahia kushuhudia pambano la ufunguzi lililozikutanisha timu za Coastal Union na Tanzania Prisons. Katika mchezo huo uliojaa ushindani, Coastal Union iliibuka kidedea baada ya kuibamiza Tanzania Prisons bao 1–0, ushindi ambao uliwapa mwanzo mzuri katika safari yao ya msimu huu mpya wa ligi. Msimu huu wa 2025/2026 unatarajiwa kuwa wenye ushindani mkubwa zaidi ukizangatia mabadiliko makubwa ya vikosi na benchi la ufundi yaliyofanywa na vilabu mbalimbali haswa Azam Fc,…

Read More

Simba vs Namungo FC Leo 01/10/2025 Saa Ngapi? Wekundu wa Msimbazi Simba leo watakua dimbani kuzisaka pointi tatu muhimu za Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara 2025/2026 mbele ya wageni wao Namungo FC katika mchezo unaotajwa kuwa wa ushindani mkubwa. Mchezo huu utapigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 2:15 usiku, ukitarajiwa kuvuta hisia za mashabiki kutokana na historia na rekodi za timu hizi mbili. Simba vs Namungo FC Leo Saa Ngapi? Mchezo kati ya Simba SC dhidi ya Namungo FC utafanyika Leo, Jumatano tarehe 01 Oktoba 2025, kuanzia saa 2:15 usiku, kwenye Uwanja wa…

Read More

Klabu ya PSG imethibitisha kuwakosa wachezaji wake wanne kwenye mchezo wa ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona siku ya kesho ambao ni Khvicha Kvaratskhelia, Désiré Doué, Marquinhos na Ousmane Dembélé . Kvaratskhelia alipata jeraha la paja kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Auxerre hivyo ataukosa mchezo huo wakati pia timu hiyo ikiendelea kumkosa mshindi wa Ballon d’Or, Ousmane Dembele, winga Desire Doue na beki wa kati Marquinhos ambao pia wanaendelea kuuguza majeraha yao.

Read More