Author: Admin

SEPTEMBA 20 2025 ni Gaborone United vs Simba SC mchezo wa hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo wababe hawa watakuwa katika dakika 90 za kusaka ushindi kabla ya mchezo wa pili utakaotoa mshindi wa jumla atakayekwenda hatua inayofuata. Fadlu Davids, Kocha Mkuu wa Simba SC amesema wanachohitaji ni ushindi ili kutimiza malengo ya kwenda hatua ya makundi. “Ili upate nafasi ya kwenda hatua ya makundi ambacho kinahitajika ni ushindi. Mechi zote iwe ugenini na nyumbani ni muhimu kushinda na sisi tumejiandaa kufanya hivyo. “Timu yangu imecheza mechi mbili zenye uzito mkubwa Simba Day na Ngao ya Jamii kwa…

Read More

FT: Wiliete SC 0-3 Yanga SC Dakika ya 88 nahodha wa Wiliete anaonyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea faulo nyota wa Yanga SC Dakika ya 86 Yanga SC wanapata pigo huru nje kidogo ya 18 linapigwa na Ecua. Goooooal Yanga SC Dakika ya 82 Prince Dube anafunga goal la 3 kwa Yanga SC akiwa ndani ya 18 Dakika ya 75 mfungaji wa bao la kwanza kwa Yanga SC, Aziz anatoka nafasi yake inachukuliwa na Conte, Zimbwe Jr naye anaingia akichukua nafasi ya Boka., Duke Abuya anakuwa mchezaji wa kwanza kuonyeshwa kadi ya njano kwenye mchezo wa leo. Goooooal Yanga SC Dakika…

Read More

SIMBA SC baada ya kupoteza Ngao ya Jamii, Septemba 16 2025 mbele ya Yanga SC msafara ulikwea pipa na umefika salama Botswana kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali dhidi ya Gaborone United. Hii hapa orodha ya wachezaji wa Simba SC waliopo Botswana watakuwa na kazi Jumamosi ya Septemba 20 2025:- Makipa Moussa Camara, Yakoub Suleiman na Alexender Erasto. Mabeki Shomari Kapombe, Anthony Mligo. Rushine De Reuck, Wilson Nangu, Naby Camara. Viungo Yusuph Kagoma, Allasane Kante, Kibu Dennis, Ellie Mpanzu. Ladack Chasambi, Mzamiru Yassin, Neo Maema. Joshua Mutale, Jean Ahoua, Daud…

Read More

IBRAHIM Bacca beki wa Yanga SC amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Williete SC ya Angola unaotarajiwa kuchezwa leo Septemba 19 2025. Septemba 18 2025 kikosi cha Yanga SC chini ya Kocha Mkuu, Romain Folz kilifanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo wao wakiwa ugenini. “Kila mchezaji yupo tayari na Wananchi waendelee kutuombea kwa ajili ya mchezo wetu tunamshukuru Mungu temefika salama. Nimekuwa hapa kwenye majukumu yangu na nikipata nafasi nitahakikisha tunapata matokeo mazuri ugenini. “Kupata nafasi kwenye mechi ambazo tunacheza kwangu ni jambo zuri hasa ukizingatia hii ni kazi yangu. Wachezaji…

Read More

Mchambuzi nguli wa soka nchini, Saleh Jembe kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika taarifa kuhusiana na Kocha wa Klabu ya Simba, Fadlu David’s kuhusu kuondoka klabuni hapo. “Hii ndio picha ya mwisho ya Kocha Fadlu David’s ambaye ameamua KUACHIA NGAZI SIMBA” “Taarifa zinaeleza aligoma hata kupanda ndege kwenda Botswana” “Alipigiwa simu na MO (Dewji) akamsihi asifanye hivyo, ndio akapanda ndege na kufika huko KATANGAZA KUACHANA NA Simba,” kilieleza chanzo, ameandika Saleh Jembe. Je, Simba wataweza kumbakisha Fadlu David’s Msimbazi? Mpaka sasa bado hakuna taarifa rasmi za kutoka ndani ya klabu ya simba juu ya ukweli wa taarifa hiyo hivyo tuendelee…

Read More

Klabu ya Singida Black Stars imeanza mazoezi kwenye ardhi ya ugenini Kigali Rwanda mara tu baada ya kuwasili Nchini humo kuelekea kwenye mchezo wao dhidi ya Rayon Sports. Wawakilishi hao wa Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho msimu huu wamefanya mazoezi ya kwanza Nchini humo asubuhi ya leo katika dimba la Pele litakalotumika kwenye mchezo wao Jumamosi septemba 20,2025.

Read More

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC amesema kuwa Simba SC ya msimu huu wa 2025/26  ni mbovu kuliko ile ya msimu uliopita wa 2024/25. Yanga SC kwa sasa mkononi wana taji la Ngao ya Jamii walitwaa kwa kushinda mbele ya Simba SC mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 16 2025 ikiwa ni mchezo wa ufunguzi wa msimu mpya wa 2025/26.. Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga SC 1-0 Simba SC, bao la ushindi likifungwa na Pacome dakika ya 53 akiwa ndani ya 18 alipomtungua Moussa Camara kipa namba moja wa Simba SC. Kamwe amesema:…

Read More

WIKIENDI imechangamka kwenye anga la kimataifa kutokana na timu zote nne kutoka Tanzania kuwa katika kazi. Ijumaa, Uwanja wa 11 de Novembro, Wiliete Sports vs Yanga SC, saa 12:00 jioni. Simba SC Jumamosi Septemba 20 itakuwa uwanjani kumenyana na Gaborone United saa 2:00 usiku. Yanga SC na Simba SC ni katika Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni hatua ya awali. Azam FC wapo Sudan Kusini watacheza dhidi ya Al Merriekh Bentiu Septemba 20 saa 11:00 jioni. Singida Black Stars wapo Reanda watakuwa na mchezo dhidi ya Rayon Sports Septemba 20 2025. Azam FC na Singida Black Stars ni katika Kombe…

Read More

NBC Premier League tayari pazia lake limefunguliwa na Septemba 17 mechi mbili za ufunguzi zilichezwa. KMC 1-0 Dodoma Jiji huu ulichezwa Uwanja wa KMC Complex na mtupiaji wa bao la kwanza msimu wa 2025/26 ni Daruesh Saliboko dakika ya 56 likidumu mpaka mwisho wa dakika 90. Mchezo wa pili ilikuwa Coastal Union 1-0 Tanzania Prisons huu ulichezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Bao la Coastal Union lilifungwa na Cleofance Mkandala dakika ya 35. Septemba 18 2025 kuna mechi tatu ambazo zinatarajiwa kuchezwa itakuwa namna hii:- Saa 8:00 mchana, Fountain Gate watakuwa Uwanja wa Tanzanite Kwaraa vs Mbeya City. Saa 10:15 jioni…

Read More

Kikosi cha Mnyama wa Afrika Mashariki, Simba SC, kimewasili nchini Botswana kwaajili ya mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) dhidi ya wenyeji Gaborone United. Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Septemba 20 kwenye Uwanja wa Obed Itani Chilume, ambapo mashabiki wa soka wanatarajia burudani ya aina yake. Simba SC inashuka dimbani ikiwa na dhamira ya kuhakikisha inapata matokeo mazuri ugenini, ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele katika hatua zinazofuata za michuano hii mikubwa barani Afrika.

Read More

Ramla Ali, mwanamichezo wa kwanza kuwakilisha Somalia katika ndondi kwenye Michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020, na mwanamke wa kwanza wa Kisomali kuingia katika mchezo huo kiushindani. Ali alizaliwa mwaka 1989, na familia yake iliondoka Somalia isiyo salama mapema miaka ya 1990 na kuwasili London miaka michache baadaye. Alianza kwenda gym baada ya kuanza kunyanyaswa shuleni kwa sababu ya kuwa na uzito mkubwa. Ali alipenda sana masomo ya mazoezi ya ndondi, na baadaye akahamia gym ya ndondi ya eneo hilo. Huko, kocha aligundua kipaji chake na hatimaye akamshawishi kushindana, jambo lililosababisha pambano lake la kwanza la ushindani akiwa na umri…

Read More

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC, Yanga SC chini ya Kocha Mkuu Romain Folz, wameondoka nchini kuelekea Angola kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Septemba 16, 2025 majira ya saa 11:00 jioni, Yanga SC walifanikiwa kutetea taji la Ngao ya Jamii baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wapinzani wao wa jadi Simba SC kwenye fainali iliyochezwa dakika 90 Uwanja wa Benjamin Mkapa. Bao pekee la mchezo huo lilifungwa dakika ya 53 na Pacome, ambaye aliwanyanyua mashabiki wa Yanga baada ya kumtungua kipa namba moja wa Simba, Moussa…

Read More

KIKOSI cha Simba SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids asubuhi ya Septemba 17 2025 kimeanza safari ya kuelekea nchini Botswana kwa kupitia nchini Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone FC. Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Jumamosi hii Septemba 20 huko Botswana kabla ya wiki moja kurudiana tena kwenye Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam. Simba imeondoka leo ikiwa ni saa chache zimeyeyuka tangu watoke kufungwa bao 1-0 katika Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga SC Septemba 16 2025 katika mchezo wa Ngao ya Jamii. Bao pekee la ushindi…

Read More

Jina la kocha wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho linatajwa huenda likarejea kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati huu ambapo mazungumzo yanaendelea ili akinoe kikosi cha Benfica. Benfica ilimtimua kocha wao siku ya Jumanne usiku kufuatia kipigo cha 3-2 walichokipata kutoka kwa klabu ya Qarabag ya Azerbaijani. Kwenye mchezo huo Benfica ilitangulia kwa mabao 2-0 lakini iliruhusu wageni wao kupambana na kushinda mchezo huo. Bruno Lage katika mwaka wake mmoja kama kocha wa Benfica, aliwaongoza kutwaa Kombe la Ligi ya Ureno na kumaliza katika nafasi ya pili msimu uliopita. Rais wa Benfica, Rui Costa amewaambia waandishi wa habari mapema leo…

Read More

YANGA SC chini ya Kocha Mkuu, Romain Folz imetwaa taji la Ngao ya Jamii kwa ushindi mbele ya watani zao wa jadi Simba SC katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa. Bao pekee la ushindi kwa Yanga SC limefungwa na Pacome dakika ya 53 akiwa ndani ya 18 akimfunga kipa Moussa Camara ambaye alianza kikosi cha kwanza. Yanga SC wameanza msimu wa 2025/26 wakitwaa taji ambalo walikuwa wanalitetea baada ya kutwaa msimu wa 2024/25 mbele ya Azam FC. Simba SC haijawa na bahati mbele ya Yanga SC kwa kuwa msimu wa 2024/25 katika mechi tatu walizokutana uwanjani walikwama kupata ushindi. Kwa…

Read More