Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Contact Us
    • Privacy Policy
    Facebook Instagram YouTube
    Chikao Media
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • MAGAZETI YA LEO
    • TETESI ZA SOKA
    • BOXING
    • FORUM
    Chikao Media
    Home ยป BAADA YA KUPOTEZA KARIAKOO DABI, SIMBA YATIMKA NCHINI
    KITAIFA

    BAADA YA KUPOTEZA KARIAKOO DABI, SIMBA YATIMKA NCHINI

    By AdminSeptember 17, 2025No Comments1 Min Read
    Share WhatsApp Facebook Twitter Pinterest Telegram Email Copy Link
    Follow Us
    Facebook Instagram YouTube
    simba
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email Copy Link

    KIKOSI cha Simba SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids asubuhi ya Septemba 17 2025 kimeanza safari ya kuelekea nchini Botswana kwa kupitia nchini Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone FC.

    Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Jumamosi hii Septemba 20 huko Botswana kabla ya wiki moja kurudiana tena kwenye Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.

    Simba imeondoka leo ikiwa ni saa chache zimeyeyuka tangu watoke kufungwa bao 1-0 katika Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga SC Septemba 16 2025 katika mchezo wa Ngao ya Jamii.

    Bao pekee la ushindi kwenye mchezo huo wa ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC msimu wa 2025/26 limefungwa na Pacome Zouzoua.

    Miongoni mwa wachezaji wa Simba SC ambao wapo kwenye msafara huo ni Moussa Camara, Jonathan Sowah, Joshua Mutale, Seleman Mwalimu, Wilson Nangu.

    Rekodi zinaonyesha kuwa inakuwa ni mara ya sita mfululizo Simba SC kupoteza mbele ya Yanga SC katika mechi za ushindani. Ikumbukwe kwamba msimu wa 2024/25 katika mechi mbili za ligi Simba SC ilifungwa nje ndani.

    Simba SC
    Follow on Facebook Follow on Instagram Follow on YouTube
    Share. WhatsApp Facebook Twitter Pinterest Email Copy Link
    Previous ArticleMOURINHO ATAJWA KUCHUKUA MIKOBA YA KOCHA MKUU WA BENFICA
    Next Article YANGA YAIANZA SAFARI YA ANGOLA BAADA YA KUMCHAPA MTANI

    Related Posts

    Ujenzi wa Arena, Serikali Yatenga Bil400

    April 3, 2026

    Selemani Mwalimu Yupo Anakuja, Mjiandae

    April 3, 2026

    MSIGWA AELEZA SABABU ZA KUONGEZEKA GHARAMA UWANJA WA ARUSHA

    March 31, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    Bernardo Apewa Thank You Rasmi Man City

    Ujenzi wa Arena, Serikali Yatenga Bil400

    Selemani Mwalimu Yupo Anakuja, Mjiandae

    MSIGWA AELEZA SABABU ZA KUONGEZEKA GHARAMA UWANJA WA ARUSHA

    Neymar amuachia Mungu kutoitwa timu ya Taifa

    “Nimehuzunika,Nimeumia lakini ndoto bado inaishi”Neymar Jr.

    © 2026 CHIKAO MEDIA | All Rights Are Reserved
    • Contact Us
    • Privacy Policy

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.