KUELEKEA msimu mpya wa 2025/26 ni Fadlu Davids, Kocha Mkuu wa Simba SC ameachiwa msala kwenye suala la usajili baada ya kupewa jukumu hilo kuhakikisha kwamba kila kitu anasimamia mwenyewe. Simba SC imeweka kambi Misri kwa maandalizi ya msimu mpya unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku wakifanya usajili wa wachezaji wapya ikiwa ni Jonathan Sowah aliyekuwa Singida Black Stars, Morice Abraham, Anthony Mligo na kuna wengine wapo kwenye majaribio. Kitendo cha mabosi wa Simba SC kubainisha kuwa ambaye anasimamia usajili kwa asilimia 100 ni sawa na kumuachia msala kocha huyo jambo lolote likitokea kwa wachezaji kufeli mzigo ataangushiwa yeye. Ahmed…
Author: Admin
Klabu ya Singida Black Stars imetangaza rasmi kuwa tamasha lao la kila mwaka la ‘Singida Big Day’ litafanyika mwaka huu kwa mara ya kwanza jijini Arusha katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, tarehe 6 Septemba 2025. Black Stars wanafanya tamasha hilo nje ya Singida ni kufuatia ukarabati unaoendelea katika uwanja wa Airtel Stadium na CCM LITI mkoani Singida pamoja na lengo la kupanua wigo wa mashabiki wa timu hiyo kutoka kanda ya Kaskazini na kuimarisha hadhi ya Singida Black Stars kitaifa. Tamasha hilo litafanyika matukio muhimu kama utambulisho wa kikosi kipya cha Singida Black Stars pamoja na ripoti ya usajili…
Mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden Alexander Isak amesisitiza kuwa hatacheza tena Newcastle – hata kama hatapata timu kwenye dirisha hili la uhamisho. Kulingana na David Ornstein, mshambuliaji huyo anachukulia kazi yake ya #NUFC kuwa imekamilika. Hata kama Newcastle watakataa kumuuza, hana hamu ya kujumuishwa tena kwenye kikosi cha 1 na kucheza mechi nyingine.
Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga Ally Kamwe ameweka wazi kuwa kuna ugumu wa kufanya sherehe za wiki ya wananchi kwa mwaka huu kutokana na ugumu wa ratiba na upatikanaji wa uwanja. “Tunapamba siku ya Wananchi iwepo lakini kuna changamoto nyingi tunapitia, ukiangalia mashindano ya CHAN yanaisha tarehe 30 na tarehe 1 kuna Kalenda ya FIFA na tarehe 11 kuna ngao ya Jamii lakini changamoto kubwa ni Uwanja”. “Ukifanya Wiki ya Wananchi maana yake tutafanya bila Wachezaji wetu wote na itakuwa kwa mara ya kwanza, tunaendelea kupambana na ikipatikana jibu sahii tutakuja kuwajibu.” Amesema Kamwe.
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetishia kuhamisha mechi zilizosalia za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) kutoka Kenya baada ya kudorora mara kwa mara kwa usalama katika Uwanja wa Kimataifa wa Michezo cha Moi, Kasarani. CAF ilitaja ukiukwaji mwingi, ikiwa ni pamoja na kukanyagana kulikosababishwa na kuingia bila kibali, mashabiki kuwasha moto, pikipiki kupita katikati ya watu, na kushambuliwa kwa wafanyikazi na wafadhili wa CAF na mlinzi aliye na kandarasi. Matukio ya ziada wakati wa mechi dhidi ya Angola na Morocco yalihusisha mashabiki kuruka vizuizi na kuwasha milipuko ndani ya uwanja. Kwa kujibu, CAF ilisitisha uuzaji wa tikiti kwa michezo…
Rais wa Kenya, William Ruto, leo amekutana na kikosi cha Harambee Stars na kutoa ahadi nono kuelekea mechi ya mwisho ya Kundi A ya michuano ya CHAN 2024 dhidi ya Zambia, itakayopigwa Jumapili katika Uwanja wa Kasarani. Ruto amethibitisha kutimiza ahadi yake ya awali ya kuwapa wachezaji KSh milioni 1 (TSH 19.2 milioni) kila mmoja kwa kila ushindi wa mechi za makundi, lakini safari hii ameongeza dau, akiahidi KSh milioni 2.5 (TSh 48 milioni) kwa kila mchezaji endapo wataibuka na ushindi dhidi ya Zambia. Zaidi ya hapo, Rais Ruto ameahidi kutoa KSh milioni 1 (TSH 19.2 milioni) na nyumba ya…
Baada ya miaka 9 ya kuwa kwenye mahusiano, nguli wa soka Cristiano Ronaldo amemvalisha rasmi pete ya uchumba mpenzi wake Georgina Rodriguez, hii ikimaanisha kuwa ndoa ya wawii hao inanukia. Ronaldo na Rodriguez wana watoto wanne pamoja mapacha Eva Maria na Mateo (aliyezaliwa 2017), Alana (aliyezaliwa 2017) na Bella (aliyezaliwa 2022). Kwa bahati mbaya, pacha wa Bella alikufa mwaka 2022. Wanandoa hao pia wanaishi na mtoto mkubwa wa Ronaldo, Cristiano Ronaldo Jr. (aliyezaliwa mwaka 2010).
WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye anga la kimataifa katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba SC wameanza kazi kupima kikosi chao wa kupata ushindi kwenye mchezo wa kirafiki. Simba SC chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids kambi yao ni nchini Misri kwa maandalizi ya msimu wa 2025/26. Agosti 11 2025 walicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Kahraba Ismailia ikiwa ni maalumu kwa ajili ya kujipima nguvu na mwisho walipata ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo huo. Wafungaji kwenye mchezo huo ni wapya ikiwa ni Mohamed Bajaber aliyefunga bao moja katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Kahraba Ismailia uliochezwa Uwanja wa Suez Canal…
Ifahamu Gaborone United Wapinzani wa Simba Ligi ya Mabingwa CAF 2025/2026 Wababe wa kulisakata kabumbu wa Tanzania Bara na Visiwani Simba SC, Yanga SC, Azam FC, Singida Black Stars, KMKM na Mlandege SC wameshajua wapinzani wao kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho kwa hatua ya awali ya kufuzu makundi. Droo hiyo, iliyofanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania, ilishuhudiwa na magwiji wa soka wa zamani, akiwemo Sunday Manara aliyeichezea Yanga na Abdallah Kibadeni aliewahi ichezea Simba, wote wakikumbukwa kwa mchango wao mkubwa miaka ya 1970. Katika matokeo ya droo hiyo iliyohusisha michuano ya ligi ya…
Wote tunajua inapofika hatua ya mikwaju ya penati, ustadi wa golikipa ndio huamua mshindi wa mchezo. Jambo hilo ndilo lililodhihirika juzi kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii nchini Uingereza ambapo akili na ustadi wa golikipa wa Crystal Palace Dean Henderson uliweza kuizawadia taji la Ngao ya Jamii Shield klabu yake iliposhinda dhidi ya Liverpool. Henderson aling’ara kwa kuweka kwapani penati mbili muhimu, akitumia “karatasi maalum ya majina” iliyokuwa imebandikwa kwenye chupa yake ya maji, yenye maelezo ya wapi wachezaji wa Liverpool hupiga penati zao. Taarifa zinaeleza kuwa Henderson alijiandaa mapema kabla ya mchezo, akitumia muda kusoma tabia za wapiga penati…
Mshambuliaji mpya wa Simba Jonathan Sowah jana alifungia bao timu hiyo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Carabat FC. Simba iko kambini nchini Misri kujiandaa na msimu mpya, jana ilicheza mchezo huo wa na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0. Bao lingine katika mchezo huo limewekwa kimiani na kiungo mpya mshambualiaji raia wa Kenya, Mohammed Bajaber.
Klabu ya kaskazini mwa London ya Tottenham sasa inahusishwa na mmoja wa washambuliaji chipukizi bora zaidi wa kiBrazil, Savinho wa Manchester City. Kwa mujibu wa The Athletic, Spurs wamewasiliana na Man City kuhusu nia yao ya kumsajili mchezaji huyo na inaelezwa mazungumzo yamekuwa yakiendelea katika siku za karibuni. Taarifa zinaweka wazi kuwa City wako tayari kumuuza Savinho ikiwa tu anataka kuhama, na ikiwa hali itakuwa hivyo basi watahitaji dau la pauni milioni 50 ili kumruhusu aondoke.
Je unajua kuwa zimebakia siku 4 pekee za kuanza kumsaka bingwa wa Laliga Hispania?. Basi anza safari yako ya ushindi ukiwa na wakali wa ubashiri Tanzania tengeneza jamvi lako la kuchagua mshindi wako unayeona atanyakua taji hilo mwisho wa msimu. Real Madrid ndio ambao wanapewa nafasi ya kwanza kabisa kuchukua taji hili wakiwa na wa ODDS 1.77. Msimu uliopita walimaliza nafasi ya 2 na kikosi hiki ambacho kinaongozwa na kocha mkuu Xabi Alonso waliamua kuongeza wachezaji wapya kikosini hapo akiwemo Trent, Dean Huijsen, Alvaro Fernandez na wengine wengi. Kwa kikosi ambacho wanacho Real kama vile Mbappe, Vini, Bellingham , wanaweza kuchukua…
SIMBA SC bado ipo sokoni kusaka wachezaji wapya kuelekea msimu mpya wa 2025/26 unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Kikosi cha Simba SC kwa sasa kipo Misri kwa maandalizi ya msimu mpya ambapo inaelezwa kuwa huenda Joshua Mutale akaachwa kuelekea msimu mpya kupisha nafasi ya mchezaji mpya. Mbali na Mutale, Leonel Ateba naye yupo kwenye hesabu za kuachwa na Simba SC kutokana na mwendo wake kutokuwa imara kwa msimu uliopita. Eneo ambalo Simba SC kwa sasa inafanyia kazi ni beki wa kushoto mgeni atakayeongeza nguvu eneo hilo ambalo Mohamed Hussen Zimbwe Jr ameondoka. Zimbwe Jr yupo ndani ya kikosi cha Yanga…
….. OFA IMEKATALIWA. Jana tulilala na neno hili. Barua za Waarabu zimeendelea kupishana pale Jangwani. Inaingia barua hii, baada ya muda inaingia barua nyingine. Zote zinazungumzia upatikanaji wa Mzize. Wanachokifanya Yanga SC ni kumtafuta yule mwenye kisu kikali ndio ale nyama. Mimi siamini kama Mzize atacheza Yanga SC msimu ujao. Hili siamini, lakini wanachokifanya Yanga SC ni kuiongezea thamani biashara ya Mzize. Itafika tu timu ambayo itatoa ofa ya maana na itakuwa ngumu ofa hiyo kukataliwa. Uzuri Mzize mwenyewe anazidi kuichonganisha biashara yenyewe. Juzi ametupia mabao mawili katika jezi za Stars. Ninachoamini iko timu itafikia kiasi ambacho Yanga SC watakipokea.…
KOCHA Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids amesema kuwa wamefanya maboresho makubwa kwenye kikosi kwa kupata saini za wachezaji ambao watakuwa na kazi kupambana kwenye mashindano ambayo watashiriki. Simba SC msimu wa 2024/25 ilishiriki Kombe la Shirikisho Afrika na kugotea hatua ya fainali ikiwa nafasi ya pili na bingwa alikuwa RS Berkane. Msimu wa 2025/26 Simba SC itapeperusha bendera kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. Fadlu ameweka wazi kuwa watakuwa kwenye aina tofauti ya mashindano ambayo yanahitaji ushindani mkubwa na aina ya wachezaji waliopo watakuwa na kazi kupambania ushindi. “Unaona kuna wachezaji ambao wamesaini kwenye kikosi. Ni aina ya wachezaji wazuri…
Mshambuliaji na nyota wa Al-Nassr, Cristiano Ronaldo amemrushia maua yake mchezaji mpya wa Arsenal, Viktor Gyokeres akimuita mwanasoka ‘Special’. Gyokeres alihamia Arsenal akitokea Sporting ambapo alifunga mabao 97 katika mechi zaidi ya 100 alizocheza na klabu hiyo kwenye mashindano yote. Hata hivyo, Ronaldo, ambaye pia alianza soka lake la kulipwa katika klabu ya Sporting, alisisitiza kwamba klabu yake ya zamani itabakia klabu bora yenye ushindani licha ya Gyokeres kuondoka. “Siku zote huwa naitakia mema Sporting na wanaweza kuwa mabingwa tena,” Ronaldo alinukuliwa na Metro UK akisema. “Viktor alikuwa mchezaji wa kipekee, lakini Sporting italazimika kuzoea.” alimalizia Ronaldo.
Washindi wa pili wa Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita Simba SC wamepangwa kucheza dhidi ya timu ya Gaborone United Botswana. Simba SC wamepangwa kuanzia ugenini kwa ratiba ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na hiyo inakuwa mara ya pili kwa miaka ya hivi karibuni Simba SC kupangiwa na timu za nchini humo. Mara ya mwisho Simba SC ilipangwa na timu ya Jwaneng Galaxy na iliondolewa mashindanoni kwa faida ya mabao ya ugenini.