Author: Admin

Makamu wa Rais wa klabu ya Yanga @arafat__ahametangaza bajeti ya klabu kwa msimu wa 2025/26 kuwa ni Shilingi Bilioni 33 za Kitanzania. MAPATO • Udhamini na Haki za Matangazo: 11,430,468,874 • Mapato ya Milangoni: 1,971,058,386 • Ada za Uanachama: 10,152,109 • Zawadi za Ushindi: 6,425,950,640 • Mapato Mengine: 500,000,000 JUMLA YA MAPATO: 20,338,588,659 MATUMIZI • Mishahara na Marupurupu Mengine: 9,637,200,000 • Gharama za Usajili na Uhamisho wa Wachezaji: 7,489,000,000 • Gharama za Maandalizi ya Mechi, Usafiri, Chakula na Malazi: 6,146,514,986 • Motisha kwa Wachezaji na Benchi la Ufundi: 4,031,800,000 • Michango ya Kisheria: 1,261,788,000 • Gharama za Kiutawala: 1,760,875,000 •…

Read More

Barcelona wako tayari kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kumnunua nahodha wa Crystal Palace Marc Guehi ambaye pia anawaniwa na Liverpool pamoja na Real Madrid. Guehi mwenye umri wa miaka 25 amebakiza mwaka mmoja pekee katika mkataba wake na Crystal Palace, ataweza kusaini mkataba wa awali wa kandarasi na vilabu vya kigeni kuanzia Januari mwakani.

Read More

PAZIA la Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC ambayo ni namba nne kwa ubora linakaribia kufunguliwa ikiwa ni siku zinahesabiki kwa kuwa Septemba 17 kazi inatarajiwa kuanza. Leo kuna tamasha kubwa nyanda za juu Kusini, ambapo Mbeya City iliyorejea kwa mara nyingine ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika watakuwa na jambo lao. Mbey City, The Purple Nation,  Uwanja wa Sokoine, Mbeya watafanya utambulisho wa kikosi chao cha msimu wa 2025/2026 unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Miongoni mwa wachezaji waliopo Mbeya City ni kipa wa zamani wa Simba SC na Yanga SC, Beno Kakolanya…

Read More

Mabingwa wa zamani wa dunia katika masumbwi, Mike Tyson na Floyd Mayweather, wanatarajiwa kukutana ulingoni kwa pambano la maonyesho mwaka 2026. Kampuni ya yenye kujihusisha na mchezo wa masumbwi, CSI Sports, imetangaza pambano hilo kati ya Tyson, ambaye atatimiza miaka 60 mwaka ujao, na Mayweather mwenye umri wa miaka 48. Hata hivyo mpaka sasa bado hakuna taarifa kuhusu mahali ambapo pambano hilo litafanyika wala tarehe rasmi ya tukio hilo. Tyson, bingwa wa zamani wa uzito wa juu duniani, alishindwa kwa pointi dhidi ya Jake Paul katika pambano la raundi 8 lililofanyika Novemba 2024. Floyd Mayweather alitwaa mataji ya dunia katika…

Read More

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Amos Gabriel Makalla leo Ijumaa Septemba 05, 2025 ametembea na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu utakaotumika kwenye mashindano ya Mataifa ya Afrika ya AFCON mwaka 2027 unaojengwa na serikali kwa gharama ya Shilingi Bilioni 340, kwenye Kata ya Olmot Jijini Arusha. Ukaguzi huo umefanyika baada ya kikao kazi kilichofanyika kikihusisha wakuu wa idara na mamlaka zinazohusika na miundombinu ya huduma za Maji, nishati, barabara na mawasiliano katika uwanja huo, wakiazimia kuteua Kikosi kazi cha wataalamu wa sekta hizo chini ya mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,…

Read More

Nyota wa zamani wa klabu ya Simba SC aliyekiwasha msimu uliopita akiwa Yanga SC Clatous Chama anatarajiwa kufanya makubwa kwenye ligi kuu msimu ujao akiwa na Singida Black Stars. Kiungo huyo wa Kimataifa wa Zambia amejiunga na walima alizeti wa Singida na kuanza mazoezi rasmi siku ya jana. Mwamba wa Lusaka alifanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu uliopita akiwa na @yangasc akiendeleza upepo wa kutwaa makombe aliouanza wa kutwaa mataji makubwa Tanzania akiwa na wekundu wa Msimbazi. Je uwepo wa Chama ndani ya  utawasaidia kutwaa taji kubwa la michuano ya ndani msimu ujao?.

Read More

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC ameweka wazi kuwa kwa sasa Yanga SC hakuna suala la kupeana matumaini bali ni mwendelezo wa dozi pale ambapo waliishia. Ipo wazi kwamba Yanga SC ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara kuelekea msimu mpya wa 2025/26. Kwa sasa wana jambo kubwa la Wiki ya Mwananchi ambalo linatarajiwa kufanyika Uwanja wa Mkapa Septemba 12 2025. Yanga SC itacheza mchezo wa kirafiki na Klabu ya Bandari ya Kenya na kwa sasa wanaendelea na hamasa kuelekea kilele cha Wiki ya Mwananchi na slogan yao inasema Tunapiga Kichwani Tu. “Wanayanga sasa wamevuka level ya kuwa…

Read More

MO Dewji amemteua Crescentius Magori kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Simba SC hivyo mipango yote itakuwa inaendelea chini ya safu mpya ya uongozi. Mo amebainisha kuwa ameamua kufanya hivyo kutokana na  kuhudumu kwa muda mrefu na majukumu yake akiwa mbali ameone ni muhimu Klabu ya Simba SC ipate kiongozi wa bodi ambaye yupo karibu na mwenye muda wa kutosha ambaye anaweza kushiriki kwa ukaribu kabisa shughuli za kila siku. Kwa mujibu wa taarifa ya MO yeye atasalia kuwa muwekezaji na Rais wa Simba SC huku akiteua wajumbe wengine wa bodi. Ni Swedi Mkwabi ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti…

Read More

Ikiwa imetajwa kuwa huenda ilikuwa mechi yake ya mwisho ya ushindani akichezea nyumbani, Lionel Messi alifunga mabao mawili na kuiongoza Argentina kupata ushindi wa 3-0 dhidi ya Venezuela katika mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la FIFA kwenye Uwanja wa Estadio Monumental jijini Buenos Aires Alfajiri ya kuamkia leo. Hali uwanjani ilikuwa ya hisia kali na sherehe, huku mashabiki wakiheshimu mchango wa Messi kwa soka ya Argentina. Ingawa Messi hajatoa tamko la uhakika kuhusu kustaafu kwake, mechi dhidi ya Venezuela iliwasilishwa kama mechi yake ya mwisho ya kufuzu Kombe la Dunia nchini Argentina. Utendaji wake uliimarisha zaidi hadhi yake…

Read More

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo Septemba 5 2025 kitakuwa kazini kwenye mchezo dhidi ya Congo Brazzaville ambao ni maalumu kwa ajili ya kufuzu kombe la Dunia 2026 utakaochezwa  Uwanja wa Alphonce Masamba Debat. Septemba 4 2025 Stars ilifanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa ambao utatumika kwa mchezo wa leo kikiwa chini ya Kocha Mkuu, Hemed Suleman. Miongoni mwa wachezaji ambao wapo katika kikosi cha Stars ni Simon Msuva, Mbwana Sammatta, Dickson Job, Clement Mzize, Mohamed Hussen, Shomari Kapombe, Nado, Bacca. Ikumbukwe kwamba Stars imetoka kushiriki CHAN 2024 ikigotea hatua ya robo fainali na mabingwa…

Read More

Nchini Brazil kumeibuka simulizi ya kushtua baada ya bilionea mwenye umri wa miaka 31 kutoka jimbo la Rio Grande do Sul kuamua kumwachia nyota wa soka Neymar Jr mali zake zote, licha ya wawili hao kutokuwa na uhusiano wowote wa karibu au hata kukutana ana kwa ana. Kwa taarifa za vyombo vya habari vya kimataifa, kijana huyo tajiri hakuwa na mke wala watoto, na mwezi Juni 2025 aliandika wosia rasmi katika ofisi ya serikali ukiwa na mashahidi. Katika hati hiyo alielekeza majumba, kampuni na vitega uchumi vyake vyote vyenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 1 (takribani shilingi trilioni 2.5…

Read More

INGIZO jipya ndani ya kikosi cha Yanga SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Romain Folz anatajwa kuwa na balaa zito kwenye uwanja wa mazoezi. Ni kiungo ambaye anatajwa kuwa mbeba mikoba ya nyota Aziz Ki ambaye hatakuwa ndani ya kikosi cha Yanga SC msimu wa 2025/26 baada ya kupata changamoto mpya. Anaitwa Mohammed Doumbia inaelezwa kuwa katika kambi ya timu hiyo iliyopo Kijiji cha Avic Town, Kigamboni anafanya kazi kubwa katika uwanja wa mazoezi ikiwa ni balaa zito. Doumbia ni kati ya wachezaji wapya waliosajiliwa Yanga SC msimu ujao, amekuja kuwa mrithi wa Stephen Aziz Ki aliyeuzwa msimu uliopita kuelekea Wydad…

Read More

Klabu ya AS Monaco imemjumuisha mchezaji Paul Pogba katika kikosi kitakachoshiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu wa 2025/26. Pogba ambaye alijunga na Monaco kama mchezaji huru mwishoni mwa mwezi Juni baada ya kumaliza kifungo chake cha miaezi 18 alichohukumiwa kwa kosa la kutumia madawa yaliyozuiliwa michezoni anatarajia kurejea uwanjani rasmi mwezi octoba akiwa na timu yake mpya. Kiungo huyo wa zamani wa Manchester United ataikosa michezo miwili ya klabu hiyo kwenye mashindano hayo Septemba 18 dhidi ya Club Brugge na Octoba 1 dhidi ya Manchester City. Endaapo atapata nafasi ya kucheza katika michano hiyo itakuwa mara yake…

Read More

Nyota wa zamani wa Chelsea na Real Madrid, Eden Hazard ametupilia mbali mastaa Cristiano Ronaldo, Lamine na Neymar huku akimtaja Lionel Messi kuwa ndiye mpiga chenga mkali kuliko yeye. Hazard alizungumza hayo katika video iliyorushwa kwenye akaunti ya X ya UEFA Champions League. Kwenye video hiyo mwanasoka huyo mstaafu aliombwa kutulia (kukaa kimya) hadi atakaposikia jina la mwanasoka, ambaye anaamini alikuwa mpiga chenga bora kuliko yeye. Katika orodha hiyo majina yalianza kama ifuatavyo; Desire Doue wa Paris Saint-Germain, Rafel Leao wa AC Milan, Khvicha Kvaratskhelia wa Paris Saint-Germain, na Raphinha wa Barcelona, lakini Hazard alikaa kimya. Uso wake ukashtuka kidogo…

Read More

Mgombea Udiwani Kata ya Kariakoo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Haji Manara, amekutuna na kufanya kikao na Mtumishi wa Mungu kutoka Kanisa la Arise and Shine International, Mtume Boniface Mwamposa leo, Septemba 3, 2025. Kikao hicho kimefanyika Jijini Dar es Salaam na kimekuwa na lengo la kuendeleza ushirikiano kati ya viongozi wa kisiasa na wa kidini, hasa katika masuala yahusuyo maendeleo ya Jamii na ustawi wa wananchi wa Kariakoo na Tanzania. Wiki iliyopita Manara alikutana na Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Bin Zubeir na Mjumbe wa Baraza la Maulamaa nchini, Sheikh Hassan Chizenga ambao walimuombea Dua. Manara amemshukuru Mtume Mwamposa…

Read More

Klabu ya Yanga imesema haifanyi utani kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii, hivyo Kocha Mkuu, Romain Folz, amekuwa na ‘programu’ nne tofauti za maandalizi kuelekea mechi hiyo inayotarajiwa kupigwa, Septemba 16, mwaka huu, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Ofisa Habari wa Klabu hiyo, Ali Kamwe, amesema kocha wa timu hiyo amekuwa na mazoezi ya gym, ufukweni, uwanjani na darasani kwa ajili ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba ambao utakuwa unaashiria kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu mpya, Septemba 17, mwaka huu. Kamwe amesema kocha Romain anataka kuendeleza rekodi za makocha wenzake, Miguel Gamondi…

Read More

Beki wa zamani wa Real Madrid Sergio Ramos ameachia wimbo unaoitwa “Cibeles” akiimba mambo ya kihisia mengi kama sintofahamu ya yeye kuondoka Madrid. Ramos hakutaka kuondoka kamwe. Ndoto yake ilikuwa kustaafu katika jezi nyeupe Madrid. Lakini hadithi haikuisha jinsi inavyopaswa kuwa, hakuna kwaheri ya Bernabéu zaidi ya mkutano na waandishi wa habari tu. Kupitia wimbo huu, hatimaye anafunguka: “Sijawahi kutaka kuondoka, uliniuliza nipande ndege.” “Ningerudi kwa furaha, mara moja na hadi mara elfu.” “Kuanzia mtoto mwenye nywele ndefu hadi kuwa nahodha ambaye alinyanyua kila taji, gwiji ambaye alistahili kuagwa vizuri. Ameimba kwa hisia Ramos.

Read More

Simba imefanikiwa kumsajili mlinzi wa kati wa JKT Tanzania na kikosi cha Taifa Stars, Wilson Nangu kwa mkataba wa miaka miwili. Nyota huyo aliyekuwa na kiwango bora msimu uliopita akiwa na kikosi hicho cha Maafande ameshajiunga na kambi ya Simba iliyopo Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Msimu uliopita katika mchezo wa JKT Tanzania na Yanga uliochezwa Uwanja wa Meja Isamhuyo, Nangu aliibuka mchezaji bora wa mchezo huo kwa kuisaidia timu yake kupata sare ya bila kufungana.

Read More

KAULI ya Kocha Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids kwamba kikosi chake kinakosa mchezaji mwenye uwezo wa kipekee wa kuamua matokeo ya mechi (maarufu kama X-Factor) imeibua majibu kutoka kwa wapinzani wao wa jadi, Yanga SC. Msemaji wa Yanga, Ally Kamwe, hakusita kumjibu Davids kwa tambo akibainisha kuwa ndani ya kikosi cha Wananchi kuna wachezaji kadhaa wenye uwezo huo na zaidi. “Hakuna changamoto ya X-Factor ndani ya Yanga. Tuna wachezaji wengi ambao wanaweza kuibadilisha mechi kwa dakika chache tu. Hata baadhi yao tumeongeza kiwango chao cha ubora kiasi kwamba sasa wana X-Factor tatu,” alisema Kamwe. Akitaja baadhi ya nyota hao,…

Read More