UONGOZI wa Simba SC umebainisha kuwa sababu kubwa ya Simba Day kufanyika Septemba badala ya Agosti ni ratiba kubana huku wakipanga uzinduzi wa Wiki ya Simba kufanyika mkoano Iringa, wilayani Mafinga. Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kuwa Simba Day ni tamasha kubwa ambalo linazidi kuboreshwa kila siku huku la msimu huu likiwa katika upekee mkubwa. “Wote mnakumbuka tulitangaza kwamba Septemba 10, 2025 ndio itakuwa Simba Day. Wote mnafahamu mara nyingi Simba Day inafanyika wiki ya kwanza ya mwezi wa nane lakini kutokana na kubanana kwa ratiba na hasa mashindano ya CHAN imefanya imesogea…
Author: Admin
PITIA MAGAZETI YA MICHEZO LEO TAREHE 26 AGOSTI 2025
Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal Bukayo Saka huwenda akakosekana uwanjani kwa kipindi cha wiki tatu hadi wiki nne baada ya kupata jeraha la misuli ya paja ‘hamstring’ katika mchezo dhidi ya Leeds United. Taarifa za awali ambazo bado hazijathibitishwa na klabu yake Saka zinaripoti kuwa nyota huyo atakaa nje ya uwanja kwa wiki nne akiuguza jeraha lake baada ya kuumia katika mchezo huo.
MSHAMBULIAJI mpya wa Simba SC raia wa Ghana, Jonathan Sowah anatarajiwa kuukosa mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga SC utakaopigwa Septemba 16 2025, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mchezo huo wa Ngao ya Jamii ni maalumu kwa ajili ya kufungua msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika. Mshambuliaji huyo mpya Sowah hatocheza kutokana na kutumikia adhabu ya kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano kwenye fainali dhidi ya Yanga SC. Sowah alipata kadi hiyo nyekundu katika mchezo wa Fainali ya Kombe la CRDB ambao ulipigwa…
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC wameanza kupiga hesabu kuelekea mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Simba SC. Mchezo huo unasubiriwa kwa shauku kubwa unatarajiwa kuwa na ushindani ndani ya dakika 90 kwa wababe hao katika uwanja kusaka ushindi. Inaelezwa kuwa tayari Kocha Mkuu wa Yanga SC, raia wa Ufaransa, Romain Folz amekabidhiwa video za michezo ya mwisho ya Ligi Kuu Bara ya wapinzani wao Simba SC ambao kwa sasa wapo nchini Misri kwa kambi kuelekea msimu mpya. Kwa mujibu wa chanzo kutoka ndani ya Yanga SC, video zaidi ya mbili tayari amepatiwa kocha huyo haraka tayari…
Droo ya makundi ya Kombe la Dunia 2026 imepangwa kufanyika tarehe 5 Disemba 2025 katika Kituo cha Kennedy, Washington DC Nchini Marekani. Mashindano hayo yanayofanyika mara ya 23 yataandaliwa kwa mara ya kwanza na mataifa matatu ambayo ni Marekani,Mexico na Canada 🇨🇦, yakihusisha timu 48 kwa mara ya kwanza katika historia. Michuano hiyo itaanza kutimua vumbi rasmi Juni 11 hadi julai 19 mwaka 2026.
Klabu ya Manchester City imepoteza mchezo wa ligi kuu ya Uingereza wakiwa nyumbani dhidi ya Tottenham Hotspur kwa magoli 2-0. Magoli ya Spurs yamefungwa na Brennan Johnson pamoja na Jao Palhina katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo
Ushindi mnono upo Jumamosi ya leo na kampuni kubwa ya ubashiri ya Meridianbet. Tengeneza jamvi lako lenye mechi nyingi sana huku machaguo zaidi ya 1000 yakiwa yanakusubiri. Napoli, City, Barcelona na wengine kibao wanakungoja. BUNDESLIGA kule Ujerumani kuendeleaBayer Leverkusen chini ya Ten Hag watamleta nyumbani kwao TSG Hoffenheimambao kushinda mechi hii wamepewa ODDS 5.20 kwa 1.57. Pesa yako unaiweka wapi kwa timu hizi mbili?. Beti hapa. Werder Bremen wao watasafiri kukiwasha dhidi ya Eintracht Frankfurt ambao ndio wanaopewa nafasi ya kushinda mechi hii ya leo wakiwa na ODDS 1.72 kwa 4.60. Takwimu zinaonesha kuwa mara ya mwisho kukutana, mwenyeji alifungwa.…
Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Crystal Palace raia wa Uingereza Eberechi Eze ni rasmi amesaini mkataba wa kuitumikia klabu ya Arsenal kilichosalia tu ni utambulisho. Siku ya jana nyota huyo aliripotiwa kufanya vipimo vya afya na leo mapema taarifa kutoka Uingereza zinaripoti kuwa nyota huyo amesaini kuitumikia klabu hiyo ya ndoto zake na muda wowote atatambulishwa.
Klabu ya Singida BS imetangaza rasmi kupitia kurasa zao za mitandaoni ya kijamii kwamba hakutakuwa na tamasha la Singida Big Day msimu huu kutokana na ufinyu wa ratiba. “Kutokana na ufinyu wa ratiba,tumelazimika kusitisha tamasha la SINGIDA BIG DAY 2025 ambalo lilikua lifanyike uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta” Wameandika Singida Black Stars.
Mkuu wa mkoa wa Dar es saalam Albert Chalamila ametoa ahadi ya zawadi ya gari aina ya Crown kwa kipa wa Taifa Stars endapo hatoruhusu goli katika mchezo wa leo dhidi ya Morocco. Sambamba na hilo pia mechi ya leo kila goli litanunuliwa kwa Sh Milioni 5 huku mfungaji wa goli atakabidhiwa Sh Milioni 1 na aliyetoa asisti atapewa Sh Laki 5 hiyo yote kwaajili ya kuendelea kuhamasisha timu ya taifa iweze kufanya vizuri.
Achana na hiyo picha iliyoko mbele ya macho yako ambayo kuanzia jana ilivyopigwa mpaka leo imekuwa picha pendwa mtandaoni. Hao ni Wakuu wa Idara za Habari na Mawasiliano wa timu pendwa za Yanga SC na Simba SC. Mmoja Ali Kamwe. Mwingine ni Ahmed Ally. Leo usiku Taifa letu la Tanzania litakuwa na mchezo wa kutafuta nafasi ya kuingia Nusu Fainali ya Mashindano ya CHAN kwa mara ya kwanza. Mpinzani wetu ni Morocco ambao ni mabingwa mara mbili wa michuano hii. Tunawaheshimu Morocco, lakini hatuwaogopi. Kimsingi Amiri Jeshi Mkuu wa nchi Dr. Samia Suluhu Hassan ameshatimiza wajibu wake kwa kutoa kiasi…
TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo Agosti 22 2025 ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali dhidi ya Morocco ikiwa ni CHAN 2024. Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa saa mbili usiku huku benchi la ufundi la Stars likibainisha kuwa lipo tayari kuhakikisha matokeo yanapatikana ndani ya dakika 90. Hemed Suleman, Kocha Mkuu wa Stars amesema wanatambua kwamba mchezo hautakuwa mwepesi kutokana na ugumu wa hatua waliyopo lakini wapo tayari kwa ajili ya kupata matokeo mazuri. “Nimefarijika kuona tunatengeneza nafasi suala la kutuma nafasi bado tunaendelea kuhakikisha tunapamana nalo, kabla ya mashindano…
PITIA MAGAZETI YA MICHEZO LEO TAREHE 22 AGOSTI 2025
Timu ya Simba SC rasmi imemtambulisha kiungoa Neo Maema akitokea katika klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini. Maema ambae anatarajiwa kuongeza nguvu katika nafasi ya kiungo kwenye kikosi cha Simba amesahiliwa kwa kandarasi ya Mwaka mmoja ndani ya Msimbazi.
YANGA SC mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika wakiwa na mataji 31 kabatini wametambulisha nyota watatu ndani ya Agosti 2025. Katika wachezaji hao usajili ambao ulitikisa ni ule wa beki Mohamed Hussen Zimbwe Jr aliyetambulishwa hapo akitokea kikosi cha Simba SC baada ya mkataba wake kugota mwisho msimu wa 2024/25. Leo Agosti 21 2025 Yanga SC imtambulisha nyota mpya kuelekea msimu wa 2025/26 ambaye ni beki wa kati. Anaitwa Frank Assinki ambaye ni raia wa Ghana na msimu wa 2024/25 alikuwa ndani ya kikosi cha Singida Black Stars. Ikumbukwe kwamba mchezaji wa kwanza…
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ameikabidhi timu ya taifa ya soka ya Tanzania (Taifa Stars) kiasi cha Milioni 200 za Kitanzania, wakati timu hiyo ikijiandaa kumenyana na Morocco katika mchezo wa robo fainali, utakaofanyika Agosti 22, 2025. Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi amesema kiasi hicho cha fedha ni kama zawadi na hamasa kwa wachezaji hao wanapojiandaa na mchezo muhimu dhidi ya Morocco.
José Mourinho amefichua kwamba Lionel Messi alimfanya kuwa kocha bora, akikiri kwamba kukabiliana na Muargentina huyo mara kwa mara kulimsukuma kutafakari upya mbinu zake na kufikia kiwango cha juu zaidi cha soka. Mtaalamu huyo wa kireno, alipambana na Messi katika baadhi ya mechi kali katika maisha yake ya soka akiwa kocha wa Inter Milan na Real Madrid. Alipoulizwa na Sporty Net ataje mchezaji ambaye amemsaidia kukua, Mourinho alijibu: “Messi, kwa sababu kila nilipocheza dhidi yake alinilazimisha kufikiria sana.” Wakati akiwa Inter, kikosi cha Mourinho kiliishinda Barcelona ya Messi kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka 2010 na baadaye akiwa…