Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Contact Us
    • Privacy Policy
    Facebook Instagram YouTube
    Chikao Media
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • MAGAZETI YA LEO
    • TETESI ZA SOKA
    • BOXING
    • FORUM
    Chikao Media
    Home » SIMBA SC KUZINDUA UZI MPYA AGOSTI 27 2025
    KITAIFA

    SIMBA SC KUZINDUA UZI MPYA AGOSTI 27 2025

    By AdminAugust 20, 2025No Comments2 Mins Read
    Share WhatsApp Facebook Twitter Pinterest Telegram Email Copy Link
    Follow Us
    Facebook Instagram YouTube
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email Copy Link

    UONGOZI wa Simba SC umetaja siku rasmi itakayokuwa ni maalumu kwa uzinduzi wa uzi mpya wa timu hiyo kuelekea msimu mpya wa 2025/26 unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

    Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC ameweka wazi kuwa uzinduzi wa uzi mpya utakuwa watofauti kidogo kutokana na mpango kazi uliopo.

    “Jezi za Simba msimu huu tutazindua kwa namna tofauti kidogo, ipo namna ambayo tumezoea jezi huwa zinazinduliwa lakini safari hii sababu tuna mdhamini mpya wa jezi kampuni ya JayRutty akishirikiana na kampuni ya kimataifa ya Diadora tukaamua kufanya kitu kipya chenye mvuto kwa jamii na biashara ya jezi kuwa na mvuto wa tofauti.

    “Jezi za Simba SC msimu wa 2025/26 zitazinduliwa tarehe 27/Agosti/2025, jezi zitazinduliwa majira ya saa 1:00 usiku na shughuli itafanyika kwenye ukumbi wa Super Dome uliopo Masaki. Safari hii tumefanya kuwa tukio kubwa, tukio lenye hadhi ya ushua na kulifanya kuwa tukio bora ambalo litakutanisha wadau wakubwa wa Simba Sports Club na ambao wanataka kununua jezi ya Simba  SC baada ya kuzinduliwa.

    “Siku hiyo wenye dhamira ya kushuhudia uzinduzi wa jezi na baada ya uzinduzi hapo hapo ukumbini watapewa jezi zao tatu. Kwanza kutakuwa na wasanii mbalimbali, tutakuja kuwatangazia msanii mmoja baada ya mwingine lakini pia kutakuwa na live band, kutakuwa na vinywaji pamoja na vyakula vya kutosha. Kwa upekee na kulifanya kuwa bora kabisa kutakuwa na mgeni rasmi ambaye ni mchezaji wa zamani bora barani Afrika, ambaye ametikisa Afrika, ambaye amefanya makubwa kwenye mpira, mchezaji ambaye anajulikana dunia nzima ndiye atakuwa mgeni rasmi na ndio ataitambulisha jezi kwa mara ya kwanza.

    “Yeyote ambaye atahitaji kuhudhuria tukio hili la uzinduzi wa jezi na kuwa mtu wa kwanza kuona jezi ya Simba SC msimu huu atalipa Tsh. 250,000. Akishalipa hiyo fedha yote ambayo atapata ndani ya ukumbi ni juu yetu na baada ya hapo atapewa jezi zote tatu za msimu huu. Vyote hivyo atakabidhiwa hapo hapo ukumbini.

    “Mara baada ya uzinduzi huo, jezi za Simba SC zitaanza kuuzwa kwenye maduka yote ambayo yameshaweka pre order na wanasubiri mzigo wao. Wakati zoezi la uzinduzi linafanyika Super Dome, kwenye maduka muda huo huo watakuwa wanachukua mizigo yao kwenda kuwauzia Wanasimba. JayRutyy ameleta jezi nyingi kwelikweli, uwe Simba SC, usiwe Simba SC zinamtosha kila Mtanzania,” amesema Ahmed Ally.

    Follow on Facebook Follow on Instagram Follow on YouTube
    Share. WhatsApp Facebook Twitter Pinterest Email Copy Link
    Previous ArticleHII HAPA TAREHE YA MECHI YA SIMBA NA YANGA MWAKA HUU 2025
    Next Article FEISAL SALUM AFICHUA HESABU ZA TANZANIA CHAN 2024

    Related Posts

    Ujenzi wa Arena, Serikali Yatenga Bil400

    April 3, 2026

    Selemani Mwalimu Yupo Anakuja, Mjiandae

    April 3, 2026

    MSIGWA AELEZA SABABU ZA KUONGEZEKA GHARAMA UWANJA WA ARUSHA

    March 31, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    Bernardo Apewa Thank You Rasmi Man City

    Ujenzi wa Arena, Serikali Yatenga Bil400

    Selemani Mwalimu Yupo Anakuja, Mjiandae

    MSIGWA AELEZA SABABU ZA KUONGEZEKA GHARAMA UWANJA WA ARUSHA

    Neymar amuachia Mungu kutoitwa timu ya Taifa

    “Nimehuzunika,Nimeumia lakini ndoto bado inaishi”Neymar Jr.

    © 2026 CHIKAO MEDIA | All Rights Are Reserved
    • Contact Us
    • Privacy Policy

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.