Author: Admin

Michezo ya Ngao ya Jamii hatua ya nusu fainali inatarajiwa kuchezwa September 11 huku mchezo wa fainali ukitarajiwa kuchezwa September 14 kabla ya kufunguliwa rasmi kwa pazi la ligi kuu msimu wa 2025/26. Nusu Fainali ya itazikutanisha timu za Yanga na Azam huku Simba akicheza dhidi ya Singida Black Stars na washindi wawili wa  michezo hiyo watafuzu kucheza fainali ya taji hilo.

Read More

Kuelekea msimu wa 2025/26, Uongozi wa Young Africans leo asubuhi umekutana na Benchi la ufundi, wachezaji na watendaji wa Klabu kwa ajili ya utambulisho na semina kuhusu historia, matarajio na majukumu ya kila mmoja ndani ya Klabu Hafla hii imefanyika kwenye hoteli ya Rotana, Jijini Dar Es Salaaam.

Read More

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amekabidhi Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) kitita cha shilingi milioni 20 (Goli la Mama) baada ya kuifunga Burkina Faso 2 – 0 katika ufunguzi wa Mashindano ya CHAN Agosti 2, 2024 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, ambazo zimetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kama alivyoahidi kila goli moja shilingi milioni kumi. Pia Prof. Kabudi nae ametoa shilingi milioni 20 pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ndg. Chalamila ambaye amewapatia kiasi cha…

Read More

Mshambuliaji wa klabu ya Pyramids ya Misri Fiston Kalala Mayele jana ametwaa tuzo ya mshambuliaji bora wa Ligi kuu soka ya Misri. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Congo DR ametwaa tuzo hiyo baada ya kucheza michezo 23 na kufunga magoli 8 huku akipika magoli mawili. Kwenye msimu huo pia Mayele alifunga magoli 6 kwenye mechi 10 za Ligi ya Mabingwa Afrika yaliyosaidia Pyramids kuwa Mabingwa Afrika.

Read More

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa Agosti 02, 2025 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye sherehe za ufunguzi rasmi wa michuano ya CHAN 2024, katika Dimba la Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam. Katika mchezo wa ufunguzi Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inachuana na Burkina Faso. Michuano hiyo inafanyika katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.

Read More

WAKATI akitajwa kuwa huenda anaweza kuwa nyeupe na nyekundu kiungo mkabaji Khalid Aucho inaelezwa kuwa mpango huo ni ngumu kukamilika. Tetesi zimekuwa zikieleza kuwa Simba SC inahitaji huduma ya Aucho ambaye mkataba wake umegota mwisho ndani ya Yanga SC msimu wa 2024/25. Kwa sasa ni mchezaji huru na amewashukuru Yanga SC na mashabiki kwa kuwa naye bega kwa bega nyakati zote hizo alipokuwa na uzi wa kijani na njano. Aucho msimu wa 2024/25 kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika alihusika kwenye mabao mawili, alifunga bao moja na kutoa pasi moja ya bao. Taarifa zinaeleza…

Read More

Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars itashuka leo dimbani majira ya saa 2 usiku katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kucheza na Timu ya Taifa ya Burkina Faso kwenye mchezo wa kwanza wa kundi B katika ufunguzi wa mashindano ya CHAN 2024. CHAN ni Mashindano yanayohusisha wachezaji wa ligi za ndani ambayo kwa mara ya kwanza yanafanyika Afrika Mashariki kwa ushirikiano wa Nchi tatu ambazo ni Tanzania Kenya na Uganda huku Tanzania ikiwa mwenyeji wa mchezo wa ufunguzi. Tanzania inakutana na Burkina Faso ambayo haijawahi kupata ushindi dhidi ya Taifa Stars wakiwa nyumbani katika michezo mitatu ya mwisho waliyokutana nayo…

Read More

Taifa la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) limetangaza rasmi kuingia makubaliano ya udhamini wa miaka minne na mabingwa wa Hispania FC Barcelona wenye thamani ya Bilioni 134 kwa ajili ya kuvutia utalii na kuhamasisha uwekezaji kutoka nje ya Taifa lao. Kutokana na mkataba huo wachezaji wa Barcelona wataanza kuvaa jezi za mazoezi zenye maandishi “DR Congo “Moyo wa Afrika” kuanzia msimu ujaohuku pia ikihusisha kambi za mafunzo kwa vijana, maonyesho ya utamaduni wa Kongo kwenye uwanja wa Camp Nou, pamoja na programu mbalimbali za michezo.

Read More

Klabu ya Yanga imemtambulisha rasmi mshambuliji Célestin Ecua, raia wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 23, kama mchezaji mpya wa kikosi chao kwa msimu ujao, akitokea klabu ya Zoman FC ya nchini kwao. Ecua alikuwa kwenye kiwango bora msimu uliopita akiwa na Zoman FC, ambapo alifunga magoli 15 na kutoa ‘assists’ 12 katika michuano yote aliyoshiriki. Uwezo huo ulimuwezesha kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Msimu (MVP) nchini Ivory Coast. Kwa ujio wake, safu ya ushambuliaji ya Yanga SC inaendelea kuimarika zaidi, ikiwa ni maandalizi ya kushiriki michuano ya ndani na kimataifa kwa mafanikio makubwa.

Read More

Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limemfuta kazi aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Waamuzi, Désiré Noumandiez Doué, kwa makosa yaliyofanywa katika Kombe la Afrika la Wanawake. Haya yanajiri baada ya Shirikisho la soka la Morocco (FRMF), kuwashutumu Waamuzi akiwemo Mukansanga Salima na Umutesi Alice kwa kuchezesha isivyo Fainali ya Kombe la Afrika kwa Wanawake. Mukansanga Salima aliongoza timu ya waamuzi waliokuwa wakifuatilia picha za VAR Nigeria iliposhinda 3-2 dhidi ya Morocco kwenye fainali. Athari kwa Waamuzi imeanza kuonekana kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa na Morocco, raia wa Ivory Coast Désiré Noumandiez Doué, ambaye alikuwa mwakilishi wa Waamuzi katika CAF akifukuzwa kazi. CAF pia…

Read More

RASMI Simba SC imemalizana na mshambuliaji wa mabao Jonathan Sowah ambaye alikuwa mali ya Singida Black Stars na sasa atakuwa mali yao. Ikumbuwe kwamba Julai 31 2025 Simba SC ilitambulisha wachezaji wawili wapya ambao ni Morice Abraham alitambulishwa ndani ya Simba SC Julai 31 2025 na Hussein Daudi Semfuko alitambulishwa Simba SC, Julai 31 2025 kuwa ni mali ya Simba SC. 2024/25 alikuwa akicheza Coastal Union ya Tanga. Jonathan Sowah alikuwa ndani ya Singida Black Stars ni raia wa Ghana ambaye msimu wa 2024/25 akiwa na Singida Black Stars alifunga jumla ya mabao 13 kwenye ligi akiwa ni ingizo jipya dirisha…

Read More

Klabu ya Yanga  imemtambulisha rasmi mshambuliaji Andy Bobwa Boyeli (24) kama mchezaji mpya wa kikosi hicho kwa mkataba wa mkopo wa msimu mmoja kutoka Sekhukhune United ya Afrika Kusini, ukiwa na kipengele cha kununuliwa kabisa mwishoni mwa mkataba. Boyeli anasifika kwa uwezo mkubwa wa kufumania nyavu na alijizolea umaarufu mkubwa msimu wa 2022/23 akiwa na Power Dynamos ya Zambia, ambapo: Alitwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Msimu (MVP) Alikuwa Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya Zambia kwa mabao 18 Ujio wake unaongeza nguvu mpya kwenye safu ya ushambuliaji ya Yanga SC inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara na michuano…

Read More

Aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Simba Queens, Precious Christopher amesaini mkataba wa mwaka mmoja na Yanga Princess wenye kipengele cha kuongeza kama atafanya vizuri. Msimu uliopita Precious aliichezea Simba Queens akifunga mabao mawili na asisti tatu kwenye mechi 18 za Ligi Kuu alizocheza. Kwa mara ya kwanza Precious alitambulishwa Yanga msimu wa 2021 akitokea kwao Nigeria na akaicheza kwa misimu miwili na uliopita akaenda kwa wapinzani wao Simba.

Read More

Unaweza kuliita pigo kuu kwa timu ya taifa ya Kenya, maarufu kama ‘Harambee Stars’ inayoshiriki michuano ya CHAN 2024, baada ya kiungo wao fundi Mohammed Bajaber kujiunga na Simba Sports Club ya Tanzania kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu na michuano mingine ya kimataifa. Bajaber anadaiwa kujiunga na klabu ya Simba ambayo iko kambini nchini Misri, kwa maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu. Hii inamaanisha kuwa, Bajaber atakosa michuano ya CHAN 2024, ambayo ni maalumu kwa wachezaji wanaoshiriki ligi za ndani.

Read More

Kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania Morice Abraham amejiunga rasmi na wekundu wa msimbazi kama mchezaji wao kuelekea msimu ujao wa mashindano akitokea Spartak Subotica ya Serbia kwa mkataba wa miaka miwili. Morice ambaye amefanya mazoezi na timu ya Simba mwishoni mwa msimu uliopita ni chaguo la kocha Fadlu Davids baada ya kuridhishwa na kiwango chake. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 amekulia katika Kituo cha kukuzia vipaji cha Alliance Academy cha jijini Mwanza anakumbukwa kuwa na nahodha wa timu ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’ kilichoshiriki AFCON mwaka 2019 ambayo Tanzania alikuwa…

Read More

Bodi ya ligi kuu soka Tanzania bara imetangaza rasmi kuwa msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara utaanza Septemba 16,2025. Kwa namna heka heka za usajili zilivyo mpaka sasa unadhani ni timu gani ina uwezo wa kutwaa ubingwa wa ligi msimu wa 2025/26?

Read More